Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumamosi, 29 Septemba 2018

SERIKALI YAWEKA MIKAKATI THABITI YA KUPAMBA DHIDI YA UGONJWA WA MOYO

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongoza Matembezi ya Siku ya Moyo Duniani yaliyoanzia viwanja vya Leaders Club na kumalizikia viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es sala, matembezi hayo yamebeba kauli mbiu ya "Moyo wangu Moyo Wako". Wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma Wizara ya Afya.

Matembezi ya Siku ya Moyo Duniani yakiendelea, ambayo kwa mwaka huu yamebeba kauli mbiu ya 'Moyo wangu, Moyo wako"

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiambatana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma kutoka Wizara ya Afya wakinyoosha viungo baada ya kumaliza matembezi ya Siku ya Moyo Duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akikagua moja kati ya mabanda yaliyokuwepo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam katika maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani. Kushoto kwake ni Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania Dkt. Robert Mvungi, kulia kwake ni Mkurugenzi wa kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma Wizara ya Afya Dkt. Amalberga Kasangala.


SERIKALI YAWEKA MIKAKATI THABITI YA KUPAMBA DHIDI YA UGONJWA WA MOYO

Na WAMJW-Dar es salaam.

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeanza kuweka mikakati thabiti ya kupambana dhidi ya maradhi ya Moyo nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile leo katika maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.

Dkt. Ndugulile alisema kwamba Serikali imeendelea kutoa Elimu kupitia vyombo vya Habari na mitandao ya kijamii, kuanzisha Mpango wa Taifa wa magonjwa yasiyo yakuambukiza, na kuhakikisha TV zote katika Hospitali na Vituo vya Afya zinaonesha jumbe zinazohusu masuala ya Afya tu. 

“Serikali tumeona kwamba tunahitaji kuongeza msukumo kwemnye magonjwa yasiyo yakuambukiza, matamasha tunayofanya ni moja ya mkakati tunaofanya wa kutoa Elimu kwa jamii, kuoa Elimu kupitia njia mbali mbali ikiwemo TV, magazeti, pamoja na mtandao wa jamii, kuanzisha Mpango wa Taifa wa magonjwa yasiyo yakuambukiza, kuelekeza hospitali zote kuonesha jumbe mbali mbali za masuala ya Afya” Alisema Dkt. Ndugulile.

Dkt. Ndugulile alisema kwamba kuna ongezeko kubwa sana la magonjwa yasiyo yakuambukiza ikiwemo maradhi ya Moyo ambayo kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na kutofanya mazoezi, aina ya vyakula tunavyokula, matumizi yaliyopitiliza ya vilevi. 

“Kama taifa tunaona kuna ongezeko kubwa la magonjwa yasiyo yakuambukiza ikiwemo ugonjwa wa Moyo, na visababishi vikubwa ni aina ya vyakula tunavyokula, watu kutofanya mazoezi, matumizi ya pombe na sigara kupita kiasi”, alisema Dkt. Ndugulile.

Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile alisema kuwa Magonjwa ya moyo yanaongoza kwa kusababisha vifo duniani na inakadiriwa kuwa watu 17,500,000 hufa kila mwaka duniani kote kutokana na magonjwa ya moyo na kiharusi. 

Aidha, Dkt Ndugulile alisema kuwa kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaeleza kwamba asilimia 40% ya vifo vyote vinavyotokea duniani vinasababishwa na magonjwa ya moyo huku nusu ya vifo ambavyo vinatokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza vinatokana na magonjwa ya moyo.

Pia, Dkt. Ndugulile alisema kuwa matumizi ya Tumbaku na bidhaa zake yanakadiriwa kusababisha vifo vya watu 6,000,000 duniani kila mwaka na pia huchangia kusababisha asilimia 10% ya wagonjwa wenye magonjwa ya moyo. 

Mbali na Hayo Dkt. Ndugulile alisema kwamba kama hatua madhubuti za kinga, uchunguzi wa mapema na tiba stahiki hazitachukuliwa haraka, tatizo la Moyo ifikapo mwaka 2035 litaongezeka na kufikia makadirio ya wagonjwa wapya milioni 131,978,870 (sawa na ongezeko la 45% kutoka hali ilivyo kwa sasa), huku ongezeko kubwa likiwa katika ukanda wa nchi zinazoendelea, Tanzania ikiwa mojawapo.

Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile alisema kuwa nia thabiti ya Serikali ya Awamu ya tano ni kuboresha huduma za afya hapa nchini ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi vinavyohitajika katika kutoa huduma za afya nchini kwa kuongeza bajeti ya afya kila mwaka. 

