Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 5 Februari 2020

MAAMBUKIZI MAPYA YA MALARIA YAMEPUNGUA KWA ASILIMIA 27

 Katibu wa Chama cha TAPAMA Mhe. Raphael Chegeni akionesha kadi ya tathmini ya Malaria, wakati wa kikao cha uraghabishaji kwa Wakurugenzi na Wakuu wa vitengo wa Wizara ya Afya.

Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi akisikiliza maoni ya washiriki, wakati kikao na umoja wa wabunge wa kupambana na malaria na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Tanzania(TAPAMA) na Alma (African Leaders Malaria Alliance).

Mwakilishi wa Alma Tanzania Bw. Diego akiwasilisha mada kuhusu namna namna ya kuingia kwenye mfumo wa simu/kompyuta ya kadi ya tathmini ya Malaria ili kujionea utendaji wa Mkoa au hatua zinazochukuliwa kutatua matatizo ya eneo husika.

Picha ya pamoja kati ya Watumishi wa Wizara ya Afya na wabunge wa kupambana na Malaria na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Tanzania(TAPAMA) na viongozi wa Alma (African Leaders Malaria Alliance) waliofika Wizara ya Afya kufanya uraghibishaji wa  kadi ya tathimini ya malaria  kwa ajili ya uwajibikaji na utendaji kwa viongozi wa wizara jijini hapa.


MAAMBUKIZI MAPYA YA MALARIA YAMEPUNGUA KWA ASILIMIA 27

Na WAMJW - Dodoma.

Maambukizi mapya ya ugonjwa wa malaria yamepungua nchini   kwa asilimia 27 na hiyo ni kutokana na kuboreka kwa utoaji huduma za mapambano ya ugonjwa huo ukilinganisha na waginjwa 164 kati ya watu 1000 mwaka 2015 hadi wagonjwa 119 kati ya watu 1000 mwaka 2018.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Kinga Dkt. Leonard Subi wakati akitoa taarifa kwa umoja wa wabunge wa kupambana na malaria na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Tanzania(TAPAMA) na Alma (African Leaders Malaria Alliance) waliofika wizara ya afya kufanya uraghibishaji wa  kadi ya tathimini ya malaria  kwa ajili ya uwajibikaji na utendaji kwa viongozi wa wizara jijini hapa.

Dkt. Subi amesema kuwa mafanikio hayo yametokana na jitahada za viongozi wa Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na muhimili wa Bunge katika ushirikiano mzuri na wadau pamoja ma wananchi katika kupambana na ugonjwa huo.

Amesema kuwa viongozi wa nchi za afrika wanawajibika kwa afya za wananchi na hivyo kwa Tanzania vifo vitokanavyo na Malaria vimepungua  kwa asilimia 63 kutoka vifo 6,737 mwaka 2015  hadi 2,540 mwaka 2018.

“Ingawa hivi sasa tupo kwenye kudhibiti ila  tunalengo la kutokomeza,hivyo tuna imani kwamba tanzania tunao uwezo mkubwa wa kufikia huko kwani kuaniza Mh. Rais Wetu hadi muhimbili kama Bunge nao wako mstari wa mbele kuondosha malaria nchini”.

Aidha, amesema kuwa hivi sasa kumekuwa na mabadiliko makubwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini kwa kupungua kwa wagonjwa wanaougua malaria kupungua pia hata kwa watoto chini ya miaka mitano vifo vimepungua.

“Tanzania tumeamua kupambana na wadudu dhurifu kuanzia ngazi ya viluilui hadi mbu wapevu waenezao maradhi, hivyo kila mwananchi anawajibu wa  kuchukua hatua, hivyo ni vyema tukaungana ili kuiondosha Malaria nchini”.Amesema Dkt. Subi

Naye Katibu wa TAPAMA Mhe. Raphael Chegeni amesema kuwa msingi wa taifa ni kuwa na afya ,hivyo wanafarijika na afua zinazochukuliwa na wizara ya afya katika kupambana na malaria nchini “Malaria inaua hivyo tunajivunia kuona tanzania inazidi kupambana kutokomeza ugonjwa huu.

Kadi ya tathimini ya malaria ni kitendea kazi cha usimamizi kilichotolewa na wizara ya afya kinachoonyesha takwimu za utendaji wa viashiria vya malaria vilivyopewa kipaumbele katika ngazi ya mikoa na wilaya  ambayo inaleta urahisi katika kutambua wapi kuna tatizo ili hatua za kuokoa maisha ziweze kuchukuliwa.

Mwisho

0 on: "MAAMBUKIZI MAPYA YA MALARIA YAMEPUNGUA KWA ASILIMIA 27"