Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumapili, 16 Februari 2020

WATUMISHI WA AFYA WAASWA KUTOSHIRIKI KWENYE UHALIFU WA KUHARIBU USHAHIDI

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisema jambo na watumishi wa afya (hawapo pichani) wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro.

Watumishi wa afya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa kwenye kikao na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (hayupo pichani) alipofanya ziara katika Hospitali hiyo.


Na Englibert Kayombo, WAMJW – Moshi Kilimanjaro.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewaasa watumishi wa afya kutoshiriki kwenye makosa ya uhalifu kwa kuharibu ushahidi wa makosa ya jinai pindi wanapofanya uchunguzi wa kitaalam.

Dkt. Ndugulile ametoa kauli hiyo alipokuwa ziarani katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro (Mawenzi) akizungumza na watumishi wa afya hospitalini hapo.

“Katika kosa ambalo hatutamsamehe mtumishi wa afya ni kushiriki katika uhalifu wa kuharibu ushahidi, hatutamvumilia mtu ambaye atashiriki kwenye makosa hayo” alisema Dkt. Ndugulile.

Alisema kuwa kesi za ukatili wa kijinsia mara nyingi huwa ni kesi za jinai huku wataalam wa afya wakipewa dhamana ya kuthibitisha ukweli wa matukio hayo na kuwataka kufuata miiko na maadili ya taaluma ya afya.

“Mtu amepata shambulio, daktari unasema kwamba huyu mtu hajashambuliwa, tumeshawahi kufanya hiyo na endapo tukithibitisha pasipo na shaka kwamba wewe mtaalam wetu umeenda kinyume na miiko na maadili ya kazi yako lazima tutakuchukulia hatua” alisisitiza Dkt. Ndugulile.

Mwisho

0 on: "WATUMISHI WA AFYA WAASWA KUTOSHIRIKI KWENYE UHALIFU WA KUHARIBU USHAHIDI"