Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 9 Septemba 2019

BILION 30 ZATOLEWA KILA MWAKA KWAAJILI YA HUDUMA ZA CHANJO

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikabidhi funguo ya gari kwa Mganga Mkuu wa Dar es Salaam Dkt. Yudas Ndungile Katika shughuli ya ugawaji wa magari kwa Halmashauri 61 nchini, shughuli iliofanyika katika ofisi za mpango wa chanjo taifa Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwasha gari ishara ya uzinduzi wa magari hayo yaliyotolewa na Serikali kwa Halmashauri 61 ili kurahisisha shughuli za chanjo nchini.
 

Baadhi ya magari ya yatayosaidia shughuli za chanjo yaliyoyolewa na Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa halmashauri 61 nchini, shughuli imefanyika katika ofisi za mpango wa chanjo wa taifa Jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikagua moja kati ya majokofu ya kuhifadhia chanjo, ameambatana na Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya Dkt Leonard Subi (wakatikati) na Meneja wa mpango wa taifa wa Chanjo Dafrosa Lyimo (wakwanza kushoto) wakati wa kukabidhi magari ya chanjo kwa Halmashauri 61 nchini.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati  wa mkutano na Waandishi wa habari wakati wa kukabidhi  magari ya  chanjo kwa Halmashauri 61 ili kurahisisha shugchanjo nchini.


Baadhi ya Waandishi wa Habari na baadhi ya Waganga Wakuu wa Wilaya waliojitokeza katika shughuli ya ugawaji wa magari ya chanjo kwa Halmashauri 61 nchini uliofanywa leo na Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu




BILION 30 ZATOLEWA KILA MWAKA KWAAJILI YA HUDUMA ZA CHANJO

Na WAMJW-DSM

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto yatoa kiasi cha shilingi Bilion 30 kila mwaka kwaajili ya huduma za Chanjo ili kuwakinga wananchi dhidi ya magonjwa mbali mbali.

Hayo yamesemwa na waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo wakati akikabidhi magari 71 ya chanjo kwaajili ya Halmashauri 61, na magari 10 kwaajili ya Mpango wa chanjo nchini ikiwa ni sehemu ya kuimarisha huduma za chanjo kwa Wananchi.

Waziri Ummy amesema kuwa, Serikali imetoa magari hayo ili kurahisisha shughuli za chanjo katika maeneo mbali mbali hivyo, ameagiza magari hayo yakafanye kazi kulingana na madhumuni yaliyokusudiwa.

Waziri Ummy aliendelea kusema, Serikali itaendelea kuhakikisha kuwa Halmashauri zote zilizobaki zinapata magari ya chanjo ili kurahisisha utendaji kazi katika maeneo yote nchini.

Kwa upande mwingine Waziri Ummy amesema kuwa, Serikali imetoa na kusambaza majokofu zaidi ya 1300 yanayotumia umeme wa sola katika Halmashauri zote nchini, jambo lililosaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa majokofu hayo.

 “Nafurahi kwamba tumeweza kugawa majokofu Zaidi ya 1300 yanayotumia umeme wa sola, lakini uzuri wa majokofu hayo ambayo tumeyasambaza mwaka huu, yanatumia umeme wa sola, hivyo kupunguza gharama za uendeshaji majokofu ambayo kwa mwezi yaligharimu kiasi cha shilingi Elfu 50 kwaajili ya mtungi wa gesi” Alisema Waziri Ummy.

Mbali na hayo, Waziri Ummy ametoa wito kwa wazazi na walezi wote nchini kuhakikisha wanawapeleka Watoto katika vituo vya kutolea huduma za Afya kupata chanjo ili kuwakinga dhidi ya magonjwa ya surau na lubena.

