Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 12 Februari 2020

ONGEZENI KASI YA KUWAHUDUMIA WANANCHI:DKT. CHAULA

 Dkt. Zainab Chaula akiangalia vifaa vilivyowekwa kwenye wodi hiyo maalum ya kuwahudumia wagonjwa wa milipuko endapo watatokea.

Mganga mfawidhi wa zahanati ya Bangwe akimuelezea Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula jinsi walivyojipanga kutoa huduma endapo atatokea muhisiwa wa magonjwa ya mlipuko kwenye jengo maalum lililotengwa na manispaa ya kigoma,




Jengo la wazazi ambalo limejengwa kutokana na fedha za malipo kwa ufanisi(RBF) ambapo imesaidia kuongezeka kwa akina mama kujifungulia kwenye zahanati kutoka akina wajawazito 10  kwa mwezi mwaka 2018 hadi akina wajawazito 30 kwa mwezi mwaka 2019



ONGEZENI KASI YA KUWAHUDUMIA WANANCHI:DKT. CHAULA

Na. Catherine Sungura-Kigoma

Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini

Rai hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto-Idara kuu Aftlya Dkt. Zainab Chaula wakati akiongea na watumishi wa zahanati ya Kigoma jijini hapa.

"Tunaboresha huduma za afya kote nchini ili watu wasisafiri umbali mrefu kwenda kutafuta huduma za afya,zahanati ni ngazi ya awali ya afya ya msingi hivyo inasaidia wagonjwa wasio na shida kubwa kupata huduma karibu na maeneo yao".Amesema Dkt. Chaula

Aidha, ameongeza kuwa kabla ya kuboresha huduma za afya nchini asilimia 80 ya akina mama walikuwa wakijifungulia majumbani,hivyo kwa hali.ya sasa akina mama  wanafika vituoni kwa sababu ya kufuata huduma zilizoboreshwa.

Hali kadharika Dkt. Chaula aliupongeza Mpango wa Malipo kwa Ufanisi(RBF) kwa kuwajengea wodi ya wazazi kwenye zahanati na kuwapatia motisha watumishi

"Kigoma imeingia katika mpango huu mwaka 2017 na hivyo niwapongeze kwa kuweza kuboresha huduma pamoja na kufanya makubwa ,kwa maboresho haya lazima wananchi wapate  huduma bila manyanyaso yeyote".Alisisitiza

Naye Mganga mfawidhi wa zahanati hiyo Godlove Myinga amesema kuwa kwa kipindi cha mwezi julai hadi septemba 2018 zahanati hiyo ilipokea kiasi cha shilingi milioni  7,924,214  ambazo asilimia 25 zitatumika kama motisha kwa watumishi na asilimia 75 itatumika kwa ajili ya ukarabati na vifaa tiba.

Kwa upande wa akina mama wanaojifungulia kwenye zahanati hiyo Mganga mfawidhi huyo amesema kumekuwa na ongezeko tangu wodi ya wazazi ilipozinduliwa  mwaka 2018 kutoka akina mama 10 kwa mwezi  hadi kufikia akina mama 30 mwaka 2019.

Mpango wa Malipo kwa Ufanisi (RBF) ni mfumo wa malipo ya fedha kwa vituo vya afya mara baada ya kufanyika uhakiki wa majukumu na viashiria vilivyowekwa na hivyo malipo hutokana na kiwango cha utendaji ,RBF ilianza kutekelezwa hapa nchini mwaka 2015 na kutarajia kuisha mwaka huu. 

Fedha za Mpango huu zimesaidia kuinua kiwango cha utoaji huduma katika vituo vya afya ambapo utumika katika kufanya ukarabati mdogomdogo wa vituo, ununuzi wa vifaa tiba, dawa na mahitaji mengine ya kituo. 

MWISHO

WANANCHI KIJIJI CHA KALENGE WAISHUKURU SERIKALI KUWAJENGEA ZAHANATI

Katibu Mkuu Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akiwa na Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe, wakati wa ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma katika  Mkoa wa Kigoma.

Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Kalenge wilayani Uvinza wakifurahia ujio wa Katibu Mkuu Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula, kwa kuwajengea Zahanati na hivyo kuwahepusha na vifo vitokanavyo na uzazi.




Zahanati iliyojengwa katika Kijiji cha Kalenga Wilaya ya Uvinza ikiwa tayari kuanza kutoa huduma



WANANCHI KIJIJI CHA KALENGE WAISHUKURU SERIKALI KUWAJENGEA ZAHANATI

Na.Catherine Sungura-Uvinza

Wananchi wa kijiji cha Kalenge wilayani hapa wameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuwajengea zahanati na hivyo kuwahepusha na vifo vitokanavyo na uzazi.

Hayo yamebainishwa jana  na wakazi wa kijiji hicho wakati walipotembelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto-Idara Kuu Afya  Dkt. Zainab Chaula ambaye ameanza ziara ya usimamizi shirikishi mkoani kigoma ambayo inafanywa na wizara ya afya pamoja na TAMISEMI.

