Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 30 Mei 2018

PICHA ZA MATUKIO YA ZIARA YA DKT. NDUGULILE KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA.

- Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Afya,  Maendeleo ya Jamii,  Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.  Faustine Ndugulile (Wapili kulia) akikagua miundombinu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma mapema leo.


Naibu Waziri wa Afya,  Maendeleo ya Jamii,  Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.  Faustine Ndugulile (wakwanza kushoto) akimjulia hali mmoja kati ya wagonjwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma mapema leo,  kulia kwake ni Mganga Mfawaidhi wa Hospitali hiyo Dkt.  Caroline Damian.

Naibu Waziri wa Afya,  Maendeleo ya Jamii,  Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.  Faustine Ndugulile akikagua cheti cha dawa cha mmoja ya wagonjwa waliofika kupata dawa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakati alipofanya ziara katika hospitali hiyo.

Naibu Waziri wa Afya,  Maendeleo ya Jamii,  Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.  Faustine Ndugulile akiongea na wagonjwa walio katika foleni ya kusubiri kupata huduma za Afya pindi alipofanya ziara mapema leo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Naibu Waziri wa Afya,  Maendeleo ya Jamii,  Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.  Faustine Ndugulile akipata maelekezo katika chumba cha utengenezaji wa miguu bandia katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma mapema leo.

Picha ya Pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya,  Maendeleo ya Jamii,  Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.  Faustine Ndugulileakiwa na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakati alipofanya ziara mapema leo.

Jumamosi, 26 Mei 2018

SERIKALI IMEJIPANGA VIZURI KUKABILIANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO,IKIWEMO EBOLA, ASEMA DKT. NDUGULILE

- Hakuna maoni

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akihoji ufanisi wa utendaji kazi wa moja ya mashine ya kupima na kutambua dalili za mgonjwa mwenye EBOLA zilizopo Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Afisa Afya Mfawidhi wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere Dkt. George Ndaki wakati alipofanya ziara katika Uwanja huo ili kujiridhisha na utendaji na ufanisi wa mitambo ya kutambua dalili za mgonjwa mwenye EBOLA.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiendelea na Ziara katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere jijini Dar es salaam akiongozana na mwenyeji wake Afisa Afya Mfawidhi wa Uwanja huo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine akitoa maelekezo kwa Afisa Afya Mfawidhi wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere Dkt. George Ndaki pindi alipofanya ziara leo katika uwanja huo.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika eneo la kupokelea mizigo wakati akiendelea na ziara yake, kulia kwake ni Afisa Afya Mfawidhi wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere Dkt. George Ndaki kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa huduma za kinga Dkt. Khalid Massa

 Picha ya muonekano wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere jijini Dar es salaam.


Na WAMJW-DSM
 
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imeridhika na maandalizi ya mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa ya milipuko ukiwemo ugonjwa wa Ebola katika mipaka yote na viwanja vya ndege nchini

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri Dkt.Faustine Ndugulile wakati wa ziara yake katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere 

Dkt.Ndugulile amesema amefika hapo ili kuangalia hali ya maandalizi na ufungaji wa mashine za kisasa za utambuzi wa ugonjwa wa Ebola endapo itatokea mtu mwenye ugonjwa huo

Aidha, alisema wizara imeimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa nchini na kuweka mfumo wa kubaini watu wanaoingia kwa kubaini hali ya joto linaloongezeka kwa  mgeni anayeingia na kufanyiwa uchunguzi zaidi.

"tumeweka mfumo wa kuwafuatilia wale ambao watakua wamebainika na joto zaidi mahali watakapofikia na mawasiliano yao ili kujua hali zao na endapo atapata mabadiliko"

Naibu huyo aliongeza kuwa wamewafanyia mazoezi ya kutosha kwa watoa huduma wa mipakani na viwanja vya ndege na pia kuwapatia elimu jinsi ya kukabiliana na ugonjwa huo.

Dkt.Ndugulile ameendekea kusisitiza na kuwatia hofu wananchi kwamba hadi sasa hakuna mtu alobainika kuwa na ugonjwa wa Ebola na hali ya mipaka ya Tanzania ni salama.