“Sisi sote ni mashahidi wa juhudi hizi za Serikali kwa uwepo wa Taasisi ya Magonjwa ya Moyo ya Jakaya Kikwete yenye wataalamu wabobezi katika tiba ya magonjwa ya moyo” Alimaliza Dkt. Ndugulile. 


Ijumaa, 28 Septemba 2018

HUDUMA ZA MRI NA CT SCAN ZAANZA KUTOLEWA MOI.

- Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua Mkono wa Bandia uliotengenezwa katika Taasisi hiyo, Kulia ni Mtaalamu wa viungo Bandia Bw. Deus David.

Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akimsalimia mtoto, aliyefika na mzazi wake kupata matibabu katika Taasisi ya mifupa ya MOI, alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kusimikwa kwa Mitambo ya MRI,CT Scan na X-Ray

Mkuu wa Kitengo cha Fiziotherapia Bw. Lucas Machage akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile, alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kusimikwa kwa Mitambo ya MRI,CT Scan na X-Ray MOI.

Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na mmoja kati ya wanufaika wa Vifaa vya Bandia katika Taasisi ya Mifupa MOI aliowekewa baada ya kukatwa Mkono wake.

Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua Cheti cha moja kati ya Wagonjwa waliofika kupata huduma za Afya katika Taasisi ya Mifupa ya MOI.

Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua moja kati ya mtambo wa kisasa uliosimikwa tayari kuanza kufanya kazi, katika Taasisi ya Mifupa ya MOI, Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Respicious Bonface.

Wataalamu mbali mbali kutoka Taasisi ya Mifupa ya MOI wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kusimikwa kwa Mitambo ya MRI,CT Scan na X-Ray.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua kitabu cha Kusaini Wataalamu wa Maabara, Kushoto ni Muuguzi wa Kitengo cha Dharura MOI Levlin Masama.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiendelea na Ziara katika Taasisi ya Mifupa ya MOI, Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Respicious Bonface.


HUDUMA ZA MRI NA CT SCAN ZAANZA KUTOLEWA MOI.

Na WAMJW-Dar es Salaam.

Huduma za kupima magonjwa mbalimbali kwa kutumia Mashine  za kisasa ya CT Scan na MRI sasa zimeanza kutolewa kwa ufanisi baada ya kusimikwa na kuanza kufanya kazi  katika Hospitali ya Mifupa ya MOI.

Hayo yamesemwa leo na  Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,JiAnsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea  na kukagua hali ya utoaji wa huduma na usimikaji wa mitambo ya kisasa katika kitengo cha radiolojia yenye thamani ya zaidi ya Tsh Bilioni 5.6 Hospitalini hapo .

"Lengo la ziara yangu ni kukagua maendeleo ya usimikaji wa mitambo hii ya kisasa  ya MRI, CT SCAN, Xray, Ultra sound, mitambo mingine , nimeona na kujiridhisha imekamilika kwa asilimia 99% " Alisema Dkt.Ndugulile.

Aidha ,  Dkt. Ndugulile ameuagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha unakamilisha  mambo machache yaliyobaki ndani ya wiki hii ili wiki ijayo wagonjwa waanze kupata huduma hapa.

 Mbali na hayo Dkt Ndugulile ameupongeza uongozi wa MOI kwa kuhakikisha usimikaji wa Mitambao unafanyika kwa wakati na hali ya utoaji huduma ni nzuri na ya kuridhisha kwani wagonjwa wamekuwa wakipata changamoto ya kwenda nje ya MOI kufuata vipimo hivi.

Mbali na hayo Dkt.  Ndugulile amesema ni adhma ya Serikali kuhakikisha huduma zote zinapatikana hapa nchini hivyo ni vyema kama kuna kifaa chochote kinachohitajika taarifa ikatolewa Wizarani ili kifaa hicho kiwekwe kwenye mpango na bajeti na kununuliwa kwani utaalamu na weledi upo wakutosha.

Dkt Ndugulule ametembelea vitengo vya mazoezi tiba pamoja na utengenezaji wa viungo bandia ambapo amekagua na kujiaone hali ya utoaji huduma na kujiridhisha kwamba huduma zimeboreka katika kipindi cha miaka 3 tangu Serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani  na kwa sasa watanzania wanapata huduma kwa wakati licha ya kuwa  kuna changamoto ya ununuzi wa vifaa tiba nje ya nchi.

