Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Alhamisi, 21 Mei 2020

WAHIMIZWA KUJIPANGA, KUENDELEA KUTOA HUDUMA ZA MKOBA ZA CHANJO

- Hakuna maoni
Bi. Ipyana Mwamwala Muuguzi Mkunga wa Kituo cha Afya Mtego wa Simba akimpima uzito mtoto Niran Daudi (7) pembeni ni mama wa mtoto huyo, Bi. Joyce Mwantobe. Picha na Englibert Kayombo

Bi. Elinivoniia Mchomvu Muunguzi Mkunga akisoma kitabu cha afya ya mtoto kabla ya kutoa chanjo katika Zahanati ya Fulwe, Wilaya ya Morogoro VIjijini. Picha na Englibert Kayombo


Ofisa Afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Lugata akitoa elimu kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Corona.kwa wananchi waliofika katika Kituo cha Afya Mtego wa Simba Wilaya ya Morogoro Vijijini kupata huduma za afya

Ofisa Miradi kutoka Mpango wa Taifa wa Chanjo, unaosimamiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Furaha Kyesi (kushoto) akimzungumza jambo na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mtego wa Simba, Luambano Ally

Wananchi wakiingia katika Kituo cha Afya Mtego wa Simba kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa kukabiliana na Ugonjwa wa Corona kwa kunawa mikono kwa maji yanayoririka na sabuni na kukaa umbali wa zaidi ya mita moja kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine


 Mwandishi Maalum - Morogoro
Huduma ya chanjo za mkoba hasa katika maeneo ya pembezoni (vijijini) zinapaswa kuendelea kutolewa kwa watoto chini ya miaka mitano ili kuhakikisha wote wanafikiwa kwa wakati unaopaswa, licha ya kuwapo kwa janga la Corona.

Pamoja na kundi hilo, kundi jingine linalopaswa kufikiwa na kupatiwa chanjo ya ni wasichana wenye umri wa miaka 14 ambao wanapaswa kupatiwa ile ya HPV inayokinga dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo vinavyosabisha ugonjwa wa saratani ya kizazi.

Rai hiyo imetolewa jana na Ofisa Miradi kutoka Mpango wa Taifa wa Chanjo wa Wizara hiyo, Dk. Furaha Kyesi alipozungumza na uongozi wa Kituo cha Afya Mtego wa Simba, kilichopo Wilaya ya Morogoro Vijijini, mkoani Morogoro wakati wa ziara ya ukaguzi wa huduma za chanjo zinazotolewa kwenye vituo vya afya kipindi hiki cha mapambano dhidi ya janga la Corona.

Timu ya ufuatiliaji huduma za chanjo kutoka Mpango wa Taifa wa Chanjo (IVD) wa Wizara hiyo, maofisa chanjo wa Mkoa wa Morogoro na wa Wilaya hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Engeder Health kupitia Merck Sharp & Dohme B.V (MSD), wapo mkoani humo kukagua namna huduma za chanjo zinavyoendelea kutolewa katika kipindi hiki cha janga la Corona.

“Kundi hili la wasichana lazima tuhakikishe tunalifikia, kwa sababu hawa awali msisitizo ulikuwa kuwapa chanjo kwa kuwafikia shuleni, lakini sasa shule zimefungwa kutokana na janga la Corona, lakini tunahitaji kuwafikia.

“Watoto chini ya miaka mitano nao lazima tuwafikie ili kwamba wakati tunapambana na Corona tuhakikishe pia tunaendelea kuwapa chanjo dhidi ya magonjwa mengine kama vile surua, polio, kuharisha na mengineyo, ili tusije tukapata mlipuko wa magonjwa,” amesema.

Kyesi ameshauri kwamba watoa huduma za afya waendelee kuzingatia mwongozo wa kujikinga na kufikia maeneo ya pembezoni hasa huko vijijini kuwapa huduma.

Awali akizungumza, Muuguzi Mkunga wa Kituo hicho, Ipyana Mwamwala alisema kila mwezi hupokea watoto wapatao saba na kuwapa chanjo mbalimbali kulingana na umri wao.

Amesema kituo hicho kimezungukwa na vijiji vinne ambavyo ni Sangasanga, New Land, Mkono wa Mara, Mkambarani na Mtego wa Simba (chenyewe).

“Wakina mama bado wana mwamko wa kuleta watoto kituoni lakini tunahitaji kwenda outreach kwa ajili ya kuwafikia pia wale ambao hawaji kituoni, vijiji vipo mbali na hapa,” amesema.

Ameongeza “Tupo tayari kwenda, tunatambua, tumetangaziwa kuna ugonjwa wa COVID -19 nchini ambao unatokana na maambukizi ya virusi vya Corona, hata hapa kituoni tumechukua hatua na hata tukienda kule tutazingatia kanuni zote za kujikinga sisi wenyewe na wale tunaokwenda kuwahudumia wasipate maambukizi.

Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho, Luambano Ally amesema kutokana na taarifa hiyo ya tahadhari iliyotolewa na Wizara ya Afya, walilazimika kuchukua hatua za kuimarisha kujikinga ikiwamo kuweka ndoo za maji katika maeneo ya kuingia ndani ya kituo hicho.

“Kwenye milango yote ya kuingia ndani ya kituo kuna ndoo ya maji safi tiririka na sabuni lazima mtu anawe ndipo aingie huku ndani, lakini kama amejisahau kunawa pale au anahitaji tena kunawa akiwa humu ndani, kuna ndoo nyingine tumeweka ataweza kunawa pia.

“Hapa kituoni tumewapa taarifa kwamba kila anayekuja kupata huduma lazima avae barakoa, utaona hilo wanakijiji wanalitii na wamekuwa na mwamko, wanakuja wakiwa wamevaa, wananawa mikono, wanapata huduma na kurudi zao nyumbani,” amesema Ally.

MWISHO

Jumatano, 20 Mei 2020

WAZIRI UMMY AMESEMA UGONJWA WA KIFUA KIKUU UNAENDELEA KUPUNGUA NCHINI

- Hakuna maoni




Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya Hadubini 7 za kuchunguza kifua kikuu zilizotolewa na Wizara kwa Wilaya ya Chamwino.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akiongea jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Bilinith Mahenge wakati wa hafla ya makabidhiano ya Hadubini 57 zilizotolewa na Wizara ya Afya katika Mkoa wa Dodoma. Hafla hiyo ilifanyika Wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akikabidhi moja ya Hadubini za kuchungua ugonjwa wa kifua kikuu kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Bilinith Mahenge, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Vumilia Nyamaga, Mbunge wa Chilonwa Mhe. Joel Mwaka huku Mkurugenzi wa huduma za kinga Dkt. Leonard Subi akishuhudia.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Bilinith Mahenge na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Vumilia Nyamaga wakibeba moja ya Hadubini zilizotolewa na Wizara ya Afya kwa Wilaya ya Chamwino.
Baadhi ya wananchi na wafanyakazi wa kituo cha afya cha Buigiri waliojitokeza kushuhudia makabidhiano ya Hadubini mpya za kupima kifua kikuu zilizotolewa na Wizara ya Afya.


Na WAJMW-Dodoma

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema maambukizi ya Kifua Kikuu (TB) yamepungua nchini kutoka wagonjwa  164,000 mwaka 2015 hadi kufikia wagonjwa 142,000 mwaka 2018.

Waziri Ummy amesema hayo leo wakati akikabidhi Hadubini 57 katika Mkoa wa Dodoma zitakazotumika kufanya vipimo vya ugonjwa wa Kifua Kikuu ambazo zitasambazwa katika Hospitali na Vituo vya Afya mbalimbali mkoani humo.

“Leo nimeanza zoezi la kukabidhi Hadubini 941 zilizonunuliwa na Serikali kwa ufadhili ya Global Fund zenye thamani ya Tsh. Bilioni 3.3 ambapo leo nitamkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Binilith Mahenge Hadubini 7 za Wilaya ya Chamwino zitakazosambazwa katika vituo vya Afya mbalimbali”. Amesema Waziri Ummy.

Pamoja na hayo Waziri Ummy ametumia muda huo kueleza mafanikio yaliyofikiwa na Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma ikiwa ni pamoja na kupungua maambukizi mapya kwa asilimia 18 lengo likiwa ni asilimia 20 na vifo vimepungua kwa asilimia 27 lengo likiwa ni asilimia 35.

Aidha, Waziri Ummy amesema ugunduzi wa Kifua Kikuu unaendelea kuimarika ambapo idadi ya wagonjwa waliogundulika na kuwekwa kwenye matibabu imeongezeka kutoka wagonjwa 62,180 mwaka 2015 hadi kufikia 82,,140 mwaka 2019.

Kwa upande wa vituo vya ugunduzi wa tiba, Waziri Ummy amesema katika kipindi cha miaka mitatu vituo vimeongezeka kutoka 662 mwaka 2016 hadi kufikia vituo 1201 mwaka 2019.

Katika kipindi cha miaka idadi ya wagonjwa waliogundulika kuwa na Kifua Kikuu imepungua kutoka wagonjwa 164,000 mwaka 2015 hadi 142,000 mwaka 2018.

Waziri Ummy amesema vifo vinavyotokana na TB vimepungua  kutoka makadirio ya vifo 30,000 mwaka 2015 hadi vifo 22,000 mwaka 2018.