Ijumaa, 25 Mei 2018

SERIKALI YA TANZANIA IMEJIPANGA KUDHIBITI MAGONJWA YA MLIPUKO

- Hakuna maoni
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga.Dkt. Khalid Massa,(kulia) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani Dar es Salaam jana,kuhusu Serikali ya Tanzania ilivyojipanga kukabiliana na magonjwa milipuko ikiwemo Ebola. kushoto ni Dakitari wa Wizara ya Afya.Dkt. Faraja Msemwa.

Mwakilishi wa Shirika La Afya Duniani (WHO) Kutoka Uganda Dkt.Miriam Nanyunja, akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Taifa ya kukabiliana na magonjwa ya Milipuko ikiwemo Ebola. wakati wa kutathimini mikakati iliyowekwa na nchi kukabiliana na magon jwa hayo.kushoto ni Ofisa anaeshughulikia  magonjwa ya Milipuko.Dkt.Grace Saguti

Baadhi ya wanakamati wa Taifa wa kukabiliana na magonjwa ya Milipuko wakifuatilia kwa makini tathimini ya mikakati ya kutekeleza mpango wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mbalimbali ikiwemo Ebola DKT. NDUGULILE AITAKA AMREF KUWEKA MIKAKATI YAKIBUNIFU KATIKA KUPAMBANA NA VVU NA KIFUA KIKUU.

- Hakuna maoni
Mwakilishi kutoka Hospitali ya Benjamini Mkapa akibadilishana mkataba wa makubaliano na Mkurugenzi Mkazi wa amref health afrika Tanzania Dkt. Florence Temu baada ya kusainiwa na pande zote mbili wakati wa uzinduzi wa mradi wa amref health afrika wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaofadhiliwa na mfuko wa dunia.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisema jambo mbele ya Wakurugenzi na Wawakilishi kutoka taasisi zisizo za Kiserikali katika siku ya uzinduzi wa mradi wa amref health afrika wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaofadhiliwa na mfuko wa dunia (global fund).

Mkurugenzi Mkazi wa amref health afrika Tanzania Dkt. Florence Temu akisoma hotuba mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa uzinduzi wa mradi wa amref health afrika wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaofadhiliwa na mfuko wa dunia (global fund).

Mkurugenzi Mtendaji wa TAYOA Peter Masika akitoa neno la shukrani mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile, Wakurugenzi na Wawakilishi wa taasisi zisizo za Kiserikali wakati wa uzinduzi wa mradi wa amref health afrika wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu.

Wakurugenzi na Wawakilishi wa taasisi zisizo za Kiserikali wakifuatilia kwa makini tamko la Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa uzinduzi wa mradi wa amref health afrika wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaofadhiliwa na mfuko wa dunia (global fund).

Mkurugenzi Mtendaji wa TAYOA Peter Masika akibadilishana mkataba wa makubaliano na Mkurugenzi Mkazi wa amref health afrika Tanzania Dkt. Florence Temu baada ya kusainiwa na pande zote mbili wakati wa uzinduzi wa mradi wa amref health afrika wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaofadhiliwa na mfuko wa dunia.

Picha ya pamoja ikiongozwa na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile na Mkurugenzi Mkazi wa amref health afrika Tanzania Dkt. Florence Temu wakiwa na Wawakilishi wa taasisi zisizo za Kiserikali wakati wa uzinduzi wa mradi wa amref health afrika wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaofadhiliwa na mfuko wa dunia.