Akitoa taarifa ya hali ya utoaji huduma na usimikaji wa mitambo hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface amesema kwamba hali ya utoaji wa huduma ni nzuri, wagonjwa wanapata huduma stahiki kwa wakati na idadi ya wagonjwa wanaopata huduma imeongezeka maradufu baada ya eneo la kutolea huduma kuboreshwa na kupanuliwa .

"Mh Naibu Waziri, hali ya utoaji huduma katika taasisi yetu ni nzuri, idadi ya wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji imeongezeka na kufikia 700-900 kwa mwezi kutoka 500 na ongezeko la vyumba 2 vya upasuaji katika jengo hili, awali tulikua na vyumba 6 sasa vimekuwa 8, hii nikutokana na uwekezaji uliofanywa na Serikali hii ya awamu ya 5 inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli" alisema Dkt Boniface. 

Jumatano, 26 Septemba 2018

OCEAN ROAD YAOKOA ZAIDI YA BILIONI 7.5 KWA MWAKA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akimsikiliza moja kati ya Wataalamu wa Picha za Mionzi kwenye jengo la Mionzi katika Taasisi ya Saratani Ocean Road jijini Dar Es salaam.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwajulia hali Wagonjwa waliofika kupata Huduma za Afya katika Taasisi ya Kansa ya Ocean Road Jijini Dar es salaa.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile  akiongea na Mgonjwa aliyetoka nchi ya Jirani ya Kenya kupata matibabu Kansa nchini katika Taasisi ya Ocean Road Jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua vifaa ambavyo vimenunuliwa na Serikali kwa gharama ya shilingi Bilion 9.5, alipofanya Ziara katika Taasisi ya Ocean Road jijini Dar es salaam. Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage.
 Baadhi ya Mitambo ya Mionzi katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road iliyogharimu jumla ya kiasi cha shilingi Bilioni 9.5.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongoza msafara wa kukagua hali ya utoaji huduma za Afya, na kukagua vifaa ambavyo vimenunuliwa na Serikali kwa gharama ya shilingi Bilion 9.5. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Julius Mwaiselage.
OCEAN ROAD YAOKOA ZAIDI YA BILIONI 7.5 KWA MWAKA.

Na WAMJW-DSM

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imefanikiwa kuokoa zaidi ya Bilion 7.5 zilizokuwa zikitumika kwaajili ya matibabu ya Wagonjwa wa Saratani nje ya nchi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma katika Taasisi ya Ocean Road na kukagua vifaa ambavyo vimenunuliwa na Serikali kwa gharama ya shilingi Bilion 9.5.

Dkt. Ndugulile aliendelea kusema kuwa vifaa hivi (Linac Mashine na CT Similator) vinaifanya nchi ya Tanzania kuwa moja kati ya Nchi chache barani Afrika ambayo inavifaa vya kisasa katika kutibu wagonjwa wa Saratani.

“Mashine hizi ambazo zipo ndani ya majengo haya yamenunuliwa na Serikali ya awamu ya Tano kwa gharama ya Shilingi Bilion 9.5, Vifaa hivi vinaitwa Linac Mashine na CT Similator vinaifanya Tanzania kuwa moja kati ya nchi chache sana Barani Afrika ambazo zinavifaa vya kisasa zaidi kwaajili ya matibabu ya Saratani” Alisema Dkt. Ndugulile

Pia, Dkt. Ndugulile alisema kuwa Vifaa hivi vyenye ufanisi mkubwa vinasaidia sana katika kuongeza idadi ya Wagonjwa kupata matibabu kutoka wagonjwa 170, mpaka 270 kwa siku, huku ikipunguza muda wa wagonjwa kusubiria matibabu kutoka wiki 6 mpaka chini ya wiki 2.

Aidha, Dkt. Ndugulile alisema kuwa Serikali inajipanga kufunga kifaa kikubwa cha Pate Scan ambacho kitasaidia kwa kiasi kikubwa wagonjwa wa Saratani.

Akisoma Risala ya Taasisi hiyo Mkurugenzi wa Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage alisema kuwa gharama za ujenzi wa jengo la vifaa vifaa hivo ni shilingi Bilion 2.3 ambazo zote zilitolewa na Serikali.

“Gharama ya ujenzi huu ni shilingi Bilion 2.33 ambapo zilitolewa zote na Serikali, Jengo hili limekwishakamilika, na liliweza kufanyiwa uhakiki na Tume ya Nguvu za Atomic Tanzania, pamoja na shilika la kimataifa la nguvu za Atomic walilipitia na kuliangalia vigezo vyake kama vimefikiwa na waliona vinafaa”. Alisema Dkt. Mwaiselage.

