Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumamosi, 25 Mei 2019

WALIMU WA SHULE YA MAALUM YA WASIOONA WAPATIWA MAFUNZO YA HEDHI SALAMA

- Hakuna maoni
Washiriki wa mafunzo ya hedhi salama kwa watoto wa kike na makundi maalum ya walemavu wakiwa katika majadiliano wakati wakiendelea na mafunzo hayo katika Shule maalum ya watoto wasioona ya Bwigiri iliyopo Wilayani Chamwino


Baadhi ya washiriki wasioona wanaohudhuria mafunzo ya hedhi salama kwa watoto wa kike na makundi maalum ya walemavu, mafunzo hayo yanaendeshwa na Shirika la Kimataifa la Water Supplies Corraboration Council katika Wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma.
Baadhi wa washiriki wa mafunzo ya hedhi salama wakifuatilia mada iliyokua ikiendelea katika Shule maalum ya watoto wasioona ya Bwigiri iliyopo Wilayani Chamwino Jijini Dodoma.


Na.WAMJW, Chamwino

Jamii imetakiwa kuchukua hatua ikiwemo ya kutoa elimu sahihi katika makundi mbalimbali ikiwemo ya walemavu wa aina zote hususan  wasioona.

Hayo yamesemwa leo  na muelimishaji mwandamizi  wa  masuala ya hedhi salama Bi.Dhahia Mbaga kutoka shirika la kimataifa la Water Suppliers Sanitation Corraborative Council wakati wa mafunzo kwa walimu na walezi wa shule maalum ya watoto wasioona ya Buigiri iliyopo wilayani hapa katika kuelekea maadhimisho ya siku ya hedhi salama duniani.

Bi.Mongi amesema malengo ya mafunzo hayo ni kuongeza maarifa  na kuweka mazingira rafiki kwenye vyoo ambapo vinatakiwa kuwa na usafi, maji yanayotirirka pamoja na chumba maalumu kwa ajili ya watoto wanaopevuka kwa kubadilisha vifaa vya hedhi.

Aidha, amesema  katika chumba maalum kunatakiwa kuwe na sanduku la huduma ya kwanza ambayo itakua na dawa za kutuliza maumivu pindi wanapopata maumivu kutokana na hedhi.
Pia Bi Mbaga amesema wanaokuwa na maumivu makali wanatakiwa  wapelekwe kwenye kituo cha huduma za afya kupata matibabu.

Hata hivyo aliongeza kuwa kufika katika shule hiyo ni pamoja na kuibua changamoto za hedhi salama kwani ni nyingi.

” kwani tunapokuwa na watoto waliopevuka na wenye ulemavu kunakuwa na changamoto nyingi zikiwemo za kuwa na vyoo vyenye kuwawezesha walemavu wa macho ambapo kuna ujenzi maalumu ambayo imeanishwa kwenye miongozo ya kitaifa ya shule kwenye masuala ya maji na masuala ya mazingira”. Alisisitiza Mbaga.

Vilevile alisema mafunzo katika shule hiyo watawafundisha walimu na wanafunzi kuweza kutengeneza taulo za kike kwa kutumia vifaa ambavyo vinapatikana katika eneo hilo na kwa bei rahisi.

Kwa upande wa unyanyapaa muelimishaji huyo alisema kuwa linakuja kutokuwa na taarifa sahihi hususani kwa wanaume kwani wanapaswa kujua ni jambo la kawaida na wapo baadhi ya wanaume hawana taarifa sahihi kwani na wanaume nao wanapevuka kwahiyo hayo ni mabadiliko ambayo hayawezi kuzuiliwa.

Maadhimisho ya siku ya hedhi salama duniani mwaka huu kitaifa yanatarajiwa kufanyika jijini Dodoma tarehe 28 mwezi Mei na kauli mbiu ya maadhimisho hayo “Ni wakati wa kuchukua hatua ili kuhakikisha hedhi salama kwa msichana/mwanamke”.