Waziri Ummy ameongeza kuwa Hadubini hizo zitapelekwa katika vituo vipya vya kutolea Huduma za afya 487 ambavyo vimejengwa, Hospitali za Mikoa 3, Hospitali za Wilaya 69 pamoja na vituo vya afya vya zamani 315 pia kubadilisha hadubini zilizoharibika katika vile vituo vyenye uhitaji.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kutambua ulazima wa kuwepo Hadubini hizo katika maeneo mbalimbali ya kutolea huduma za afya lengo likiwa ni kuondoa usumbufu kwa wananchi kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma hiyo.

MWISHO

MSIBWETEKE KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UGONJWA WA CORONA

- Hakuna maoni
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashid Mfaume akipokea msaada wa barakoa 17,500 na vipukusi lita 700 kutoka kwa Mwakilishi Mkazi kutoka Shirika lisilo Lakiserikali la Medipeace Tanzania Bi. Sukyung Kim leo Jijini Dar es Salaam.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashid Mfaume akiwa ameshika box la barakoa 17,500 na vipukusi lita 700, kulia ni, Mwakilishi Mkazi kutoka Shirika lisilo Lakiserikali la Medipeace Tanzania Bi. Sukyung Kim.



MSIBWETEKE KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UGONJWA WA CORONA.

Na Rayson Mwaisemba, WAMJW- DSM

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashid Mfaume ametoa wito kwa wananchi, hususan Jijini Dar es Salaam kutobwete na kuwataka kuendelea kuchukua hatua za tahadhari ili kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona katika kipindi hiki.

Dkt. Rashid Mfaume ametoa wito huo leo, wakati akipokea msaada wa barakoa 17,500 sawa na maboksi 350, na vipukusi (sanitizers) lita 700 ambayo ni sawa na madumu 140 yenye ujazo wa lita 5 kutoka kwa Shirika lisilo Lakiserikali la Medipeace linalohusika na mradi wa mama na mtoto katika Mkoa wa Dar es Salaam.

"Licha ya elimu tunayoendelea kutoa juu ya namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona, tunawahamasisha wananchi wasibweteke katika kipindi hiki, ili kuumaliza kabisa ugonjwa huu katika nchi yetu, na hili linawezekana kabisa" alisema

Dkt. Rashid Mfaume aliendelea kusema kuwa, Msaada huo utaelekezwa katika vituo vya kutolea huduma za Afya vya Sinza Hospitali, Vijibweni Hospitali, Rangi Tatu Hospitali, Kituo cha afya Kimara, Kituo cha afya Tandale, Kituo cha afya Mbezi, Kituo cha afya Round table, Kituo cha afya Kimbiji, Kituo cha afya Buguruni, Tegeta Dispensari, Bunju Dispensari.

Aidha, amefafanua kuwa, kumekuwa na ongezeko la wagonjwa katika vituo vya kutolea huduma za Afya, hususan katika Jiji la Dar es Salaam baada ya Serikali kuziteua baadhi ya Hospitali kuwa vituo vya kutolea huduma za Corona, hivyo kuelekezwa msaada huo katika vituo vya Afya kutasaidia mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya Corona.

"Sasa hivi tumeona wagonjwa wameongezeka sana katika vituo vya kutolea huduma za Afya, mfano katika Mkoa wa Dar es Salaam baada ya Serikali kuitangaza Hospitali ya Amana kuwa kituo cha kuhudumia wagonjwa wa COVID-19, wagonjwa wengi wamekuwa wakienda katika vituo vingine, hivo msaada huu utasaidia sana kupambana dhidi ya maambukizi mapya" alisema.

Mbali na hayo, Dkt. Mfaume amewataka Wadau wengine kutoka Mashirika mbali mbali nchini kuendelea kuisaidia Serikali vifaa kinga vya kupambana dhidi ya ugonjwa wa Corona ili kuvisaidia vituo vya kutolea huduma za Afya vyiweze kujitosheleza mahitaji hayo, hasa kutokana na vituo vya Afya kuwa sehemu inayopokea watu tofauti kwa wingi.

Hata hivyo, Dkt. Mfaume amewatoa wasi wasi Wananchi kuwa, hali ya Afya katika Mkoa wa Dar es Salaam ni shwari, huku akisisitiza kuwa Serikali inaendelea kuchukua tahadhari za karibu dhidi ya maambukizi hayo ili kuumaliza kabisa ugonjwa huo nchini.

Nae, Mwakilishi Mkazi kutoka Shirika lisilo Lakiserikali la Medipeace Tanzania Bi. Sukyung Kim amesema kuwa, Medipeace inayofadhiliwa na KOICA imekuwa ikishirikiana na Wizara ya Afya pamoja na TAMISEMI katika kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto katika mkoa wa Dar-es-salaam.

Aliendelea kusema kuwa, kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona, Shirika hilo linaunga mkono juhudi za Serikali za kupambana dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo kwa kutoa vifaa kinga ambavyo vitasaidia kwa Watoa huduma za Afya na wagonjwa wataofika kupata matibabu katika vituo hivyo.

Mwisho.