Mbali na hayo Dkt. Mwaiselage alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kugharamia Mradi huo uliogharimu jumla ya shilingi Bilion 9.5, zilizojumuhisha gharama za kupeleka Wataalamu kwaajili ya kupata mafunzo nje na ndani ya nchi.

“Mradi ulikuwa na sehemu ya Mafunzo kwa Wataalamu nje na ndani ya nchi, jumla ya gharama ya mradi huu ilikuwa ni Bilion 9.5, na fedha zote hizi, ziligharamiwa na Serikali chini ya Raisi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na tunamshukuru sana kwa kuweza kutoa fedha kwaajili ya mradi huu”. Alisema Dkt. Mwaiselage.

Jumanne, 25 Septemba 2018

KANUSHO KUHUSU AKAUNTI BATILI YA WAZIRI UMMY MWALIMU


Jumamosi, 22 Septemba 2018

WAKUU WA MIKOA NCHINI WATAKIWA KUTENGA VITUO MAALUM VYA KUHUDUMIA WAGONJWA WA EBOLA.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongoza Matembezi ya Hiari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yalipoanzia katika viwanja vya Mnazi Mmoja na kuishia viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhamad Bakari Kambi (Wakwanza Kulia) akiwa na Mwakilishi Mkazi kutoka Shirika la Afya la Kimataifa (WHO) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakiwa katika matembezi ya Hiari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yalipoanzia katika viwanja vya Mnazi Mmoja na kuishia viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam. 

Kikundi Shupavu cha Vijana wa Skauti kikiwa kimeshika Bango lenye maandishi ya kutoa Elimu kuhusu ugonjwa wa Ebola wakati wa matembezi ya Hiari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yalipoanzia katika viwanja vya Mnazi Mmoja na kuishia viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam. 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mwongozo utaosaidia jinsi ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola katika nchi yetu endapo utainia nchini.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa ameshika Mwongozo utaosaidia jinsi ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola katika nchi yetu endapo utaingia nchini.
 
WAKUU WA MIKOA NCHINI WATAKIWA KUTENGA VITUO MAALUM VYA KUHUDUMIA WAGONJWA WA EBOLA. 

Na WAMJW - DSM 

WAZIRI  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewataka Wakuu wa mikoa wote kutenga vituo maalumu katika kila halmashauri cha kuhudumia na  kuhifadhi wagonjwa wa Ebola endapo wataingia nchini.

Waziri Ummy Ameyasema hayo mapema leo katika Matembezi ya Hiari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yalipoanzia katika viwanja vya Mnazi Mmoja na kuishia viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam. 

"Lazima kila mikoa, Halmashauri kutenga kituo maalumu cha kuhudumia wagonjwa wa Ebola endapo watatokea, katika kila mkoa, kila Wilaya lazima wawe na chumba maalumu kwaajili ya kuhifadhi wagonjwa wa Ebola endapo wataingia "alisema Waziri Ummy Mwalimu. 

Aidha, Waziri Ummy aliwaomba Viongozi wa Dini kutumia majukwaa yao katika Maubiri yao kutoa tahadhari kwa wananchi kuhusu ugonjwa huu wa Ebola,  huku akiwaomba wasanii na viongozi wa Siasa nchini kutumia majukwaa yao ili kutoa madaraja kufikisha taarifa kwa wananchi.

Kwa mujibu wa Waziri  Ummy  amesema kuwa licha ya ugonjwa wa Ebola kutoingia nchini, bado tupo katika hatari kubwa ya kuupata ugonjwa huu kutokana na muingiliano wa wananchi baina ya nchi ya Tanzania na eneo la Kivu Kaskazini ambalo ni karibu na nchi ya Tanzania.

"Ebola bado haijaingia nchini Tanzania, lakini ni Kweli Kwamba tupo katika hatari kubwa zaidi kupata Ugonjwa huu wa Ebola, hii inatokana Na mlipuko wa ugonjwa huu kuwepo katika eneo la Kivu Kaskazini ambalo ni karibu na nchi ya Tanzania na kutokana na muingiliano wa wavuvi baina ya nchi hizi", Alisema Waziri Ummy. 

Aidha Waziri Ummy alisema kuwa Tanzania inaweza   kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini kwa vitengo vinavyihusika  kutoa elimu na uelewa wananchi kuhusu ugonjwa wa Ebola, itakuwa ni moja ya njia kubwa ya kuzuia ugonjwa huu usiingie. 

