Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Ijumaa, 10 Mei 2019

WAANDISHI WA HABARI WAELIMISHWA KUHUSU USALAMA WA BARABARANI

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge katika Usalama Barabarani Mhe. Adad Rajab (kushoto) akigawa vitendea kazi kwa mwandishi wa habari wakati wa mafunzo ya usalama barabarani kwa waandishi wa habari Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge katika Usalama wa Barabarani nchini Mheshimiwa. Adad Rajab (Mbunge wa JImbo la Muheza) akisema jambo kwa washiriki wa mafuzo ya usalama barabarani kwa waandishi wa habari yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Tingest Mengenstu akiwasilisha hotuba yake wakati wa mafunzo ya Usalama wa Barabarani kwa waandishi wa habari yaliyofanyika  Jijini Dodoma.
 
Maafisa wa Polisi wakisikiza mada zinazoendelea katika mafunzo ya Usalama wa Barabarani kwa waandishi wa habari , Jijini Dodoma.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma Afande. Nuru Selemani Akizungumza jambo na washiriki wa mafunzo ya Usalama Barabarani (hawapo pichani) yaliyofanyika Jijini Dodoma.
icha ya washiriki wa mafunzo ya Usalama wa Barabarani kwa waandishi wa habari.
Na. WAMJW – Dodoma.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Shirikia la Afya Duniani (WHO) wamefungua rasmi programu ya mafunzo ya usalama barabarani kwa waandishi wa habari katika jitihada za kuelimisha jamii juu ya usalama wa barabarani na kuepuka ajali nchini.

Mafunzo hayo ambayo yamefunguliwa rasmi na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge katika Usalama Barabarani nchini Mheshimiwa Adad Rajab (Mbunge wa Jimbo la Muheza) yanaenda sambamba na maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Mei 6 – 12 kila mwaka huku kwa mwaka huu yakiwa na kauli mbiu “Uongozi kwa usalama wa barabarani”

“Mafunzo hayo yana umuhimu kwa waandishi ili kuwawezesha kupasha habari za ajali barabarani  na kupunguza ajali hizo nchini” alisema Mhe. Adad.

Naye Mwakilishi Mkazi wa WHO nchini Tanzania Dkt. Tingest Mengestu amesema kuwa vifo vitonakavyo na ajali badoni tishio nchini na duniaini kwa ujumla huku akiiomba Serikali kuweka juhudi madhubuti juu ya suala hilo.

“Licha ya hatua mbalimbali ambazo zimechukuliwa, bado vifo vitokanavyo na ajali barabarani vimeendelea kuongezeka, takwimu zinaonyesha Duniani kwa mwaka kuna vifo milioni 1.35 vinavyosababishwa na ajali” amesema Dkt. Mengestu.

Akaendelea kwa kusema kuwa ajali za barabarani sasa ndizo zinazoongoza kusababisha vifo vya watu wenye umri mdogo huku akitaja waathirika zaidi ni kundi la wenye umri wa miaka 5 – 29.

Dkt. Mengestu amesema kuwa ulimwenguni, vifo vinavyotokana na ajali za barabarani, kwa upande wa watembea kwa miguu na waendesha baiskeli vimefikia asilimia 26 na kwa waendesha pikipiki pamoja na abiria vimefikia asilimia 28.

Hatari ya vifo vitonakavyo na ajali za barabarani imeendelea kuwa juu mara tatu zaidi katika nchi zenye kipato cha chini. Huku takwimu zikionyesha Bara la Afrika kuwa na ongezeko kubwa la ajali (Asilimia 26.6 kati ya watu 100,000), na Bara la Ulaya likiwa chini kwa nchi za (Asilimia 9.3 kati ya watu 100,000)

Akizungumzia takwimu za ajali za barabarani kwa Mkoa wa Dodoma, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani humo Afande Nuru Selemani amesema kwa mwaka 2018 ajali za barabarani zilikuwa 350 zilizohusisha magari 155 na pikipiki 195, huku kwa mwaka huu ajali zilizotokea mpaka sasa zikiwa ni 75.

Afande Selemani amesema kuwa Kikosi cha Trafiki Polisi kimejipanga kuhakikisha Sheria za Usalama Barabarani zinafuatwa ili kupunguza ajali za barabani nchini na wale ambao watakuwa wamehusika kwa uzembe na kusababisha ajali wanachukuliwa hatua madhubuti.

“Kupitia mafunzo haya tunaamini tunaweza kushirikaina vizuri na waandishi wa habari ili kuweza kupaza sauti na kuwaelimisha na kuwakumbusha watumiaji wa barabara kuzingatia Sheria za usalama barabarani na kuweza  kupunguza ajali za barabarani” alisema Afande Sulemani.

0 on: "WAANDISHI WA HABARI WAELIMISHWA KUHUSU USALAMA WA BARABARANI"