Jumanne, 19 Mei 2020

WAZAZI, WALEZI WAHIMIZWA KUVAA BARAKOA WANAPOPELEKA WATOTO KLINIKI.

- Hakuna maoni
Muuguzi Mkunga Mwanaidi Khalfan akitoa chanjo kwa mtoto wa Bi. Sofia Yusuph katika Zahanati ya Madizini, Wilayani Mvomero. Picha na Englibert Kayombo.

Mhudumu wa Afya Zahanati ya Madizini, Wilayani Mvomero Bi. Grace Ligombi akitakasa mikono kabla ya kuanza kutoa huduma za chanjo kwa mtoto. Picha na Englibert Kayombo.


Muuguzi wa Zahanati ya Madizini, Wilayani Mvomero Bi. Eliainenyi Tarimo akijaza taarifa kwenye rejesta ya kliniki ya watoto. Picha na Englibert Kayombo.

Mtoto Mustapha Pangani (14) akiwa amempeleka mdogo wake Ismail Pangani (Mwaka mmoja na nusu) kliniki katika Zahanati ya Madizini wakihojiwa na mwandishi mwandamizi wa Gazeti la JAMVI LA HABARI, Veronica Mrema. Picha na Englibert Kayombo.

Ofisa Miradi kutoka Mpango wa Taifa wa Chanjo, unaosimamiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Furaha Kyesi (kulia) akimhoji Muuguzi wa Zahanati ya Madizini, Wilayani Mvomero Bi. Eliainenyi Tarimo wakati wa ziara katika zahanati hiyo. Picha na Englibert Kayombo.

Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Morogoro Bw. Abdulkadiri Kakai akikau jotoridi kwenye jokofu la kuhifadhi chanjo katika Zahanati ya Madizini Wilayani Mvomero.
Wazazi na walezi wakiwa katika Zahanati ya Madizini iliyopo Kata ya Mtibwa Wilayani Mvoremo kuhudhuria kliniki za watoto wao. Picha na Englibert Kayombo.



Na Mwandishi Maalum - Morogoro

WAZAZI na walezi wamehimizwa kuzingatia kuavaa barakoa kila wanapowapeleka watoto wao hospitalini, vituo vya afya na zahanati kupatiwa huduma mbalimbali za kiafya ikiwamo zile za chanjo.

Rai hiyo imetolewa leo Mkoani hapa na Ofisa Miradi kutoka Ofisi ya Mpango wa Taifa wa Chanjo (IVD), Dk. Furaha Kyesi alipozungumza na wazazi na walezi waliofika katika Zahanati ya Madizini iliyopo Kata ya Mtibwa Wilayani Mvomero kupata chanjo na kupima uzito wa watoto wao.

Maofisa wa Mpango huo wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Mkoa wa Morogoro na wa Manispaa wako katika ziara ya kukagua utoaji huduma za chanjo katika Mkoa huo kwa kushirikiana na Shirika la Engender Health kupitia Merck Sharp & Dohme B.V (MSD).

Dk. Kyesi amesema huduma za chanjo nchini hazijasitishwa bado zinaendelea kutolewa kulingana na ratiba za watoto walizopangiwa na kulingana na umri wao hata hivyo jambo la msingi ni kila mmoja kuhakikisha anajikinga kila anapompeleka mtoto.

“Kila mmoja anapaswa kuvaa barakoa, jikinge ili uwakinge na wengine kwa sababu hapa hakuna anayejua mwenzake ametoka wapi, amekutana na nani hadi amefika hapa kwenye zahanati.

“Ukiwa umevaa barakoa inasaidia kukukinga lakini pia unawakinga na wale wanaokuzunguka, vile vile mnapofika hapa kituoni zingatieni kunawa mikono na kukaa umbali wa mita moja, hakikisha unapokaa mkono wako ukiunyoosha hauwezi kugusa bega la mwenzako aliye pembeni yako,” amesisitiza Dk. Kyesi.

Amesema ni muhimu pia mama kuzingatia kunawa au kutakasa mikono kila anapohitaji kumnyonyesha mtoto wake ili aendelee kumkinga naye pia, watoto wadogo hatushauri wavalishwe barakoa.

Awali, Muuguzi wa Zahanati hiyo, Eliainenyi Tarimo amesema kila mwezi wamelenga kuwachanja watoto 34 lakini kwa kuwa jamii ina mwamko mkubwa wa chanjo wamefanikiwa kuvuka lengo hilo na kuchanja watoto zaidi ya 100.

“Tunaendelea kutoa chanjo kwa kuzingatia mwongozo tuliopewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa kujikinga tusipate maambukizi.” Amesema Eliainenyi na kuendele kusema  kuwa kabla ya mzazi au mlezi kuingia ndani ya kituo hicho kwanza anatakiwa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni ambapo ndoo imewekwa katika eneo la kuingilia katika Zahanati hiyo.