Akiongea kwa furaha bi. Marystela Chishako alisema kuwa wanaishukuru serikali ya awamu ya tano kwani kwa kupata zahanati hiyo imewasaidia kupata huduma za afya ikiwemo huduma ya kujifungua ambayo awali walikua wakiifuata kigoma mjini.

"Tunashukuru kwa serikali hii kutukumbuka mkoa wa kigoma,siku za nyuma mama akitaka kujifungua ilibidi aende kigoma mjini,ila hivi sasa tunajifungulia hapa hapa kwenye zahanati na tunapata huduma muhimu hapa hapa".

Aidha, alisema zahanati hiyo imewasaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto kwani kipindi cha nyuma walikua wakipata matatizo njiani kwa sababu walikua wakisafiri umbali mrefu na kupelekea kupata matatizo wakiwa njiani.

Katika Ziara hiyo Katibu Mkuu Dkt.Chaula aliwahidi kulifanyia kazi ombi lao la kupatiwa kituo cha afya kwani wameshaomba kwa kufuata utaratibu kupitia mkoa.

"Ninawapongeza kwa sababu mmejua umuhimu wa kuwa na kituo cha afya,kwahiyo maombi yataletwa wizara ya afya kutoka TAMISEMI,na katika ziara yangu nimeongozana nao hapa na nimepokea ombi hili najua ukitoa ahadi lazima utimize".Alisema Dkt. Chaula

Hata hivyo Katibu Mkuu huyo amesema atahakikisha wanapata fedha ili kutimiza ndoto za wananchi hao"mmefanya wajibu wenu na uzalendo mkubwa wa kuipenda nchi yenu kwa kujituma mpaka mmetenga eneo na kuweka mawe na mchanga, hivyo serikali itaongezea nguvu pale mlipoanzisha.

Wakazi wa kijiji hicho wametenga eneo la hekari ishiriki,kukusanya mawe pamoja na mchanga kwa kujitolea ili kuweza kujenga kituo cha afya ikiwa ni juhudi za kuiunga mkono serikali kwa kutatua changamoto za huduma za afya karibu na wananchi.

MWISHO

Jumatano, 5 Februari 2020

MAAMBUKIZI MAPYA YA MALARIA YAMEPUNGUA KWA ASILIMIA 27

 Katibu wa Chama cha TAPAMA Mhe. Raphael Chegeni akionesha kadi ya tathmini ya Malaria, wakati wa kikao cha uraghabishaji kwa Wakurugenzi na Wakuu wa vitengo wa Wizara ya Afya.

Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi akisikiliza maoni ya washiriki, wakati kikao na umoja wa wabunge wa kupambana na malaria na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Tanzania(TAPAMA) na Alma (African Leaders Malaria Alliance).

Mwakilishi wa Alma Tanzania Bw. Diego akiwasilisha mada kuhusu namna namna ya kuingia kwenye mfumo wa simu/kompyuta ya kadi ya tathmini ya Malaria ili kujionea utendaji wa Mkoa au hatua zinazochukuliwa kutatua matatizo ya eneo husika.

Picha ya pamoja kati ya Watumishi wa Wizara ya Afya na wabunge wa kupambana na Malaria na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Tanzania(TAPAMA) na viongozi wa Alma (African Leaders Malaria Alliance) waliofika Wizara ya Afya kufanya uraghibishaji wa  kadi ya tathimini ya malaria  kwa ajili ya uwajibikaji na utendaji kwa viongozi wa wizara jijini hapa.


MAAMBUKIZI MAPYA YA MALARIA YAMEPUNGUA KWA ASILIMIA 27

Na WAMJW - Dodoma.

Maambukizi mapya ya ugonjwa wa malaria yamepungua nchini   kwa asilimia 27 na hiyo ni kutokana na kuboreka kwa utoaji huduma za mapambano ya ugonjwa huo ukilinganisha na waginjwa 164 kati ya watu 1000 mwaka 2015 hadi wagonjwa 119 kati ya watu 1000 mwaka 2018.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Kinga Dkt. Leonard Subi wakati akitoa taarifa kwa umoja wa wabunge wa kupambana na malaria na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Tanzania(TAPAMA) na Alma (African Leaders Malaria Alliance) waliofika wizara ya afya kufanya uraghibishaji wa  kadi ya tathimini ya malaria  kwa ajili ya uwajibikaji na utendaji kwa viongozi wa wizara jijini hapa.

Dkt. Subi amesema kuwa mafanikio hayo yametokana na jitahada za viongozi wa Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na muhimili wa Bunge katika ushirikiano mzuri na wadau pamoja ma wananchi katika kupambana na ugonjwa huo.

Amesema kuwa viongozi wa nchi za afrika wanawajibika kwa afya za wananchi na hivyo kwa Tanzania vifo vitokanavyo na Malaria vimepungua  kwa asilimia 63 kutoka vifo 6,737 mwaka 2015  hadi 2,540 mwaka 2018.