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa kwa mujibu wa taarifa kutoka WHO watu 111 wametolewa taarifa kuugua ugonjwa huu wa Ebola na watu 75 sawa na Asilimia 67% wamefariki kutokana na ugonjwa huu, vifo ni zaidi ya Asilimia 50%. Maana yake kukiwa na wagonjwa 100, tunapoteza wagonjwa 50.

"Kwa mujibu wa Takwimu za shirika la Afya Duniani (WHO) Mpaka sasa, watu 111 wametolewa taarifa ya kuugua ugonjwa huu wa Ebola, watu 75 sawa na Asilimia 67% wamefariki, ndiomaana tunaogopa sana kama tutaruhusu ugonjwa huu utaingia nchini, vifo ni zaidi ya Asilimia 50%, maana yake tukiwa na wagonjwa 100 , tunaweza kupoteza wagonjwa 50, kwakweli tusikubali ugonjwa huu kuingia nchini "Alisema Waziri Ummy . 

.


Ijumaa, 21 Septemba 2018

MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YA SIMU KUSAIDIA KUTOKOMEZA TATIZO LA KIFUA KIKUU (TB)

- Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na Wadau wa Masuala ya Afya wakati akizindua Huduma ya TB kupitia Teknolojia ya simu za mikononi leo jijini Dar Es salaam.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akimsikiliza Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na na Ukoma wakati akizindua Huduma ya TB kupitia Teknolojia ya simu za mikononi leo jijini Dar Es salaam.

Wadau mbali mbali wa Masuala ya Afya wakishiriki katika Uzinduzi wa Huduma ya TB kupitia Teknolojia ya simu za mikononi leo jijini Dar Es salaam uliofanywa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile.

Picha ya pamoja ikionesha nyuso za Bashasha kuashiria Uzinduzi rasmi wa Huduma ya TB kupitia Teknolojia ya simu za mikononi leo jijini Dar Es salaam uliofanywa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati akizindua Huduma ya TB kupitia Teknolojia ya simu za mikononi leo jijini Dar Es salaam.
MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YA SIMU KUSAIDIA KUTOKOMEZA TATIZO LA KIFUA KIKUU (TB)

Na WAMJW-DSM

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa wito kwa wananchi kutumia Teknolojia ya simu vizuri ikiwemo kupata Elimu kuhusiana na masuala ya Afya.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katika Uzinduzi wa huduma ya TB kupitia Teknolojia ya simu za mikononi leo jijini Dar Es salaam.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa zaidi ya Wananchi wa Tanzania Milion 40 wanamiliki simu hivyo kuwataka kutumia fursa hiyo kupata Elimu ya Afya ikiwemo Elimu ya maambukizi ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB).

“zaidi ya Watanzania Milion 40 wanamiliki simu za mikononi, wapo kwenye mfumo wa mawasiliano katika taifa lenye watu zaidi ya Milioni 55,  nawapongeza kwa kuliona na kutambua hili kuangalia jinsi gani tunaweza kutumia teknolojia katika masuala ya Afya” Alisema Dkt. Ndugulile.

Dkt. Ndugulile aliendelea kusema kuwa Ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) unashika nafasi ya 9 kwa kusababisha vifo duniani kote na ni ugonjwa pekee wa kuambukiza unaoongoza ukifuatiwa na VVU.

Aidha, Dkt Ndugulile alisema kuwa mwaka 2016 watu milioni 10.4 duniani waliugua  TB, milioni  1.7 walifariki dunia wakati milioni 4.3 million hawakugunduliwa huku ripoti ya TB ya Shirika la Afya Duniani ya mwaka 2017 ikibainisha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 30 duniani zenye wagonjwa wengi wa TB.

Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile alisema kuwa jumla ya wagonjwa 69,818 wa TB waligunduliwa ambapo asilimia 90 walitibiwa na kupona, huku ikikadiliwa wagonjwa wanaofikiwa ni asilimia 44  ambapo kuna wagonjwa 84,000 wenye TB ambao bado wapo kwenye jamii na wanaendelea kuambukiza. 

Mbali na hayo Dkt Ndugulile alisema kuwa Lengo la Mpango Mkakati huo ni kupunguza maambukizi ya TB nchini Tanzania ifikapo mwaka 2020 na kupunguza maambukizi mapya ya TB kwa asilimia 20 na idadi ya vifo vinavyotokana na TB kwa asilimia 35.

