Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Ijumaa, 25 Mei 2018

DKT. NDUGULILE AITAKA AMREF KUWEKA MIKAKATI YAKIBUNIFU KATIKA KUPAMBANA NA VVU NA KIFUA KIKUU.

Mwakilishi kutoka Hospitali ya Benjamini Mkapa akibadilishana mkataba wa makubaliano na Mkurugenzi Mkazi wa amref health afrika Tanzania Dkt. Florence Temu baada ya kusainiwa na pande zote mbili wakati wa uzinduzi wa mradi wa amref health afrika wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaofadhiliwa na mfuko wa dunia.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisema jambo mbele ya Wakurugenzi na Wawakilishi kutoka taasisi zisizo za Kiserikali katika siku ya uzinduzi wa mradi wa amref health afrika wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaofadhiliwa na mfuko wa dunia (global fund).

Mkurugenzi Mkazi wa amref health afrika Tanzania Dkt. Florence Temu akisoma hotuba mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa uzinduzi wa mradi wa amref health afrika wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaofadhiliwa na mfuko wa dunia (global fund).

Mkurugenzi Mtendaji wa TAYOA Peter Masika akitoa neno la shukrani mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile, Wakurugenzi na Wawakilishi wa taasisi zisizo za Kiserikali wakati wa uzinduzi wa mradi wa amref health afrika wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu.

Wakurugenzi na Wawakilishi wa taasisi zisizo za Kiserikali wakifuatilia kwa makini tamko la Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa uzinduzi wa mradi wa amref health afrika wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaofadhiliwa na mfuko wa dunia (global fund).

Mkurugenzi Mtendaji wa TAYOA Peter Masika akibadilishana mkataba wa makubaliano na Mkurugenzi Mkazi wa amref health afrika Tanzania Dkt. Florence Temu baada ya kusainiwa na pande zote mbili wakati wa uzinduzi wa mradi wa amref health afrika wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaofadhiliwa na mfuko wa dunia.

Picha ya pamoja ikiongozwa na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile na Mkurugenzi Mkazi wa amref health afrika Tanzania Dkt. Florence Temu wakiwa na Wawakilishi wa taasisi zisizo za Kiserikali wakati wa uzinduzi wa mradi wa amref health afrika wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaofadhiliwa na mfuko wa dunia.


Na WAMJW.DSM
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile amelitaka Shirika la Afya lisilo Lakiserikali Amref kuweka mbinu na mikakati ya kibunifu katika kuanikisha afua mbali mbali za kupambana na magonjwa ya VVU na Kifua Kikuu.
Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mradi wa amref health afrika wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaofadhiliwa na mfuko wa dunia (global fund) mapema leo jijini Dar es salaam.
“Niwaombe watekelezaji wote wa Afua, katika mambo ambayo tunataka kuyaona ni pamoja na ubunifu, ubunifu wakufikia malengo lakini kitu kingine ni mikakati ya kufikia malengo” alisema Dkt. Ndugulile
Dkt. Ndugulile aliendelea kusema kuwa Serikali inatarajia kuona ifikapo 2020 malengo yote yanafanikiwa huku akiwataka kuzingatia matumizi sahihi ya fedha kulingana na malengo waliojiwekea.
“Tunatarajia, kwasababu ni nyinyi mlioandika uhitaji wa fedha na mlijiamini kabisa kwamba mnaweza kutekeleza hizo afua nendeni mkatekeleze, sisi Serikali tutaendelea kuwapa ushirikiano muda wowote na wakati wowote” alisema Dkt. Ndugulile
Aidha, Dkt Ndugilile alisema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau tumefanikiwa kutengeneza na kuweka miongozo mbalimbali ili kuhakikisha ufanisi na utaratibu mzuri unafuatwa katika kutekeleza mipango iliyoainishwa jambo litalosaidia kuepuka utendaji usio  sahihi na kutekeleza kwa namna yake.
Mbali na hayo alisema kuwa Serikali ya Tanzania inakusudia ifikapo mwaka 2022 asilimia 95% ya watu wote wanaoishi na Virusi vya UKIMWI kuwa kwenye dawa, Vile vile, kuhakikisha ifikapo 2022 asilimia 90% watoto waliofikia vigezo na wanaoishi na maambukizi wanabaki kwenye dawa na 95% ya watu wazima wanapatiwa ART na kuendelea kubaki kwenye dawa.
Kwa upande wa Kifua Kikuu Ndugulile alisema kuwa Kifua kikuu (TB) bado ni tatizo nchini kwetu huku jumla ya watu 160,000 wanakadiriwa kuwa na ugonjwa huu nchini Tanzania. Jumla ya Wagonjwa wapya wapatao 68,819 waliibuliwa  mwaka 2017 ikilinganishwa na 62,182 mwaka 2015.
Nae Mkurugenzi Mkazi kutoka Amref Dkt. Florence Temu alisema kuwa katika kufikia adhma ya Serikali kufikia asilkmia 90 ya waishio na VVU kuwa wamepima na kujua majibu yao, asilimia 90 ya wenye VVU kupatiwa tiba na asilimia 90 ya walio kwenye tiba za VVU wafanikiwe kufubaza VVU (90 90 90) Amref health Afrika ilihidhinishwa rasmi kuwa asasi itakayochukua jukumu la kusimamia na kuratibu afua za kwenye jamii zihusuzo VVU na Kifua Kikuu kwa kupitia Asasi ya kijamii.

Dkt. Temu aliendelea kusema kuwa mradi huu wa VVU na Kifua Kikuu wenye thamani ya shilingi Billioni 55 na Million 256 na Laki 7 ($ 24,969,174) wenye dhamira ya kufikia Watanzania 546,880 watafikiwa na huduma ya kupima VVU na kujua majibu, huku wasichana wa umri balehe na wanawake 162,064 ili kuibua na kuwapatia rufaa wenye maambukizi ya Kifua Kikuu wapatao 16,465 katika mikoa 15 ya Arusha, Dodoma, Kilimanjaro, Manyara, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Pwani, Shinyanga, Simiyu, Singida, Tanga na Ruvuma.

0 on: "DKT. NDUGULILE AITAKA AMREF KUWEKA MIKAKATI YAKIBUNIFU KATIKA KUPAMBANA NA VVU NA KIFUA KIKUU."