Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiongoza Matembezi ya Siku ya Moyo Duniani
yaliyoanzia viwanja vya Leaders Club na kumalizikia viwanja vya Mnazi
Mmoja jijini Dar es sala, matembezi hayo yamebeba kauli mbiu ya "Moyo
wangu Moyo Wako". Wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa kitengo cha Elimu ya
Afya kwa Umma Wizara ya Afya.
Matembezi ya Siku ya Moyo Duniani yakiendelea, ambayo kwa mwaka huu yamebeba kauli mbiu ya 'Moyo wangu, Moyo wako"
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiambatana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Elimu ya
Afya kwa Umma kutoka Wizara ya Afya wakinyoosha viungo baada ya kumaliza
matembezi ya Siku ya Moyo Duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini
Dar es salaam.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt
Faustine Ndugulile akikagua moja kati ya mabanda yaliyokuwepo katika
viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam katika maadhimisho ya Siku
ya Moyo Duniani. Kushoto kwake ni Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania
Dkt. Robert Mvungi, kulia kwake ni Mkurugenzi wa kitengo cha Elimu ya
Afya kwa Umma Wizara ya Afya Dkt. Amalberga Kasangala.
SERIKALI YAWEKA MIKAKATI THABITI YA KUPAMBA DHIDI YA UGONJWA WA MOYO
Na WAMJW-Dar es salaam.
Serikali
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imeanza kuweka mikakati thabiti ya kupambana dhidi ya maradhi ya Moyo
nchini.
Hayo yamesemwa na
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile leo katika maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani
yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Dkt.
Ndugulile alisema kwamba Serikali imeendelea kutoa Elimu kupitia vyombo
vya Habari na mitandao ya kijamii, kuanzisha Mpango wa Taifa wa
magonjwa yasiyo yakuambukiza, na kuhakikisha TV zote katika Hospitali na
Vituo vya Afya zinaonesha jumbe zinazohusu masuala ya Afya tu.
“Serikali
tumeona kwamba tunahitaji kuongeza msukumo kwemnye magonjwa yasiyo
yakuambukiza, matamasha tunayofanya ni moja ya mkakati tunaofanya wa
kutoa Elimu kwa jamii, kuoa Elimu kupitia njia mbali mbali ikiwemo TV,
magazeti, pamoja na mtandao wa jamii, kuanzisha Mpango wa Taifa wa
magonjwa yasiyo yakuambukiza, kuelekeza hospitali zote kuonesha jumbe
mbali mbali za masuala ya Afya” Alisema Dkt. Ndugulile.
Dkt.
Ndugulile alisema kwamba kuna ongezeko kubwa sana la magonjwa yasiyo
yakuambukiza ikiwemo maradhi ya Moyo ambayo kwa kiasi kikubwa
yanasababishwa na kutofanya mazoezi, aina ya vyakula tunavyokula,
matumizi yaliyopitiliza ya vilevi.
“Kama
taifa tunaona kuna ongezeko kubwa la magonjwa yasiyo yakuambukiza
ikiwemo ugonjwa wa Moyo, na visababishi vikubwa ni aina ya vyakula
tunavyokula, watu kutofanya mazoezi, matumizi ya pombe na sigara kupita
kiasi”, alisema Dkt. Ndugulile.
Kwa
upande mwingine Dkt. Ndugulile alisema kuwa Magonjwa ya moyo yanaongoza
kwa kusababisha vifo duniani na inakadiriwa kuwa watu 17,500,000 hufa
kila mwaka duniani kote kutokana na magonjwa ya moyo na kiharusi.
Aidha,
Dkt Ndugulile alisema kuwa kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya
Duniani (WHO) zinaeleza kwamba asilimia 40% ya vifo vyote vinavyotokea
duniani vinasababishwa na magonjwa ya moyo huku nusu ya vifo ambavyo
vinatokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza vinatokana na magonjwa ya
moyo.
Pia, Dkt. Ndugulile
alisema kuwa matumizi ya Tumbaku na bidhaa zake yanakadiriwa
kusababisha vifo vya watu 6,000,000 duniani kila mwaka na pia huchangia
kusababisha asilimia 10% ya wagonjwa wenye magonjwa ya moyo.
Mbali
na Hayo Dkt. Ndugulile alisema kwamba kama hatua madhubuti za kinga,
uchunguzi wa mapema na tiba stahiki hazitachukuliwa haraka, tatizo la
Moyo ifikapo mwaka 2035 litaongezeka na kufikia makadirio ya wagonjwa
wapya milioni 131,978,870 (sawa na ongezeko la 45% kutoka hali ilivyo
kwa sasa), huku ongezeko kubwa likiwa katika ukanda wa nchi
zinazoendelea, Tanzania ikiwa mojawapo.
Kwa
upande mwingine Dkt. Ndugulile alisema kuwa nia thabiti ya Serikali ya
Awamu ya tano ni kuboresha huduma za afya hapa nchini ikiwa ni pamoja na
upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi vinavyohitajika
katika kutoa huduma za afya nchini kwa kuongeza bajeti ya afya kila
mwaka.
“Sisi sote ni
mashahidi wa juhudi hizi za Serikali kwa uwepo wa Taasisi ya Magonjwa ya
Moyo ya Jakaya Kikwete yenye wataalamu wabobezi katika tiba ya magonjwa
ya moyo” Alimaliza Dkt. Ndugulile.
0 on: "SERIKALI YAWEKA MIKAKATI THABITI YA KUPAMBA DHIDI YA UGONJWA WA MOYO"