Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumapili, 14 Juni 2020

WAZIRI UMMY AZITAKA HOSPITALI ZOTE NCHINI KUACHA KUWADAI DAMU WAGONJWA KABLA YA HUDUMA

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wachangia Damu Duniani ambayo kitaifa yamefanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma mapema leo.
Meneja wa Mpango wa Damu Salama nchini Dkt. Magdalena Lyimo akifafanua jambo kwa Waziri Ummy Mwalimu wakati alipotembelea kituo cha damu salama kilichopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.





Picha mbalimbali zikionesha Waziri Ummy Mwalimu akiwajulia hali wananchi waliojitokeza kutoa damu katika Kituo cha Damu Salama kilichopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.


NA WAJMW-DODOMA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameziagiza Hospitali zote nchini za Serikali na binafsi, Zahanati na Vituo vya Afya kuacha kuwadai damu wagonjwa kabla ya kuwapa huduma.

Waziri Ummy amesema hayo leo wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya wachangia damu duniani yenye kauli mbiu “Damu Salama inaokoa maisha” ambayo kitaifa yamefanyika katika kituo cha kidogo cha damu salama kilichopo katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma.

“Nazitaka Hospitali zote za Serikali na binafsi kuacha tabia ya kuwadai damu wagonjwa na ndugu kabla ya kumpatia mgonjwa huduma, mnatakiwa kutoa huduma kwanza na masuala ya wanandugu kuambiwa walete watu wa kuchangia damu kabla ya huduma ni kinyume na taratibu na kanuni za utoaji wa huduma za afya”. Amesisitiza Waziri Ummy.

Waziri Ummy amezitaka Hospitali zote za Serikali na binafsi na vituo vya Afya nchini kushirikiana na Mpango wa taifa wa damu salama katika kukusanya damu na wasibaki wao kuwa watumiaji wa damu bila kuweka fedha au jitihada zozote za ukusanyaji.

Waziri Ummy amesema  takwimu zinaonyesha kuwa, wakati Serikali ya awamu ya tano inaingia madarakani mwaka 2015 jumla ya chupa za damu 104,632 zilikusanywa, kupimwa na kusambazwa. Idadi hii imeongezeka hadi kufikia chupa 309,376 ziizokusanywa mwaka 2019 ambayo ni ongezeko la chupa 204,744 ambayo ni sawa na asilimia 195 ikilinganishwa na chupa za damu zilizokusanywa mwaka 2015.

“Tumeboresha huduma kwenye Mpango wa Taifa wa Damu Salama kwa kuwapitia mashine za kisasa za kupimia damu ambapo uwekezaji huo umegharimu karibu Bilioni 13. Kwa kutumia mashine hizi Mpango una uwezo wa kufanya vipimo 4000 kwa masaa 6 kutoka vipimo 1404 kwa mashine zilizokuwepo awali kabla Serikali ya Awamu ya Tano haijaingia madarakani”. Amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amesema kuchangia damu ni tendo la huruma, utu na upendo hivyo amewashukuru wachangia damu wote nchini hususani wale wanaochangia mara kwa mara. Pia amewahamasisha wananchi ambao hawajawahi kuchangia waweze kuchangia damu angalau mara moja kwa mwaka.

Waziri Ummy ametaka Mpango wa damu salama nchini kuweka utaratibu wa kufikia kaya zote nchini na kuhamasisha angalau awepo mtu mmoja kwa kila kaya ambae atakua anachangia damu mara kwa mara ili kuweza kukidhi mahitaji ya kitaifa ya damu salama.

Mwisho Waziri Ummy ameipongeza mikoa ya Mtwara na Lindi kwa kuweka mikakati mizuri ya uchangiaji damu ambapo mgonjwa mwenye uhitaji wa damu anahudumiwa kwanza kabla ya kutafuta ndugu wa kuchangia damu.

MWISHO

DKT. MOLLEL APIGA MARUFUKU RAMLI CHONGANISHI.

- Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel akieleza jambo wakati wa hafla fupi ya wahitimu wa mafunzo ya uboreshaji wa utoaji huduma za tiba asili yaliyofanyika katika chuo ya Mirembe Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel akiteta jambo na Mwenyekiti wa wahitimu hao Dkt. John Kabadi Lupimo wakati wa hafla fupi ya wahitimu wa mafunzo ya uboreshaji wa utoaji huduma za tiba asili iliyofanyika Jijini Dodoma.

Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya uboreshaji wa utoaji huduma za tiba asili wakifuatilia kwa makini neno kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel (hayupo kwenye picha) wakati wa hafla fupi ya wahitimu wa mafunzo ya uboreshaji wa utoaji huduma za tiba asili.

Wanafunzi wa fani ya uuguzi katika taasisi ya Afya na Sayansi shirikishi Dodoma (DIHAS) wakifuatilia neno kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel wakati wa hafla fupi ya wahitimu wa mafunzo ya uboreshaji wa utoaji huduma za tiba asili.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel akimkabidhi cheti Nicholous Makoye Lupimo wakati wa hafla fupi ya wahitimu wa mafunzo  ya uboreshaji wa utoaji huduma za tiba asili.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Ajmii, Jinsaia, Wazee na Watoto Dkt. Mollel wakati wa hafla fupi ya wahitimu wa mafunzo  ya uboreshaji wa utoaji huduma za tiba asili.


DKT. MOLLEL APIGA MARUFUKU RAMLI CHONGANISHI.

Na WAMJW- DOM

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel amepiga marufuku tabia za Waganga wa tiba asili kupiga ramli chonganishi kwa lengo la kuwasaidia wananchi jambo ambalo ni kinyume na taratibu na miongozo ya Serikali.

Dkt. Mollel ameyasema hayo leo, wakati wa hafla fupi ya wahitimu wa mafunzo ya uboreshaji wa utoaji huduma za tiba asili iliyohudhuriwa na baadhi ya wawakilishi kutoka Wizara ya Afya na baadhi ya wanafunzi wa taaluma ya uuguzi Mirembe Jijini Dodoma.

"Mambo ya ramli chonganishi, hayatakiwi kabisa katika nchi yetu, kitu tunachosisitiza ni tiba kwa kutumia mimea yetu ambayo Mungu alipomuumba mwanadamu aliumba akaweka mimea ya chakula, mimea ya matunda na mimea dawa, mimea dawa hiyo ndio tunataka wakaibue huko walete itusaidie kutibu watu wetu" alisema

Dkt. Mollel aliendelea kukemea tabia za baadhi ya Waganga kutumia Imani potofu katika taaluma ya tiba asili, huku akisisitiza kuwa, Serikali inatambua juhudi zinazofanywa na Waganga wa tiba asili nchini wanaofuata taratibu na miongozo ya Wizara ya Afya katika kuwahudumia wananchi.

"Hatutegemei mtu atuambie jiwe litutawale, hizo Imani ambazo mtu anatawaliwa na jiwe, mtu anatawaliwa na ilizi, sisi ndio tulipewa tuvitawale vitu vyote na Mungu, kwahiyo sisi tunataka tiba ambayo sisi binadamu tutatawala vitu vyote na Imani potofu isisogelee kabisa kwenye utaratibu wetu wa tiba asili " alisema

Aidha, Dkt. Mollel amesema kuwa, Serikali inawatambua na itaendelea kushirikiana na Wataalamu wa tiba asili na tiba mbadala nchini kutokana na kuwa na mchango chanya katika kuwahudumia wananchi hasa katika kipindi hiki ambacho nchi na Dunia kwa ujumla imepitia changamoto ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wa mafunzo ya uboreshaji wa tiba asili, Mwenyekiti wa wahitimu Dkt. John Kabadi Lupimo mesema, wamepata mafanikio mengi ikiwemo, kufungua viwanda vidogo vya kuchakata dawa asili, basdhi kusajiliwa kama Waganga wa tiba asili, kusajili dawa mbali mbali na kujua Sheria ya Afya ya tiba asili.