Eliainenyi amesema awali utaratibu waliokuwa wakiutumia kabla ya kuchukuliwa kwa tahadhari ya mlipuko wa Corona walikuwa hawana kabisa utaratibu huo.

“Walikuwa tu wakifika wanakwenda moja kwa moja sehemu ya kuweka kadi, wanakaa kwenye mabenchi na kusubiri kuitwa majina, tukaona tuanze kuwapa namba na kuwaruhusu wakae kwa kupeana nafasi ya mita moja kwenye mabenchi.

“Mabenchi tuliyonayo hayatoshelezi lakini eneo letu ni kubwa hivyo wanakaa na hapo nje kwa kupeana nafasi, tunapomaliza kumhudumia mtoto, tunawaomba waondoke mapema kwenda nyumbani na si kuendelea kukaa hapa,” amesisitiza.

Amesema changamoto pekee inayowakabili sasa ni wazazi na walezi hao kuwa na mwitikio mdogo wa uvaaji barakoa jambo ambalo hawachoki kuwasisitiza na kuwahimiza kuzingatia ili kuendelea kujikinga.

Amesema kwa upande wa chanjo ya HPV ambayo hupatiwa wasichana wenye umri wa miaka 14 iliyokuwa ikitolewa shuleni na kwa kuwa sasa zimefungwa kutokana na mlipuko wa CORONA, hivi sasa zinaendelea kutolewa katika Zahanati hiyo.

“Japo bado hatujawaona wengi wakija, wachache wameshakuja tumewachanja, tunaendelea kuwahimiza waje kupitia watoa huduma za afya wa ngazi ya jamii (CHW’s) na hapa kituoni huwa tunawaeleza wanajamii wanaokuja kliniki kwamba waende wakawahimize wasichana waje kupata chanjo ya pili,” amesema.

MWISHO

ZINGATIENI MWONGOZO WA KUJIKINGA NA CORONA HUKU MKITOA HUDUMA ZA CHANJO INAVYOPASWA

- Hakuna maoni
Ofisa Miradi kutoka Mpango wa Taifa wa Chanjo, kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Furaha Kessy akiwasikiliza Wauguzi wa Kituo cha Afya Uhuru, Tumaini Majoji na Zawadi Rashid  namna wanavyotoa huduma za chanjo kwa kuzingatia mwongozo wa kujikinga  na maambukizi ya virusi vya Corona, wao na wateja wanaowahudumia.

Ofisa Miradi kutoka Mpango wa Taifa wa Chanjo, unaosimamiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Furaha Kessy akizungumza na Muuguzi wa Kituo cha Afya Sabasaba, Celina Daffa wakati wa ziara ya kukagua namna wanavyotoa huduma za chanjo wakizingatia  wakijikinga na maambukizi ya virusi vya Corona, wao na wateja wanaowahudumia.

Askari wa Jeshi la Akiba Morogoro (Mgambo), Nuhu Said Hashim akiwaelekeza wakina mama wajawazito kukaa kwa kuzingatia umbali wa mita moja wakati wakisubiri huduma katika Kituo cha Afya, Mafiga. Askari huyo huwaongoza pia wakina mama wanaohudhuria kliniki ya chanjo kituoni hapo.

Ofisa Miradi kutoka Mpango wa Taifa wa Chanjo, unaosimamiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Furaha Kyesi akimsikiliza Muuguzi wa Kituo cha Afya Sabasaba, Celina Daffa alipokuwa akieleza namna wanavyotoa huduma za chanjo huku wakijikinga na maambukizi ya virusi vya Corona, wao na wateja wanaowahudumia, katikati ni Mratibu wa Huduma za Chanjo wa Manispaa ya Morogoro, Hidaya Omari 

Mratibu wa Chanjo wa Mkoa wa Morogoro, Abdulkadiri Kakai akifafanua jambo wakati wa ziara hiyo.


Na Mwandishi Maalum – Morogoro

Watoa huduma za chanjo katika vituo vya afya nchini wamehimizwa kuzingatia mwongozo wa kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona na kuendelea kutoa chanjo kwa watoto na wasichana kwa wenye umri wa miaka 14  inavyostahili kwa mujibu wa ratiba zao.

Rai hiyo imetolewa leo mjini hapa na Ofisa Miradi kutoka Ofisi ya Mpango wa Taifa wa Chanjo, Furaha Kessy alipozungumza na watoa huduma hao katika Kituo cha Afya Sabasaba, Kituo cha Afya Mafiga na Kituo cha Afya Uhuru wakati wa ziara ya kukagua namna wanavyotoa huduma huku wakijikinga dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo.

“Ndiyo tupo kwenye janga la Corona lakini ni muhimu mno chanjo kuendelea kutolewa kwa watoto kama ambavyo inatakiwa kulingana na ratiba zao.

“Pia kuna kundi la wasichana wenye umri wa miaka 14 ambao wanastahili kupata chanjo ya HPV inayokinga dhidi ya maambukizi ya kirusi hicho kinachosababisha saratani ya kizazi.

