Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Mohammad Bakari Kambi akizungumza jambo
kuhusu ugonjwa dengue na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Picha ya pamoja Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohhamad Bakari Kambi (meza kuu) akizungumza na waandishi wa habari.
Na WAMJW - DSM
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea kuimarisha upatikanaji wa vipimo vya
ugonjwa wa Degue kwa kununua vipimo 30,000 kwa ajili ya kupima ugonjwa
huo.
Hayo yamesemwa na
Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohhamad Bakari Kambi alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari mapema leo katika ofizi ndogo za
Wizara Jijini Dar Es Salaam.
Prof.
Kambi amesema kuwa vipimo hivyo tayari vimeshanunuliwa na vitaingia
nchini hivi karibuni na kusambazwa kwenye vituo vya umma JIjini Dar Es
Salaam pamoja na mikoa mingine yenye athari za ugonjwa huo.
Amesema
kuwa ugonjwa wa dengue hauna chanjo wala tiba ya moja kwa moja na
kuwataka wananchi kuacha kutoa taarifa za upotoshaji kuhusu tiba za
ugonjwa huo.
“Niwakumbushe tena wananchi kinga ni bora kuliko tiba, jikinge na ugonwja huu wewe mwenyewe, kaya na familia yako pamoja na jamii kwa ujumla” amesema Prof. Kambi.
Mganga
Mkuu amesema kuwa mpaka sasa vituo vinavyopima ugonjwa wa homa ya
Dengue katika Mkoa wa Dar es Salaam ni Muhimbili, Maabara kuu Muhimbili,
Amana, Temeke, Mwananyamala, Sinza, Vijibweni, Mnazi mmoja, Lugalo,
Mbagala, FFU Ukonga. Katika mkoa wa Tanga; vituo vya Bombo na Horohoro,
vituo vingine ni Tumbi Mkuranga, Utete Rufiji na Mafia, Morogoro na
Manyara Aidha natambua vipo pia vituo binafsi vinavyotoa huduma za
upimaji. Katika mikoa mingine ufuatiliaji unaendelea na hatujapa
wagonjwa wenye dalili za Homa ya Dengue.
Aidha
Prof. Kambi amesema kuwa Wizara inatambua juhudi zinazofanywa na Mkoa
wa Dar Es Salaam na kuwapongeza kwa kazi kubwa wanayofanya ya udhibitiwa
ugonjwa huo kupitia zoezi la kunyunyizia dawa viuadudu (Biolarvicides)
kwa ajili ya kuangamiza mazalia ya mbu sambamba na elimu ya kujikinga
dhidi ya ugonjwa huo.
Kwa
upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Dkt. Yudas Ndungile
Amesema kuwa idadi kubwa ya wagonjwa wanaojitokeza katika vituo vya afya
kupata vipimo ni kutokana na wananchi kupata uelewa wa ugonjwa huo
baada ya kupatiwa elimu dhidi ya ugonjwa huo.
“Tumepita
kwenye maeneo ya kata zenu kufanya ueleimishaji wa namna ya kujikinga
na kutambua dalili za ugonjwa huu” amesema Dkt. Ndungile na kuendelea
kusema kuwa vyombo vya habari vimetoa mchango mkubwa katika kuelimisha
wananchi dhidi ya ugonjwa wa dengue.
Aidha
Dkt. Ndungile amesema kuwa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya wameweza
kuandaa vituo vya upimaji wa homa ya dengue ambapo huduma za upimaji
zinatolewa bure.
Mwisho
0 on: "SERIKALI YAIMARISHA UPATIKANAJI WA VIPIMO VYA UGONJWA WA DENGUE"