Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 27 Februari 2019

NHIF YATAKIWA KUTOCHELEWESHA KADI ZA WANACHAMA


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akimkabidhi kadi ya Bima ya Afya Bw. Said Akili kutoka AMCOS ya Nyundo B iliyopo Halmashauri ya Nanyamba kijiji cha Nyundo, wakati alipofanya ziara ya kukagua utendaji kazi wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Mtwara na Lindi.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipitia majarada ya wateja wanalioomba kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya, wakati wa ziara ya kukagua utendaji kazi wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Mtwara na Lindi, na muitikio wa Wakulima kujiunga na Bima ya Afya Mkoa wa Mtwara na Lindi.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua idadi ya watu walioingizwa kwenye mfumo ili kupata kadi za Bima ya Afya, wakati wa ziara ya kukagua utendaji kazi wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Mtwara na Lindi, na muitikio wa Wakulima kujiunga na Bima ya Afya Mkoa wa Mtwara na Lindi.


Na WAMJW - MTWARA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameuagiza uongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kutatua changamoto ya uchelewaji wa vitambulisho vya bima ya afya kwa wananchi.

Ameyasema hayo mapema leo wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utendaji kazi wa mfuko huo Mkoa wa Mtwara, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya Mkoani hapo.

DKt. Ndugulile amesema kuwa NHIF ni lazima ihakikishe inawahudumia vizuri wananchi wanaokuja kujiunga katika mfuko huo, ikiwemo kuhakikisha ndani ya wiki mbili baada ya kujaza fomu, wateja wapate kadi zao.

"Tuendelee kuwahudumia vizuri, na kuhakikisha kwamba, ndani ya wiki mbili baada ya kujaza fomu na kukamilisha taratibu, waweze kupata kadi zao" alisema DKt. Ndugulile

Pia, Dkt. Ndugulile amesema Serikali imeridhishwa kwa kiasi kikubwa na mwitikio mzuri wa wananchi kujiunga na Bima ya Ushirika jambo litalowasaidia kupata huduma za afya katika vituo takribani 6,000 nchi nzima.

Aidha, Dkt. Ndugulile ameagiza NHIF kuweka utaratibu wa kuwafuata na kuwapatia kadi za bima wateja waliojiandikisha ili kuweka hamasa kwa wananchi wengine kujiunga na bima ya afya na kuwapunguzia usumbufu.

Mbali ya hayo DKt. Ndugulile ametoa onyo kwa watoa huduma za afya wanaofanya udanganyifu, na kuwataka watoe huduma kwa kufata sheria, na kwa mujibu wa miongozo ya Wizara ya Afya,

DKt. Ndugulile aliendelea kusema kuwa Serikali ipo katika hatua za mwisho za maboresho ya sheria ambazo zitatoa adhabu kali kwa yeyote atakayehusika na udanganyifu wowote utaopelekea hasara kwa Serikali.

Kwa upande mwingine DKt. Ndugulile amewaagiza watoa huduma za afya kuhakikisha wanawasilisha madai yao kwa NHIF kwa wakati, huku akisisitiza kuwa NHIF nayo inapaswa kulipa madeni kwa wakati.

"Haipendezi wananchi wanahudumiwa katika vituo vyetu vya kutolea huduma za Afya, na madai yanakaa zaidi ya miezi miwili au mitatu, kwahiyo niombe watoa huduma waharakishe madai yao, ili waweze kulipwa kwa wakati" alisema DKt. Ndugulile.

Nae Mkulima wa Korosho kutoka Halmashauri ya Nanyamba kijiji cha Nyundo, amewataka wakulima kupitia vyama vya Ushirika wajiunge na Bima ya Afya ili kuepuka gharama kubwa za matibabu na ugonjwa hauchagui muda wa kuja.

"Nimehamasika kujiunga na bima ya afya baada ya kuelewa kwamba ukulima una muda wa kupata pesa na una muda wa kukosa, alafu homa haichagui muda," alisema Bw. Said Akili.