Hata hivyo Dkt Ndugulile alisema kuwa Wizara itawezesha ufanisi na ufuatiliaji wa mfumo huo na kuhakikisha kuwa taarifa zinakusanywa na kutumika ipasavyo mfano idadi ya watu waliosajiliwa, idadi ya ujumbe uliotumwa kwa walengwa, idadi ya wagonjwa wa TB waliogunduliwa na ufuatiliaji wa wagonjwa kwa wakati muafaka. 

Mwisho Dkt. Ndugulile alitoa Rai kwa Wadau wote wa Masuala ya Afya kwenda kutoa Elimu ya kupambana dhidi ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu kwenye maeneo yenye changamoto ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu.

“Niwaombe sana Wadau wetu, tusiende kwenye maeneo kwa urahisi wenu nyie wa kufika, nawataka muende kwenye kwenye maeneo ambayo yanachangamoto kweli ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu” alisema Dkt. Ndugulile.

Nae Afisa Mwamasishaji kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kikufua Kikuu na Ukoma Agatha Mshanga alisema kuwa Malengo ya Huduma ya TB kupitia Mtandao wa Simu ni kuongeza uibuaji wa Wagonjwa wa Kifua Kikuu, Waliopo kwenye matibabu waweze kuwa na ufuasi mzuri wa Matibabu, kupambana na unyanyapaa na kutengwa kwa wagonjwa wa TB na kupeleka Elimu ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB).


Ijumaa, 14 Septemba 2018

VIDONDA VIUGUZWE KWA USAFI KUEPUKA SEPSIS

- Hakuna maoni
 Katibu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akitoa ufafanuzi juu ya Ugonjwa wa Sepsis katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es salaam.
 
VIDONDA VIUGUZWE  KWA USAFI KUEPUKA SEPSIS

Na WAMJW- DAR ES SALAAM. 

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto imewataka watanzania kuuguza vidonda kwa usafi na uangalizi mkubwa  pale wanapopata majeraha ili kuepuka kupata Bakteria wa Sepsis. 

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya  Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati akitoa tamko kuhusu uwepo wa bakteria hao na jinsi ya kujikinga leo jinini Dar es salaam. 

"Watoa huduma za afya hususan wale wanaofunga vidonda wanatakiwa kujirinda na kuhudumia kwa kujistiri zaidi ili kuepuka kupata bakteria  hao kwani vidonda vinapokuwa wazi inakua rahisi kupata bakteria hao" alisema Dkt. Ulisubisya.

Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa wamama wanaojifungua na watoto wachanga wapo katika hatari zaidi kwani tafiti zinaonesha kuwa asilimia 8 ya vifo vya wajawazito na asilimia 32 ya vifo vya watoto wachanga huchangiwa na bakteria hao. 

Dkt. Ulisubisya amesema kuwa kutokana na  takwimu za Shirika la Afya Duniani WHO zinaonesha kuwa watu milioni 30  duniani kote wanapata bakteria  wa Sepsis na milioni 6 hupoteza maisha kutokana na bakteria hao kila mwaka. 

Kwa mujibu wa Dkt.  Ulisubisya amebainisha kuwa watu wenye ugonjwa wa Ukimwi, Kisukari,utapia mlo uliopitiliza,  wanaotumia dawa za saratani pamoja na wenye usugu wa dawa wapo kwenye mazingira hatarishi ya kupata bakteria hao. 

Aidha Dkt. Ulisubisya alisema kuwa dalili za mwenye bakteria hao ni homa kali kupindukia, mapigo ya moyo kwenda haraka sana au polepole sana pamoja na kuhema harakaharaka na madhara yake hayaachi maeneo yeyote ya mwili. 

Dkt. Ulisubisya amesema kuwa jinsi ya kujikinga na bakteria hao  ni kufanya usafi wa mwili ikiwemo  kuoga mara kwa mara na kunawa mikono kwa maji safi na salama 

Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa Wizara ya Afya  imetoa mafunzo ya Kukinga na Kudhibiti Maambukizo kwenye ngazi ya Kitaifa, Kanda, Mikoa, Halmashauri pamoja Vituo vya Afya na Zahanati. 

"Kama Wizara tutaendelea Kuimarisha huduma na Maabara ili kuweza kubaini aina ya Vijidudu vinavyohusika na Sepsis kwa mgonjwa husika pamoja na hali ya usugu wa viuavivyasumu ili Madaktari na Matabibu waweze kutoa tiba sahihi ili kutokomeza bakteria hao" alisema Dkt. Ulisubisya.  