“Tumeona mafanikio mazuri katika kuwekeza kwenye chanjo, ikiwemo kupunguza vifo vya Watoto wenye umri chini ya miaka mitano, kwa mfano mwaka 2005 tulikuwa na vifo 112 katika kila vizazi hai 1000, laini sasahivi takwimu rasmi zinaonesha vifo 67” Alisema Waziri Ummy

Hata hivyo, Waziri Ummy amewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya wote nchini kuhakikisha wanawafikia Watoto wote nchini walio na umri wa chini ya miaka mitano, kuwapa huduma za chanjo ili kuwakinga dhidi ya magonjwa.

“Katika kila Watoto 100 ambao wanatakiwa kufikiwa kupatiwa chanjo, tumewafikia Watoto 98, kimataifa ni Zambia na Rwanda ndio waliotuzidi, lakini lengo letu ni kuwafikia hata hao Watoto wawili waliobaki” Alisema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy Amesisitiza Serikali itaendelea kuwekeza katika masuala ya chanjo kwani zipo shahidi ya kisayansi ambazo zinaeleza kwa kuwekeza kila dola moja huokoa kiasi cha dola 16.
“Kila mwaka serikali inatupa angalau sh. bilioni 30 kwa kuwekeza katika chanjo tumeweza kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano kutoka vifo 112 katika kila vizazi hai 1000 hadi kufikia vifo 67 kwa kila vizazi hai 1000 hivi sasa,” amesema.

Amesema Tanzania kupitia jitihada ilizofanya sasa hivi katika kila watoto 100 ambao wanatakiwa kupatiwa chanjo, watoto 98 wanafikiwa. “Ni watoto wawili ambao tunawakosa...Barani Afrika, Tanzania ni nchi ya tatu, tumezidiwa na Rwanda ambayo imewafikia zaidi ya asilimia 99 na Zambia tupo nao sawa kwa asilimia 98,” amesema.

Ameongeza “Lengo letu japo tupo namba tatu kwanini tunawakosa hawa wawili katika 100 ambao wanatakiwa kupata huduma za chanjo.

Kwa upande wake Meneja Mpango wa Taifa wa Chanjo, Dk. Dafrosa Lyimo amesema ni jukumu la Serikali kuhakikisha chanjo zipo na zinapatikana kwa wakati.

“Hadi sasa hatuna upungufu wa chanjo, hatua hii (kukabidhi magari) ni muhimu sana, katika utunzaji wa chanjo tunahakikisha kuna utunzaji kuanzia ngazi ya Taifa na tunahakikisha zinasafirishwa katika mnyororo baridi na zinatunzwa vizuri,” alisema.

Mwisho

HOSPITALI YA BUGANDO YAFUFUA VIWANDA VYA OKSIJENI NA MAJI TIBA

Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Ziwa, Bugando Prof. Abel Makubi akifafanua jambo kwa Maofisa Habari wa Wizara ya Afya na Taasisi zake (hawapo pichani) walipotembelea Hospitali hiyo.

Mfamasia Fransisco Chibunda akiweka majitiba kwenye chupa maalum tayari kwa matumizi.

Majitiba ambayo tayari yameshatengenezwa katika Kitengo cha Kuzalisha Majitiba katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa, Bugando tayari kwa matumizi.


Na.Catherine Sungura-Mwanza

Katika kutekeleza kauli mbiu ya Serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya viwanda,hospitali ya rufaa ya kanda Bugando (BMC) imefanikiwa kufufua viwanda viwili kwa ajili ya mahitaji ya hospitali za kanda ya ziwa

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu Prof. Abel Makubi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando(BMC) mwishoni mwa wiki jijini hapa.

Prof. Makubi alisema kuwa katika kutimiza hayo wamefanikiwa kufufua viwanda ambavyo vilikua vinaelekea kufa.

Alitaja viwanda hivyo ni pamoja na kiwanda cha kuzalisha oksijeni na kingine ni cha kuzalisha maji tiba ya wagonjwa katika chupa mchanganyiko.

"Mahitaji ya oksijeni kwa  hospitali yetu ni mitungi 4000 ila hivi sasa tunazalisha zaidi ya mitungi 2000 na lengo letu ni kuzalisha mitungi 5100.