Aidha Bw. Said Akili ameiomba Serikali kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za afya hasa kwa Wateja wanaotumia kadi za Bima ya Afya, jambo litalo wahamasisha wakulima wengi zaidi kujiunga na mfuko huo.

Jumanne, 26 Februari 2019

WATUMISHI SEKTA YA AFYA WAASWA KUTOFANYA KAZI KWA MAZOEA


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua Kadi inayoonesha Idadi ya Dawa katika Chumba cha dawa, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua  Idadi ya Wagonjwa waliosajiliwa kwenye mfumo, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipokea daftari la mama aliyemleta mwanae kupata huduma katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali hiyo. Wakatikati ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Lobikieki Kissambu

Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile baada ya kumaliza ukaguzi wa utoaji wa huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.


Na WAMJW - MTWARA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewaasa watumishi wa wekta ya afya nchini kuacha tabia ya kufanya kazi kwa mazoea, na wajikite katika kutoa huduma kulingana na sheria na taratibu za taaluma zao.

Ameyasema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya kwa wananchi katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara - Ligula.

Katika ziara hiyo Dkt. Ndugulile amesema kuwa licha ya jitihada za kuboresha huduma za afya kwa wananchi, ni wajibu wa kila mtoa huduma za afya nchini kuhakikisha anatimiza wajibu wake bila shurti na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

"Nyinyi mnafanya kazi kwa mazoea, kwa nini hamjajaza taarifa wala kusaini katika fomu ya wagonjwa, na hili linaendana na maelekezo ambayo Serikali tunawapa, kwamba kila mtu aandike tarehe na muda ambao amefanya kazi, nyinyi maabara hamfanyi" alisema Dkt. Ndugulile

Pia, Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeboresha vituo vya afya zaidi ya 300, ambavyo vitatoa huduma za dharura za upasuaji wakumtoa mtoto tumboni, na hospitali za wilaya 67, katika Mkoa wa Mtwara hospitali za wilaya 3 zinaenda kujengwa, ili kupunguza mzigo katika hospitali za mikoa,

Aidha, DKt. Ndugulile amesema kuwa amesema kuwa kutokana na Hospitali hiyo kuwa na Changamoto za x-ray na gari la kubebea Wagonjwa, Serikali imeahidi kuzitatua changamoto hizo kwa muda mfupi ili wananchi wa Mtwara waanze kupata huduma hizo mara moja.

"Mmeongelea huduma za mionzi (x-ray), niwaahidi tutawaletea mashine mpya ya x-ray za kidigitali, lakini vile vile kama kuna changamoto ya gari la kubebea wagonjwa, zikija tutazigawa, tunataka hospitali za mikoa zianze kuonekana kwamba ni hospitali za mikoa kweli" alisema Dkt. Ndugulile

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali inatambua pengo la watumishi katika sekta ya afya,  hivyo mwaka uliopita iliweza kuajiri watumishi takribani 11,000, huku watumishi 3000 kuziba pengo la watumishi ambao hawakuwa na vigezo, na 8000 walikuwa ni ajira mpya.

"Tumeweza kuajiri Watumishi takribani 11,000, 3000 kuziba pengo la watumishi ambao hawakuwa na vigezo na vyeti, na ajira mpya ni 8000, kuwahiyo jumla watumishi 11, kadri tunavoendelea kupata uwezo tutaendelea kuongeza rasilimali watu kuhakikisha kwamba tunaziba mapengo yaliyopo" alisema DKt. Ndugulile.

Jumatatu, 25 Februari 2019

TANZANIA NI MIONGONI MWA NCHI 50 ZENYE MIFUMO IMARA YA UDHIBITI UBORA BIDHAA ZA VYAKULA NA DAWAKatibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akisema jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wataalam wa udhibiti ubora wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA na Wakala wa Chakula, Dawa na vipodozi Zanzibar (ZDFA) Jijini Dar Es Salaam.