Sepsis ni uwepo wa bakteria hatari kwenye mwili hivyo uwepo wa bakteria hawa mwilini husababisha uzalishaji wa kemikali hatari ambazo husababisha mtu kuumwa sana na wakati mwingine kufikia kupata mshituko ambao kitaalamu huitwa "septic shock". 

MWISHO.

Jumatano, 12 Septemba 2018

TENDER

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF HEALTH, COMMUNITY DEVELOPMENT, GENDER,
ELDERLY AND CHILDREN



TENDER No. ME/007/2018/HQ/G/113

FOR
PRINTING AND SUPPLY OF
REDESIGNED LOGISTICS SYSTEM FOR PUBLIC HEALTH COMMODITIES IN TANZANIA MAINLAND

Invitation for Tenders

Date: 10th September, 2018
1.      The Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children has secured funds from Global Fund towards the cost of Implementation of the Health System Strengthening Program (HSS), and it intends to apply part of the proceeds of the funds to cover payments under the contract for Printing and Supply of Redesigned Logistics System for Public Health Commodities in Tanzania Mainland.

2.      The Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children now invites sealed tenders from eligible Suppliers for Printing and Supply of Redesigned Logistics System for Public Health Commodities in Tanzania Mainland as follows:
Item No.
Item Description
Quantity
1
Logistics System – Standard Operating Procedure Manual.
8807
2
Logistics System – Facilitator’s Guide TOT Team.
300
3
Logistics System – TOT Participants Work book.
600
4
Logistics System – Facilitator’s Guide for Health Facilities.
600
5
Logistics System- Participants Work book for health facilities.
7500
6
Logistics Management Services – Standard Operating Procedure Manual.
1000
7
TB Facility Monthly Report Form – Triple carbonated.
5000
8
MDR TB Facility Monthly Report Form - Triple carbonated.
1000


TOTAL
24807

  1. Tendering will be conducted through the National Competitive Bidding procedures specified in the Public Procurement Act 2011 as amended 2016 and related Regulations, 2013 – Government Notice No. 446 as amended in 2016, and is open to all Tenderers as defined in the Regulations.
  2. Interested eligible Tenderers may obtain further information from and inspect the Tendering Documents at the office of the Secretary, Ministerial Tender Board, Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children, University of Dodoma, Faculty of Social Science in Community Development, P. O Box 743, Dodoma, Building No. 11, 40478 Dodoma, Room 203, from 9.00-3.30 hrs. on Mondays to Fridays inclusive except on public holidays .
5.      Tender Document in English may be purchased by interested Tenderers on the submission of a written application to the address given under paragraph 4 above and upon payment of a non-refundable fee of Tanzania Shillings One Hundred Thousands Shillings Only (TZS. 100,000.00/=). Payment should either be by Cash or Banker’s Draft, or Banker’s Cheque, payable to Principal Secretary, Ministry of Health and Social Welfare, Bank of Tanzania, Account No. 9921145201.

6.      All tenders must be accompanied by a Bid Security or Bid Securing Declaration in the format provided in the Tendering Documents.

  1. All tenders in one original plus two copies, properly filled in, and enclosed in plain envelopes must be delivered to the Secretary, Ministerial Tender Board, Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children; University of Dodoma, Faculty of Social Science in Community Development, P. O Box 743, Dodoma, Building No. 11, 40478 Dodoma, Room 203, 1st Floor, before 11:00 hrs. on 24th September, 2018.

  1. Tenders will be opened thereafter in public and in the presence of Tenderers’ representatives who choose to attend in the opening at the Minister’s Conference Hall, Area D, Sengia Street at Ministry of Health, community Development, Gender, elderly and Children Offices, Dodoma.

9.      Late Tenders, Portion of Tenders, Electronic Tenders, Tenders not received, Tenders not opened and not read out in public at the tender opening ceremony shall not be accepted for evaluation irrespective of the circumstances.




Permanent Secretary,
Ministry of Health, Community Development,
Gender, Elderly and Children,
P.O Box 743, Dodoma,
Tanzania.




Jumanne, 11 Septemba 2018

WABUNGE WATAKIWA KUWAHAMASISHA WANANCHI KUTOKOMEZA KIFUA KIKUU NCHINI.

Kikao cha Uzinduzi wa Mtandao wa Wabunge duniani wenye dhamira ya kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu uliofanyika katika ukumbi wa bunge jijini Dodoma.