Na WAMJW.DSM
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile amelitaka Shirika la Afya lisilo Lakiserikali Amref kuweka mbinu na mikakati ya kibunifu katika kuanikisha afua mbali mbali za kupambana na magonjwa ya VVU na Kifua Kikuu.
Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mradi wa amref health afrika wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaofadhiliwa na mfuko wa dunia (global fund) mapema leo jijini Dar es salaam.
“Niwaombe watekelezaji wote wa Afua, katika mambo ambayo tunataka kuyaona ni pamoja na ubunifu, ubunifu wakufikia malengo lakini kitu kingine ni mikakati ya kufikia malengo” alisema Dkt. Ndugulile
Dkt. Ndugulile aliendelea kusema kuwa Serikali inatarajia kuona ifikapo 2020 malengo yote yanafanikiwa huku akiwataka kuzingatia matumizi sahihi ya fedha kulingana na malengo waliojiwekea.
“Tunatarajia, kwasababu ni nyinyi mlioandika uhitaji wa fedha na mlijiamini kabisa kwamba mnaweza kutekeleza hizo afua nendeni mkatekeleze, sisi Serikali tutaendelea kuwapa ushirikiano muda wowote na wakati wowote” alisema Dkt. Ndugulile
Aidha, Dkt Ndugilile alisema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau tumefanikiwa kutengeneza na kuweka miongozo mbalimbali ili kuhakikisha ufanisi na utaratibu mzuri unafuatwa katika kutekeleza mipango iliyoainishwa jambo litalosaidia kuepuka utendaji usio  sahihi na kutekeleza kwa namna yake.
Mbali na hayo alisema kuwa Serikali ya Tanzania inakusudia ifikapo mwaka 2022 asilimia 95% ya watu wote wanaoishi na Virusi vya UKIMWI kuwa kwenye dawa, Vile vile, kuhakikisha ifikapo 2022 asilimia 90% watoto waliofikia vigezo na wanaoishi na maambukizi wanabaki kwenye dawa na 95% ya watu wazima wanapatiwa ART na kuendelea kubaki kwenye dawa.
Kwa upande wa Kifua Kikuu Ndugulile alisema kuwa Kifua kikuu (TB) bado ni tatizo nchini kwetu huku jumla ya watu 160,000 wanakadiriwa kuwa na ugonjwa huu nchini Tanzania. Jumla ya Wagonjwa wapya wapatao 68,819 waliibuliwa  mwaka 2017 ikilinganishwa na 62,182 mwaka 2015.
Nae Mkurugenzi Mkazi kutoka Amref Dkt. Florence Temu alisema kuwa katika kufikia adhma ya Serikali kufikia asilkmia 90 ya waishio na VVU kuwa wamepima na kujua majibu yao, asilimia 90 ya wenye VVU kupatiwa tiba na asilimia 90 ya walio kwenye tiba za VVU wafanikiwe kufubaza VVU (90 90 90) Amref health Afrika ilihidhinishwa rasmi kuwa asasi itakayochukua jukumu la kusimamia na kuratibu afua za kwenye jamii zihusuzo VVU na Kifua Kikuu kwa kupitia Asasi ya kijamii.

Dkt. Temu aliendelea kusema kuwa mradi huu wa VVU na Kifua Kikuu wenye thamani ya shilingi Billioni 55 na Million 256 na Laki 7 ($ 24,969,174) wenye dhamira ya kufikia Watanzania 546,880 watafikiwa na huduma ya kupima VVU na kujua majibu, huku wasichana wa umri balehe na wanawake 162,064 ili kuibua na kuwapatia rufaa wenye maambukizi ya Kifua Kikuu wapatao 16,465 katika mikoa 15 ya Arusha, Dodoma, Kilimanjaro, Manyara, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Pwani, Shinyanga, Simiyu, Singida, Tanga na Ruvuma.

Alhamisi, 24 Mei 2018

WANAOHUSIKA NA KUUZA VIWANJA KATIKA ENEO LA KAMBI YA WAZEE NUNGE WAKAMATWE.

- Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua chakula wanachopikiwa wazee wa kambi ya Nunge iliyopo Kigamboni wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma kituoni hapo mapema leo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na moja ya binti wa Mhitaji anaeishi katika kambi hiyo ya Nunge iliyopo Wilaya ya Kigamboni, huku lengo la ziara hiyo likiwa kukagua hali ya utoaji huduma kituoni hapo.


Baadhi ya Wazee waliojitokeza katika ukumbi wa Kituo cha kulelea Wazee wa Nunge ili kupata fursa ya kuzungumza na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile pindi alipofanya ziara kituoni hapo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wananchi wake wa jimbo la Kigamboni Wilayani Kigamboni pindi alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma kituoni hapo mapema leo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya viongozi wa kituo cha kulelea wazee cha Nunge na wazee waliojitokeza kumsikiliza pindi alipofanya ziara kituoni hapo.


