Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 17 Februari 2020

WATAALAM WA AFYA WATAKIWA KUHUWISHA LESENI ZAO

 Msajili wa Baraza la Famasi Elizabeth Shekhalage akikagua moja ya stoo ya dawa kwenye hospitali

Mfamasia kutoka kitengo cha huduma za dawa, wizara ya afya Daniel Pyuza akikagua moja ya stoo kwenye ziara ya katibu mkuu wa wizara hiyo.



WATAALAM WA AFYA WATAKIWA KUHUWISHA LESENI ZAO

Na. Catherine Sungura-Kasulu

Wataalam wa kada mbalimbali za afya nchini wametakiwa kuhuwisha leseni zao  kila mwaka.

Hayo yamesemwa na msajili wa baraza la wafamasia kutoka wiza ya afya Elizabeth Shekhalage wakati akiongea na watumishi wa hospitali ya halmashauri ya mji kasulu kwenye ziara ya katibu mkuu wa wizara ya afya

Msajili amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya mabaraza ya kitaaluma,kila anayestahili kuwa na leseni ni wajibu wake kuzingatia takwa hilo na hivyo kutimiza kwa mustakabari wa taaluma zao

"Kila mwaka mnatakiwa kutoka kwenye gazeti la serikali,hakikisheni wote mna leseni ili mtimize takwa la kisheria".Alisisitiza Shekhalage.

Kwa upande mwingine  Shekhalage aliwataka watumishi wa afya wenye maduka ya dawa,wawe na maduka ya mfano kwa kusajiliwa  kwani hakuna kifungu kinacho wazuia wasiwe nayo.

Aidha, aliwataka watumishi hao kutoa elimu kwa jamii kuhusu matumizi holela  ya dawa ambayo husababisha usugu wa vimelea  vya dawa kwa binadamu.

“Matumizi yasiyo sahihi ikiwemo kutumia dawa bila.kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na wataalam au kutotunza dawa vizuri  husababisha  athari  nyingi kwa binadamu ikiwemo kuongezeka kwa ugonjwa ama madhara yasiyo ya lazima kwa wagonjwa".Alisisitiza

Hata hivyo aliwataka wananchi  kuacha kununua dawa bila kwenda kwenye kituo cha kutolea huduma za afya kupara vipimo na kupata ushauri kutoka kwa wataalam.

-Mwisho-

0 on: " WATAALAM WA AFYA WATAKIWA KUHUWISHA LESENI ZAO"