“Ingawa hivi sasa tupo kwenye kudhibiti ila  tunalengo la kutokomeza,hivyo tuna imani kwamba tanzania tunao uwezo mkubwa wa kufikia huko kwani kuaniza Mh. Rais Wetu hadi muhimbili kama Bunge nao wako mstari wa mbele kuondosha malaria nchini”.

Aidha, amesema kuwa hivi sasa kumekuwa na mabadiliko makubwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini kwa kupungua kwa wagonjwa wanaougua malaria kupungua pia hata kwa watoto chini ya miaka mitano vifo vimepungua.

“Tanzania tumeamua kupambana na wadudu dhurifu kuanzia ngazi ya viluilui hadi mbu wapevu waenezao maradhi, hivyo kila mwananchi anawajibu wa  kuchukua hatua, hivyo ni vyema tukaungana ili kuiondosha Malaria nchini”.Amesema Dkt. Subi

Naye Katibu wa TAPAMA Mhe. Raphael Chegeni amesema kuwa msingi wa taifa ni kuwa na afya ,hivyo wanafarijika na afua zinazochukuliwa na wizara ya afya katika kupambana na malaria nchini “Malaria inaua hivyo tunajivunia kuona tanzania inazidi kupambana kutokomeza ugonjwa huu.

Kadi ya tathimini ya malaria ni kitendea kazi cha usimamizi kilichotolewa na wizara ya afya kinachoonyesha takwimu za utendaji wa viashiria vya malaria vilivyopewa kipaumbele katika ngazi ya mikoa na wilaya  ambayo inaleta urahisi katika kutambua wapi kuna tatizo ili hatua za kuokoa maisha ziweze kuchukuliwa.

Mwisho

Jumatatu, 3 Februari 2020

SERIKALI YAZINDUA MWONGOZO WA MATIBABU YA SARATANI NCHIN

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisema jambo kwa wadau wa Sekta ya Afya (hawapo pichani) katika siku ya Saratani Duniani iliyofanyika katiaka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizindua mwongozo wa matibabu ya saratani, kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya Dkt. Grace Maghembe, aliye kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisoma mwongozo wa matibabu ya saratani nchini aliozindua katika siku ya Saratani Duniani katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya Dkt. Grace Maghembe.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimtunuku cheti mdau wa Sekta ya afta katika magonjwa ya Saratani mapema leo kwenye kuadhimisha siku ya Saratani duniani yaliyofanyika katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.
Na Mwandishi Wetu - Dar Es Salaam

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imezindua mwongozo wa kitaifa wa tiba ya magonjwa ya saratani utakaoziwezesha hospitali za serikali na binafsi katika kutoa matibabu kwa usawa na kurahisisha mawasiliano kati ya madaktari bingwa na wataalamu wengine.

Kuzinduliwa kwa mwongozo huo kumefuatia baada ya hospitali za kanda kuanza kutoa tiba za saratani, kuongezeka kwa hospitali binafsi na za umma zinazotibu ugonjwa huo kwa sasa nchini, huku kwa kipindi kirefu hospitali nyingi zikitumia miongozo tofauti na ile ya nje ya nchi.

Akizindua mwongozo huo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema huduma za saratani zinasambaa katika hospitali mbalimbali nchini kwa sasa hivyo utoaji wa huduma lazima uangaliwe ili zitoke kwa kiwango kinachopaswa.

Amesema kuwepo kwa miongozo tofauti ilisababisha kutokuwepo kwa usawa katika tiba za wagonjwa lakini pia kulikuwa na changamoto ya mgonjwa kuendelea na tiba sahihi pindi akipewa rufaa kwenda hospitali nyingine.

“Kuwepo kwa mwongozo huu kutawezesha kurahisisha mawasiliano kati ya madaktari bingwa na wataalamu wengine wa matibabu ya saratani kote nchini,

“Kurahisisha uandaaji wa maoteo na ununuzi wa dawa na vitendanishi vinavyotumika katika matibabu ya saratani, mwongozo huu pia umetoa orodha ya dawa na vifaa tiba kwa ajili ya matibabu ya saratani ambayo itatumika kama mwongozo kwa ajili ya manunuzi na matumizi nchini,” amesema Ummy Mwalimu.

Amesema mwongozo huo pia itawezesha wananchi kupata huduma bora na za viwango vya juu katika vituo vyote vya matibabu kwa kuwa tiba zote zitapangwa kwa kufuata mwongozo huo.

Waziri Ummy amesema pia utawezesha kutoa mwongozo kwa mfuko wa taifa wa bima ya afya NHIF kuhusu dawa na vipimo mbalimbali stahiki kwa wagonjwa wa saratani.

