Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiongea na wakazi wa Naipanga wilaya ya Nachingwea
Mkoani Lindi wakati wa kilele cha Kampeni ya Furaha yangu iliyofanyika
mkoani humo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akipima Virusi vya Ukimwi wakati wa kilele cha
kampeni ya Furaha yangu iliyofanyika katika wilaya ya Nachingwea mkoani
Lindi.
Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile katikati ajumjulia hali mkazi wa Nachingwea
aliyejifungua wakati wa ziara yake ya kuangalia hali ya utoaji huduma
katika hospitali ya Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi .
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akikagua dawa zilizopo kwenye stoo ya kuhifadhia dawa
wakati wa ziara yake ya kujua hali ya utoaji huduma za afya katika
hospitali ya Wilaya ya Nachingwea mkoani lindi.
Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile wa pili kulia akisikiliza taarifa ya Wilaya ya
Nachingwea kutoka kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Bi. Rukia Mwango aliyesimama
kushoto wakati wa ziara yake Wilayani humo Mkoa wa Lindi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile kushoto akisikiliza maelezo kuhusu upimaji wa VVU
kutoka kwa Muuguzi Mkunga Bi. Hidaya Nyenje Hospitali ya Nachingwea
wakati wa Kilele cha kampeni ya Furaha yangu Wilayani humo.
WANAUME WASISITIZWA JUU YA KUPIMA VVU.
Na WAMJW-NACHINGWEA.
WANAUME
Mkoani Lindi Wilaya ya Nachingwea wamesisitizwa juu ya masuala ya
kupima virusi vya Ukimwi ili kujua hali ya maambukizi kwa wakazi wa mkoa
huo.
Hayo yamesemwa na
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile wakati wa kilele cha kampeni ya Furaha yangu leo
katika Tarafa ya Naipanga wilaya ya Nachingwea Mkoani humo.
"Kwa
sasa Serikali imejipanga kutomomeza maambukizi ya Ukimwi kwani kila
takayepima na kugundulika ana maambukizi ataanza kutumia dawa za
kufubaza virusi vya Ukimwi mara moja ili kufikia lengo la 909090 ifikapo
mwaka 2020" alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha
Dkt. Ndugulile amesema kuwa bado idadi ya wanaume wanaojitokeza kupima
VVU ni ndogo hivyo kuwataka wanawake wawahimize waume na vijana wao wa
kiume kujitokeza kutambu afya zao.
Sambamba
na hilo Dkt. Ndugulile aliutaka uongozi w Hospitali ya Wilaya ya
Nchingwea kuboresha mazingira ya kutunzia dawa, chanjo , damu na
vitendanishi kwani bado havipo kwenye mpangilio mzuri wa kuhifadhi.
"Kiukweli
mazingira ya Hospitali sijayapenda hivyo nawapa onyo kwa mara ya mwisho
na mchukue hatua haraka ya kuboresha mazingira yenu na hali ya utoaji
huduma na kuhakikisha kila mtumishi awe Daktari au Muuguzi kujaza
taarifa za mgonjwa kila anapomuhudumia kabla ya Serikali kuchukua hatua
stahiki dhidi yenu" alisisitiza Dkt. Ndugulile.
Aidha
Dkt. Ndugulile alibainisha kuwa Serikali imeipatia Wilaya hiyo kiasi
cha shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu
ya Hospitali ya Wilaya hiyo ili kuweza kutoa huduma bora za Afya kwa
wananchi wa Wilaya hiyo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya Mhe. Rukia Mwango amesema kuwa anayo furaha
kusikia hali ya maambukizi katika mkoa wao umepungua kutoka asilimia 3.
7 mpaka kufikia asilimia 0. 3.
Aidha Bi. Mwango
amesema kuwa wananachingwea hawana budi kujitokeza kupima VVU kwani
maendeleo yao yataletwa na wananchi wenye afya njema na kujitambua kwa
uchumi wa Nachingwea.
0 on: " WANAUME WASISITIZWA JUU YA KUPIMA VVU."