Wizara ya Afya Tanzania

Pages

▼

Alhamisi, 11 Oktoba 2018

TAARIFA KWA UMMA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO


TANGAZO KWA UMMA
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya) anawatangazia watumishi wote waliopata udahili wa kusoma masomo ya Shahada ya Uzamili (Masters Degree) katika fani za Afya kwa mwaka 2018/2019, kwamba Wizara inaanza kupokea maombi ya Ufadhili kwa mwaka 2018/2019. Maombi haya yatawasilishwa kwa njia ya kielektroniki kwa kujisajili kupitia fomu zilizopo kwenye tovuti ya Wizara www.moh.go.tz (https://sponsorship.moh.go.tz).Maombi yatakayofanyiwa kazi ni yale yaliyowasilishwa kwa njia ya mfumo huu tu, hivyo waombaji waliowasilisha maombi yao kabla ya tangazo hili wanapaswa kurudia kuomba kupitia  utaratibu huu.

Ufadhili huu ni kwa ajili ya kulipiwa ada ya mafunzo (Tuition fee), pamoja na posho ya utafiti  (Dissertation allowance). 

Vigezo vitakavyotumika kuchagua ni hivi vifuatavyo :

Kuwasilishwa kwa maombi rasmi ya ufadhili kwa njia ya mfumo (online application)
Mwombaji kuwa Raia wa Tanzania.
Awe amedahiliwa Chuoni kuanza masomo kwa mwaka wa kwanza 2018/2019
Kipaumbele kitatolewa kwa:
Watumishi wa Serikali waliomo kwenye sekta ya Afya wanaofanya kazi katika vituo vilivyoko Wilayani/Mikoani hususani katika Hospitali za Rufaa za Mikoa ambao baada ya mafunzo watarudi kuendelea kufanya kazi katika vituo vyao vya awali, au watapangiwa vituo vya kazi sehemu nyingine yeyote nchini
Waombaji waliodahiliwa katika fani ambazo ni za msingi katika utoaji wa huduma za rufaa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa. Nyanja hizo ni Anaesthisiology, Surgery, Neurosurgery, Obstetrics and Gynaecology, Orthopaedics Surgery, Emergency Medicine, Paediatrics, Internal Medicine, Critical Care in Nursing na Midwifery and Womens Health, Radio-pharmacy,Epidemiology and Lab.Management
Waombaji waliodahiliwa katika nyanja za Ubingwa/Ubingwa wa Juu (Specialities na Super-specialities) zenye umuhimu mkubwa katika Hospitali za Kitaifa (kama Cardiology, Nephrology,Opthalmology,Radiography na Oncology) ili kujenga uwezo wa ndani ya nchi katika jitihada za kupunguza wagonjwa wa rufaa wanaotibiwa nje ya nchi.


Aidha, mwombaji atatakiwa aambatanishe nyaraka zifuatazo wakati wa kufanya maombi:
Barua ya ruhusa ya masomo kutoka kwa mwajiri wake
Barua ya udahili kutoka chuoni
Cheti cha taaluma
Cheti cha kuzaliwa



Mwisho wa kupokea maombi haya ni tarehe  10/11/2018.  

Imetolewa na:

Katibu Mkuu,
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Chuo Kikuu Dodoma,
Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Maendeleo ya Jamii
S.L.P 743
DODOMA
11/10/20




Wizara ya Afya kwa Alhamisi, Oktoba 11, 2018
Shiriki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

‹
›
Nyumbani
Ona toleo la wavuti
Inaendeshwa na Blogger.

Kunihusu

Wizara ya Afya
Tazama wasifu wangu kamili