“Mfuko wa Taifa NHIF uhakikishe unatumia mwongozo huu katika kuweka vitita vya huduma za saratani hapa nchini kwani katika ile standard treatment guideline kuna baadhi ya dawa za kutibu saratani hazikuorodheshwa, na niwaambie mmeweka masharti magumu sana katika vipimo hivi CT Scan na MRI nani anapima mara kwa mara tuondoe baadhi ya vikwazo na hili NHIF mkalitekeleze,” ameagiza.

Ameagiza mwongozo huo utumike na vituo vyote vinavyotoa tiba za saratani nchini;
“Ninafahamu hospitali zote zilishiriki kuuandaa hivyo sitegemei  kusikia kuna hospitali inafanya tiba nje ya mwongozo huu, ninaagiza pia wizara kufanya mapitio ili kuhakikisha dawa zote zinazotibu saratani zinakumuishwa katika mwongozo huu.”

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) Dk Julius Mwaiselage amesema, “Matumizi ya mwongozo huu yamefanyiwa majaribio kwa kipindi cha miezi sita katika taasisi hii kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha St Francisco.”

Ijumaa, 31 Januari 2020

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA UNAOSABABISHWA NA KIRUSI CHA CORONA (Novel Corona Virus 2019-nCoV) ULIOIKUMBA NCHI YA CHINA NA MATAIFA MENGINE DUNIANI.

- Hakuna maoni

                      Bofya hapa kupata kiunganishi cha Tamko kuhusu Virusi vya Corona

WAFAMASIA WATAKIWA KUFUATA MISINGI YA KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI

- Hakuna maoni
Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula akizungumza na Wahitimu wa kada ya Famasi (Hawapo pichani) wakati wa warsha fupi ya kutoa vyeti vya kuhitimu na usajili iliyofanyika katika ukumbi wa Takwimu jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Huduma za Afya kutoka TAMISEMI Dkt. Ntuli Kapologwe akiongea neno kwa wahitimu wa kada ya Famasi (Hawapo pichani) wakati wa warsha fupi ya kutoa vyeti vya kuhitimu na usajili iliyofanyika katika ukumbi wa Takwimu jijini Dodoma.

Mfamasia Mkuu Bw. Daud Mmasi  akizungumza na wahitimu wa kada ya Famasi (Hawapo pichani) wakati wa warsha fupi ya kutoa vyeti vya kuhitimu na usajili iliyofanyika katika ukumbi wa Takwimu jijini Dodoma.

Msajili wa Baraza la Famasi nchini Bi. Elizabeth Shekalaghe akiongoza kiapo cha Wafamasia waliohitimu kutoka vyuo mbalimbali nchini walipokutana katika warsha fupi ya kukabidhi vyeti vya taaluma na usajili iliyofanyika katika ukumbi wa Takwimu Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula akimkabidhi mmoja wa wahitimu wa kada ya Famasi cheti cha taaluma pamoja na usajili katika warsha iliyofanyika jijini Dodoma.


Picha mbalimbali zikionesha Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula (aliyekaa katikati) na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu na Sekretarieti ya Baraza la famasi katika warsha fupi ya kutoa vyeti vya taaluma na usajili kwa wahitimu hao. 


Na Emmanuel Malegi- Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula amewasihi wahitimu wa kada ya famasi kutoka vyuo mbalimbali nchini na nje ya nchi kuheshimu na kufuata misingi na miongozo ya taaluma hiyo ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi.

Dkt. Chaula amesema hayo mapema leo wakati alipohudhuria warsha fupi ya kuwatunuku vyeti vya kuhitimu na usajiri wahitimu zaidi ya 100 waliohitimu shahada ya Famasi katika vyuo mbalimbali nchini.

“Ninaomba mkawe wanyenyekevu mkiwa maeneo yenu ya kazi, kuzingatia kanuni na misingi ya taaluma ni jambo muhimu la kufuata kwa kila mmoja wetu, nidhamu mahala pa kazi huleta umakini katika kazi yako, jamii inawategemea ili muweze kutoa huduma nzuri kwa wananchi”. Amesema Dkt. Chaula.

Dkt. Chaula ameendelea kusisitiza kuwa taaluma hiyo ni muhimu sana nchini kwani wagonjwa wanategemea kupata dawa sahihi ambazo zitatolewa na wafamasia hao ili ziwasaidie kupona maradhi yanayowasumbua.

Aidha, Dkt. Chaula amewataka Wahitimu hao kushirikiana kwa karibu na madaktari pamoja na wahudumu wengine wa afya wakiwemo manesi ili waweze kusaidia katika kutoa huduma bora za afya na kusaidia wananchi kupata nafuu na kupona kabisa maradhi yanayowasumbua.

Kwa upande wake Msajili wa Baraza la Famasi nchini Bi. Elizabeth Shekalaghe amewataka wahitimu hao kwenda kuisaidia jamii na kuziba baadhi ya mapengo ya taaluma hiyo ambayo ina watumishi wachache na uhitaji ni kubwa nchini ambapo hivi sasa Tanzania ina wafamasia takribani 1200 waliosajiliwa na Baraza hilo nchi nzima.

