Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa taarifa mbele ya Waandishi wa Habari (Hawapo kwenye picha) juu ya ugonjwa wa Ebola wakati akifungua Semina juu ya kurepoti kuhusu Ugonjwa wa Ebola iliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara leo jijini Dar es salaam.
Waandishi wa Habari waliojitokeza waliojitokeza kupata Elimu juu ya namna kurepoti kuhusu Ugonjwa wa Ebola iliyozinduliwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika Ofisi ndogo za Wizara leo jijini Dar es salaam.
Picha ya Pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu naMganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohamed Bakari Kambi leo akifungua Semina juu ya kurepoti kuhusu Ugonjwa wa Ebola iliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara leo jijini Dar es salaam.
Waandishi wa Habari wakiendelea na Semina kuhusu namna ya kuripoti Ugonjwa wa Ebola iliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara leo jijini Dar es salaam.
Dkt. Mohamed Ally Mohamed akitoa Elimu juu ya Ugonjwa wa Ebola na namna ya Kuripot ugonjwa huo mbele ya Waandishi wa Habari waliojitokeza leo katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.
WANAHABARI
WAFUNDWA JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA
EBOLA NCHINI
Na
WAMJW-DAR ES SALAAM.
Waandishi wa Habari wametakiwa kushirikiana na
Serikali katika kuihabarisha jamii ili kuepukana na janga hatari la ugonjwa wa
Ebola.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
ameyabainisha hayo wakati wa kufungua mafunzo maalum kwa waandishi wa
namna ya kutoa taarifa za ugonjwa huo wa Ebola.
“Ugonjwa
huu wa Ebola kiukweli ni ugonjwa hatari. Na tokea kutokea katika nchi za
wenzetu umesababisha madhara makubwa sana ikiwemo Uchumi ikiwemo masuala ya
biashara na uwekezaji na Sisi tulikuwa na wasiwasi sana ndio maana tulienda
wenyewe huko kufuatilia ,mimi nilienda mipakani Rusumo na Mganga Mkuu yeye
alienda mipaka ya Ngala na maeneo mengine.” Amesema Waziri Ummy Mwalimu.
Aidha Waziri Ummy ameongeza kuwa, tatizo kubwa ni
suala la wasafiri wanaopita njia za panya kwani zimekuwa zikiwapa changamoto na
wameomba Kamati za Ulinzi na Usalama kuhakikisha wanalinda maeneo hayo.
Hata hivyo Waziri Ummy amebainisha kuwa, Wizara
imejipanga kutafuta njia bora zaidi mara
kwa mara ambapo wameomba Wanahabari kushirikiana na Wizara kupata taarifa na
uelewa zaidi.
“Ndugu wanahabari kupitia semina hii itaongeza
uelewa wa ugonjwa wa Ebola. Nimefurahi sana Wanahabari na wachora vibonzo
wameanza kutoa taarifa na kuchora vibonzo juu ya ebola.
“Nimalizie kwa kusema tena Hadi saa Tanzania hakuna
mgonjwa yeyote aliyehisiwa au kuthibitishwa kuwa na Virusi vya Ebola hapa
Nchini. Hata hivyo kutokana na ukweli kwamba kuna mwingiliano mkubwa wa wananchi
kati ya nchi hizi mbili na ugonjwa huu kugunduliwa kwenye jimbo la Kivu
Kaskazini ambalo linapakana na nchi ya Uganda ni ukweli unaotuweka kwenye hali
ya wasiwasi mkubwa” Alimalizia Waziri Ummy.
Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Afya Duniani (WHO), Dkt. Adiele Onyeze amebainisha kuwa wataendelea
kushirikiana na Tanzania katika kuzuia milipuko ya magonjwa mbalimbali
ikiwemo ugonjwa huo wa Ebola ambao
umekuwa ukiripotiwa mara kwa mara katika nchi za Afrika.
“Dunia kwa sasa ipo katika mapambano ya kuzuia
milipuko ya magonjwa. Sisi WHO tumejipanga kusaidia juhudi za Mataifa yote
yenye hatari hivyo tutasaidia kutoa elimu na uwelewa kwa Wananchi wote”
alieleza Dkt. Adiele Onyeze.
Kwa upande wa mafunzo hayo kwa wanahabari
yaliyotolewa watalaam mbalimbali kutoka nje ya Nchi na wa hapa nchini akiwemo
Mkurugenzi wa Idara ya Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya Wizara ya Afya Dkt.
Mohammed Ally Mohammed alibainisha kuwa:
tangu kuripotiwa kwa taarifa kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchi jirani ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) uliotangazwa na WHO, Agosti Mosi Mwaka
huu, Jumla ya wagonjwa 26 na vifo 10 (CFR = 38.5%) vilitokea katika Nchi hiyo.
Hata hivyo tangu kutoka kwa tamko hilo hali ya
ugonjwa imeendelea kwa kasi sana na kufikia wagonjwa 91 na vifo 50 (CFR =
54.9%). Aidha wagonjwa hao imeelezwa kutokea maeneo matano ya afya (Health
zones) katika jimbo la Kivu Kaskazini na eneo jingine moja la Ituri ambapo huu
ni mlipuko wa 10 wa ugonjwa wa Ebola kutokea nchini DRC, na umetokea wiki moja
tu baada ya nchi hiyo kutangaza kumalizika kwa mlipuko mwingine uliotokea mwezi
Mei 2018.
Takwimu
zilizotolewa na WHO, Wafanyakazi tisa (9) wa Afya wamethibitishwa kuugua
ugonjwa huu, huku ikifanya jumla yao kufikia 10 (9 wamethibitika na 1
anafuatiliwa); na hadi sasa mfanyakazi mmoja amepoteza maisha.
MWISHO.
0 on: "WANAHABARI WAFUNDWA JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA EBOLA NCHINI"