“Kundi hili awali wapo ambao walikuwa wakipatiwa chanjo shuleni, lakini kwa sababu ya Corona shule zimefungwa, lazima tujue namna gani hawa tutawapata kuwapa chanjo ya pili ili kukamilisha ratiba zao,” ametoa rai.

Kessy ameongeza “Wataalamu wanapaswa kutoa chanjo hizo huku wazingatia mwongozo uliotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo, Jinsia, Wazee na Watoto wa kujikinga ili wasipate maambukizi wao huku wakiwakinga pia wateja wanaowahudumia.

“Zingatieni kujikinga vema, chanjo ziendelee kutolewa na tunazo, kundi la wasichana wale lazima nalo tulifikie ili tusije tukajikuta siku zijazo tunapata milipuko ya magonjwa mengine ambayo yanaweza kuzuilika kwa chanjo, hili muhimu tulizingatie,” amesisitiza.

Muuguzi wa Kituo cha Afya Uhuru, Tumaini Majoji amesema awali janga hilo lilipotangaza kuwapo nchini walikuwa na hofu jinsi watakavyoweza kuhudumia wateja huku nao wakibaki kuwa salama bila kupata maambukizi kwa sababu ni ugonjwa mpya na hawakuwa na uelewa wa kutosha jinsi ya kujikinga.

“Uongozi wa kituo umetupatia elimu jinsi ya kujikinga na timu maalum ya kutoa elimu ya kujikinga pia ilikuja kutuelimisha, sasa tunaelewa, hatuna hofu tena, tunazingatia mbinu za kujikinga na tunatoa huduma za chanjo na elimu kwa jamii jinsi ya kujikinga pia,” amesema.

Muuguzi wa Kituo cha Afya Sabasaba, Celina Daffa amesema wanaendelea kutoa huduma na kwamba kwa wiki hupokea wateja  wapatao 50 na kuwapa chanjo mbalimbali.

Mratibu wa Huduma za Chanjo wa Manispaa hiyo, Hidaya Omari amesema wana jumla ya vituo 47 vinavyotoa huduma za chanjo kila siku.

“Katika vituo vinavyotoa huduma ya uzazi (kujifungua) na kwa vituo ambavyo havitoi huduma ya kujifungua vyenyewe hutoa kwa siku tano pekee katika wiki,” amebainisha.

Ameongeza “Huduma zinaendelea isipokuwa tulipata changamoto kwa kundi hili la wasichana wa miaka 14 kwa sababu chanjo zilikuwa zinatolewa shule lakini zilipofungwa kutokana na Corona kuna ambao bado hatujaweza kuwapata kuwapa chanjo.

“Kutokana na hali hiyo, jitihada mbalimbali zinaendelea kufanyika, sasa tumekubaliana kuanza kuwatumia watoa huduma za afya ngazi ya jamii (CHW’s) kuwahimiza wasichana hawa kwenda katika vituo vya afya kupatiwa chanjo maana tunazo,” amesisitiza.

Amesema makadirio yao kwa mwaka ni kuwafikia wasichana wapatao 4,762 wa umri wa miaka 14 kuwapatia chanjo hiyo ikiwa ni sawa na wasichana  395 kwa mwezi.

“Katika chanjo ya kwanza tulifanikiwa kwa kiwango cha asilimia 100 kulifikia kundi hili, katika kipindi cha mwaka huu Januari hadi Machi, tumepata changamoto tumeweza kuwafikia asilimia 80 tu, kwa sababu ya janga la Corona, shule zimefungwa na sasa wapo nyumbani,” amebainisha.

MWISHO

LICHA YA JANGA LA CORONA, HUDUMA ZA CHANJO NA UFUATILIAJI WA MAGONJWA YANAYOZUILIKA KWA CHANJO ZAENDELEA KWA UANGALIFU MKUBWA TANGA

- Hakuna maoni
Ofisa Mradi wa Ofisi ya Mpango wa Taifa wa Chanjo, Richard Magodi (katikati) akikagua namna ya uingizaji wa data za chanjo pamoja na muongozo wa kujikinga na janga la COVID 19 katika Hospitali ya Wilaya ya Pangani, Mkoani Tanga

Ofisa Mradi wa Ofisi ya Mpango wa Taifa wa Chanjo, Richard Magodi akipitia data za chanjo kwenye mfumo maalumu wa kieletroniki wakati wa ziara maalum ya muongozo wa kujikinga na COVID19 kwa watoa huduma za chanjo katika kituo cha Chanjo Zabanati ya Bushiri, Pangani Mkoani Tanga.


Na Mwandishi Maalum –Pangani,Tanga.

