Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 12 Februari 2020

WANANCHI KIJIJI CHA KALENGE WAISHUKURU SERIKALI KUWAJENGEA ZAHANATI

Katibu Mkuu Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akiwa na Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe, wakati wa ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma katika  Mkoa wa Kigoma.

Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Kalenge wilayani Uvinza wakifurahia ujio wa Katibu Mkuu Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula, kwa kuwajengea Zahanati na hivyo kuwahepusha na vifo vitokanavyo na uzazi.




Zahanati iliyojengwa katika Kijiji cha Kalenga Wilaya ya Uvinza ikiwa tayari kuanza kutoa huduma



WANANCHI KIJIJI CHA KALENGE WAISHUKURU SERIKALI KUWAJENGEA ZAHANATI

Na.Catherine Sungura-Uvinza

Wananchi wa kijiji cha Kalenge wilayani hapa wameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuwajengea zahanati na hivyo kuwahepusha na vifo vitokanavyo na uzazi.

Hayo yamebainishwa jana  na wakazi wa kijiji hicho wakati walipotembelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto-Idara Kuu Afya  Dkt. Zainab Chaula ambaye ameanza ziara ya usimamizi shirikishi mkoani kigoma ambayo inafanywa na wizara ya afya pamoja na TAMISEMI.

Akiongea kwa furaha bi. Marystela Chishako alisema kuwa wanaishukuru serikali ya awamu ya tano kwani kwa kupata zahanati hiyo imewasaidia kupata huduma za afya ikiwemo huduma ya kujifungua ambayo awali walikua wakiifuata kigoma mjini.

"Tunashukuru kwa serikali hii kutukumbuka mkoa wa kigoma,siku za nyuma mama akitaka kujifungua ilibidi aende kigoma mjini,ila hivi sasa tunajifungulia hapa hapa kwenye zahanati na tunapata huduma muhimu hapa hapa".

Aidha, alisema zahanati hiyo imewasaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto kwani kipindi cha nyuma walikua wakipata matatizo njiani kwa sababu walikua wakisafiri umbali mrefu na kupelekea kupata matatizo wakiwa njiani.

Katika Ziara hiyo Katibu Mkuu Dkt.Chaula aliwahidi kulifanyia kazi ombi lao la kupatiwa kituo cha afya kwani wameshaomba kwa kufuata utaratibu kupitia mkoa.

"Ninawapongeza kwa sababu mmejua umuhimu wa kuwa na kituo cha afya,kwahiyo maombi yataletwa wizara ya afya kutoka TAMISEMI,na katika ziara yangu nimeongozana nao hapa na nimepokea ombi hili najua ukitoa ahadi lazima utimize".Alisema Dkt. Chaula

Hata hivyo Katibu Mkuu huyo amesema atahakikisha wanapata fedha ili kutimiza ndoto za wananchi hao"mmefanya wajibu wenu na uzalendo mkubwa wa kuipenda nchi yenu kwa kujituma mpaka mmetenga eneo na kuweka mawe na mchanga, hivyo serikali itaongezea nguvu pale mlipoanzisha.

Wakazi wa kijiji hicho wametenga eneo la hekari ishiriki,kukusanya mawe pamoja na mchanga kwa kujitolea ili kuweza kujenga kituo cha afya ikiwa ni juhudi za kuiunga mkono serikali kwa kutatua changamoto za huduma za afya karibu na wananchi.

MWISHO

1 on: "WANANCHI KIJIJI CHA KALENGE WAISHUKURU SERIKALI KUWAJENGEA ZAHANATI"
  1. Kwakweli kuhusu kituo cha afya kwa hapa kalenge nimuda muafaka kwani sisi Wana nchi tunapata taabu sna.ndio maana tumesha jitolea mawe mchanga na tofari bila kusahau na hekati20.

    JibuFuta