Aidha, Prof. Makubi alisema kuwa wamepanga kuzalisha mitungi mingi zaidi ili kuweza kuhudumia  hospitali nyingine za kanda ya ziwa kwa bei nafuu na ya nusu bei.

Kwa upande wa kiwanda cha kuzalisha maji tiba ya wagonjwa mkurugenzi huyo alisema "tumefanikiwa kuzalisha maji tiba ya wagonjwa katika chupa mchanganyiko na za kutosha kwa wastani tunazalisha chupa 6000 kwa mwezi na hivyo kuokoa pesa ambazo zingetumika kununua nje".

Hata hivyo Prof. Makubi alisema wanahitaji kiasi cha shilingi bilioni tano ili waweze kuzalisha maji tiba hayo ya kutosheleza kanda yote ya ziwa  na hivyo kusaidia hospitali zingine kutonunua maji ya wagonjwa kutoka nchi za jirani.

Naye Mkuu wa kitengo cha kuzalisha maji tiba Mfamasia Fransisco Chibunda alisema  kwa sasa upatikanaji wa dawa hospitalini hapo ni asilimia 96 ukilinganisha na asilimia 60 ya nyuma.

"Katika kiwanda cha maji tiba tunazalisha aina 17 za dawa,kati ya hizo aina tisa hazipatikani kabisa kwenye soko letu".Alisema Chibunda

Chibunda alisema katika kuwahudumia wagonjwa kwa wakati wamepanua  vituo nane vya kutolea dawa kutoka vituo vinne na kituo kimoja kinahudumia kwa masaa 24.

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando inayo wafamasia wabobezi katika kuzalisha madawa ya aina mbalimbali.

TANZANIA NA CUBA KUENDELEZA USHIRIKIAKO KWENYE SEKTA YA AFYA

Picha ya Pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile pamoja na mgeni wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa Cuba Mhe. Marcelino Medina Gonzalez

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa Cuba Mhe. Marcelino Medina Gonzalez (hayupo pichani) katika kikao kujadili mahusiano baina ya nchi mbili kwenye Sekya ya Afya.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa Cuba Mhe. Marcelino Medina Gonzalez akifafanua jambo kwenye kikao kujadili mahusiano baina ya nchi mbili kwenye Sekya ya Afya.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akiagana na mbeni wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa Cuba Mhe. Marcelino Medina Gonzalez (kushoto) mara baada ya kumaliza kikao kujadili mahusiano baina ya nchi mbili kwenye Sekya ya Afya.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt. Faustine Ndugulile leo amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba Mhe. Marcelino Medina Gonzalez Jijini Dodoma.

Katika mazungumzo yao, Dkt. Ndugulile ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Cuba kwa kuendelea kusaidia Sekta ya Afya nchini kwa kutoa madaktari bigwa kufanya kazi kwenye hospitali hapa nchini Tanzania.

Dkt. Ndugulile ametaka mahusiano hayo chanya yaendelee kuimarika ili Watanzania wengi wanufaike kwa kuweza kupata huduma bora za matibabu ya kibingwa. 

“Nchi ya Cuba imepiga hatua kubwa kwenye Sekta ya Afya na wana madaktari bingwa wengi ambao tunaweza kuwatumia kuja hapa nchini kuhudumia Watanzania wengi zaidi ndani ya muda mfupi kuliko kupeleka wagonjwa nje” amesema Dkt.Ndugulile na kuendelea kusema kuwa pindi Madaktari hao wa kigeni wanapokuja hapa nchini, madaktari wa Kitanzania wanapata fursa ya kujifunza kwa vitendo na kutibu hapa hapa nchini kwa kutumia miundombinu iliyokuwepo hivyo kupunguza gharama kwa Serikali kusafirisha wagonjwa kwenda nje ya nchi.

Kwa upande wake Mhe. Marcelino Gonzalez ameipongeza Tanzania kwa juhudi kubwa inazozifanya kuwekeza kwenye Sekta ya Afya na kuhakikisha Madaktari wanapata utaalamu wa kutosha ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

Amesema kuwa nchi ya Cuba iko tayari kutoa nafasi za masomo kusomea fani ya udaktari ili kuja kutibu Watanzania.