LICHA ya janga la Virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa homa kali ya Mapafu (COVID19), Watoa huduma za chanjo na ufuatiliaji wa magonjwa yanayozuilika kwa Chanjo hizo Wilayani Pangani Mkoani Tanga zinaendelea kama kawaida huku wahudumu wakichukua tahadhari kubwa kwa kuzingatia muongozo wa kujikinga na janga hilo.

Hayo yameelezwa na  Mratibu wa Huduma za Chanjo Mkoa wa Tanga,  Seif Shaib wakati wa ziara maalum ya usimamizi elekezi na uhamasishaji wa muongozo wa kujikinga na COVID 19 kwa watoa huduma hizo iliyofanywa na Ofisa Mradi wa Ofisi ya Mpango wa Taifa wa Chanjo, Richard Magodi.

Mratibu huyo wa Chanjo mkoa, Seif Shaib alisema chanjo zipo na huduma vituoni zinaendelea kwa kuzingatia muongozo.

Kwa upande wake, Ofisa Mradi wa Ofisi ya Mpango wa Taifa wa Chanjo, Richard Magodi ameweza kushuhudia uwepo wa chanjo hizo kwenye vituo sambamba na watoa huduma wakifuata miongozo ikiwemo kukaa umbali wa mita moja kati ya mtu na mtu kwa kuacha nafasi, uwapo wa maji safi na tiririka ya kunawa mikono na uvaaji barakoa.

"Watoa huduma za chanjo na wafuatiliaji wa magonjwa yanayozuilika kwa chanjo kwa watoto wanatakiwa waendelee  kulingana na ratiba za chanjo zao lakini kwa kuzingitia muongozo wa kujikinga dhidi ya COVID 19." Alisema Richard Magodi

Akielezea upande wa chanjo ya kukinga ugonjwa wa Saratani ya mlango wa kizazi (HPV) inayotolewa kwa wasichana  wa umri wa miaka 14 ipo na inatolewa kwa walengwa hao.

"Chanjo hii ya HPV bado ipo lakini tunacho sisitiza kwa watoto ambao ratiba zao zinafikia hivi sasa wanaweza kufika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

Kamati za afya za kituo  na Uongozi  wa vijiji ama mtaa wahusishwe kuhamasisha wananchi kuwapeleka watoto wa kike wenye miaka 14 kupatiwa chanjo hiyo." Alisema Magodi.

Sambamba na hilo, watoa huduma hao wametakiwa kufuatiliaji pia magonjwa yanayozuilika kwa chanjo hususani ugonjwa wa Surua, Polio na Pepopunda kwa watoto kwa kipindi hiki cha COVID19.

"Tuongeze jitihada za chanjo. Kwani tusipofanya hivyo watu wengi wanaweza kufariki na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.

"Mfano tukiangalia takwimu za mwaka jana nchini Congo (DRC), ugonjwa wa Ebola uliua watu wachache kuliko Surua hii ni kutokana na kuipa kipaumbele Ebola na kuacha magonjwa yanayozuilika kwa chanjo nchini humo..Hivyo sisi Tanzania tunaendelea na huduma kwa kufuata muongo na tahadhari kubwa ikiwemo kuhimiza suala hilo la chanjo." Alisema Magodi.

Aidha aliwataka watoa huduma hao kuzingatia  matumizi sahihi  ya mfumo wa kieletroniki ngazi ya kituo (Tanzania Immunizations Registry -TImR) ili kuwa na takwimu sahihi na zitakazosaidia kufanya maamuzi bora kwa  wakati kwenye ngazi ya kituo hadi ngazi ya Taifa.

"Katika vituo ambavyo tumetembelea Watumishi wameendelea kutumia mfumo huu kwa kuchanja na kuomba dawa, vifaa vya chanjo na kupata taarifa mbalimbali  wanazozihitaji kwa wakati kupitia  Vishishwambi (tablets) na wamefundishwa namna ya kutumia mfumo huo ambao umekuwa ukisaidia sana" alisema.

Awali Magodi aliweza kutembelea vituo vya chanjo hizo katika Hospitali ya Wilaya ya Pangani, kituo cha chanjo Zahanati ya Bushiri, kituo chanjo Zahanati ya Madanga na kituo cha Chanjo Zahanati ya Kimang'a.

Nae Muuguzi mkunga wa Kituo cha Chanjo Zahanati ya Madanga alisema tokea uwepo  wa COVID 19, wamechukua hatua mbalimbali na kutoa elimu kwa wananchi wa Kijiji hicho cha Madanga.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kimang'a, Dkt. Mohammed Kombo alisema wameweza kuchukua hatua dhidi ya COVID19 ikiwemo kutoa elimu kwa wanakijiji.

"Tumechukua tahadhari ya COVID19  ikiwemo pia kutoa elimu kwa wanakijiji. Lakini wanakijiji nao wameweka utaratibu mgeni akija kijijini hapa lazima ajitenge kwa maangalizio na kuchukuliwa taarifa zake mpaka tunapojiridhisha" alisema Dkt kombo.

