Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumapili, 22 Septemba 2019

KINGA NI BORA KULIKO TIBA – RC SHINYANGA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Tellack akisisitiza jambo wakati akiongea na Wananchi wa Shinyanga katika mji wa Kahama ikiwa ni siku ya kufunga kwa Kampeni ya Kitaifa ya ” USICHUKULIE POA, NYUMBA NI CHOO” iliyofanyika katika viwanja vya Majengo, Kahama.

Mkuu wa Wilaya ya SShinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akieleza jambo wakati akiongea na Wananchi wa Shinyanga katika mji wa Kahama ikiwa ni siku ya kufunga kwa Kampeni ya Kitaifa ya ” USICHUKULIE POA, NYUMBA NI CHOO” iliyofanyika katika viwanja vya Majengo, Kahama.

Mratibu wa kampeni  ya ” USICHUKULIE POA, NYUMBA NI CHOO” akitoa salamu za Wizara ya  Afya mbele ya Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa ya Shinyanga Mhe Zainab Tellack, wakati wa kufunga Kampeni hiyo katika mikoa ya kanda ya ziwa, tukio limefanyika katika viwanja vya Majengo, Kahama Shinyanga.

Meza kuu ikiongozwa na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Tellack  wakati wa kufunga kwa Kampeni ya Kitaifa ya ” USICHUKULIE POA, NYUMBA NI CHOO” iliyofanyika katika viwanja vya Majengo, Kahama.

Umati wa watu uliojitokeza kumsikiliza mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Tellack wakati wa  kufunga Kampeni ya Kitaifa ya ” USICHUKULIE POA, NYUMBA NI CHOO” iliyofanyika katika viwanja vya Majengo, Kahama.


KINGA NI BORA KULIKO TIBA – RC SHINYANGA

Na Rayson Mwaisemba WAMJW-SHINYANGA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Tellack amewaasa Wananchi wa Mkoa huo kujikita katika huduma za kukinga kuliko kutibu magonjwa ili kuondokana na gharama kubwa zinazotumika katika kutibu kwenye ngazi ya familia na Serikali.

Wito huo ameutoa wakati akiongea na Wananchi wa Shinyanga katika mji wa Kahama ikiwa ni siku ya kufunga kwa Kampeni ya Kitaifa ya ujenzi wa vyoo bora na kuvitumia kwa usahihi ” USICHUKULIE POA, NYUMBA NI CHOO” iliyofanyika katika viwanja vya Majengo, Kahama.

Mhe. Zainab Tellack amesema kuwa idadi kuwa ya magonjwa ya mlipuko nchini kama vile kuhara na kipindupindu yanatokana na tatizo la kutokuwa na vyoo bora na kutonawa mikono kwa maji safi chirizika na sabuni hali inayopelekea kuingia gharama kubwa kutibu magonwa hayo.

“kuna maradhi mbali mbali ambayo Watanzania wanayapata, ambayo si ya lazima, maradhi kama Kipindupindu, Kuhara, Minyoo ambayo yanasababishwa na ukosefu wa vyoo, na kuvitumia kwa usahihi, huku wengine wakitoka vyooni hawanawi mikono matokeo yake wanakula kinyesi jambo linalopelekea kupata magonjwa ambayo yanawagharimu katika matibabu” Alisema Mhe. Zainab Tellack.

Aliendelea kutoa wito kwa kusisitiza, ujenzi wa choo bora na matumizi sahihi utasaidia kupunguza  matumizi ya dawa mara kwa mara ambayo hayana ulazima, jambo litalosaidia kupunguza usugu dawa, na madhara mengine madogo madogo yatokanayo na matumizi ya dawa.

Aidha, Mhe. Zainab Tellack ameahidi kuwa, kama Mkoa ifikapo Disemba 31 kaya zote katika Mkoa wa Shinya lazima zitakuwa na vyoo bora, na kuvitumia vyoo hivyo kwa usahihi ili kuendelea kujikinga dhidi ya magonjwa ya Kipindu pindu, kuhara na minyoo.

“Ndugu zangu Wanakahama na Shinyanga kwa ujumla sisi kama Mkoa tumeahidi, kwamba ifikapo Disemba 31, kaya zetu zote kwenye Mkoa huu lazima ziwe na vyoo, hilo ndugu zangu tunaweza, kama vijana wetu wanathamani kubwa kwanini tushindwe kujenga vyoo” alisema  Mhe. Zainab Tellack.

Katika Mkutano huo, Mhe. Zainab Tellack alikubaliana na Wananchi wa Mkoa huo kuwa ifikapo Disemba 31 kwa Wananchi wataokuwa hawana vyoo watapigwa faini ya kiasi cha shilingi 500,000 na kuchukuliwa hatua kali dhidi yao.

“Ambae hatokuwa na Choo bora ifikapo Disemba 31, faini 500,000 tumekubaliana hivyo, na mmesema wenyewe, na mimi nabariki hilo, kwa hiyo tujipange ili tusifike huko” Mhe. Zainab Tellack.

Kwa upande wake Mratibu wa Kampeni ya “USICHUKULIE POA, NYUMBA NI CHOO” Bw. Anyitike Mwakitalima amesema kuwa kila dakika moja Dunia inapoteza watu 4,  sawa na  watu 6000 kila siku, huku sababu ya vifo hivyo ikiwa kula  kinyesi hali inayotokana na kutotumia vyoo na kunawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni, huku wahanga wakubwa wa tatizo hili wakiwa Watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

"Kila dakika moja Dunia inapoteza watu 4, ikiwa inamaana kwamba kila siku Dunia inapoteza watu 6000, na hawa ni kwasababu tu wamekula kinyesi na wengi wao ni Watoto wenye umri chini ya miaka mitano" alisema Bw. Anyitike Mwakitalima

MWISHO.

