Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe akipima msukumo wa damu katika Zahanati ya Makole Jijini Dodoma, baada ya kuzindua mradi wa Healthy Heart Africa (HHA) unaoratibiwa na AstraZeneca katika Mikoa ya Dodoma na Dar es salaam.
Wananchi walioshiriki tukio la uzinduzi wa mradi wa Healthy Heart Africa (HHA) unaoratibiwa na AstraZeneca katika Mikoa ya Dodoma na Dar es salaam, wakifuatilia kwa makini neno kutoka kwa Mganga Mkuu wa Serikali aliyeongoza zoezi la uzinduzi wa mradi huo
Picha ya pamoja ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe.
ASILIMIA 26 YA WATU WAZIMA WANASHINIKIZO LA JUU LA DAMU.
Na Rayson Mwaisemba WAF- DOM.
MGANGA Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe amebainisha kuwa asilimia 26 ya watu wazima wenye umri wa miaka kati ya 25 hadi 64 wana shinikizo la juu la damu, hali inayosababishwa na mtindo wa maisha ikiwemo ulaji wa vyakula vya mafuta mengi, matumizi ya pombe kupita kiasi na kutofanya mazoezi.
Dkt. Sichalwe amebainisha hayo leo Aprili 13, 2022 wakati akifungua Mradi wa Healthy Heart Africa tukio lililofanyika katika zahanati ya Makole Jijini Dodoma.
"Tumefanya utafiti mwaka 2012 na kukagundua kwamba asilimia 26 ya watu wazima kati ya miaka 25 na 64 wana shinikizo la juu la damu na tatizo hili linatarajia kuongezeka kwa kiasi kikubwa endapo hatutachukua hatua." Amesema Dkt. Sichalwe.
Aliendelea kusema kuwa, tafiti zinaonesha kuwa, zaidi ya asilimia 75% ya Wagonjwa hao wenye shinikizo la juu la damu hawatumii tiba yoyote, huku akiweka wazi kuwa zaidi ya robo tatu kati yao hawajui kama wana shinikizo la juu la damu.
Aidha, Dkt. Sichalwe amesema kuwa, taarifa za utafiti zilizofanywa katika baadhi ya hospitali za Rufaa zimebaini kuwa, wastani wa watu 19 katika kila watu 100 wanaolazwa kwa tatizo la shinikizo la juu la damu hufariki Dunia.
Sambamba na hilo, ameweka wazi kuwa, hali ni mbaya zaidi kwa wagonjwa wa kiharusi, ambapo katika kila watu 100 wanaolazwa, watu 39 wanafariki kwa tatizo hilo la shinikizo la juu la damu, hivyo Serikali kupitia Wizara ya Afya itaendelea kutoa elimu na kuhamasisha jamii ili kuongeza nguvu za kupambano dhidi ya ugonjwa huo.
Mbali na hayo Dkt. Sichalwe ameendelea kusisitiza juu ya kuzingatia utoaji huduma za afya kwa kufuata miongozo, huku akisisitiza weledi na umahiri wakati wa kutoa huduma ili kuepusha malalamiko yanayoweza kuzuilika kutoka kwa wananchi.
Naye, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashid Mfaume amewashukuru Wadau wa PATH kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo ugonjwa wa Shinikizo la juu la damu.
Amesema, Ukuaji wa miji, Maendeleo ya Sayansi na teknolojia na mabadiliko ya mtindo wa maisha kwa kiasi kikubwa yanaendana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo ugonjwa wa shinikizo la juu la damu, hivyo kuwaomba Wadau kuendelea kushirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya magonjwa hayo hasa katika miji inayoendelea kwa kasi ikiwemo Dodoma, Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya.
Mpango wa Healthy Heart Africa (HHA) ni mpango wa miaka miwili unaoratibiwa na AstraZeneca katika Mkoa wa Dodoma (HF 13) na Dar es salaam (HF 22), na unajumuisha jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 35 (zahanati 25 na hospitali 10). Mradi huu unashughulikia magonjwa ya moyo na mishipa, haswa Shinikizo la damu (HTN).
Mwisho.
Thanks for sharing the information. High blood pressure, or hypertension, increases the risk of heart disease, stroke, and other health problems. Lifestyle changes such as diet, exercise, and medication are often recommended for managing it. This statistic highlights the widespread nature of the issue and the importance of monitoring and controlling blood pressure for better health outcomes.
JibuFutabland county va speeding ticket
can a reckless driving charge be expunged in virginia