Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na kikundi cha watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI wakati alipotembelea mabanda mbalimbali kabla hajafungua kongamano la wadau wa Masuala ya UKIMWI linaloendelea Jijini Arusha.
Baadhi ya wajumbe wanaohudhuria kongamano la wadau mbalimbali wanaojihusisha na takwimu za ugonjwa wa UKIMWI linaloendelea jijini Arusha.
|
Na WAJMW-ARUSHA
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ametaka maboresho ya mifumo ya takwimu za tafiti
mbalimbali zinazofanyika nchini.
Dkt. Ndugulile amesema hayo wakati akizindua kongamano linalohusisha
wadau mbalimbali wa masuala ya UKIMWI ambao wanawasilisha tafiti na takwimu
mbalimbali ambazo zinaendelea kufanyiwa kazi nchini.
“Tunahitaji tuboreshe mifumo yetu ya takwimu ili tuwe na
uwiano wa takwimu ambazo zinawasilishwa katika mkutano huu, hapa nimeona takwimu
mbalimbali zimewasilishwa, ninaomba takwimu hizo ziwe za wote kwa sababu tuna
wadau wengi wanaoshiriki katika mapambano haya dhidi ya Ugonjwa wa UKIMWI hivyo
maelekezo yangu kuwe na mfumo mmoja wa takwimu ambao kila mmoja atakua anachangia
takwimu zake na mfumo huo uwe wa mwisho utakaotoa takwimu za wote”. Amesema
Dkt. Ndugulile.
Hata hivyo Dkt. Ndugulile amehamashisha makongamano kama
hayo yafanyike mara kwa mara ili kuwawezesha wanazuoni, watunga sera na
walengwa kukaa pamoja ili kujadiliana mambo mbalimbali ambayo yanahusuana na
afua ambazo zinatekelezwa hapa nchini.
Kongamano hilo limeshirikisha taasisi za Serikali ambazo ni
NIMR na TACAIDS pamoja na wadau mbalimbali wanaofanya tafiti kuhusiana na
ugonjwa wa UKIMWI ambao wamekutana ili kuwasilisha takwimu za tafiti mbalimbali
ambazo wanazifanyia kazi katika maeneo yao.
0 on: "DKT. NDUGULILE ATAKA MABORESHO YA MIFUMO YA TAKWIMU "