-Mwisho-

Alhamisi, 23 Mei 2019

MKUTANO WA WATAALAMU WA TEHAMA WIZARA YA AFYA NA TAASISI ZAKE WAFUNGULIWA

- Hakuna maoni
Mkurugenzi wa Sera na Mipango ambae pia ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Bw. Edward Mbanga akifungua Mkutano wa Wataalamu wa TEHAMA (ICT) wa Wizara ya Afya na Taasisi zake pamoja na Hospitali za Mikoa na Mabalaza ya kitaaluma uliofanyika leo Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Sera na Mipango ambae pia ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Bw. Edward Mbanga akisema jambo mbele ya Maofisa TEHAMA kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake pamoja na Hospitali za Mikoa na Mabalaza ya kitaaluma katika kikao cha siku mbili kilichofanyika jijini Dodoma ili kujadili changamoto na mapendekezo ili kuboresha utendaji kazi wao. Kushoto kwake ni Mkurugenzi anaesimamia viwango, usalama na miongozo ya TEHAMA (EGA) Bw. Moses Makoko na kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA Wizara ya Afya Bw. Walter Ndesanjo.

Mkurugenzi anaesimamia viwango, usalama na miongozo ya TEHAMA (EGA) Bw. Moses Makoko akiwasilisha mada mbele ya jopo la Wataalamu wa masuala ya TEHAMA (ICT) kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake pamoja na Hospitali za Mikoa na Mabalaza ya kitaaluma katika kikao cha siku mbili kilichofanyika jijini Dodoma ili kujadili changamoto na mapendekezo ili kuboresha utendaji kazi wao.

Jopo la Wataalamu wa masuala ya TEHAMA (ICT) kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake pamoja na Hospitali za Mikoa na Mabalaza ya kitaaluma wakifuatilia kwa karibu ujumbe kutoka Mkurugenzi anaesimamia viwango, usalama na miongozo ya TEHAMA (EGA) Bw. Moses Makoko 

Picha mbali mbali za Maofisa TEHAMA wakifuatilia kwa makini mada iliyotolewa na Mkurugenzi anaesimamia viwango, usalama na miongozo ya TEHAMA (EGA) Bw. Moses Makoko katika kikao cha siku mbili kilichofanyika jijini Dodoma ili kujadili changamoto na mapendekezo ili kuboresha utendaji kazi wao.

Jopo la Wataalamu wa masuala ya TEHAMA (ICT) kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake pamoja na Hospitali za Mikoa na Mabalaza ya kitaaluma wakifuatilia kwa karibu ujumbe kutoka kwa Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Sera na Mipango ambae pia ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Bw. Edward Mbanga

Picha ya pamoja ikiongozwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya ambae pia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Edward Mbanga baada ya kufungua kikao cha siku mbili cha Maofisa TEHAMA (ICT) kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake pamoja na Hospitali za Mikoa na Mabalaza ya kitaaluma kilichofanyika jijini Dodoma ili kujadili changamoto na mapendekezo ili kuboresha utendaji kazi wao.Na WAMJW- DOM

Mkutano wa siku mbili wa  Maafisa TEHAMA (ICT) kutoka wa Wizara ya Afya naTaasisi zake pamoja na Hospitali za Mikoa na Mabalaza ya kitaaluma umefunguliwa leo na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Edward Mbanga Jijini Dodoma.

Lengo la Mkutano huo ni kupitia miongozo ya matumizi sahihi ya TEHAMA Serikalini ili kuongeza ufanisi wenye tija katika matumizi ya TEHAMA utaosaidia kuboresha utoaji huduma katika Sekta ya Afya nchini.

Mbali na hayo kikao hicho kimelenga kupitia mbali mbali wanazokumbana nazo Wataalamu hao katika utoaji huduma na kutoa mapendekezo ya kutatua changamoto hizo ili kuboresha utendaji wao katika Sekta ya Afya.

Hata hivyo kikao hicho kilichowakutanisha Wataalau wa masuala ya TEHAMA kimekusudia  kujenga uelewa wa pamoja baina ya Wataalamu hao hususan katika masuala ya Sera, Sheria, Kanuni, Miongozo na matumizi sahihi ya TEHAMA Serikalini.

