Picha ya Pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile pamoja na mgeni wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa Cuba Mhe. Marcelino Medina Gonzalez
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa Cuba Mhe. Marcelino Medina Gonzalez (hayupo pichani) katika kikao kujadili mahusiano baina ya nchi mbili kwenye Sekya ya Afya.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa Cuba Mhe. Marcelino Medina Gonzalez akifafanua jambo kwenye kikao kujadili mahusiano baina ya nchi mbili kwenye Sekya ya Afya.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akiagana na mbeni wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa Cuba Mhe. Marcelino Medina Gonzalez (kushoto) mara baada ya kumaliza kikao kujadili mahusiano baina ya nchi mbili kwenye Sekya ya Afya.
Katika mazungumzo yao, Dkt. Ndugulile ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Cuba kwa kuendelea kusaidia Sekta ya Afya nchini kwa kutoa madaktari bigwa kufanya kazi kwenye hospitali hapa nchini Tanzania.
Dkt. Ndugulile ametaka mahusiano hayo chanya yaendelee kuimarika ili Watanzania wengi wanufaike kwa kuweza kupata huduma bora za matibabu ya kibingwa.
“Nchi ya Cuba imepiga hatua kubwa kwenye Sekta ya Afya na wana madaktari bingwa wengi ambao tunaweza kuwatumia kuja hapa nchini kuhudumia Watanzania wengi zaidi ndani ya muda mfupi kuliko kupeleka wagonjwa nje” amesema Dkt.Ndugulile na kuendelea kusema kuwa pindi Madaktari hao wa kigeni wanapokuja hapa nchini, madaktari wa Kitanzania wanapata fursa ya kujifunza kwa vitendo na kutibu hapa hapa nchini kwa kutumia miundombinu iliyokuwepo hivyo kupunguza gharama kwa Serikali kusafirisha wagonjwa kwenda nje ya nchi.
Kwa upande wake Mhe. Marcelino Gonzalez ameipongeza Tanzania kwa juhudi kubwa inazozifanya kuwekeza kwenye Sekta ya Afya na kuhakikisha Madaktari wanapata utaalamu wa kutosha ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
Amesema kuwa nchi ya Cuba iko tayari kutoa nafasi za masomo kusomea fani ya udaktari ili kuja kutibu Watanzania.
Nchi ya Cuba imekuwa na mahusiano ya karibu na Tanzania kwa kipindi kirefu. Mnamo Mwaka 1964 ubalozi wa Cuba ulifunguliwa rasmi nchini Tanzania na miaka 10 baadaye mwaka 1974 Rais Fidel Castrol, alifika Tanzania kumtembelea Mwl.Julius Nyerere.Nchi ya Cuba na Tanzania Imekuwa na Mahusiano kwenye mambo mengi ikiwemo ushirikiano katika kutoa huduma za Afya.
0 on: "TANZANIA NA CUBA KUENDELEZA USHIRIKIAKO KWENYE SEKTA YA AFYA"