Mbali na hayo, Dkt. John Kabadi Lupimo ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa mafunzo hayo, huku akisisitiza wataendelea kushirikiana na Serikali ili kuikuza taaluma ya tiba asili ambayo inaendelea kuwa msaada mkubwa kwa wananchi hususan katika kipindi hiki ambacho Dunia imekumbwa na mlipuko wa virusi vya Corona.

Mwisho.

Ijumaa, 12 Juni 2020

WITO WATOLEWA WANANCHI KUENDELEA KIJIKINGA NA CORONA ILI PIA KUJIKINGA NA MAGONJWA MENGINE.

- Hakuna maoni



 
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi (kushoto) akizungumza na wananchi waliofika katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma kupata huduma ambapo amezungumza nao kuendelae kujilinda na ugonjwa wa corona kwa mbinu zinatotolewa na Wizara ya Afya ikiwemo tiba asili ya kujifukiza. 


 
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi (kulia) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika wakielekea kwenye kituo kilichotengwa kuhudumia wagonjwa wa corona  ambacho hakina mgonjwa yeyote.

 

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi akizunguma na watumishi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa alipotembelea hospitlai hiyo, Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika.




WITO WATOLEWA WANANCHI KUENDELEA KIJIKINGA NA CORONA ILI PIA KUJIKINGA NA MAGONJWA MENGINE.

Na WAMJW-DOM

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi ametoa wito kwa wananchi kuendelea kujikinga dhidi ya ugonjwa wa corona na kudhibiti magonjwa mengineyo ya kuambukiza.

Prof. Makubi ametoa wito huo leo alipofanya ziara ya kuona hali ya utoaji huduma katika Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Jijini Dodoma.

“Katika kudhibiti ugonjwa wa corona wananchi walipokea kwa mikono miwili mbinu za kuepuka kuambukizwa ugonjwa wa corona ikiwemo unawaji mikono kwa maji yanayotirika na sabuni, uvaaji wa barakoa, kuepuka mikusanyiko na misongamano pamoja na mbinu za tiba asilia/tiba mbadala ili kutibu ugonjwa wa corona”. Amesema Prof. Makubi

Pamoja na kupungua kwa ugonjwa wa corona nchini, Prof. Makubi amesema kuwa bado Watanzania tunatakiwa kuendelea kuchukua tahadhari za kinga ili hatimae tuweze kutokomeza kabisa ugonjwa wa corona au pale ambapo bado utaendelea kuwepo tuweze kuishi nao bila madhara makubwa.

Prof Makubi amesema kuwa Serikali inawapongeza wananchi kwa kuipokea na kutumia njia zote zilizotelewa kukabiliana na ugonjwa wa corona pamoja na magonjwa mengine ya kuambukiza na kuwataka wananchi kuendelea na mbinu walizoelimishwa kujikinga na magonjwa ya kuambukiza.

“Mwamko tulio nao sasa hivi wananchi juu ya mbinu hizi tusiziache, tukiendelea nazo zitatusaidia kujikinga na magonjwa mengine” amesisitiza Prof. Makubi.

Hatukuwa na utamaduni wa kunawa mikono mara kwa mara, lakini tuelewe pia usafi wa mikono unatusaidia pia kupunguza hatari ya kupata magonjwa mengine yanayotokana na uchafu yakiwemo magonjwa ya kuhara, au hata kipindupindu.
Prof. Abel Makubi amesema kuwa kufanya mazoezi ya mwili na kula lishe bora yanasaidia pia kujenga afya ya mwili uimara na pia kujikinga na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama shinikizo la damu, kisukari na moyo.
Ni vema wanachi wakaendelea na utamaduni huu huku wakiendelea kupata lishe bora aili kujenga kinga zao dhidi ya mgonjwa mengine” Amesisitiza Prof. Makubi
Kuhusu mbinu ya tibaasili, Prof. Makubi amewapongeza wananchi kwa kuipokea na kuikubali mbinu hiyo katika kusaidia kutibu ugonjwa wa corona na kutumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzana Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuelekeza bajeti ya tiba asili/mbadala na tafiti za dawa asilia iweze kuongezwa ili kuwawezesha wataalam wanaotengeneza dawa hizo zinazosaidia kutibu magonjwa mbalimbali na kupambana na maambukizi ya virusi vya corona nchini.