Kwa upande mwingine Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya ambae pia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Edward Mbanga amepongeza uwepo wa mkutano huo jambo litalosaidia kuiboresha zaidi taaluma hiyo, hovyo kuahidi kumwalika Afisa Mwandamizi wa Idara ya Utawala ataesikiliza na kutatua changamoto zinazowakumba.Mwisho.

MAPINDUZI KATIKA SEKTA YA AFYA KUPITIA MIFUMO

- Hakuna maoni
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na Taasisi isiyo ya kiserikali( Path) inaendelea na vikao vyenye lengo la kuandaa mpango (blue print) utaoelezea namna gani mifumo itasaidia kuboresha huduma katika Sekta ya Afya nchini.

Katika kikao hicho jumla ya kamati ndogo ndogo sita ziliundwa lengo ni kuhorodhesha Wadau muhimu katika kila kamati hizo wataosaidia katika kutatua changamoto katika maeneo ya Sekta ya Afya. 

Pamoja na hayo, kamati hizo zimejadili juu changamoto zinazoikumba Sekta ya Afya katika kila kamati zilizoundwa na namna ya kukabiliana na changamoto hizo ili kufikia malengo ya kutoa huduma za Afya zilizo bora kwa kila Mtanzania.

Wizara ya Afya,  TAMISEMI na Pathinatekeleza mradi wa "Matumizi ya takwimu za Afya (Data Use Partnership)" chini ya ufadhili wa Taasisi ya Bill and Melinda Gate Foundation ili kuboresha huduma za Afya nchini. 


Kikao cha Maandalizi ya EA kikiendelea Mkoani Morogoro.


Na WAMJW- Morogoro

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na Taasisi isiyo ya kiserikali( Path) inaendelea na vikao vyenye lengo la kuandaa mpango (blue print) utaoelezea namna gani mifumo itasaidia kuboresha huduma katika Sekta ya Afya nchini.

Katika kikao hicho jumla ya kamati ndogo ndogo sita ziliundwa lengo ni kuhorodhesha Wadau muhimu katika kila kamati hizo wataosaidia katika kutatua changamoto katika maeneo ya Sekta ya Afya.

Pamoja na hayo, kamati hizo zimejadili juu changamoto zinazoikumba Sekta ya Afya katika kila kamati zilizoundwa na namna ya kukabiliana na changamoto hizo ili kufikia malengo ya kutoa huduma za Afya zilizo bora kwa kila Mtanzania.

Wizara ya Afya,  TAMISEMI na Pathinatekeleza mradi wa "Matumizi ya takwimu za Afya (Data Use Partnership)" chini ya ufadhili wa Taasisi ya Bill and Melinda Gate Foundation ili kuboresha huduma za Afya nchini.

#tunaboreshaafya
#DUP
#DigitalForHealth

Ijumaa, 17 Mei 2019

SERIKALI YAIMARISHA UPATIKANAJI WA VIPIMO VYA UGONJWA WA DENGUE

- Hakuna maoni
Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Mohammad Bakari Kambi akizungumza jambo kuhusu ugonjwa dengue na waandishi wa habari (hawapo pichani).

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Dkt. Yudas Ndungile akizungumza jambo na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Picha ya pamoja Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohhamad Bakari Kambi (meza kuu) akizungumza na waandishi wa habari.


Na WAMJW - DSM


Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea kuimarisha upatikanaji wa vipimo vya ugonjwa wa Degue kwa kununua vipimo 30,000 kwa ajili ya kupima ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohhamad Bakari Kambi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mapema leo katika ofizi ndogo za Wizara Jijini Dar Es Salaam.

Prof. Kambi amesema kuwa vipimo hivyo tayari vimeshanunuliwa na vitaingia nchini hivi karibuni na kusambazwa kwenye vituo vya umma JIjini Dar Es Salaam pamoja na mikoa mingine yenye athari za ugonjwa huo.

Amesema kuwa ugonjwa wa dengue hauna chanjo wala tiba ya moja kwa moja na kuwataka wananchi kuacha kutoa taarifa za upotoshaji kuhusu tiba za ugonjwa huo.

“Niwakumbushe tena wananchi kinga ni bora kuliko tiba, jikinge na ugonwja huu wewe mwenyewe, kaya na familia yako pamoja na jamii kwa ujumla” amesema Prof. Kambi.

Mganga Mkuu amesema kuwa mpaka sasa vituo vinavyopima ugonjwa wa homa ya Dengue katika Mkoa wa Dar es Salaam ni Muhimbili, Maabara kuu Muhimbili, Amana, Temeke, Mwananyamala, Sinza, Vijibweni, Mnazi mmoja, Lugalo, Mbagala, FFU Ukonga. Katika mkoa wa Tanga; vituo vya Bombo na Horohoro, vituo vingine ni Tumbi Mkuranga, Utete Rufiji na Mafia, Morogoro na Manyara Aidha natambua vipo pia vituo binafsi vinavyotoa huduma za upimaji. Katika mikoa mingine ufuatiliaji unaendelea na hatujapa wagonjwa wenye dalili za Homa ya Dengue.

Aidha Prof. Kambi amesema kuwa Wizara inatambua juhudi zinazofanywa na Mkoa wa Dar Es Salaam na kuwapongeza kwa kazi kubwa wanayofanya ya udhibitiwa ugonjwa huo kupitia zoezi la kunyunyizia dawa viuadudu (Biolarvicides) kwa ajili ya kuangamiza mazalia ya mbu sambamba na elimu ya kujikinga dhidi ya ugonjwa huo.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Dkt. Yudas Ndungile Amesema kuwa idadi kubwa ya wagonjwa wanaojitokeza katika vituo vya afya kupata vipimo ni kutokana na wananchi kupata uelewa wa ugonjwa huo baada ya kupatiwa elimu dhidi ya ugonjwa huo.

“Tumepita kwenye maeneo ya kata zenu kufanya ueleimishaji wa namna ya kujikinga na kutambua dalili za ugonjwa huu” amesema Dkt. Ndungile na kuendelea kusema kuwa vyombo vya habari vimetoa mchango mkubwa katika kuelimisha wananchi dhidi ya ugonjwa wa dengue.

Aidha Dkt. Ndungile amesema kuwa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya wameweza kuandaa vituo vya upimaji wa homa ya dengue ambapo huduma za upimaji zinatolewa bure.

Mwisho

Ijumaa, 10 Mei 2019

WAANDISHI WA HABARI WAELIMISHWA KUHUSU USALAMA WA BARABARANI

- Hakuna maoni
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge katika Usalama Barabarani Mhe. Adad Rajab (kushoto) akigawa vitendea kazi kwa mwandishi wa habari wakati wa mafunzo ya usalama barabarani kwa waandishi wa habari Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge katika Usalama wa Barabarani nchini Mheshimiwa. Adad Rajab (Mbunge wa JImbo la Muheza) akisema jambo kwa washiriki wa mafuzo ya usalama barabarani kwa waandishi wa habari yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Tingest Mengenstu akiwasilisha hotuba yake wakati wa mafunzo ya Usalama wa Barabarani kwa waandishi wa habari yaliyofanyika  Jijini Dodoma.
 
Maafisa wa Polisi wakisikiza mada zinazoendelea katika mafunzo ya Usalama wa Barabarani kwa waandishi wa habari , Jijini Dodoma.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma Afande. Nuru Selemani Akizungumza jambo na washiriki wa mafunzo ya Usalama Barabarani (hawapo pichani) yaliyofanyika Jijini Dodoma.
icha ya washiriki wa mafunzo ya Usalama wa Barabarani kwa waandishi wa habari.
Na. WAMJW – Dodoma.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Shirikia la Afya Duniani (WHO) wamefungua rasmi programu ya mafunzo ya usalama barabarani kwa waandishi wa habari katika jitihada za kuelimisha jamii juu ya usalama wa barabarani na kuepuka ajali nchini.