 -MWISHO-


Jumatano, 29 Januari 2020

TANZANIA HAINA MGONJWA WA CORONA


Picha mbalimbali zikionesha Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliojitokeza kusikiliza tamko la Wizara kuhusiana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona uliotokea China na kutoa taarifa za Tanzania ilivyojiandaa katika kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo nchini. Kushoto ni Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndugulile na kulia ni Mkurugenzi wa huduma za Dharura na Majanga Dkt. Elias Kwesi.

Na. WAMJW-Dodoma
Mpaka sasa Tanzania haina Mgonjwa wala muhisiwa wa ugonjwa  unaosababishwa na kirusi cha Coromna (Hona kali ya mafua) hata hivyo  kutokana na mwingiliano mkubwa uliopo hasa kibiashara na kijamii kati ya Tanzania na nchi za bara la Asia ikiwemo nchi ya China nchi  inakuwa katika hatari pia ya ugonjwa huo.

Haya yamesemwa leo na Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akitoa tarifa kwa umma kuhusu mwenendo wa ugponjwa huo jijini hapa.

“Ugonjwa huu unasababiswa na kirusi jamii ya Corona na ni kipya “Novel (New) Corona virus 2019” (2019-nCOV) ambacho ni tofauti na virusi vingine vya jamii hiyo ambavyo viliwahi kusababisha milipuko ya ugonjwa uliojulikana kama ‘SARS-CoV’ mwaka 2003 na MERS-CoV Corona Virus mwaka 2013”.Amesema Waziri Ummy.
 
Aidha, waziri Ummy amesema ugonjwa huo huambukizwa kwa njia ya hewa kwa kuingiwa na majimaji yenye virusi kutoka mtu mmoja kwa njia ya kukohoa au kupiga chafya au kwa kugusa majimaji au makamasi kutoka kwa mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na dalili za ugonjwa huo na dalili huanza kuonekana kati ya siku moja hadi kumi na nne tangu kupata maambukizo.

Hata hivyo ametaja dalili za ugonjwa huu ni pamoja na Homa, mafua, kuumwa kichwa, mwili kuchoka, kikohozi, kubanwa mbavu, maumivu ya misuli, vidonda vya koo, mapafu kuathirika, kupumua kwa shida na hata kifo.
“Ugonjwa huu hauna chanjo wala tiba ya moja kwa moja, hivyo kama yalivyo magonjwa mengine yanayosababishwa na virusi, matibabu hufanyika kwa kuzingatia dalili zilizopo na ufuatiliaji wa karibu” Amesisitiza Waziri Ummy.

Wakati huo huo waziri huyo amewashauri wananchi kuchukua hatua ili kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo kuzingatia kanuni za afya na usafi ikiwa ni pamoja na kukaa mbali na mtu mwenye dalili za mafua mwenye historia ya kusafiri katika nchi zilizokumbwa na mlipuko na kufunika mdomo na pua wakati wa kukohoa kwa kitambaa safi au nguo uliyovaa sehemu za mikono

“Kutokana na mwenendo na kasi ya kusambaa kwa ugonjwa huo kipindi hiki cha mlipuko, Wizara inashauri kusubiri na kuepuka safari zisizo za lazima kwenda kwenye maeneo yaliyoathirika na inapolazimu kusafiri basi wapate maelezo ya kitaalamu kabla ya kuondoka nchini pamoja na kuepuka kugusana na mgonjwa mwenye dalili za magonjwa ya njia ya hewa”.

Vile vile wananchi wanatakiwa kutoa taarifa ya uwepo wa mtu mwenye dalili zinazohiswa kuwa za ugonjwa huu kwenye kituo cha huduma za afya kilicho karibu nawe au piga simu namba 0800110124 au 0800110125 bila malipo.
-Mwisho_

Jumapili, 26 Januari 2020

KINU CHA KUFUA OKSIJENI KCMC KUWA MSAADA KWA WENYE MATATIZO YA UZAZI

Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) Dkt. Sarah Urasa akizungumza katika Mkutano wa Maafisa Habari wa Wizara ya Afya na Taasisi zake katika kampeni ya "TumeboreshaAfya".

Bibi Catherine Mushi akiendesha  kinu cha kuzalisha hewa safi (Oxygen plant) katika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC.

 Mtaalam wa kutengeneza baskeli za magurudumu matatu(wheelchair) Bw. Samson Shirima akiwa katika kiwanda cha kuzalisha bidhaa hizo katika hospitali ya rufaa ya KCMC.

Madaktari pamoja na wauguzi wakiwahudumia watoto  njiti katika wodi maalum ya watoto hao   KCMC.

Mtaalam kutoka Idara ya ngozi Bw. Maghembe Juma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kilimanjaro KCMC akitengeneza dawa na mafuta maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi katika Hospitali hiyo.

