Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Serikali ambaye ni
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Mohammed Bakari Kambi wakati akitoa
tamko la saratani ya macho kwa watoto kwa niaba ya Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika ofisi ndogo za Wizara
Jijini Dar es salaam.
“Iwapo mtoa huduma za afya unahisi kuwa mtoto ana tatizo
kwenye jicho usimrudishe nyumbani hadi uhakikishe mtoto huyo ameonwa na
mtaalamu wa macho ili kugundua kama ana tatizo kwenye macho yake” alisema Prof.
Kambi.
Aidha Prof. Kambi amesema kuwa katika kuboresha huduma
hizo Wizara imeandaa mwongozo ambao utasaidia kuinua uelewa wa wataalamu wa
afya ili waweze kuwatambua watoto wenye tatizo hilo na kuwapa rufaa mapema.
Kwa Mujibu wa Prof. Kambi amesema kuwa takwimu za
hapa nchini zinaonesha kuwa watoto137 wenye saratani hii walionwa kwenye vituo
vya kutolea huduma za afya kwa mwaka 2017 na watoto 80 hadi 100 hupewa rufaa na
kufika kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na wengine hutibiwa KCMC Moshi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa mpango wa Macho wizara ya Afya Dkt.
Benadertha Shilio amesema kuwa anawashukuru wadau wote wa macho ambao wamekuwa
bega kwa began a Serikali ya Tanzania katika kufanikisha kuboresha huduma za
Macho kwa watoto.
“Tunawashukuru Rotary Club ya Dar es salaam Oysterbay
wakishirikiana na Rotary Club ya Chelsea nchini Uingereza ambao wametoa msaada
wa vifaa mbalimbali vya kutibu Saratani ya macho vinavyogharimu kiasi cha Dola
za Kimarekani 65,000 na Kampuni ya Pricewaterhouse ya Tanzania ambayo imetoa
vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 25 ambavyo vimesambazwa Muhimbili na
Mloganzila” alisema Dkt. Shilio.
Maadhimisho ya Wiki ya sarani ya Macho kwa watoto
kwa mawaka 2018 imebeba kauli mbiu isemayo “MBONI NYEUPE KWENYE JICHO LA MTOTO
INAWEZA KUWA SARATANI YA MACHO”.
0 on: "WATUMISHI WA AFYA NCHINI WANATAKIWA KUCHUNGUZA WATOTO SARATANI YA MACHO KILA WANAPOHUDHURIA KLINIKI."