 

Picha ya Pamoja wajumbe wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula (aliyeketi wa tatu kulia)Na WAMJW- Dar es Salaam

TANZANIA yatajwa miongoni mwa nchi 50 kati ya 194 duniani zenye mifumo imara na madhubuti ya udhibiti wa ubora wa bidhaa za vyakula, dawa na vipodozi.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Zainab Chaula leo wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tano kwa wataalam wa udhibiti ubora wa Mamlaka ya Chakula na Dawa  Tanzania (TFDA), Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi (ZDFA) na wenzao kutoka nchi ya Malawi.

Mafunzo hayo maalum yameandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO-Tanzania) kwa lengo la kuwaongezea mbinu mbalimbali zitakazowasaidia kuimarisha nchi hizo kuongeza nguvu ya udhibiti wa bidhaa hizo.

 “WHO imetutambua na imetupa level (daraja) la tatu, hii ni hatua nzuri, TFDA imefanya kazi kubwa, hii inamaanisha mifumo ya udhibiti tanzania inatambulika duniani kote na kwamba misingi ya udhibiti ya mamlaka yetu imefikia ngazi ya kimataifa". Amesema Dkt. Chaula na kuongeza “Lakini pamoja na hatua hiyo lazima iendelee kujiimarisha ili ikiwezekana tupande daraja tufikie level 4 ambayo ndiyo kiwango cha juu zaidi".

“Ili tuweze kuhakikisha tunafanya vizuri zaidi, mamlaka yetu inapaswa kutengeneza mifumo ya ufuatiliaji ubora na usalama wa bidhaa kuanzia viwandani hadi kwa mtumiaji, ili kuhakikisha hakuna dawa bandia zinaingia nchini mwetu”.

Akiwasilisha mada Dkt. Alireza Khadem Broojerdi kutoka WHO amesema ili kuongeza nguvu ya udhibiti nchi zinapaswa kushirikiana kwa ukaribu.

“Tunayo malengo 17 ya kidunia (SDGs), lengo namba tatu linasisitiza juu ya afya bora kwa wote, tunayo pia malengo ya mwaka 2019- 2030, mpaka sasa nchi 50 ikiwamo Tanzania sawa na asilimia 26 zimefikia daraja la tatu na nne. Nchi 45 sawa na asilimia 23 zipo daraja la pili, nchi 96 zimefikia daraja la kwanza na zingine zilizobaki bado hazijafikia viwango hivyo,” amesema Dkt. Khademu.

Awali akizungumza Kaimu Mkurugenzi wa  TFDA, Dkt. Candida Shirima amesema kupitia semina hiyo iliyoandaliwa na WHO watajifunza mbinu mbalimbali  zitakazowasaidia kuweza kufikia malengo waliyojiwekea katika kuendelea kuimarisha mifumo ya udhibiti wa bidhaa hizo.

Jumamosi, 23 Februari 2019

HOSPITALI ZOTE NCHINI ZATAKIWA KUWA NA ICU YA WATOTO WACHANGA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akimtazama mtoto njiti, aliyepakatwa na mamaye,  wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiongea na mama Mjamzito wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akieleza Waandishi wa Habari (hawapo kwenye picha) umuhimu wa kifaa kinacho rekodi mahudhurio na muda wa watumishi kufika ofisini (Biometric)  wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akimjulia hali mama aliyetoka kujifungua, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akitoa maelekezo kwaMganga Mfawidhi, wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali hiyo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari Bingwa wa Hospitali teule ya Mkoa wa Pwani Tumbi, baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali hiyo.HOSPITALI ZOTE  NCHINI ZATAKIWA KUWA NA ICU YA WATOTO WACHANGA


NA WAMJW - PWANI

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameziagiza Hospitali za rufaa zote nchini kuwa na ICU kwaajili ya watoto wachanga ili kupunguza vifo vifo vyao.