Grace Manyika akiweka alama za ukomo wa matumizi ya mafuta maalum kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) katika kiwanda hicho  kilichopo hospitali ya KCMC, Kilimanjaro.

Mtambo wa kinu cha kisasa cha kuzalisha hewa safi (oxygen plant)wenye uwezo wa kuzalisha mitungi 400 kwa siku ambao upo katika hospitali ya Rufaa ya kanda ya kaskazini KCMC.

KCMC



KINU CHA KUFUA OKSIJENI KCMC KUWA MSAADA KWA WENYE MATATIZO YA UZAZI

Na Mwandishi wetu, KILIMANJARO.

IMEELEZWA kuwa uwepo wa kinu kipya na cha kisasa chenye uwezo wa kufua hewa ikiwemo hewa safi ya Oxygen na ile ya  Naitrojeni kitakuwa msaada kwa wenye tatizo la uzazi nchini.

Akizungumzia hospitalini hapo ikiwa ni utekelezaji wa kampeni ya Tumeboresha sekta ya Afya yenye lengo la kuonyesha mafanikio makubwa yaliyopatikana katika uwamu ya tano ndani ya Wizara ya afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Kaimu Mkurugenzi wa KCMC Dkt. Sarah Urasa alisema:

"Uhifadhi wa mbegu za kiume  na kike upo mbioni kuanza hapo baadae. Hatua hiyo kwani tayari tumeanzisha klininiki maalumu kwa ajili ya watu wenye matatizo ya uzazi ambayo tunaonana na wagonjwa kwa wiki mara moja  ambapo huwahudumia watu 10 mpaka 12." Alisema.

Mbali na kazi hiyo  kinu hicho kinauwezo wa kufua hewa ya Oksijeni ambayo kwa kiwango kikubwa hutumika kuwasaidia watu wenye matatizo ya kupumua ambapo kwa siku mitungi 400 hufuliwa katika kinu hicho.

Dkt. Sarah Urasa aliongeza kuwa: "Hii ni hospitali ya kwanza kuwa na kinu ya kufua hewa ya oksijeni na Nitrogen  hapa nchini.

Hewa ya Oksijeni pia inatumika kwa wale wagonjwa wanaopewa dawa za usingizi kwaajili ya upasuaji, hewa ya nitrogen inatumika kuhifadhi sampuli kutoka kwa wagonjwa,tiba kwa magonjwa ya ngozi vile vile hutumika kukata matokeo kwenye ngozi au kwenye viungo vya uzazi" alisema.
 
Huduma hiyo ambayo imeanza mwaka huu Dkt. Sarah alisema ununuzi wa mitungi ya gesi ya oksijeni pekee ulikuwa ukiwagharimu takribani milioni tatu kwa wiki huku gharama za usafirishaji ikiwa haijajumuishwa hatua ambayo imeokoa gaharama za uendeshaji hospitalini hapo.

Dkt.Sarah alieleza kuwa kwa kadiri uzalishaji unavyoongezeka katika kinu hicho wataanza kutumia mfumo wa kuunganisha gesi moja kwa moja hadi katika kitanda cha mgonjwa.

"Tumeona uharibifu mkubwa unaotokana namitungi hii ya gesi sakafu yetu imekuwa ikiharibika kutokana na uzito wa mitungi yenyewe kwahiyo mfumo tutakapkuja kuutumia utakuwa bora zaidi tofauti na sasa "alisema.

Mafanikio mengine aliyoyataja Dk.Sarah alisema katika utawala wa Rais Dk.John Magufuli wamefanikiwa kuanza kutengeneza maji tiba 'dripu' kwaajili ya kuwasaidia wagonjwa ndani na nje ya hospitali.

"Hii inetusaidia kwa kiwango kikubwa hata hospitali zingine zimekuwa zikifika hapa kwaajili ua kujifunza namna ya kutengeneza maji tiba "alisema.

Pia alisema KCMC ndio kituo pekee inayotambulika kimaitafa kutoa mafunzo ya magonjwa ya ngozi na zinaa kwa nchi zote za Afrika Mashariki.

"Kituo hiki ndio kinachozalisha mafuta ya ngozi kwaajili ya watu wenye ualbino na tayari tumeingia makubaliano na Bohari kuu ya Dawa MSD kwaajili ya kusambaza dawa na tayari tumefikia mikoa 25 kwa kutumia mfumo wetu wa usambazaji na sasa MSD watatuongezea nguvu ili kusambazwa nchi mzima "alisema

Kwa upabde wake,  Mhandisi KCMC Dustan Kanza alisema mgonjwa mmoja hutumia mtungi mmoja lengo kuepukana na maambukizi.

Alisema katika kinu hicho kwa saa 24 inauwezo wa kuzalisha mitungi 400 na mpaka sasa tayari zaidi ya mitungi 600 imezalishwa tangu kuanza kufanya kazi kwa kinu hicho januari mwaka huu.

Mwisho.




