Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwasha gari
ishara ya uzinduzi wa magari hayo yaliyotolewa na Serikali kwa Halmashauri 61
ili kurahisisha shughuli za chanjo nchini.
Baadhi ya magari ya
yatayosaidia shughuli za chanjo yaliyoyolewa na Serikali kupitia Wizara ya Afya
kwa halmashauri 61 nchini, shughuli imefanyika katika ofisi za mpango wa chanjo
wa taifa Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikagua moja
kati ya majokofu ya kuhifadhia chanjo, ameambatana na Mkurugenzi wa Kinga
Wizara ya Afya Dkt Leonard Subi (wakatikati) na Meneja wa mpango wa taifa wa
Chanjo Dafrosa Lyimo (wakwanza kushoto) wakati wa kukabidhi magari ya chanjo
kwa Halmashauri 61 nchini.
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo
wakati wa mkutano na Waandishi wa habari
wakati wa kukabidhi magari ya chanjo kwa Halmashauri 61 ili kurahisisha
shugchanjo nchini.
Baadhi ya Waandishi wa
Habari na baadhi ya Waganga Wakuu wa Wilaya waliojitokeza katika shughuli ya
ugawaji wa magari ya chanjo kwa Halmashauri 61 nchini uliofanywa leo na Waziri
wa Afya Mhe Ummy Mwalimu
BILION 30 ZATOLEWA
KILA MWAKA KWAAJILI YA HUDUMA ZA CHANJO
Na WAMJW-DSM
Serikali kupitia
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto yatoa kiasi cha
shilingi Bilion 30 kila mwaka kwaajili ya huduma za Chanjo ili kuwakinga wananchi
dhidi ya magonjwa mbali mbali.
Hayo yamesemwa na
waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
leo wakati akikabidhi magari 71 ya chanjo kwaajili ya Halmashauri 61, na magari
10 kwaajili ya Mpango wa chanjo nchini ikiwa ni sehemu ya kuimarisha huduma za
chanjo kwa Wananchi.
Waziri Ummy amesema
kuwa, Serikali imetoa magari hayo ili kurahisisha shughuli za chanjo katika
maeneo mbali mbali hivyo, ameagiza magari hayo yakafanye kazi kulingana na
madhumuni yaliyokusudiwa.
Waziri Ummy
aliendelea kusema, Serikali itaendelea kuhakikisha kuwa Halmashauri zote
zilizobaki zinapata magari ya chanjo ili kurahisisha utendaji kazi katika
maeneo yote nchini.
Kwa upande mwingine
Waziri Ummy amesema kuwa, Serikali imetoa na kusambaza majokofu zaidi ya 1300
yanayotumia umeme wa sola katika Halmashauri zote nchini, jambo lililosaidia
kupunguza gharama za uendeshaji wa majokofu hayo.
“Nafurahi kwamba tumeweza kugawa majokofu
Zaidi ya 1300 yanayotumia umeme wa sola, lakini uzuri wa majokofu hayo ambayo
tumeyasambaza mwaka huu, yanatumia umeme wa sola, hivyo kupunguza gharama za
uendeshaji majokofu ambayo kwa mwezi yaligharimu kiasi cha shilingi Elfu 50
kwaajili ya mtungi wa gesi” Alisema Waziri Ummy.
Mbali na hayo,
Waziri Ummy ametoa wito kwa wazazi na walezi wote nchini kuhakikisha
wanawapeleka Watoto katika vituo vya kutolea huduma za Afya kupata chanjo ili
kuwakinga dhidi ya magonjwa ya surau na lubena.
“Tumeona mafanikio
mazuri katika kuwekeza kwenye chanjo, ikiwemo kupunguza vifo vya Watoto wenye
umri chini ya miaka mitano, kwa mfano mwaka 2005 tulikuwa na vifo 112 katika
kila vizazi hai 1000, laini sasahivi takwimu rasmi zinaonesha vifo 67” Alisema
Waziri Ummy
Hata hivyo, Waziri
Ummy amewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya wote nchini kuhakikisha
wanawafikia Watoto wote nchini walio na umri wa chini ya miaka mitano, kuwapa
huduma za chanjo ili kuwakinga dhidi ya magonjwa.
“Katika kila Watoto 100 ambao wanatakiwa kufikiwa kupatiwa chanjo, tumewafikia Watoto 98, kimataifa ni Zambia na Rwanda ndio waliotuzidi, lakini lengo letu ni kuwafikia hata hao Watoto wawili waliobaki” Alisema Waziri Ummy.
Aidha, Waziri Ummy
Amesisitiza Serikali itaendelea kuwekeza katika masuala ya chanjo kwani zipo
shahidi ya kisayansi ambazo zinaeleza kwa kuwekeza kila dola moja huokoa kiasi
cha dola 16.
“Kila mwaka serikali inatupa angalau sh.
bilioni 30 kwa kuwekeza katika chanjo tumeweza kupunguza vifo vya watoto chini
ya miaka mitano kutoka vifo 112 katika kila vizazi hai 1000 hadi kufikia vifo
67 kwa kila vizazi hai 1000 hivi sasa,” amesema.
Amesema Tanzania
kupitia jitihada ilizofanya sasa hivi katika kila watoto 100 ambao wanatakiwa
kupatiwa chanjo, watoto 98 wanafikiwa. “Ni watoto wawili ambao
tunawakosa...Barani Afrika, Tanzania ni nchi ya tatu, tumezidiwa na Rwanda
ambayo imewafikia zaidi ya asilimia 99 na Zambia tupo nao sawa kwa asilimia
98,” amesema.
Ameongeza “Lengo
letu japo tupo namba tatu kwanini tunawakosa hawa wawili katika 100 ambao
wanatakiwa kupata huduma za chanjo.
Kwa upande wake Meneja Mpango wa
Taifa wa Chanjo, Dk. Dafrosa Lyimo amesema ni jukumu la Serikali kuhakikisha chanjo
zipo na zinapatikana kwa wakati.
“Hadi sasa hatuna
upungufu wa chanjo, hatua hii (kukabidhi magari) ni muhimu sana, katika
utunzaji wa chanjo tunahakikisha kuna utunzaji kuanzia ngazi ya Taifa na
tunahakikisha zinasafirishwa katika mnyororo baridi na zinatunzwa vizuri,”
alisema.
Mwisho
0 on: "BILION 30 ZATOLEWA KILA MWAKA KWAAJILI YA HUDUMA ZA CHANJO "