Waziri Ummy amesema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.

Waziri Ummy  ameagiza hayo kupitia kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo kuwa ahakikishe watoto wachanga lazima wawe na ICU yao ili kuhakikisha vifo vya Watoto wachanga vinapungua nchini.

"Watoto wachanga wagonjwa, wawe na ICU yao, lengo letu kama Serikali ni kupunguza Vifo vya Watoto wachanga, kwasababu tukipunguza vifo vya Watoto wachanga, tutakuwa tumepunguza vifo vya Watoto wanye umri wa chini ya miaka mitano" alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa karibu 40% ya vifo vya watoto ni watoto wachanga na katika kila Watoto 100, Watoto 40% ni Wachanga, hivyo Serikali inaendelea kuchukua jitihada za makusudi ili kupunguza vifo hivi, ikiwemo kusisitiza kila Hospitali nchini kuwa na ICU.

"Karibu 40% ya vifo vya watoto ni watoto wachanga na katika kila Watoto 100, Watoto 40% ni Wachanga, kwahiyo Daktari ni lazima tulifanyie kazi agizo hilo" alisema Waziri Ummy.

Licha ya changamoto alizokutana nazo Waziri Ummy amesema kuwa Serikali inatarajia kujenga jengo mahususi kwaajili ya huduma za Dharura katika Hospitali zote za Rufaa za Mikoa nchini ili kuokoa maisha ya wagonjwa, hasa waliopata ajali.

"Nafurahi kusema, Serikali imeahapata fedha kwahiyo tutakuwa na jengo mahususi kwaajili ya huduma za Dharura na wagonjwa wa ajali, na hii tunataka iwe katika Hospitali za Rufaa za Mikoa zote ili mgonjwa aweze kuokolewa maisha muda mfupi anapofika Hospitali" alisema Waziri Ummy.

Pia, Waziri Ummy ameridhishwa kwa kiasi kikubwa juu ya hali ya upatikanaji wa dawa nchini, huku akiwatoa hofu Mwananchi kuwa Serikali kupitia Bohari ya Dawa (MSD) ina dawa zakutosha.

Aliendelea kusema kuwa Serikali imeainisha fani nane nane za kipaumbele ili kuwa na madaktari Bingwa wawili katika kila fani ikiwemo, Daktari Bingwa wa Watoto, Daktari Bingwa wa magonjwa yakina mama na uzazi, Daktari Bingwa wa upasuaji wajumla, Bingwa wa upasuaji wa mifupa, Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani (Physician) n.k

Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa katika Mkoa wa Pwani Serikali imejenga na kuboresha vituo vya Afya zaidi ya 16, Hospitali za Wilaya 3, na kuboresha Hospitali ya Mikoa ili kuwa na huduma za wagonjwa mahututi na wagonjwa wa Dharura.

Mbali na hayo Waziri Ummy amewahasa Mwananchi kujiunga na mfuko wa Bima ya Afyà ili kujihakikishia matibabu wakati wa ugonjwa, jambo litalosaidia kuokoa gharama kubwa za matibabu pindi Mwananchi anapopata ugonjwa.

"Nitoe Wito kwa Wananchi kujenga utaratibu wakujiunga na Bima ya Afya, kwasababu ndio njia ya uhakika yakujihakikishia matibabu kabla hawajaugua" alisema Waziri Ummy.

Mwisho.

