Muuguzi Mkuu - Hospital ya Rufaa ya Mkoa- Amana,Beauty Mwambebule akitoa maelezo kwa wageni kutoka nchi ya Bangladesh namna mfumo wa KAIZEN unavyofanya kazi katika Hospital hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Hospitali za Rufaa za Mikoa kutoka Wizara ya Afya -Idara ya Tiba -Kitengo cha Uratibu wa Hospitali za Rufaa za Mikoa,Dkt. Angelina Clarisa Sijaona (kushoto) akiwa na wageni kutoka nchi ya Bangladesh akiwaonesha mambo mbalimbali yanayo tumika kwenye mfumo wa KAIZEN katika Hospital Amana jijini Dar es Salaam.
Wangeni kutoka Bangladesh wakiwa katika Hospital ya Amana iliyopo Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam
Na.WAMJW,Dsm
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Mradi wa Kuimarisha Hospitali za Rufaa za Mikoa (RRHMP) katika kuendelea kuziwezesha Hospitali za Rufaa za Mikoa ilipanga kukaribisha wageni kutoka katika nchi mbalimbali za Afrika ili kubadilishana uwezo katika utekelezaji wa 5S-KAIZEN katika kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini.
Kulingana na mpango kazi wa mwaka huu, Mradi ukishirikiana na Wizara ya Afya ulitarajia kupokea wageni kutoka Wizara ya Afya na watumishi wa sekta hiyo kutoka nchini Ghana (7) na Bangladesh (7) kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya Falsafa ya 5S-KAIZEN-TQM pamoja na wawakilishi wa JICA wawili kutoka kila nchi. Pamoja na hao, tulitegemea kupokea watumishi wa Afya 14 kutoka nchi za kiafrika zikiwemo Uganda, Kenya, Malawi, Liberia, Siera Leoni, Sudan, Zambia, Zimbabwe na Benin.
Tayari wageni wote hawa waliishafika na kupata mafunzo kutoka haya.
Wiki hii, tumewapokea wageni kutoka Katika Wizara ya Afya na watumishi 7 wa sekta na wawakilishi wawili wa JICA-Bangladesh. Wageni hawa watakuwepo hapa nchini kwa wiki moja Katika kipindi hicho watapata mafunzo ya KAIZEN na leo wametembelea Hospitali za Rufaa ya Mkoa Amana na kesho wanategemewa kutembelea Hospitali za Taifa Muhimbili.
Lengo la ziara hii ni kubadilishana uzoefu katika utekelezaji wa 5S-KAIZEN-TQM katika hospitali zetu kwa ajili ya kujifunza na kuiga mazuri ya kujifunza watakaporejea nchini kwao. Aidha, Timu zetu zinategemewa kupata nafasi ya kupata uzoefu kutoka kwa nchi zinazotutembelea.
Falsafa ya 5S-KAIZEN-TQM hii inalenga kuboresha mazingira ya kutoa huduma za afya na kukidhi mahitaji ya wateja wetu, wale wa ndani na wa nje.
Kwa ujumla wake, falsafa ya 5S-KAIZEN-TQM hii inarahisha kazi, inahakikisha usalama kwa wateja wa ndani na nje na inapunguza upotevu wa rasilimali, napunguza makosa na inapunguza gharama za uendeshaji.
Kwa Hospitali za Rufaa za Mikoa ambayo wanaitimia falsafa hii wameweza kufanya vizuri katika kutoa huduma bora, kuongeza katika mapato na wafanyakazi kufurahia mazingira yao ya kazi.
Ni falsafa inayoweza kutumika katika maeneo mbalimbali pamoja na viwandani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni