Katibu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akitoa ufafanuzi juu ya Ugonjwa wa Sepsis katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es salaam.
VIDONDA VIUGUZWE KWA USAFI KUEPUKA SEPSIS
Na WAMJW- DAR ES SALAAM.
SERIKALI
kupitia Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto
imewataka watanzania kuuguza vidonda kwa usafi na uangalizi mkubwa pale
wanapopata majeraha ili kuepuka kupata Bakteria wa Sepsis.
Hayo
yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati
akitoa tamko kuhusu uwepo wa bakteria hao na jinsi ya kujikinga leo
jinini Dar es salaam.
"Watoa
huduma za afya hususan wale wanaofunga vidonda wanatakiwa kujirinda na
kuhudumia kwa kujistiri zaidi ili kuepuka kupata bakteria hao kwani
vidonda vinapokuwa wazi inakua rahisi kupata bakteria hao" alisema Dkt.
Ulisubisya.
Aidha Dkt.
Ulisubisya amesema kuwa wamama wanaojifungua na watoto wachanga wapo
katika hatari zaidi kwani tafiti zinaonesha kuwa asilimia 8 ya vifo vya
wajawazito na asilimia 32 ya vifo vya watoto wachanga huchangiwa na
bakteria hao.
Dkt.
Ulisubisya amesema kuwa kutokana na takwimu za Shirika la Afya Duniani
WHO zinaonesha kuwa watu milioni 30 duniani kote wanapata bakteria wa
Sepsis na milioni 6 hupoteza maisha kutokana na bakteria hao kila
mwaka.
Kwa mujibu wa
Dkt. Ulisubisya amebainisha kuwa watu wenye ugonjwa wa Ukimwi,
Kisukari,utapia mlo uliopitiliza, wanaotumia dawa za saratani pamoja na
wenye usugu wa dawa wapo kwenye mazingira hatarishi ya kupata bakteria
hao.
Aidha Dkt.
Ulisubisya alisema kuwa dalili za mwenye bakteria hao ni homa kali
kupindukia, mapigo ya moyo kwenda haraka sana au polepole sana pamoja na
kuhema harakaharaka na madhara yake hayaachi maeneo yeyote ya mwili.
Dkt.
Ulisubisya amesema kuwa jinsi ya kujikinga na bakteria hao ni kufanya
usafi wa mwili ikiwemo kuoga mara kwa mara na kunawa mikono kwa maji
safi na salama
Aidha
Dkt. Ulisubisya amesema kuwa Wizara ya Afya imetoa mafunzo ya Kukinga
na Kudhibiti Maambukizo kwenye ngazi ya Kitaifa, Kanda, Mikoa,
Halmashauri pamoja Vituo vya Afya na Zahanati.
"Kama
Wizara tutaendelea Kuimarisha huduma na Maabara ili kuweza kubaini aina
ya Vijidudu vinavyohusika na Sepsis kwa mgonjwa husika pamoja na hali
ya usugu wa viuavivyasumu ili Madaktari na Matabibu waweze kutoa tiba
sahihi ili kutokomeza bakteria hao" alisema Dkt. Ulisubisya.
Sepsis
ni uwepo wa bakteria hatari kwenye mwili hivyo uwepo wa bakteria hawa
mwilini husababisha uzalishaji wa kemikali hatari ambazo husababisha mtu
kuumwa sana na wakati mwingine kufikia kupata mshituko ambao kitaalamu
huitwa "septic shock".
MWISHO.
0 on: "VIDONDA VIUGUZWE KWA USAFI KUEPUKA SEPSIS"