Mafunzo hayo ambayo yamefunguliwa rasmi na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge katika Usalama Barabarani nchini Mheshimiwa Adad Rajab (Mbunge wa Jimbo la Muheza) yanaenda sambamba na maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Mei 6 – 12 kila mwaka huku kwa mwaka huu yakiwa na kauli mbiu “Uongozi kwa usalama wa barabarani”

“Mafunzo hayo yana umuhimu kwa waandishi ili kuwawezesha kupasha habari za ajali barabarani  na kupunguza ajali hizo nchini” alisema Mhe. Adad.

Naye Mwakilishi Mkazi wa WHO nchini Tanzania Dkt. Tingest Mengestu amesema kuwa vifo vitonakavyo na ajali badoni tishio nchini na duniaini kwa ujumla huku akiiomba Serikali kuweka juhudi madhubuti juu ya suala hilo.

“Licha ya hatua mbalimbali ambazo zimechukuliwa, bado vifo vitokanavyo na ajali barabarani vimeendelea kuongezeka, takwimu zinaonyesha Duniani kwa mwaka kuna vifo milioni 1.35 vinavyosababishwa na ajali” amesema Dkt. Mengestu.

Akaendelea kwa kusema kuwa ajali za barabarani sasa ndizo zinazoongoza kusababisha vifo vya watu wenye umri mdogo huku akitaja waathirika zaidi ni kundi la wenye umri wa miaka 5 – 29.

Dkt. Mengestu amesema kuwa ulimwenguni, vifo vinavyotokana na ajali za barabarani, kwa upande wa watembea kwa miguu na waendesha baiskeli vimefikia asilimia 26 na kwa waendesha pikipiki pamoja na abiria vimefikia asilimia 28.

Hatari ya vifo vitonakavyo na ajali za barabarani imeendelea kuwa juu mara tatu zaidi katika nchi zenye kipato cha chini. Huku takwimu zikionyesha Bara la Afrika kuwa na ongezeko kubwa la ajali (Asilimia 26.6 kati ya watu 100,000), na Bara la Ulaya likiwa chini kwa nchi za (Asilimia 9.3 kati ya watu 100,000)

Akizungumzia takwimu za ajali za barabarani kwa Mkoa wa Dodoma, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani humo Afande Nuru Selemani amesema kwa mwaka 2018 ajali za barabarani zilikuwa 350 zilizohusisha magari 155 na pikipiki 195, huku kwa mwaka huu ajali zilizotokea mpaka sasa zikiwa ni 75.

Afande Selemani amesema kuwa Kikosi cha Trafiki Polisi kimejipanga kuhakikisha Sheria za Usalama Barabarani zinafuatwa ili kupunguza ajali za barabani nchini na wale ambao watakuwa wamehusika kwa uzembe na kusababisha ajali wanachukuliwa hatua madhubuti.

“Kupitia mafunzo haya tunaamini tunaweza kushirikaina vizuri na waandishi wa habari ili kuweza kupaza sauti na kuwaelimisha na kuwakumbusha watumiaji wa barabara kuzingatia Sheria za usalama barabarani na kuweza  kupunguza ajali za barabarani” alisema Afande Sulemani.

Alhamisi, 9 Mei 2019

TAHADHARI YA HOMA YA DENGUE YAZIDI KUTOLEWA

- Hakuna maoni
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Kambi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kuwepo kuendelea kuwepo kwa ugonjwa wa Homa ya Dengue nchini.

Baadhi ya waandishi wa habari waliojitokeza kusikiliza tamko la kuhusu kuwepo kwa ugonjwa wa Homa ya Dengue nchini wakati likitolewa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Kambi Jijini Dodoma.


NA WAJMW-DODOMA

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imezidi kutoa tahadhari ya  kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya Dengue nchini hususani katika Jiji la Dar Es Salaam na Tanga.

Tahadhari hiyo imetolewa leo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Kambi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za wizara hiyo zilizoko jijini Dodoma.

