Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na Wadau wa Masuala ya Afya wakati akizindua Huduma ya TB kupitia
Teknolojia ya simu za mikononi leo jijini Dar Es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akimsikiliza Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na na
Ukoma wakati akizindua Huduma ya TB kupitia
Teknolojia ya simu za mikononi leo jijini Dar Es salaam.
Wadau mbali mbali wa Masuala ya Afya wakishiriki katika Uzinduzi wa Huduma ya TB kupitia
Teknolojia ya simu za mikononi leo jijini Dar Es salaam uliofanywa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile.
Picha ya pamoja ikionesha nyuso za Bashasha kuashiria Uzinduzi rasmi wa Huduma ya TB kupitia
Teknolojia ya simu za mikononi leo jijini Dar Es salaam uliofanywa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile.
Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati akizindua Huduma ya TB kupitia
Teknolojia ya simu za mikononi leo jijini Dar Es salaam.
MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YA SIMU KUSAIDIA KUTOKOMEZA TATIZO LA KIFUA KIKUU (TB)
Na WAMJW-DSM
SERIKALI
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imetoa wito kwa wananchi kutumia Teknolojia ya simu vizuri ikiwemo
kupata Elimu kuhusiana na masuala ya Afya.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katika Uzinduzi wa huduma ya TB kupitia
Teknolojia ya simu za mikononi leo jijini Dar Es salaam.
Dkt.
Ndugulile amesema kuwa zaidi ya Wananchi wa Tanzania Milion 40
wanamiliki simu hivyo kuwataka kutumia fursa hiyo kupata Elimu ya Afya
ikiwemo Elimu ya maambukizi ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB).
“zaidi
ya Watanzania Milion 40 wanamiliki simu za mikononi, wapo kwenye mfumo
wa mawasiliano katika taifa lenye watu zaidi ya Milioni 55, nawapongeza
kwa kuliona na kutambua hili kuangalia jinsi gani tunaweza kutumia
teknolojia katika masuala ya Afya” Alisema Dkt. Ndugulile.
Dkt.
Ndugulile aliendelea kusema kuwa Ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) unashika
nafasi ya 9 kwa kusababisha vifo duniani kote na ni ugonjwa pekee wa
kuambukiza unaoongoza ukifuatiwa na VVU.
Aidha,
Dkt Ndugulile alisema kuwa mwaka 2016 watu milioni 10.4 duniani
waliugua TB, milioni 1.7 walifariki dunia wakati milioni 4.3 million
hawakugunduliwa huku ripoti ya TB ya Shirika la Afya Duniani ya mwaka
2017 ikibainisha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 30 duniani zenye
wagonjwa wengi wa TB.
Kwa
upande mwingine Dkt. Ndugulile alisema kuwa jumla ya wagonjwa 69,818 wa
TB waligunduliwa ambapo asilimia 90 walitibiwa na kupona, huku
ikikadiliwa wagonjwa wanaofikiwa ni asilimia 44 ambapo kuna wagonjwa
84,000 wenye TB ambao bado wapo kwenye jamii na wanaendelea kuambukiza.
Mbali
na hayo Dkt Ndugulile alisema kuwa Lengo la Mpango Mkakati huo ni
kupunguza maambukizi ya TB nchini Tanzania ifikapo mwaka 2020 na
kupunguza maambukizi mapya ya TB kwa asilimia 20 na idadi ya vifo
vinavyotokana na TB kwa asilimia 35.
Hata
hivyo Dkt Ndugulile alisema kuwa Wizara itawezesha ufanisi na
ufuatiliaji wa mfumo huo na kuhakikisha kuwa taarifa zinakusanywa na
kutumika ipasavyo mfano idadi ya watu waliosajiliwa, idadi ya ujumbe
uliotumwa kwa walengwa, idadi ya wagonjwa wa TB waliogunduliwa na
ufuatiliaji wa wagonjwa kwa wakati muafaka.
Mwisho
Dkt. Ndugulile alitoa Rai kwa Wadau wote wa Masuala ya Afya kwenda
kutoa Elimu ya kupambana dhidi ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu kwenye maeneo
yenye changamoto ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu.
“Niwaombe
sana Wadau wetu, tusiende kwenye maeneo kwa urahisi wenu nyie wa
kufika, nawataka muende kwenye kwenye maeneo ambayo yanachangamoto kweli
ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu” alisema Dkt. Ndugulile.
Nae
Afisa Mwamasishaji kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kikufua Kikuu na
Ukoma Agatha Mshanga alisema kuwa Malengo ya Huduma ya TB kupitia
Mtandao wa Simu ni kuongeza uibuaji wa Wagonjwa wa Kifua Kikuu, Waliopo
kwenye matibabu waweze kuwa na ufuasi mzuri wa Matibabu, kupambana na
unyanyapaa na kutengwa kwa wagonjwa wa TB na kupeleka Elimu ya Ugonjwa
wa Kifua Kikuu (TB).
0 on: "MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YA SIMU KUSAIDIA KUTOKOMEZA TATIZO LA KIFUA KIKUU (TB)"