Nchi ya Cuba imekuwa na mahusiano ya karibu na Tanzania  kwa  kipindi kirefu. Mnamo Mwaka 1964 ubalozi wa Cuba ulifunguliwa rasmi nchini Tanzania na miaka 10 baadaye  mwaka 1974 Rais Fidel Castrol, alifika Tanzania kumtembelea Mwl.Julius Nyerere.Nchi ya Cuba na Tanzania Imekuwa na Mahusiano kwenye mambo mengi ikiwemo ushirikiano katika kutoa huduma za Afya.

BUGANDO YAOKOA BILIONI 2 KWA MATIBABU YA SARATANI

Mtaalam wa mionzi Alex Mpugi akitoa maelezo jinsi mashine ya mionzi inavyofanya kazi

Mashine ya kisasa ya kutambua(kupanga) sehemu inayotakiwa kupatiwa mionzi iliyoko kwenye hospitali  ya kanda ya rufaa Bugando
Mfizikia Tiba wa Idara ya Mionzi katika hospitali ya Bugando Prof. Pradumna Chaurassia  akiwaelekeza maofisa habari jinsi wanavyozuia eneo jingine ambalo halijaathirika na saratani isipate mioni piasaratani isienee mahali pengine

Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando (BMC) imefanikiwa kuokoa zaidi ya Shilingi bilioni mbili kwa wananchi wa kanda ya ziwa kusafiri kwenda jijini Dar es Salaam kupata matibabu ya saratani kila mwaka.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi  Mkuu wa Hospitali hiyo Prof. Abel Makubi wakati akiongea na Maofisa habari wa Wizara  ya Afya na Taasisi zake waliokuwepo jijini Mwanza kwa ajili ya kujionea mafanikio ya utoaji huduma za afya kwa wananchi.

Prof. Makubi alisema kuwa kuanza kwa tiba ya saratani katika Hospitali ya Kanda Bugando imesaidia kuokoa kiwango cha fedha hizo kutoka kwa wananchi wa kanda ya ziwa ambapo awali iliwalazimu kusafiri  hadi Jijini Dar es Salaam kupata huduma hizo kwenye Hospitali ya Saratani ya Ocean Road.

“Tunaishukuru Wizara ya Afya  ambayo ilitupatia kiasi cha Shilingi bilioni 5.5 kwa ajili ya kujenga jengo  la saratani. Kama hospitali  tumeweza kununua  mashine nne za mionzi na dawa kwa kushirikiana na wafadhili wengine".

Aidha, alisema, hivi sasa asilimia 90 ya wagonjwa hawapelekwi wanapata huduma hapa hivyo kuwaondolea adha ya kusafiri na kupata huduma mbali wananchi wa kanda ya ziwa ambapo awali zaidi ya asilimia 50 ya wagonjwa wa saratani wa Ocean Road walikuwa wakitoka kanda hiyo.

Naye Mtaalam wa Tiba Mionzi wa Idara ya Saratani wa BMC, Alex Mpugi alisema kabla ya mashine hizo walikua wakitoa huduma za saratani kwa kutumia kemikali.

"Naomba nitoe wito kwa wananchi hususan wanawake  kujitokeza kufanya uchunguzi wa saratani ya shingo ya uzazi na matiti kila siku ya Jumanne na Alhamis".Alisisitiza Mpungi.

Kwa upande wa Upasuaji  Mkurugenzi wa Upasuaji Dkt.Fabian Massaga  alisema kuwa,Hospitali  imefanikiwa kufanya ukarabati na upanuzi wa vyumba vya upasuaji kutoka vyumba sita hadi kumi na tatu ambapo vyumba viwili hutumika kwa upasuaji wa dharura na kimoja kwa ajili ya upasuaji  kwa akina mama wajawazito.

