Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Alhamisi, 13 Februari 2020

KITENGO CHA MAGONJWA YA DHARURA KANDA YA KATI CHAZINDULIWA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge akiongoza zoezi la kukata utepe, ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Kitengo cha matibabu ya Magonjwa ya Dharura na Majeruhi kanda ya kati katika Hospitali ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma.

Muonekano wa vitanda na vifaa vya matibabu ndani ya Kitengo cha matibabu ya Magonjwa ya Dharura na Majeruhi kanda ya kati katika Hospitali ya Benjamini Mkapa iliyopo Jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge, akisalimiana na Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya Dkt. Leonard Subi baada ya tukio uzinduzi wa Kitengo cha matibabu ya Magonjwa ya Dharura na Majeruhi kanda ya kati katika Hospitali ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma.

Baadhi ya Watumishi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa waliojitokeza kushuhudia tukio la uzinduzi wa Kitengo cha matibabu ya Magonjwa ya Dharura na Majeruhi kanda ya kati katika Hospitali ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge baada ya  uzinduzi wa Kitengo cha matibabu ya Magonjwa ya Dharura na Majeruhi kanda ya kati katika Hospitali ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma.

Muonekana wa Jengo la Kitengo cha matibabu ya magonjwa ya dharura na majeruhi kanda ya kati katika Hospitali ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma.



KITENGO CHA MAGONJWA YA DHARURA KANDA YA KATI CHAZINDULIWA.

Na Rayson Mwaisemba, WAMJW-DOM

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge, leo amezindua Kitengo cha matibabu ya Magonjwa ya Dharura na Majeruhi kanda ya kati katika Hospitali ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma.

Katika uzinduzi huo Mhe. Dkt. Binilith Mahenge amesema kuwa, kitengo hiki ni mkombozi kwa wanachi wa Kanda ya kati hasa ukizingatia kuwa ujio wa Serikali hapa Dodoma umechagiza ongezeko na muingiliano wa watu jambo linaloweza kuongeza matukio ya ajali na magonjwa ya dharura.

“Kitengo hiki ni mkombozi kwa Wanachi wa Kanda hii hasa ukizingatia kuwa ujio wa Serikali hapa Dodoma umechagiza ongezeko na muingiliano wa watu jambo linaloweza kuongeza matukio ya ajali na magonjwa ya dharura jijini na maeneo yanayozunguka jiji la Dodoma,” alisema.

Aliendelea kusema kuwa, Hospitali ya Benjamin Mkapa pamoja na huduma zingine za afya ilianzishwa ili kutoa huduma za Kibingwa, hivyo Serikali inategemea  kuona kitengo hiki kikitoa huduma za kibingwa  kwa magonjwa ya dharura na majeruhi.

Aidha, Dkt. Binilith Mahenge amesema, Serikali iliingia makubaliano na Shirika la misaada la Israel (MASHAV- ISRAEL AGENCY FOR INTERNATIONAL DEVELOPMENT COOPERATION) kwa ajili ya kuboresha huduma za afya zinazotolewa BMH hususan wagonjwa wa dharula na majeruhi,

Mbali na hayo amesema kuwa, Shirika hilo limekubali kutoa  msaada wa vifaa vya kutoa huduma za dharula na kwa majeruhi na kutoa mafunzo kwa wataalamu wa afya wa Hospitali ya Benjamin Mkapa  juu ya utoaji wa huduma  hizo.

“Serikali iliingia makubaliano na Shirika la misaada la Israel (MASHAV- ISRAEL AGENCY FOR INTERNATIONAL DEVELOPMENT COOPERATION) kwa ajili ya kuboresha huduma za afya zinazotolewa hususan wagonjwa wa dharula na majeruhi, kwa kuboresha eneo la kutolea huduma pamoja na kutoa  msaada wa vifaa vya kutoa huduma za dharula na kwa majeruhi. Vilevile kutoa mafunzo kwa wataalamu wa afya” alisema.

Kwa upande mwingine amempongeza Mkurugenzi wa Hospitali ya benjamini mkapa na Watumishi  wake wote kwa jitihada kubwa mnazozifanya katika kuhudumia wananchi wa Kanda ya Kati na Tanzania kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa wa Dkt. Alphonce Chandika amesema kuwa, mpaka sasa kitengo hiki cha dharura na majeruhi kimeshahudumia zaidi ya wagonjwa  3,000.

“Kwa Kanda ya Kati, Kitengo hiki kiko  hapa Hospitali ya Benjamin Mkapa pekee. Na mpaka sasa zaidi ya wagonjwa 3,000 wamepata huduma kutoka katika kitengo hiki,” alisema Dkt. Chandika.

Aidha, Dkt. Chandika amemuomba Naibu Balozi kuendelea kutoa msaada wa  mafunzo mbalimbali kwa watumishi wa Benjamin Mkapa ili kuwajengea uwezo zaidi katika kitengo hiki cha dharula na kwenye maeneo mengine ya kibingwa, katika huduma ambazo zinatarajiwa kuanzishwa ikiwemo huduma za matibabu ya moyo, matibabu ya saratani, upandikizaji wa viungo.

Nae Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi ameishukuru amemuomba Naibu balozi Mheshimiwa Eyal David pamoja na madaktari alioambatana nao wasisite kuendelea kuisaidia Hospitali hii pale watakapohitaji msaada toka kwenu, huku akisisitiza kuwa, huu ni mwanzo mzuri wa ushirikiano kati ya Hospitali ya Benjamin Mkapa na Serikali ya Israel.

0 on: " KITENGO CHA MAGONJWA YA DHARURA KANDA YA KATI CHAZINDULIWA"