Aidha Prof Makubi amewaagiza wataalam wa afya hasa Wakurugenzi, Waganga wa Mikoa, Wilaya, Maafisa wa afya ngazi za jamii, viongozi wa mashule, vyuo, michezo, na mamlaka za mitaa kuendelea kutoa elimu ya kupambana ugonjwa wa corona na kuendelea kuhamasisha mbinu za kuthibiti CORONA ambazo  zikiendelezwa zitapunguza uwezekano wa kuibuka magonjwa mengine hivyo kuokoa afya za wanachi na fedha nyingi ambazo zingetumika  kutibu wagonjwa.

Mwisho.

DKT. MOLLEL ATETA NA MADEREVA WA MALORI, NAMANGA

- Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel akiongea na madereva malori mpaka wa Tanzania na Kenya Namanga Jijini Arusha, lengo kuwasikiliza changamoto zao.





Baadhi ya madereva wa malori waliokwama katika mpaka wa Tanzania na Kenya Namanga Jijini Arusha wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel.




DKT. MOLLEL ATETA NA MADEREVA WA MALORI, NAMANGA 

Na WAMJW- Arusha. 

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel amefanya ziara katika mpaka wa Tanzania na Kenya Namanga Jijini Arusha na kuzungumza na madereva wa malori yanayokwenda Kenya ili kusikiliza changamoto zinazowakumba. 

Dkt. Mollel amefanya ziara hiyo leo, ikiwa ni sehemu ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakumba madereva hao, katika kipindi hiki ambacho Dunia imekumbwa na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona. 


Dkt. Mollel amesema kuwa, Serikali imeliona tatizo hilo na kuweka wazi kuwa itaongeza kasi katika kuhakikisha inapata suluhu ya changamoto wanazokumbana nazo madereva hao katika eneo la mpaka wa Namanga. 

"Nimekuja kuwaambia poleni, lakini Serikali yetu itaenda kwa kasi ya ajabu kuhakikisha kwamba hili tatizo lenu katika mpaka huu linatatuliwa " alisema. 

Aidha, Dkt. Mollel amewataka madereva hao kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho, Serikali inatafuta utatuzi wa changamoto yao, huku akiwapa salamu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli na kusema anawapenda sana.

Mbali na hayo Dkt. Mollel alisema kuwa changamoto hii iliyojitokeza katika mpaka wa Namanga ni suala mtambuka ambalo linahusisha Wizara zaidi ya moja, huku akiweka wazi kuwa suala hili lina uhusiano wa kibiashara na uchumi baina ya nchi hizo.

Nae, dereva wa malori yanayokwenda nchini Kenya Bw. Abdullah Hassan amesema kuwa, kama madereva hawakubaliani na majibu ya vipimo wanavyopewa kutoka Kenya kutokana na vipimo hivyo kuonesha idadi kubwa ya madereva kuwa na ugonjwa wa Corona jambo ambalo sio kweli.

"Tunaishi maisha magumu sana kutokana na hali iliyojitokeza, na kunachosikitisha zaidi, sisi hatukubaliani na vipimo ambavyo tunapimwa upande wa pili. 

Kwa upande wake, Japhet Jeremiah alisema kuwa, wamekuwa wakiombwa kiasi cha shilingi 2000 za Kenya ili kuandikiwa kuwa hawana Corona, hali aliyeweka wazi kuwa ni uonevu kwa madereva kutoka Tanzania. 

"Sisi kero yetu, tumekuwa tukipima Kenya tumeambiwa tuna Corona, na mimi wiki mbili nilipima nikapewa cheti nina Corona lakini ukweli ni kwamba sina Corona na sijawai tumia dawa yoyote mpaka sasahivi" alisema 

Mwisho.