Na WAMJW-DSM.
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imeutaka uongozi wa Kambi ya Wazee na watu wasiojiweza Nunge kuwakamata wahusika wanaouza viwanja katika eneo la kambi hiyo .
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati akijibu kero za  Wazee wa  Nunge alipotembelea  kambi hiyo  iliyopo Kigamboni jijini Dar es salaam.
Sambamba na hilo Dkt. Ndugulile alisimamisha ujenzi wa nyumba ya mwananchi wan je na kambi hiyo  uliokuwa unaendelea katika eneo hilo ambalo inadaiwa sio muhusika wa eneo la kambi ya wazee ya Nunge na kusema aliyeuziwa katika eneo hilo Serikali haitamtambua.
“Marufuku kwa mtu yeyote kuuza,kununua wala kujenga  pamoja na kuchimba mchanga katika eneo la kambi hii na mtu atakayebainika anajihusisha na vitendo hivyo basi hatua za sharia zitafuata zidi yake “ alisisitiza Dkt. Ndugulile.
Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa misaada inayokuja katika kambi hiyo iwe inawekwa kwenye utaratibu maalumu ili kila mmoja aweze kupata mahitaji anayostahili kwa wakati husika na viorodheshwe kwenye daftari la kambi hiyo kama kumbukumbu ili kuondoa changamoto ya kurumbana kuhusu mahitaji kwa wazee hao.
Mbali na hayo Dkt.  ametoa muda wa wiki mbili tatizo la usafiri kwa wazee wa kambi hiyo liwe limeshughukulikiwa kwa kutengeneza bajaji iliyotolewa na Serikali kwa manufaa ya Wazee wa kambi hiyo na si vinginevyo.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha kambi ya wazee  Nunge Dkt. Dismas Chihwalo wakati akisoma taarifa fupi ya kituo hiko amesema kuwa ili uwepo utaratibu mzuri wa kuhudumia walengwa katika kambi hiyo ni lazima kuwepo na makualiano maalumu kwa kutia saini baina ya wanaoletwa kwa mahitaji maalum na viongozi wa kambi hiyo.
“Serikali inatakiwa kuhakikisha wanaoletwa kwa ajili ya huduma maalum na kwa muda maalum wanatia saini mkataba wa makubaliano ili kuweza kuepusha migogoro ya kutoa huduma katika kambi hiyo kwa wanaostahili” alisema Dkt. Chihwalo.
Kambi ya Wazee na wasiojiweza Nunge ilianzishwa mwaka 1936 kwa makusudi ya kuwahudumia Wazee na wasiojiweza pamoja na wenye ukoma ili wasipate shida za mahittaji muhimu na huduma za afya kwa wakati sahihi.
                                                                  

Jumatano, 23 Mei 2018

WANAWAKE WAJAWAZITO WANATAKIWA KUHUDHURIA KLINIKI MARA KWA MARA KUZUIA FISTULA.

- Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wakati akitoa tamko la ugonjwa wa Fistula katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam. 
Mkurugenzi wa Shirika la Amref Afrika Dkt. Floriance Temu akiongea na waandishi wa habari wakati maazimisho ya siku ya ugonjwa wa fistula Duniani mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la kimataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA) Bi Jacqueline Mahon akiongea na waandishi wa habari mbele ya Waandishi wa habari na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile.

