Naibu
waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiongea na wagonjwa waliokua wanasubiri huduma
katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma.
Naibu Waziri
wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt. Faustine
Ndugulile akikagua maboksi ya sindano katika stoo wakati alipofanya
ziara ya kushtukiza katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma.
Naibu
waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto akikagua
kitabu cha taarifa mbalimbali za hospitali wakati alipofanya ziara ya
kushtukiza katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma, kulia kwake ni
katibu wa afya wa hospitali hiyo Mwanaisha Hassan
Naibu Waziri
wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto akitoa maelekezo
kwa viongozi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma wakati alipofanya
ziara ya kushtukiza katika Hospitali hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua mashine ya X Ray.
DKT. NDUGULILE ATOA SIKU 14 KUKAMILISHWA KWA MASHINE YA X RAY HOSPITALI YA RUFAA DODOMA.
NAIBU
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile ameutaka uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma
kuhakikisha mashine ya kutolea huduma za X-ray inafanya kazi ndani ya
siku 14.
Ameyasema
hayo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza yenye lengo la kuangalia na
kujiridhisha na hali ya utoaji huduma za afya katika Hospitali hiyo leo
jijini Dodoma.
"Ifikapo
Septemba 21 nataka kuona mashine ya kutolea huduma za X-ray na vifaa
vingne viwe tayari kutoa huduma kwa wananchi wa Dodoma na maeneo
yanayoizunguka kwani Hospitali hii ni tegemezi kwa wakazi wa mkoa huu la
sivyo hatua stahiki zitachukuliwa bila ya kumuonea mtu haya"
alisisitiza Dkt. Ndugulile
Aidha,Dkt.
Ndugulile ametoa siku 30 kwa uongozi wa hospitali hiyo kukarabati jengo
la bima ya afya baada ya kukagua na kutoridhishwa na muonekano wake
kwani linaleta kero kwa wateja wanaokwenda kupata huduma Hospitalini
hapo.
Mbali
na hayo Dkt. Ndugulile ameonekana kukerwa na uzembe wa watendaji wa
Hospitali hiyo na kusababisha kuwakemea vikali na kuhaidi maagizo
aliyoyatoa yasipotekelezwa kwa wakati hatua za kinidhamu zitakuchululiwa
kwa vitendo.
Wakati
huo huo dkt.Ndugulile ameuagiza uongozi wa hospitali hiyo kuwarudishia
fedha wagonjwa walizotumia kununua dawa pamoja na sindano kwenye maduka
yaliopo nje ya hospitali hiyo ilihali wana vifaa hivyo takribani ya
kutosha miezi sita kwenye stoo yao
0 on: "DKT. NDUGULILE ATOA SIKU 14 KUKAMILISHWA KWA MASHINE YA X RAY HOSPITALI YA RUFAA DODOMA."