Naibu wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile katikati akipata maelekezo kuhusu ujenzi wa Maabara
ya afya ya jamii ya Taifa kutoka kwa Mkandarasi Alex Musumi wa kwanza
kulia kutoka kampuni ya Ukandarasi WCEC wakati alipotembelea kuangalia
ujenzi huo leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt
Faustine Ndugulile katikati akikagua michoro ya jengo la Maabara ya
Taifa ya Afya ya Jamii wakati alipotembelea ujenzi wa maabara hiyo
unaoendelea jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile kulia akikagua jengo la Maabara ya Taifa ya Afya ya
Jamii wakati aliootembelea kukagua ujenzi huo leo jijini Dar es salaam ,
kushoto ni Mkurugenzi wa Ugavi na Manunuzi Wizara ya Afya Bw. Castro
Simba.
Muonekano wa jengo la Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii liliopo jijini Dar es salaam likiwa bado linaendelea na ujenzi.
Sambamba na hilo Dkt. Ndugulile ametembelea Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akikagua kitabu cha usajili wa dawa wakati alipotembelea Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA leo jijini Dar es salaam, kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bi. Agness Kijo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiangalia mitambo iliyo katika maabara ya chakula, wakati alipofanya ziara katika mamlaka hiyo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile katikati akipata maelezo kutoka kwa Mchunguzi wa Dawa
na vipodozi Gerald Sambu kulia wakati alipitembelea TFDA leo jijini Dar
es salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi TFDA Bi. Agness Kijo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile katikati akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa
Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA wakati alipotembelea mamlaka hiyo leo
jijini Dar es salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bi. Agness
Kijo.
Na WAMJW- DAR ES SALAAM.
UJENZI wa Maabara ya Afya ya Jamii ya Taifa inayohusiana na magonjwa ya mlipuko unatarajia kukamilika ifikapo Julai mwaka huu.
Hayo
yamebainishwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa ziara yake ya
kuangalia hali ya ujenzi wa maabara hiyo jijini Dar es salaam.
"Mpaka
hivi sasa asilimia 60 ya ujenzi imekamilika hivyo namsisitiza
Mkandarasi kwamba Serikali haitaongeza muda wa ziada mpaka kufikia
Julali 9 mwaka huu tuwe tumeshakabidhiwa jengo hili" alisema Dkt.
Ndugulile
Aidha, Dkt.
Ndugulile alisema kuwa Maabara hiyo ya Afya ya Jamii ya Taifa ni kwa
ajili ya kupima sampuli ya magonjwa ya mlipuko na itakuwa ni maabara
kubwa Afrika yenye kiwango cha ubora wa BS3 ambayo imegharimu kiasi cha
shilingi Bilioni 7. 6.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya ukandarasi ya WCEC Injinia Edwins
Shittindi amesema kuwa ujenzi huo ulitakiwa uwe umekamilika Oktoba mwaka
jana badala ya Julai 2018.
"Tulitakiwa
kukabidhi hiki jengo Oktoba 2017 lakini kutokana na vifaa ya kazi
tulivyoviagiza kuchelewa kuwasili tutajitahidi mpaka kufikia Julai 9
mwaka huu tuwe tumekabidhi jengo" alisema Eng. Shittindi.
Sambamba
na hilo Dkt. Ndugulile ametembelea Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA na
kuwataka waangalie sana watu wanaotangaza vipodozi vyao kwenye mitandao
ya jamii na kuandaa utaratibu husika kuhusu bidhaa hizo.
"Kila
kukicha kuna matangazo mengi sana kwenye mitandao ya jamii
yanayohusiana na vipodozi hivyo mnatakiwa kuchukua tahadhari na
kufuatilia kwa ukaribu kuhusu ubora wa bidhaa zao" alisema Dkt.
Ndugulile.
Dkt.
Ndugulile amesema kuwa TFDA wanatakiwa kuhakikisha ubora wa dawa ,
chakula pamoja na vipodozi unastahili ili watanzania waweze kutumia
bidhaa zenye usalama zaidi.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile leo ametembelea maeneo mbalimbali ya TFDA ikiwemo
sehemu ya usajili wa Dawa, maabara na kuweza kuongea na Uongozi wa
Mamlaka hiyo.
0 on: " MAABARA YA AFYA YA JAMII YA TAIFA KUKAMILIKA JULAI 2018"