Mbunge wa Viti Maalumu kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mh. Najma Giga aliyemuwakilisha Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai katika kikao cha Uzinduzi wa Mtandao wa Wabunge duniani wenye dhamira ya kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu uliofanyika katika ukumbi wa bunge jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa taarifa juu ya jitihada zinazoendelea kufanywa na Serikali katika kudhibiti ugonjwa wa Kifua Kikuu mbele ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ukumbi wa Bunge jijini Dododma.

Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua kikuu na Ukoma Dkt Beatrice Mutayoba akitoa Elimu Mbele ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu na Jitihada mbali mbali za kudhibiti ugonjwa huo katika kikao cha Uzinduzi wa Mtandao wa Wabunge duniani wenye dhamira ya kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu uliofanyika katika ukumbi wa bunge jijini Dodoma.

Bi. Agatha Chikoti aliewai kuugua ugonjwa wa Kifua Kikuu na kupona kabisa akitoa ushuhuda  mbele ya Wabunge katika kikao cha Uzinduzi wa Mtandao wa Wabunge duniani wenye dhamira ya kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu uliofanyika katika ukumbi wa bunge jijini Dodoma.

Picha ya Pamoja ikiongozwa na Mgeni rasmi ambae ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mh. Najma Giga aliyemuwakilisha Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai katika kikao cha Uzinduzi wa Mtandao wa Wabunge duniani wenye dhamira ya kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu uliofanyika katika ukumbi wa bunge jijini Dodoma.


WABUNGE WATAKIWA KUWAHAMASISHA WANANCHI KUTOKOMEZA KIFUA KIKUU NCHINI.

Na WAMJW-DODOMA

Wabunge nchini wamehamasishwa kushiriki katika kuongoza juhudi za kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu (TB) ambao unaonekana kuwa tishio kubwa.

Hayo yameelezwa na mbunge wa viti maalumu (CCM) Mh. Najma Giga aliyemuwakilisha Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai katika uzinduzi wa mtandao wa wabunge duniani wenye dhamira ya kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu uliofanyika katika ukumbi wa bunge jijini Dodoma.

Mhe.  Giga amesema kuwa ni wajibuwa kila mbunge nchini kuisimamia serikali ili ishughulikie kikamilifu tatizo la kifua kikuu kwa kutenga rasilimali za kutosha kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo hatari.

“Kifua kikuu kinaleta madhara kiafya na huongeza umasikini katika jamii, takribani watu 154,000 uugua kila mwaka na 27,000 ufariki duniani ikiwa ni sawa vifo 74 kwa siku, hii inaonesha ni jinsi gani ugonjwa wa TB ni hatari na hivyo juhudi za ziada zinahitajika ili kuutokomeza”. Amesema Mh. Giga.

Aidha Mh. Giga ameipongeza serikali na wataalamu wa afya kwa kuweza kuchunguza na kutoa matibabu kwa wagonjwa wa kifua kikuu na kuhakikisha wagonjwa wanapata matibabu bure na wanapona kabisa katika hospitali zote nchini.

Mh. Najma amesema kuwepo kwa mtandao wa wabunge wa kupambana na TB nchini (Parliamentary TB Focus) kutawezesha kufikia malengo ya kimataifa na kitaifa ya kutokomeza TB kwa kutambua kuwa ni janga la kitaifa.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema wizara hiyo inatoa kipaumbele juu ya ugonjwa wa TB kwa kufanya juhudi kubwa ya kuutokomeza ugonjwa huu nchini ikiwemo kuweka teknolojia za kisasa za mashine za Genex part zaidi ya 209.

“Jambo ambalo tumelifanya kama serikali ni kujaribu kufanya utaratibu tofauti wa jinsi gani ya kufanya upimaji wa ugonjwa huu. Hadi hivi sasa tumeweka teknolojia za kisasa za mashine za Genex part zaidi ya 209 nchi nzima ambazo utoa majibu ndani ya masaa mawili”. Alisema Dkt. Ndugulile.

Pia Dkt. Ndugulile amesema kuwa dawa zote zinazotibu kifua kikuu cha kawaida na kifua kikuu sugu zinapatikana nchini na matibabu yake pamoja na vipimo vyote vinavyohusiana na ugonjwa wa TB yanatolewa bure.

Sambamba na hayo, Shuhuda Bi. Agatha Chikoti aliyewahi kuugua ugonjwa wa kifua kikuu ameiasa jamii kuacha kwenda kutafuta dawa za kienyeji na badala yake kwenda hospitali kupima na kupewa tiba sahihi.