Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 24 Februari 2020

VIFO VYA WANAWAKE WAJAWAZITO VYAPUNGUA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA TEMEKE



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiangalia kifaa cha uchunguzi kwenye idara ya meno    ambapo hivi sasa hospitali ya rufaa ya mkoa temeke wanatoa huduma za kibingwa za huduma ya meno.
Waziri Ummy Mwalimu akiwajulia hali wagonjwa waliofika hospitalini hapo

Waziri Ummy Mwalimu akiwajulia hali akina mama wajawazito waliolazwa kwenye wodi ya uzazi hospitalini hapo


Jengo la huduma za dharura lililofanyiwa ukarabati


Na. Catherine Sungura - Dar es Salaam 
 
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa temeke imejipanga kuokoa maisha ya wakina mama, wajawazito hususan katika kipindi cha kujifungua, kutimiza lengo hilo imeboresha miundombinu yake, vifaa tiba pamoja na kuimarisha huduma za afya kwenye ngazi za msingi.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, wakati wa ziara yake ya kikazi hospitalini hapo, ambako alikwenda kwa lengo la kusikiliza maoni na changamoto kutoka kwa wananchi na watumishi wa hospitali hiyo.

“Mwaka 2018 walikuwa na vifo 19 vya wajawazito na 2019 walikuwa na vifo 8 tu, lakini kwa takwimu za kuanzia Novemba 2019 hadi leo hakuna mwanamke mjamzito aliyekuja hospitalini hapa na kupoteza maisha, niwapongeze madaktari, wauguzi na watoa huduma wote wa hapa kwa hatua hii," amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa jitihada za makusudi, kuwekeza kwenye huduma za afya nchini sambamba na ujenzi wa vituo vya afya na ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa.

“Sasa hivi hapa temeke kuna huduma za kibingwa za meno ambapo zamani haikuwepo," amesema.

Waziri Ummy amesisitiza Wizara ina mpango pia wa kuhakikisha huduma zote za kibingwa zinazohitajika zinakuwepo kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa.

Hata hivyo amesema kuwa wanawake 15 kati ya wanawake 100 ndio ambao huhitaji kupelekwa kujifungulia kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa hususan wale wenye changamoto za ujauzito, kwa mfano mtoto amekaa vibaya au viashiria vya uzazi pingamizi.

Kwa upande  wa vipimo waziri huyo amesema kuwa Wizara yake imeongeza vipimo vya utra sound hivi sasa serikali imeboresha vituo vya afya na kwamba vipimo hivyo vinaanza kutolewa kuanzia ngazi za vituo vya afya vya umma na hospitali za wilaya nchini.

Amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma kuanzia ngazi ya msingi na hospitali za rufaa za mikoa ni kwa wagonjwa watakaopata rufaa.

“Kwa yeyeote atakayefanya makusudi kukorofisha vipimo ili watu waende kupima kwenye vutuo binafsi tutawachukulia hatua kwani ni wahujumu uchumi, tunataka vipimo vyote vifanyike ndani ya hospitali ila pale mashine haipo tutaruhusu, lengo letu ni kujitosheleza kwa vipimo vyote kwenye vituo vya afya vya umma," amesisitiza Waziri Ummy.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Yudas Ndungile amesema kuwa kutokana na maboresho ya miundombinu, wataalam na vifaa tiba kwa mkoa huu wameweza kupunguza vifo vipatavyo arobaini kwa mwaka ukilinganisha na vifo186 mwaka 2018 hadi vifo 140 mwaka 2019 na matarajio yao ni kupunguza zaidi.

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke Dkt. Meshack Shimwela amesema kuwa  hospitali hiyo imeondoa msongamano wa wajawazito kwa kuwa hivi sasa wananchi wengi wanafuata mfumo wa rufaa.

"Hivyo wakina mama wajawazito wanaofika kwenye hospitali hii ni wale wenye changamoto ya uzazi kwa maana hiyo wengi wanajifungulia kwenye ngazi za chini ambapo huduma za afya nazo zimeboreshwa," amesema.

MWISHO

Jumanne, 18 Februari 2020

WAGANGA WA TIBA ASILI/MBADALA FUATENI SHERIA-DKT. CHAULA


Dkt. Zainab Chaula, Katibu Mkuu Wizara ya AAfya akiongea na waandishi wa habari 

Na.Catherine Sungura, Chato

Waganja  wa Tiba asili na tiba mbadala wote  nchini, wametakiwa kufanya kazi zao kwa kufuata Sheria, kanuni, taratibu zilizowekwa na Serikali .

Hayo yamesemwa juzi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto-Idara kuu afya Dkt. Zainab Chaula alipozungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua kongamano la wajasiriamali lililoandaliwa na Chama cha Wanataaluma Waadventista Tanzania (ATAPE).

Dkt. Chaula alisema hadi sasa Tanzania  hakuna mgonjwa Corona wala dawa iliyothibitishwa kuwa na uwezo wa kutibu ugonjwa huo hapa nchini.

“Tanzania hakuna mgonjwa wa Corona wala dawa iliyothibitishwa kuwa na  uwezo wa kutibu ugonjwa huo, kwa yule ambaye ametangaza kwamba ana dawa, Serikali imechukua hatua".

Aidha, aliwataka waganga wa tiba asili/mbadala wote  wazingatie kufanya kazi zao kwa mujibu wa matakwa ya Serikali, "wizara kupitia kitengo cha tiba asili na tiba mbadala pamoja na msajili wa baraza hilo wametoa sheria na taratibu za kujisajili,lazima wajisajili, lakini wakifanya kazi bila kufuata ile misingi, bila kutii mamlaka iliyopo madarakani, hatutasita kumchukulia hatua yeyote atakayekiuka,” alisisitiza.

Dkt. Chaula aliwahimiza wananchi kuendelea kufuata kanuni za afya na maelekezo yanayotolewa na wataalamu ili kujikinga dhidi ya magonjwa ya mlipuko ambayo yanaendelea kuripotiwa katika maeneo mengine duniani kama vile Ebola na Corona.

Aliwahimiza wazazi kuwakatia watoto  wadogo na wale wanafunzi waliopo sekondari na vyuoni bima ya afya ili waweze kupata huduma za matibabu popote nchini wanapokuwa wagonjwa.

"Nawaona wanafunzi wa sekondari hapa ni vyema mzazi akakata bima ile ya elfu hamsini na mia nne(50,400) ili iweze kuwasaidia kupata matibabu mahali popote na kuwapunguzia mzigo wazazi pindi mtoto anapougua".