Aliongeza kuwa kwa upande wa upasuaji  wameweza kuongeza idadi ya wagonjwa kutoka ishirini na tano hadi hamsini na hivyo kupunguza idadi ya wagonjwa wengi waliokuwa wanasubiri upasuaji kwa miezi mitatu lakini hivi sasa wanafanyiwa upasuaji ndani ya wiki moja.

Hata hivyo Dkt. Massaga alisema upanuzi huo umeendana na ununuzi wa vifaa vipya na vya kisasa  ikiwemo vitanda vya kufanyia upasuaji, taa maalumu za vyumba vya upasuaji na mashine za kisasa kabisa za kutolea dawa ya usingizi. Vifaa hivi vimeagizwa moja kwa moja viwandani kwa takribani Shilingi bilioni 1.4 badala ya Shilingi bilioni 3 kama wangenunua kwa wauzaji hapa nchini.

-Mwisho-

Ijumaa, 6 Septemba 2019

BUGANDO YAKUSANYA ZAIDI YA BILIONI TATU KWA MWEZI

- Hakuna maoni


Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Prof. Abel Makubi akiongea na maofisa habari wa wizara ya afya na taasisi zake. 

Wafamasia kitengo cha kuchanganya dawa kwa ajili ya matumizi ya binadamu ikiwemo magonjwa ya moyo,ngozi kwa akina mama na watoto.

Jengo lenye huduma za  kibingwa ambalo linahudumia hadi wanachama 350 wa Mfuko wa Taifa wa  Bima ya Afya (NHIF) wanahudumiwa kwa siku. Limegharimu Shilingi Milioni 800 tulizowezeshwa na NHIF na  tangu 2017 wameshamaliza kurejesha malipo.


 Maabara ya Vinasaba iliyopo kwenye hospitali ya rufaa ya kanda ya Bugando
Picha ya pamoja ya Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Prof. Abel Makubi akiwa na Maofisa Habari na Mahusiano kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake ambao wapo mkoani Mwanza kujionea hali ya maboresho ya hospitali hiyo.
Na.Catherine Sungura, Mwanza

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni tatu kwa mwezi  baada ya kuimarisha mfumo wa makusanyo wa kieletroniki katika utoaji huduma.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo Prof. Abel Makubi wakati akielezea mafanikio ya hospitali hiyo kwa  maofisa habari wa Wizara ya Afya na Taasisi zake waliotembelea hospitali hiyo kujionea maboresho ya sekta ya afya katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Prof.Makubi alisema kuwa baada ya kuimarisha mfumo huo hospitali hiyo imeweza kukusanya kiasi hicho cha fedha tofauti na awali ambapo walikua wakikusanya shilingi milioni mia nane kwa mwezi.

“Licha ya makusanyo haya mfumo huu pia umesaidia kurahisisha utoaji wa huduma kwa wepesi na kwa haraka kwani zamani  kulikuwa na upotevu wa mafaili na hivyo kuleta malalamiko kwa wagonjwa”. Alisema Prof.Makubi.

Kwa upande kwa huduma za kibingwa na bobezi mkurugenzi huyo alisema kuwa baada ya Serikali kushusha huduma za kibingwa kwenye hospitali za rufaa za kanda hospitali hiyo imefanikiwa kununua mashine kadhaa za uchunguzi wa magonjwa ikiwemo CT- SCAN ya kisasa,  kwa mapato ya ndani yenye thamani ya shilingi bilioni 1.7 na hivyo kuweza kuwaondolea adha  wakazi wa mwanza na majirani zake.

“Pia tumeboresha huduma za maabara kwa kununua vifaa vya kisasa zaidi ya nane kwa ajili ya kupima magonjwa mbalimbali kwa muda wa masaa matatu kutoka masaa 12 yaliyokuwa yakitumika kutokana na vifaa vya zamani na hivyo imeleta faraja kwa wagonjwa kuongezeka kupata huduma hospitalini hapa tofauti na nyuma ambapo vipimo vingi walikua wanavipata nje ya hospitali yetu”. Alisema Mkurugenzi huyo.