Ziara ya usimamizi elekezi inaendelea tena katika Wilaya mbalimbali za mkoa huo wa Tanga kwa uratibu wa Mpango wa Taifa wa Chanjo kwa kushirikiana na wadau wake.

MWISHO

Jumatano, 13 Mei 2020

WAMILIKI WA VIWANDA WATAKIWA KUZALISHA VIFAA KINGA KUKABILIANA NA CORONA

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akionesha moja ya kifaa kinga dhidi ya maambukizi ya Corona wakati akiongea na Umoja wa Wazalishaji Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba (TPMA) nchini kwenye mkutano wa kuangalia jinsi gani wanaweza kuzalisha vifaa kinga kutoka wazalishaji wa ndani hapa nchini.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiteta jambo na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa wakati akiongea na Umoja wa Wazalishaji Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba (TPMA) nchini.

Baadhi ya Wazalishaji Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba (TPMA) nchini wakitizama vazi la kujikinga dhidi ya Corona wakati wa mkutano wa kuangalia jinsi gani wanaweza kuzalisha vifaa kinga kutoka wazalishaji wa ndani hapa nchini ulioongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa.

Umoja wa Wazalishaji Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba (TPMA) nchini wakiendelea na mkutano wa kuangalia jinsi gani wanaweza kuzalisha vifaa kinga kutoka wazalishaji wa ndani hapa nchini ulioongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa.


WAMILIKI WA VIWANDA WATAKIWA KUZALISHA VIFAA KINGA KUKABILIANA NA CORONA

Na.WAMJW- Dar es Salaam

Wamiliki wa viwanda vya Dawa, Vifaa na vifaa tiba nchini wametakiwa kuanza kuzalisha vifaa kinga kuweza kukabiliana na janga la Corona nchini ili kuondokana na changamoto ya ucheleweshaji wa kupata vifaa kinga toka nje ya nchi pamoja na kupunguza gharama.

Wito huo umetolewa leo jijini hapa  na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiongea na Umoja wa Wazalishaji Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba (TPMA) nchini kwenye mkutano wa kuangalia jinsi gani wanaweza kuzalisha vifaa kinga kutoka wazalishaji wa ndani hapa nchini.

“Tukizalisha hapa nchini tutaokoa rasiliamali fedha nyingi, muda pia tutazalisha ajira na kuwa na uhakika wa   ubora na usalama unaohitajika kupitia mamlaka zetu za ndani kwa urahisi”. Alisema Waziri Ummy.

Waziri amesema kuwa bado kuna uhitaji mkubwa wa vifaa kinga , hivyo wale wote wanaozalisha vifaa kinga wanatakiwa kuongeza uzalishaji ili kutosheleza mahitaji ya soko nchini na hata kuweza kuuza nchi za jirani.

Aidha, amesema  Wizara inahitaji kuipa nguvu  huduma salama kwenye vituo vya kutolea huduma za afya  vya serikali na visivyo vya Serikali kwa watumishi wa afya kuzingatia miongozo ya kukinga na kudhibiti maambukizi angalau kuvaa barakoa,glove na eproni hivyo amewasisitiza kuzalishaji vifaa vyenye  viwango vyenye  ubora ili kukidhi soko la ndani nan chi za jirani.

Naye Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amewapongeza wamiliki wa viwanda hivyo kwa kubuni na kugundua teknolojia na uzalishaji wa  vifaa kinga kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo.

“Kuanzisha viwanda ni sehemu ya ulinzi wa nchi,hivyo kuwa na viwanda vyetu nchini hususani wakati wa shida imesaidia upatikanaji wa baadhi za vifaa kinga kwa bei nafuu”.Alisema Waziri Bashungwa.

Amesema katika kikao hicho wamekubalia kujipanga vizuri katika uzalishaji wa vifaa kinga na hivyo wamewataka Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kujikita katika kuzalisha barakoa aina ya N95 na glove kutokana na kwamba viwanda vya namna hii havipo nchini.

Pia Waziri Bashungwa ameitaka TMDA kushirikia na wizara ya viwanda kuisaidia NDC kuweza  kufanya kiwanda hicho kuanza kuzalisha kwa wakati na hivyo kusaidia watumishi wa afya walio mstari wa mbele kutoa huduma bila hofu.

Kwa upande wa MSD, Waziri Bashungwa ameitaka  kununua vifaa kinga vinavyozalishwa na viwanda vya ndani ambavyo vimekidhi viwango na vimesajiliwa na TMDA badala ya kutumia fedha iliyotengwa na Serikali kununua vifaa hivyo nje ya nchi.

Waziri Bashungwa ameahidi kukitembelea kiwanda cha Msagala Investment kilichopo Bagamoyo ambacho kinatarajia kuanza kuzalisha malighafi za utengenezaji wa barakoa kutokana na pamba zinazolimwa nchini.

 -Mwisho-