Prof. kambi amesema hadi kufikia tarehe 6 Mei 2019, kati ya watu waliopimwa, wagonjwa 1237 wamethibitishwa kuwa na virusi au walikwishapata ugonjwa wa Dengue na kati yao 1150 ni kutoka Dar Es Salaam, 86 ni kutoka Tanga na mtu mmoja kutoka Singida.

Aidha, Prof Kambi amesema takwimu za ugonjwa wa Dengue kwa kipindi cha Januari hadi Aprili 2019 zinaonesha mwenendo wa ugonjwa huu kuwa na idadi ya wagonjwa 1237, vifo vya watu wawili na kuongeza kuwa waliofariki walikua na maradhi mengine.

Pamoja na hayo Mganga Mkuu huyo wa Serikali amelipongeza jiji la Dar Es Salaam kwa kuanza kunyunyizia dawa viuadudu (Biolarvicides) kwa ajili ya kuangamiza mazalia ya mbu ili kupambana na ugonjwa huu.

Vile vile amesema Wizara inaelekeza Mikoa na Halmashauri zote nchini kuendelea kuchukua hatua katika kudhibiti ugonjwa huu ikiwa ni pamoja na kufukia madimbwi ya maji, kunyunyizia dawa ya kuua viluwiluwi, kuondoa vitu vinavyosababisha mazalia ya mbu, kufyeka vichaka, kufunika mashimo ya maji taka kwa mifuniko pamoja kusafisha gata za paa la nyumba na kutoruhusu maji kusimama.

Prof. Kambi amesema Wizara kwa kushirikiana na Mikoa na Halmashauri zote nchini itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kudhibiti ugonjwa huu ikiwa ni pamoja na kuendelea kuangamiza mazalia ya mbu na viluwiluwi, kuweka mpango wa dharura wa miezi sita kuanzia Mei mpaka Oktoba ili kukabiliana na ugonjwa huu. Pia amesema Serikali imenunua Vitendanishi vyenye uwezo wa kupima wagonjwa 1870 na vimesambazwa kwenye vituo maalum vya ufuatiliaji wa ugonjwa huu nchini kote.

Mwisho Prof. Kambi amewataka wananchi kuendelea kuchukua hatua za kujikinga kuumwa na mbu kwa kuvaa nguo ndefu, kutumia vyandarua vyenye viuatilifu, kutumia dawa za kufukuza mbu na kuweka nyavu kwenye madirisha na milango ya nyumba za kuishi ili kukabiliana na ugonjwa huu.

MWISHO

Jumatano, 8 Mei 2019

HOTUBA YA WAZIRI UMMY MWALIMU KUHUSU MAKADIRIO YA BAJETI YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2019-2020

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Ally Mwalimu akiwasilisha makadirio ya Bajeti ya Wizara yake katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mei, 07, 2019 Jijini Dodoma.

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akijibu hoja za wabunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mei 07, 2019.


Jumatatu, 6 Mei 2019

DKT. NDUGULILE ATOA RAI KWA VIONGOZI WA KISIASA KUTOINGILIA KAZI ZA TAALUMA YA AFYA

- Hakuna maoni

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (kulia ) akiangalia baadhi ya vitabu vinvyotuika kutoa elimu kwa wananchi wakati alipotembelea banda la maonesho la Shirika lisio la kiserikali la AGPAHI, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (kulia ) akipokea maelezo kutoka kwa mmoja wa wakunga ya namna wanavyowahudumia wakina mama wajawazito na watoto wakati alipotembelea Banda la Chama cha Wakunga Tanzania(TAMA),  katika Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa katika Uwanja wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Baadhi ya wakunga wakiwa katika maandamano wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akimkabidhi mmoja wa kunga wa moa wa Simiyu cheti kama zawadi ya kufanyakazi nzuri, katika Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.


Na WAMJW - Simiyu
 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile ametoa rai kwa viongozi wa Kisiasa hapa nchini kuacha kuingilia kazi za Kitaaluma katika sekta ya Afya na kuwaomba wawaache wataalam wafanye kazi zao kwa misingi na miiko ya Kitaaluma inayowaongoza.