Hata hivyo Prof. Makubi alisema  katika kuboresha miundombinu  wameweza kujenga jengo zuri lenye huduma zote za madaktari bingwa ambapo wanapokea wagonjwa 350 kwa siku wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Taifa (NHIF) ambalo limegharimu shilingi milioni 800 walizowezeshwa  na NHIF  na tangu mwaka 2017 wamefanikiwa kumaliza kulipa mkopo huo.

Prof.Makubi ameipongeza Wizara ya Afya pamoja na NHIF kuhamasisha wananchi kukata bima ya afya na hivyo kuongeza watumiaji wa bima hiyo kwa asilimia 70 tofauti na awali ambapo walikuwa wakipata wanachama hao kwa asilimia 30 hadi 40. 

-Mwisho-

Jumatatu, 2 Septemba 2019

HABARI PICHA: WATAALAM WA MAWASILIANO WAJIDHATITI KUTANGAZA MAFANIKIO YA SEKTA YA AFYA NCHINI.

Na Englibert Kayombo, WAMJW - Mwanza

Habari Picha
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu AFYA) Bw. Gerard Chami akisema jambo kwa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake katika Kikao kazi Jijini Mwanza kupanga mkakati wa mawalisiano wa mafanikio ya Sekta ya Afya.

"Ni lazima tufanye kazi kwa umoja na ushirikiano kuhakikisha kwamba tunatangaza vyema mafanikio ya Sekta ya Afya nchini" Bi. Anjela Mziray Meneja Mawasiliano Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)

"Mikakati yote ya kuboresha Sekta ya Afya imewekwa kwenye Ilani ya Chama Tawala (Chama Cha Mapinduzi CCM), ni vyema kuielewa vizuri ili kujua dira ya Serikali ya Awamu ya Tano kwenye Sekta ya Afya nchini" Bw. Aminiel Aligaesha Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Afisa Mawasiliano kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) Bw. Hamza Mwangomale akiteta jambo na Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Tawi la Mloganzila Bi. Neema Mwangomo (kushoto) kwenye kikao kazi cha  Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake Jijini Mwanza.

Afisa Habari na Uhusiano kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa Bw. Karimu Meshack (wa katikati) akisema jambo wakati wa kikao kazi cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake Jijini Mwanza.

Afisa Uhusiano kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bi. Grace Michael akirejea kusoma Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kufahamu zaidi malengo ya Chama Tawala kwenye Sekta ya Afya nchini.
_________________________________________________________________________________

Picha Mbalimbali za Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake wakiwa kwenye kikao kazi Jijini Mwanza wakijadili mpango kazi wa utekelezaji wa mkakati wa mawasiliano ya Sekta ya Afya katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.












CHMTs KAGERA WAFUNDWA KUJIKINGA DHIDI YA UGONJWA WA EBOLA

Afisa kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Alex Sanga akieleza namna ya uvuaji wa maski baada ya kumuudumia mgonjwa wa Ebola endapo atatokea, mbele ya Wataalamu wa Sekta ya Afya, wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa kwa kufuata mmiongozo ya (IPC guideline).

Afisa kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Alex Sanga akionesha vazi la kujikinga wakati wa kumuudumia mgonjwa wa Ebola endapo atatokea, mbele ya Wataalamu wa Sekta ya Afya, kutoka Halmashauri za Mkoa wa Kagera.

Baadhi ya Wataalamu wa Sekta ya Afya kutoka Halmashauri mbali mbali za Mkoa wa Kagera wakijipima uelewa kupitia maswali yaliyotolewa na Wizara ya Afya, katika mafunzo ya namna ya kujikinga dhidi ya mmagonjwa ikiwemo ugonjwa wa Ebola endapo utaingia nchini.

Mtaalamu wa Maabara Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikikishi MUHAS Bw. Akili Mawazo Mwakabhana akiendelea na kutoa mafunzo  kwa Wataalamu wa Sekta ya kutoka Halmashauri  za Mkoa wa Kagera wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi kwa kufuata miongozo ya utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).

