JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WAZEE NA WATOTO
TANGAZO LA WATUMISHI
WALIOPATA UFADHILI KWA AWAMU YA PILI KWA MASOMO YA UZAMILI KWA MWAKA 2017/2018
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, anawatangazia
watumishi walioomba ufadhili wa masomo ya Uzamili kwa mwaka wa masomo 2017/2018
kuwa zoezi la uchambuzi wa maombi ya ufadhili kwa awamu ya pili umekamilika.
Jumla ya watumishi 17 wamechaguliwa kwa
awamu hii ya pili hivyo kukamilisha idadi ya watumishi 90 ambao wamepata ufadhili kwa mwaka wa masomo 2017/2018, ufadhili
huu unahusisha kulipiwa gharama za ada kwa kipindi chote cha masomo pamoja na
posho ya utafiti.
Watumishi
hawa waliochaguliwa wanatakiwa kuandika barua ya kukubali ufadhili huu pamoja
na kujaza mkataba wa makubaliano ya ufadhili (Bonding Agreement) na Wizara.
Wizara inasisitiza kuwa haitahusika kugharamia mafunzo ya mtumishi yeyote
ambaye hayuko kwenye orodha hii au ambaye yuko kwenye orodha hii lakini hatojaza
mkataba wa makubaliano ya ufadhili.
Kila
mtumishi aliyepata ufadhili atalazimika kuingia kwenye tovuti ya Wizara ya afya
ili kupata nakala ya mkataba ambao atatakiwa kujaza nakala tatu katika sehemu
zinazomhusu na sehemu ya “First guarantor” atajaza mwajiri wake au yeyote
mwenye mamlaka ya kusaini kwa niaba ya mwajiri wake kisha agonge muhuri wa
mwajiri na “guarantor” wa pili anapaswa kuwa mtu yeyote mwenye sifa za kuingia
mkataba kwa mujibu sheria za nchi. Mikataba hiyo (nakala tatu) ikikamilika
kujazwa itawasilishwa wizarani kwa kuambatishwa na picha 3 (passport size) ili
Wizara iweze kukamilisha kusaini mikataba hiyo. Kwa watumishi waliopo Dar es
Salaam wawasilishe mikataba hiyo ofisi ndogo ya Wizara iliyopo Dar es Salaam, na
wengine wawasilishe Makao Makuu ya Wizara yaliyopo Dodoma
Mwisho
wa kuwasilisha mikataba hiyo ni tarehe 25/05/2018. Mkataba wa makubaliano ya
Ufadhili (Bonding Agreement) unapatikana kwenye tovuti ya Wizara www.moh.go.tz.
Imetolewa
na;
Katibu
Mkuu (Afya),
Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Kitivo
cha Sanaa na Sayansi ya Maendeleoya Jamii,
Jengo
11,
S.L.P
743.
40478 DODOMA
04/05/2018.
0 on: "TAARIFA KWA UMMA"