Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia
Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua Mkono wa Bandia uliotengenezwa katika Taasisi hiyo, Kulia ni Mtaalamu wa viungo Bandia Bw. Deus David.
Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia
Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akimsalimia mtoto, aliyefika na mzazi wake kupata matibabu katika Taasisi ya mifupa ya MOI, alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kusimikwa kwa Mitambo ya MRI,CT Scan na X-Ray
Mkuu wa Kitengo cha Fiziotherapia Bw. Lucas Machage akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia
Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile, alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kusimikwa kwa Mitambo ya MRI,CT Scan na X-Ray MOI.
Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia
Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na mmoja kati ya wanufaika wa Vifaa vya Bandia katika Taasisi ya Mifupa MOI aliowekewa baada ya kukatwa Mkono wake.
Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia
Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua Cheti cha moja kati ya Wagonjwa waliofika kupata huduma za Afya katika Taasisi ya Mifupa ya MOI.
Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia
Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua moja kati ya mtambo wa kisasa uliosimikwa tayari kuanza kufanya kazi, katika Taasisi ya Mifupa ya MOI, Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Respicious Bonface.
Wataalamu mbali mbali kutoka Taasisi ya Mifupa ya MOI wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia
Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kusimikwa kwa Mitambo ya MRI,CT Scan na X-Ray.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia
Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua kitabu cha Kusaini Wataalamu wa Maabara, Kushoto ni Muuguzi wa Kitengo cha Dharura MOI Levlin Masama.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia
Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiendelea na Ziara katika Taasisi ya Mifupa ya MOI, Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Respicious Bonface.
HUDUMA ZA MRI NA CT SCAN ZAANZA KUTOLEWA MOI.
Na WAMJW-Dar es Salaam.
Huduma
za kupima magonjwa mbalimbali kwa kutumia Mashine za kisasa ya CT Scan
na MRI sasa zimeanza kutolewa kwa ufanisi baada ya kusimikwa na kuanza
kufanya kazi katika Hospitali ya Mifupa ya MOI.
Hayo
yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,JiAnsia
Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea na kukagua hali
ya utoaji wa huduma na usimikaji wa mitambo ya kisasa katika kitengo cha
radiolojia yenye thamani ya zaidi ya Tsh Bilioni 5.6 Hospitalini hapo .
"Lengo
la ziara yangu ni kukagua maendeleo ya usimikaji wa mitambo hii ya
kisasa ya MRI, CT SCAN, Xray, Ultra sound, mitambo mingine , nimeona na
kujiridhisha imekamilika kwa asilimia 99% " Alisema Dkt.Ndugulile.
Aidha
, Dkt. Ndugulile ameuagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha
unakamilisha mambo machache yaliyobaki ndani ya wiki hii ili wiki ijayo
wagonjwa waanze kupata huduma hapa.
Mbali
na hayo Dkt Ndugulile ameupongeza uongozi wa MOI kwa kuhakikisha
usimikaji wa Mitambao unafanyika kwa wakati na hali ya utoaji huduma ni
nzuri na ya kuridhisha kwani wagonjwa wamekuwa wakipata changamoto ya
kwenda nje ya MOI kufuata vipimo hivi.
Mbali
na hayo Dkt. Ndugulile amesema ni adhma ya Serikali kuhakikisha huduma
zote zinapatikana hapa nchini hivyo ni vyema kama kuna kifaa chochote
kinachohitajika taarifa ikatolewa Wizarani ili kifaa hicho kiwekwe
kwenye mpango na bajeti na kununuliwa kwani utaalamu na weledi upo
wakutosha.
Dkt Ndugulule
ametembelea vitengo vya mazoezi tiba pamoja na utengenezaji wa viungo
bandia ambapo amekagua na kujiaone hali ya utoaji huduma na kujiridhisha
kwamba huduma zimeboreka katika kipindi cha miaka 3 tangu Serikali ya
awamu ya tano kuingia madarakani na kwa sasa watanzania wanapata huduma
kwa wakati licha ya kuwa kuna changamoto ya ununuzi wa vifaa tiba nje
ya nchi.
Akitoa taarifa
ya hali ya utoaji huduma na usimikaji wa mitambo hiyo Mkurugenzi
Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface amesema kwamba hali ya utoaji wa
huduma ni nzuri, wagonjwa wanapata huduma stahiki kwa wakati na idadi
ya wagonjwa wanaopata huduma imeongezeka maradufu baada ya eneo la
kutolea huduma kuboreshwa na kupanuliwa .
"Mh
Naibu Waziri, hali ya utoaji huduma katika taasisi yetu ni nzuri, idadi
ya wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji imeongezeka na kufikia 700-900 kwa
mwezi kutoka 500 na ongezeko la vyumba 2 vya upasuaji katika jengo hili,
awali tulikua na vyumba 6 sasa vimekuwa 8, hii nikutokana na uwekezaji
uliofanywa na Serikali hii ya awamu ya 5 inayoongozwa na Dkt John Pombe
Magufuli" alisema Dkt Boniface.
0 on: " HUDUMA ZA MRI NA CT SCAN ZAANZA KUTOLEWA MOI."