Ijumaa, 24 Januari 2020

HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA YATAKIWA KUJIUNGA NA TIBA MTANDAO

- Hakuna maoni

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akionyesha mashine ya kufanyia uchunguzi wa matiti ijulikanayo kwa jina la Mamograhy katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma. 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa kwenye  kwenye chumba cha kipimo cha CT-Scan kwenye hospitali hiyo



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa kwenye wodi ya wagonjwa  walioupandikiza


Na. Catherine Sungura-Dodoma

Hospitali ya Benjamin Mkapa imetakiwa kujiunga na tiba mtandao ili kuweza kutoa tiba kwa wagonjwa  kwa haraka na kwa ufanisi ili kuwapunguzia wagonjwa muda wa kusubiri majibu hususani ya mionzi .

Rai hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati alipoitembelea hospitali hiyo kujionea hali ya utoaji huduma.

“Nawaelekeza ni vyema mkajiunga na huduma ya tiba mtandao ili muweze kutoa huduma kwa haraka na kwa ufanisi zaidi, mnatakiwa mkajifunze huduma hii kutoka hospitali ya Muhimbili au MOI". Amesema waziri Ummy.

Aidha, Waziri huyo amesema kuwa hivi sasa kwenye hospitali nyingi kuna changamoto za wataalam wa kusoma picha kwani wataalam wengi waliopo ni wale wa kupiga ”bahati nzuri sisi tunao wataalam wengi wa kupiga picha mana kwenye mionzi kuna aina mbili za wataalam wapo wa kupiga picha (radiographer) na wa kusoma picha, hivyo serikali itahakikisha inapata wataalam wengi zaidi wa kusoma ili kukidhi mahitaji.

Waziri Ummy amesema wizara ina lengo la kuziunganisha hospitali za wilaya pamoja na vituo vya afya kwenye mfumo wa hospitali za rufaa za mikoa kwa kufunga senta zitakazosaidia hospitali za wilaya na vituo vya afya vinavyofanya vipimo vya ‘utra sound’ na ‘x-ray’ na majibu yakasomwa haraka na wataalam wa Hospitali za rufaa na kutoa majibu haraka bila kumsubirisha mgonjwa kwa muda mrefu.

Alitaja hospitali zilizojiunga na tiba mtandao  ni pamoja na hospitali za rufaa za mikoa ya Lindi na Morogoro , pia hospitali teule za wilaya  za Nyangao,Turiani na hospitali za wilaya  ya Nachingwea,kilosa na Mvomero.

Wakati huo huo Waziri Ummy ameitaka hospitali hiyo kupunguza gharama za kulipia uchunguzi wa saratani ya matiti kwa wanawake kutoka elfu sabini hadi elfu thelathini kama hospitali zingine za taifa zinavyofanya.

Hata hivyo waziri huyo ametoa wito kwa wananchi wa Dodoma na mikoa jirani  kutosafiri hadi dar es salaam kupata huduma za kibingwa kwani huduma zote karibu zinapatikana hapo na hivyo ameahidi wizara wataleta madaktari bingwa wa mishipa ya fahamu pamoja na mifupa.

_Mwisho-

NIMR YATENGA MILIONI 800 TIBA YA MITISHAMBA NCHINI

- Hakuna maoni
Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof. Yunus Mgaya akisisitiza jambo wakati wa kikao na Maafisa Habari wa Wizara ya Afya na Taasisi zake pamoja na Waandishi wa Habari kilichofanyika katika ofisi za Taasisi hiyo Muhimbili, Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kituo cha Muhimbili Prof. Mfinanga akieleza jambo wakati wa kikao na Maafisa Habari wa Wizara ya Afya na Taasisi zake pamoja na Waandishi wa Habari kilichofanyika katika ofisi za Taasisi hiyo Muhimbili, Jijini Dar es Salaam.

Msanifu wa Maabara ya NIMR-Muhimbili Said Omary akielezea namna vimelea  vya ugonjwa wa kifua kikuu vinavyokuzwa kwenye utafiti.

Kikao cha Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof. Yunus Mgaya na Maafisa Habari wa Wizara ya Afya na Taasisi zake pamoja na Waandishi wa Habari kilichofanyika katika ofisi za Taasisi hiyo Muhimbili, Jijini Dar es Salaam.

Maafisa Habari wa Wizara ya Afya na Taasisi zake pamoja na Waandishi wa Habari,





NIMR YATENGA MILIONI 800 TIBA YA MITISHAMBA NCHINI

Na WAMJW - DSM

TAASISI ya    Taifa    ya    Utafiti    wa     Magonjwa     ya    Binadamu    (NIMR) imesema ipo mbioni kusimika mitambo ya kisasa itakayosaidia kuzalisha dawa za mitishamba kutoka miti dawa ili kukabiliana na magonjwa mbalimbali nchini.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa NIMR, Profesa Yunus Mgaya wakati akizungumza katika  ziara ya 'Tumeboresha Sekta ya Afya' inayoendeshwa na Maafisa Habari waandamizi wa Wizara ya Afya na Taasisi zake.