Picha ya Pamoja ikiongozwa na Wataalamu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto sambamba na Wataalamu wa Sekta ya Afya kutoka Halmashauri za Mkoa wa Kagera baada ya kumaliza mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa Magonjwa ikiwemo ugonjwa wa Ebola kwa kufuata muongozo wa utoaji huduma kwa Wagonjwa (IPC guideline).


CHMTs KAGERA WAFUNDWA KUJIKINGA DHIDI YA UGONJWA WA EBOLA

Na Rayson Mwaisemba WAMJW- KAGERA

Timu za uendeshaji huduma za Afya za Halmashauri (CHMTs) za Mkoa wa Kagera zimeelekezwa jinsi ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Ebola, ikiwa ni moja kati ya mikakati ya Serikali kuwakinga Watumishi wa Sekta ya Afya endapo ugonjwa huo utaingia nchini.

Hayo yamejiri wakati wa  mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kuzingatia hadhari zinazokubalika  za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC Standard precausion) inayoendelea Mkoani Kagera ikiwa ni moja kati ya mikoa iliyo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola.

Katika Mafunzo hayo, Afisa kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Wizara ya Afya Dkt. Alex Sanga amesema kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo zipo katika hatari ya kupata wagonjwa wa Ebola kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu na ukaribu na Nchi ya Uganda na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo ambazo tayari zimekwishapata janga hilo.

Dkt. Sanga amesema kuwa, taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinasema kuwa takribani zaidi ya Wagonjwa 2950 wamethibitika kuwa na Ugonjwa wa Ebola, huku zaidi ya Wagonjwa 2000 wakipoteza maisha tokea mlipuko huo ulipojitokeza Agosti 2018, huku Wataalamu wa Afya 131 walipata maambukizi, ambapo 41 kati yao wamepoteza maisha.

Aidha,  Dr. Sanga amesema kuwa Serikali ya Tanzania imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha utayari wa kukabiliana na tishio la Ugonjwa huo ili kuhakikisha hauingii nchini, ikiwemo kuelimisha jamii njia za kujikinga na Ugonjwa ili kuzuia usiingie nchini, na kutoa Elimu kwa Watoa huduma za Afya juu ya kumuhudumia mtu mwenye dalili za Ebola endapo atatokea.

"Watoa huduma wanatakiwa kuzingatia hadhari zinazokubalika  za kujikinga na kudhibiti maambukizi (IPC Standard precautions) kwa kadri Miongozo inavyoelekeza wakati wote watoapo huduma kwa Wagonjwa, jambo litalosaidia kuwaepusha kupata maambukizi, au kumsaidia mgonjwa kupata maambukizi mapya wakati wa matibabu” Alisema Dkt. Alex Sanga

Hata hivyo, Dkt.  Sanga amesema kuwa, Shirika la Afya Duniani (WHO) inakusudia kuzuia Ugonjwa wa Ebola kwa kuimarisha huduma za uchunguzi na kusaidia nchi zilizo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola.

Kwa upande wake Mtaalamu wa Maabara kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi MUHAS Bw. Akili Mawazo Mwakabhana amesisitiza umuhimu wa kufuata taratibu na miongozo wakati wa kutoa huduma kwa mgonjwa kuzuia maambukizi mapya kwa Mgonjwa au Mtoa huduma za Afya jambo ambalo litasaidia kupunguza idadi ya Wagonjwa na kuokoa fedha ambazo zingetumika katika matibabu.

Aliendelea kusisitiza kwa kutoa wito kwa watoa huduma za Afya kuacha kufanya kazi kwa mazoea hali itakayosaidia kuondoa tatizo la usugu wa magonjwa (Wadudu) kutokana na matumizi mara kwa mara ya dawa, ambayo daktari angeweza kuyazuia kwa kufuata miongozo wakati wakutibu ugonjwa.

MWISHO