Ijumaa, 20 Septemba 2019

SASA NI ZAMU YA DAR - MAFUNZO YA KUDHIBITI MAGONJWA KATIKA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA


Afisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora Wizara ya Afya Dkt. Joseph Hokororo akitoa mafunzo mbele ya Watumishi wa Sekta ya Afya wakati wa Semina ya mafunzo juu ya  kujikinga dhidi ya Maambukizi kwa kufuata miongozo yakutoa huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).


Bi. Laura Marandu, Afisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora Wizara ya Afya akitoa mafunzo ya jinsi yakumkinga kichanga dhidi ya maambukizi mapya kwa kufuata miongozo ya IP.

Mtaalamu wa Maabara Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikikishi MUHAS Bw. Akili Mawazo Mwakabhana akisisitiza jambo mbele ya Watumishi wa Sekta ya Afya Jijini Dar es salaam, wakati wa Semina ya mafunzo yakujikinga dhidi magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).
 
Afisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora wa Huduma Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Chrisogone Justine akijibu hoja wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata miongozo ya IPC wakati wa utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).
 

Baadhi ya Watoa Huduma za Afya na Watumishi wa Sekta ya Afya wakiwa katika  Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).Baadhi ya wawezeshaji wa Semina ya mafunzo juu ya namna yakujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline) wasahisha mitihani ya kupima uelewa iliyofanywa na Watumishi wa Sekta ya Afya ngazi ya Mkoa (RHMTs) na ngazi ya Halmashauri(CHMTs).


Picha ya Pamoja ikiongozwa na Wataalamu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto sambamba na Watoa Huduma za Afya na Watumishi wa Sekta ya Afya baada ya kumaliza Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline), Jijini Dar es salaam.SASA NI ZAMU YA DAR -  MAFUNZO YA KUDHIBITI MAGONJWA KATIKA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA.

Na WAMJW - DSM

Watu zaidi ya milioni.1.4 duniani wanaugua magonjwa yanayosababishwa na kupata maambukizi mapya wakati wa kupata huduma.

Hayo yameelezwa na Afisa kutoka kitengo  cha Uhakiki Ubora Wizara ya Afya Dkt. Joseph Hokololo wakati wa mafunzo njia ya kujikinga dhidi ya Magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa, katika maeneo ya utoaji huduma yaendelea Jijini Dar es salaam, ikiwa ni moja kati ya mikoa iliyo katika hatari ya kupata magonjwa ya  mlipuko ikiwemo ugonjwa wa Ebola kutokana na muingiliano wa watu kutoka nchi mbali mbali 

Dkt.Hokololo alisema kuwa maambukizi hayo hutokana na watoa huduma za afya afya kutofuata taratibu za namna ya kutoa huduma.

Katika mafunzo hayo ambayo yametolewa na Kitengo cha Uhakiki Ubora, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa timu za uendeshaji huduma za Afya ngazi ya Mkoa (RHMT) na za Halmashauri (CHMTs) za Mkoa wa Dar es salaam

"Timu za uendeshaji huduma za Afya mnatakiwa kusimamia miongozo ya kukinga na kudhibiti maambukizi (Magonjwa) wakati mnatoa huduma za Afya kwa Wagonjwa ili kudhibiti maambukizi mapya"Alisisitiza Dkt.Hokololo

Aliendelea kusema kuwa Asilimia 15 ya Wagonjwa hupata maambukizi ya magonjwa mapya pindi waendapo kupata huduma za Afya katika Vituo vya kutolea Huduma za Afya, kutokana na kutofuatwa kwa miongozo ya kutoa huduma za Afya (IPC Guideline, SOP).

Aidha, Dkt. Hokororo amesema kuwa Tanzania ipo kwenye hatari ya kupata wagonjwa wa Ebola kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu na ukaribu na Nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo ambako Mlipuko unaendelea.

Aliendelea kusisitiza kuwa, Serikali ya Tanzania tayari imekwisha kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha utayari wa kukabiliana na tishio la Ugonjwa huo ili kuhakikisha hauingii nchini, ikiwemo kuelimisha jamii njia za kujikinga na Ugonjwa ili kuzuia usiingie nchini, na kutoa Elimu kwa Watoa huduma za Afya juu ya kumuhudumia mtu mwenye dalili za Ebola endapo atatokea.

Kwa upande mwingine, Afisa kutoka Kitengo cha uhakika ubora Wizara ya Afya Bi. Laura Edward Marandu amesema kuwa kufuata miongozo ya utoaji huduma katika vituo vya kutolea huduma za Afya kusaidia kupunguza vifo vya vichanga pindi vinapozaliwa kwa kuvikinga dhidi ya maambukizi ya magonjwa yanayohusiana na sehemu za kutolea huduma za Afya (Health care associated infections)

Naye Mtaalamu wa Maabara kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi MUHAS Bw. Akili Mawazo Mwakabhana amesema kuwa kutofuata miongozo ya IPC ni moja ya chanzo kikubwa cha ongezeko la maambukizi ya magonjwa yanayopatikana katika vituo vya kutolea huduma (nosalcomial diseases)

Mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Medipeace, yanatarajia kuendelea katika mikoa yote iliyo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola ili kuhakikisha ugonjwa huo hauingii nchini.

MWISHO.