Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Alhamisi, 13 Februari 2020

NARUDISHA HUDUMA ZA CHAKULA CHUONI - DKT.CHAULA

 Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula na Watumishi wengine kutoka Sekta ya Afya wakimpiga jeki moja kati ya mwanachuo wa mwaka wa tatu wa chuo cha afya ya mazingira Kagemu.

Baadhi ya wanachuo wa chuo cha afya mazingira Kagemu wakimsikiliza Katibu Mkuu ambapo anewaahidi kurudisha huduma ya chakula na kufanya ukarabati jiko la chuoni hapo.

Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula akiwa kwenye picha ya pamoja na Wanachuo wa mwaka wa tatu wa chuo cha afya ya mazingira Kagemu.


NARUDISHA HUDUMA ZA CHAKULA CHUONI - DKT.CHAULA

Na. Catherine Sungura-Kagera

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula ameahidi kurudisha chakula kwa wanachuo wote ili kuondoa kupoteza muda wa kujipikia.

Dkt. Chaula ameyasema hayo mara baada ya kukitembelea chuo cha afya mazingira-Kagemu kwenye ziara ya usimamizi shirikishi akishirikiana na  TAMISEMI ambao wamefika chuoni hapo kuona mazingira ya chuo hicho ambacho kilipata madhara ya tetemeko la ardhi  lililotokea mkoani hapa mwaka 2016.

"Nitaanza ukarabati wa jiko na darasa,ninamwagiza  mkuu wa chuo afanye tahimini ili kila mwanafunzi awe na utulivu wa mwili na roho".

Aidha,Dkt. Chaula amekitaka chuo hicho kuanza mara moja kusafisha eneo la chuo hicho ili waanze kutengeneza matuta kwa ajili ya kulima bustani ambayo itasaidia kupunguza gharama ya kununua mahitaji mengine nje ya nchi.

"Uzalendo unaanzia vyuoni hivyo nitatoa fedha kwa ajili ya vibarua wasafishe eneo la shamba lote  na muanze kulima bustani,lazima mjifunze ujasiliamali mkiwa chuoni".

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera Dkt. Hasan Kawia  amesema wamepokea maagizo yote na kuahidi kuyafanyia kazi ikiwemo tatizo la gari la kuwapeleka mafunzo kwa vitendo wanafunzi hao mipakani

Dkt. Kawia amesema atamfikishia Katibu Tawala wa mkoa suala hilo kwani serikali  bado inawahitaji maofisa afya katika kulinda jamii isipate magonjwa hususani yale ya milipuko na vile vile kudhibiti magonjwa kutoka nchi jirani yasiingie nchini.

MWISHO

0 on: "NARUDISHA HUDUMA ZA CHAKULA CHUONI - DKT.CHAULA"