Maofisa Habari hao wapo katika ziara ya Kampeni iitwayo Tumeboresha Sekta ya Afya ambayo inalenga kuonesha mafanikio yaliyopatikana katika sekta hiyo kipindi cha Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Joseph  Magufuli

Alisema Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Afya imetoa fedha shilingi Milioni 800 ambazo zitasaidia kununulia mitambo na kukarabati eneo itakaposimikwa mitambo hiyo.

"NIMR tupo mbioni kuleta mitambo kutoka China. mitambo ambayo itatoa uwezo wa kuzalisha dawa kutoka kwenye miti dawa kwa ajili ya kuongeza uwezo wa kukabiliana dhidi ya magonjwa mbalimbali ambayo yanawagusa wananchi."

"Watalaam wetu tayari wameshaenda China kujifunza na pia wametembelea kampuni za mitambo hiyo ya kisasa na tumejiridhisha.

Mtambo mmoja unagharimu kati ya shilingi za kitanzania Milioni 500 hadi milioni 600 hivyo milioni 800 zitatosha kabisa kukamilika zoezi zima" alisema.

Pia alisema kuwa, dawa hizo zitatokana na miti dawa mbalimbali ikiwemo na kwa Waganga hapa nchini.

"Sisi tutatengeneza dawa kutokana na asili ya miti dawa.Tunachokifanya ni kutafiti. Baada ya kwenda kwa Mganga ambaye atakumiminia kwenye kikombe, Sisi tutakachokuambia ni kuwa dawa hiyo inamchanganyiko wa kiambata fulani na utaitumia kwa kiwango fulani." Alisema.

Aidha, alisema katika tiba ya mitishamba Duniani inatumika kwa wingi katika nchi mbili pekee ikiwemo China na India.

"China na India kuna Hospitali kabisa zinatibu kwa kutumia dawa za mitishamba na Nchi ya Korea pia" Alisema Profesa Mgaya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa NIMR kituo cha Muhimbili, Profesa Sayoki Mfinanga  alieleza kuwa miongoni mwa mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya tano ni pamoja na kuongezeka kwa tafiti kutoka 10 hadi 20 kwa mwaka.

"NIMR-Muhimbili  tumefanikiwa kufanya tafiti mbalimbali kwenye magonjwa ya Kifua kikuu, Vimelea vya Ukimwi na Magonjwa yasiyoambukiza (Non Communicable Diseases).

"Uwezo wa kituo wa kufanya tafiti umeongezeka kutoka wastani wa tafiti kubwa 10 kwa mwaka kwenye miaka ya nyuma ya 2010 mpaka  wastani  wa tafiti kubwa 20 kwenye miaka ya kuanzia 2017." Alisema Profesa Mfinyanga.

Ambapo alibainisha kuwa, miongoni mwa tafiti hizo ni pamoja zile za huduma za kudhibiti Ukimwi na Kifua Kikuu.

"Tafiti hizi kupitia NIMR-Muhimbili zimechangia kuboresha au kutoa taarifa zilizoboresha huduma za kudhibiti UKIMWI na kifua kikuu.

"NIMR-Muhimbili imekamilisha utafiti uliotathimini mkakati tiba kwa kupunguza vifo kwa wagonjwa  wenye  maambukizi ya fangasi (Cryptococcus Neofroman)  na kusababisha homa ya Uti wa mgongo (Cryptococcal meningitis) kwa wagonjwa walioathirika na Ukimwi.
 Utafiti huu umehusisha wagonjwa 721 toka Tanzania,  Malawi, Zambia,  na Cameroon. "Alisema profesa Mfinanga.

Aidha, katika ziara hiyo pia wanahabari na maafisa hao wa Wizara ya Afya waliweza kitembelea Maabara kubwa ya NIMR -Muhimbili  na kujionea jinsi inavyofanya kazi huku wakishuhudia vifaa na mashine za kisasa kabisa zenye ubora na ufanisi wa hali ya juu.

NIMR    ilianzishwa    kwa    sheria    ya    Bunge    la    Jamhuri ya    Muungano    wa    Tanzania    Namba    23    ya    mwaka    1979. NIMR    ni    taasisi iliyo     chini    ya    Wizara    ya    Afya,    Maendeleo ya Jamii, Jinsia,    Wazee    na    Watoto huku kazi yake kubwa ni    pamoja     na    kufanya    utafiti,    inaratibu,    inakuza na kusimamia tafiti za afya zinazofanyika    nchini     na    kukuza    matumizi ya matokeo ya tafiti hizo.

Ambapo pia hadi sasa ina    idara    ya    tafiti     za    Tiba     Asili    ambayo    jukumu    lake    ni    kufanya    utafiti    juu    ya    dawa    za    miti-shamba, ambazo nyingine zimekuwa zinatumika    miaka    mingi na bibi na babu  zetu.

Mwisho