Na WAMJW-DSM.
WANAWAKE wajawazito wanatakiwa kuhudhuria Kliniki mara kwa mara ili kuangalia maendeleo ya ujauzito wao na kupata vipimo na matibabu kama itagundulika kuna uwezekano wa kupata ugonjwa wa Fistula.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa kutoa tamko la ugonjwa wa Fistula katika kuadhimisha siku ya ugonjwa huo duniani.
“Asilimia 60 ya wanawake nchini ndiyo wanahudhuria Kliniki mara kwa mara hii ni dalili mbaya kwani kama mwanamke mjamzito anaweza kuwa na viashiria vya fistula hatoweza kugundulika mapema na kupata matibabu na badala yake asilimia 40 tu ndo wanaohudhuria Kliniki” alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha, Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kutokomeza ugonjwa huo Serikali kupitia Wizara ya Afya imeandaa mkakati wa kupeleka wataalam kwenye kila mkoa kujua idadi ya wagonjwa wa fistula ili kuweza kutokomeza ugonjwa huo.
Vilevile Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeimarisha na kukarabati vituo vya Afya vipatavyo 288 katika vitengo vya kuhudumia wenye uzazi pingamizi kwani hiyo nayo ni sababu inayopelekea kwa wanamke kupata fistula.
Hata hivyo Dkt. Ndugulile amesema kuwa huduma za Fistula zinapatikana Bure nchini hasa kwenye hospitali za CCBRT,Bugando na Celian hivyo mwanamke akijiona ana dalili za ugonjwa huo anatakiwa kuwahi katika kituo cha kutolea huduma za afya na kupata ushauri.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali linayoshughulikia mambo ya afya Dkt. Frolence Temu amesema kuwa katika kupambana na ugonjwa wa Fistula nchini wanajenga uwezo kwa watumishi wa Hospitali za Wilaya na Mkoa.
Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia idadi ya Watu UNFPA Bi. Jacqueline  Mahon amesema kuwa Shirika hilo limetoa mafunzo kwa watoa huduma za afya wapatao elfu nne ili kupamabana na ugonjwa huo.
“Mbali na kujengea uwezo watumishi hao pamoja na ukarabati wa vituo vya afya ,watanzania wanatakiwa kuacha vitendo vya udhalilishaji kwa wagonjwa wa fistula na wenye ugonjwa huu wajitokeze mara moja kwa ajili ya kupata matibabu” alisema Bi. Mahon.
Mbali na hayo Mkurugenzi Mkuu wa uendeshaji  hospitali ya CCBRT inashirikkiana na Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Fistula Hospitali yake inafanya matibabu kwa wagonjwa 1500 kila mwaka .
Ugonjwa wa Fistula huadhimishwa Mei 23 kila mwaka na maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo “BILA YA KUMUACHA MWANAMKE YEYOTE MWENYE TATIZO LA FISTULA NYUMA SHARTI TUDHAMIRIE KUTOKOMEZA FISTULA SASA”

HAKUNA MTU ALIYETHIBITIKA KUWA NA UGONJWA WA EBOLA NA HAKUNA UGONJWA HUU TANZANIA.

- Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari, viongozi wa Wizara na wawakilishi wa WHO wakati akitoa tamko kuhusu ugonjwa wa Ebola mapema leo katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.
 
Waandishi wa Habari kutoika vyombo mbali mbali wakifuatilia kwa makini tamko kuhusu gonjwa wa Ebola alilotoa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.


Na WAMJW - DSM.
NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto dkt. Faustine Ndugulile amethibitisha kuwa hakuna mtu aliyethibitika kuwa na ugonjwa wa EBOLA hapa nchini wala hakuna ugonjwa huo hapa Tanzania.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam mbele ya waandishi wa habari wakati akitoa tamko kuhusu ugonjwa wa EBOLA kama ilivyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwepo kwa ugonjwa huo hapa nchini.
“Napenda kuwatoa hofu watanzania kwamba hakuna ugonjwa wa EBOLA na wala hakuna mtu aliyethibitika kuwa na ugonjwa huo, hivyo tuendelee na shughuli za kujenga Taifa ila tunatakiwa tuchukue tahadhari za kujikinga juu ya ugonjwa huu” alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha, Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa EBOLA usiingie nchini Serikali imeweka vifaa vya kupima joto la mwili (themo scaner) pia wapo wataalamu wa Afya ambao  wanauliza hali ya wageni wanaoingia katika mipaka yote inayoizunguka nchi yetu ili kuzuia ugonjwa huo kuingia.
Dkt. Ndugulile amesisitiza kuwa, Serikali haijafunga mipaka ya nchi kwa sababu ya kujikinga na EBOLA.
"Tanzania hatujafunga mipaka na hatuwezi kufunga biashara za mipakani ila tumeimarisha ufuatiliaji wa watu wanaoingia nchini hususani maeneo ya viwanja vya ndege na mipaka mingine yote."
Mbali na hayo Dkt. Ndugulile ameitaka mikoa yote iliyo mipakani kudhibiti watu wote wanaoingia nchini kwa njia za panya ili kuepusha uingizaji wa ugonjwa huo kwa wananchi  huku akiwataka wafanyabiashara wa mipakani kutoa ushirikiano ili kudhibiti ugonjwa huo usiingie nchini.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani ambaye pia ni Afisa wa kushughulikia magonjwa ya kuambukiza Dkt. Grace Saguti amesema kuwa Wananchi wanatakiwa kupata elimu juu ya kujikinga na ugonjwa huo.
“Elimu inahitajika ya kutosha kwa wananchi wote hasa katika kufichua wagonjwa wa Ebola kama watagundulika hasa wanaotoka nje ya nchi ili kupata msaada kutoka kwa watoa huduma za afya walio yao juu ya kujikinga na ugonjwa huo.