Dkt. Ndugulile ameyasema hayo katika Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, chini ya Kauli Mbiu “Wakunga Watetezi wa Haki za Wanawake”, ambapo alikuwa akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Amesema hivi karibuni kumekuwa na matamko yanayotolewa na baadhi ya viongozi wa kisiasa yanayowakatisha tamaa watumishi wa sekta ya afya na baadhi ya viongozi wameanza kuingilia masuala ya kitaalum, hivyo akawaomba ikiwa viongozi hao  watakutana na changamoto za watendaji wa afya waishirikishe wizara ya afya ili wachukuliwe  hatua kwa mujibu wa taaluma zao.

“Niwaombe sana viongozi wa Serikali na Viongozi wa vyama, masuala ya kitaaluma yanashughulikiwa kitaaluma kama kuna changamoto na wanataaluma ndiyo maana tuna mabaraza ya taaluma na ndiyo maana sisi wizara tupo mtushirikishe, nimelisema hili kwa sababu nimeona sekta imeanza kuingiliwa” alisema Dkt. Ndugulile.

Aidha, Dkt. Faustine Ndugulile amewataka wakunga hapa nchini kuendelea kuzingatia miiko na misingi ya taaluma yao katika huduma wanazotoa kwa jamii na kuahidi kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua wale wote watakaokiuka misingi hiyo kwa kuwa jamii inahitaji heshimu, utu, upendo na kutiwa moyo

Katika hatua nyingine Dkt. Ndugulile ametoa wito kwa  wadau mbalimbali wa maendeleo na jamii kwa ujumla kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha huduma za afya ili changamoto ya vifo vitokanavyo na uzazi vibaki kuwa historia ambapo amesema kwa sasa wanawake 11,000 wanakufa kila mwaka kutokana na uzazi.

Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania, Bibi. Feddy Mwanga ameiomba Serikali kuongeza idadi ya wakunga ili mkunga aweze kutoa huduma kwa kiwango kinachokubalika Kitaifa na kimataifa huku akisisitiza Serikali kuona haja ya kujenga nyumba za wakunga katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya vinavyoboreshwa na vinavyojengwa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthoy Mtaka amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa shilingi bilioni saba  fedha kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na shilingi bilioni 4.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali tatu za Wilaya Bariadi, Busega na Itilima ambazo ujenzi wake unaendelea vizuri.

Aidha, Kiswaga ameshukuru Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNPFA) kwa namna linavyoshirikiana na Serikali mkoani Smiyu kwa kukarabati baadhi ya vituo, kununuaa vifaa mbalimmbali, kutoa mafunzo kwa wakunga jitihada ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

Akitoa taarifa ya Mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema
Idadi ya wakunga katika vituo vya kutolea huduma za afya Simiyu imeongezeka hali iliyofanya wajawazito wengi kujifungulia katika vituo vya afya kutoka asilimia 62 mpaka asilimia 68, hivyo vifo vya mama wajawazito vimepungua kutoka vifo 48 mwaka 2017 mpaka vifo 40 mwaka 2018.

Naye Makamu Mwakilishi Mkaazi wa UNFPA hapa nchini, Dkt.Hashina Begum amesema kwa kushirikiana na Chama cha Wakunga nchini (TAMA) limetoa mafunzo kwa wakunga 90 kutoka katika vituo vilivyoboreshwa ili kuwasaidia wakina mama wajawazito na watoto kupata huduma za dharura na kupunguza vifo kwa mama na mtoto vitokanavyo na uzazi.  

Grace Magengeni Mkunga kutoka Jijini Dodoma amesema” siku yetu imefana tunashukuru hotuba ya Naibu Waziri imetutia moyo katika kuwahudumia wanawake na watoto, nawashauri wenzangu tusimamie taaluma zetu tufanye kazi kwa bidii naamini hao wanaotuingilia majukumu yetu wataachaa maana ni kweli,  tunashukuru Naibu Waziri kulisemea hili suala”

Mwisho