Jumatano, 16 Mei 2018

WATUMISHI WA AFYA NCHINI WANATAKIWA KUCHUNGUZA WATOTO SARATANI YA MACHO KILA WANAPOHUDHURIA KLINIKI.

- Hakuna maoni
Mganga Mkuu wa Serikali ambaye ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Mohammed Bakari Kambi akitoa tamko la Saratani ya Macho kwa watoto mbele ya waandishi wa Habari hawapo pichani leo katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es salaam.

 Mkurugenzi wa Ubora wa Huduma za Afya Dkt. Mohammed Ali Mohammed kushoto na Mkurugenzi wa Kinga Dkt. Leonard Subi wote kutoka wizara ya Afya wakifuatilia kwa makini maelezo ya Mganga Mkuu wa Serikali ambaye ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Mohammed Bakari Kambi alipotoa tamko la Saratani ya Macho kwa watoto.

Kaimu Mkurugenzi  wa mpango wa Macho wizara ya Afya Dkt. Benadertha Shilio akizumza na waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusu wiki ya elimu ya Saratani ya Macho kwa watoto leo katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es salaam.

NA WAMJW-DAR ES SALAAM 

WATUMISHI wa Afya wa ngazi ya Jamii,Zahanati , Vituo vya afya vya na Hospitali za Kliniki za Mama na Mtoto za Wilaya zinatakiwa kuchunguza Uakisi wa mwanga kwenye mboni za watoto kila wanapoenda kucheki ukuaji wa watoto hao ili kupunguza uwepo wa saratani ya macho kwa watoto.
Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Serikali ambaye ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Mohammed Bakari Kambi wakati akitoa tamko la saratani ya macho kwa watoto kwa niaba ya Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es salaam.
“Iwapo mtoa huduma za afya unahisi kuwa mtoto ana tatizo kwenye jicho usimrudishe nyumbani hadi uhakikishe mtoto huyo ameonwa na mtaalamu wa macho ili kugundua kama ana tatizo kwenye macho yake” alisema Prof. Kambi.
Aidha Prof. Kambi amesema kuwa katika kuboresha huduma hizo Wizara imeandaa mwongozo ambao utasaidia kuinua uelewa wa wataalamu wa afya ili waweze kuwatambua watoto wenye tatizo hilo na kuwapa rufaa mapema.
Kwa Mujibu wa Prof. Kambi amesema kuwa takwimu za hapa nchini zinaonesha kuwa watoto137 wenye saratani hii walionwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kwa mwaka 2017 na watoto 80 hadi 100 hupewa rufaa na kufika kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na wengine hutibiwa KCMC Moshi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi  wa mpango wa Macho wizara ya Afya Dkt. Benadertha Shilio amesema kuwa anawashukuru wadau wote wa macho ambao wamekuwa bega kwa began a Serikali ya Tanzania katika kufanikisha kuboresha huduma za Macho kwa watoto.
“Tunawashukuru Rotary Club ya Dar es salaam Oysterbay wakishirikiana na Rotary Club ya Chelsea nchini Uingereza ambao wametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya kutibu Saratani ya macho vinavyogharimu kiasi cha Dola za Kimarekani 65,000 na Kampuni ya Pricewaterhouse ya Tanzania ambayo imetoa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 25 ambavyo vimesambazwa Muhimbili na Mloganzila” alisema Dkt. Shilio.
Maadhimisho ya Wiki ya sarani ya Macho kwa watoto kwa mawaka 2018 imebeba kauli mbiu isemayo “MBONI NYEUPE KWENYE JICHO LA MTOTO INAWEZA KUWA SARATANI YA MACHO”.