TAARIFA WAKATI WA UPOKEAJI WA MAJOKOFU YA KUTUNZIA CHANJO NA VISHIKWAMBI KWA AJILI YA KUKUSANYA TAARIFA ZA CHANJO KATIKA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA HAPA NCHINI

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akitoa mfano kupitia kadi ya Kliniki, namna gani Mfumo utafanyakazi kwa kutumia kishikwambi, wakati akipokea majokofu ya kutunzia chanjo na vishikwambi (tablets) kwaajili ya kukusanyia taarifa katika vituo vya Afya hapa nchini, tukio limefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akipokea majokofu ya kutunzia chanjo, kutoka kwa Mkuu wa Masuala ya Afya UNICEF Kyaw Aung (Watatu kushoto)  tukio limefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam. Kulia kwa Waziri Ummy ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof Muhammad Bakari Kambi, Mkurugenzi wa Kinga Dkt. Leonard Subi na Meneja wa Mpango wa chanjo Taifa Dafrosa Lyimo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu   akipokea vishikwambi (tablets) kwaajili ya kukusanyia taarifa katika vituo vya Afya hapa nchini, kutoka kwa Mkuu wa Masuala ya Afya UNICEF Kyaw Aung, (Wakwanza kushoto)  tukio limefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam. Pembeni kwa Waziri Ummy ni Meneja wa Mpango wa chanjo Taifa Dafrosa Lyimo.TAMKO LA WAZIRI WA AFYA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), WAKATI  WA UPOKEAJI WA MAJOKOFU YA KUTUNZIA CHANJO NA VISHIKWAMBI KWA AJILI YA KUKUSANYA TAARIFA ZA CHANJO KATIKA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA HAPA NCHINI TAREHE 22.02.2019, D’ SALAAM.

Ndugu Wanahabari,
Naomba nichukue fursa hii kumshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kutuwezesha kukutana hii leo katika hafla muhimu.
Ndugu Wanahabari,
Kama mnavyofahamu, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  ilikusudia kuwa kila kijiji kiwe na zahanati na kila kata iwe na kituo cha afya kwa nia ya kuzileta na kusogeza huduma za afya karibu zaidi na wananchi. Kati ya huduma hizo muhimu ni pamoja na upatikanaji wa chanjo mbalimbali kwa ajili ya kuzuia magonjwa mbalimbali yakiwamo ugonjwa kupooza unaosababishwa na virusi ya Polio, ugonjwa wa kifaduro na donda koo, surUu rubella, kansa ya mlango wa kizazi, n.k. Chanjo hizi hutunzwa, kusafirishwa na kutolewa kwa walengwa zikipitia mfumo wa mnyororo baridi toka zinakotengenezwa hadi kituo cha kutolea huduma. Aidha, Wizara hutunza na kufuatilia takwimu mbalimbali za chanjo zinazoonyesha maendeleo ya utoaji huduma kwa kutumia mtandao wa komputa kote nchini.
Ndugu Wanahabari,
Napenda kuutarifu umma wa Tanzania kuwa, Serikali kwa kushirikiana na shirika la Gavi, imefanikiwa kununua jumla ya majokofu 1,385 yenye thamani ya shilingi bilioni 13,991,270,300 (serikali imechangia 20% na Gavi 80%) kwa ajili ya kuimarisha mnyororo baridi wa utunzaji wa chanjo katika vituo vya kutolea huduma za afya hapa nchini. Majokofu 1,190 yanatumia nishati ya jua na kila jokofu lina thamani ya shilingi milioni 10,879,000 (USD 4,730) na majokofu 195 yanatumia umeme, na kila jokofu lina thamani ya shilingi milioni 5,361,000 (USD 2,331). Vilevile Serikali na shirika la Gavi imenunua jumla ya vishikwambi (tablets) 1,249 vyenye gharama ya shilingi  bilioni 1,598,720,000 kwa ajili ya kukusanya na kuhifadhi taarifa za chanjo kwa njia ya mtandao, na kila kishikwambi kina thamani ya shilingi milioni 1,280,000.
Ndugu Wanahabari,
Majokofu na vishikwambi tunavyopokea leo ni awamu ya kwanza, ambapo mapema mwezi Mei tutapokea jumla ya vishikwambi 2100 venye thamani ya shilingi bilioni 2,688,000,000 na mwishoni mwa mwaka huu, tutapokea awamu nyingine ya majokofu (kati ya 800-1000) yenye thamani ya shilingi bilioni 11,533,357,820 (USD 5,014,503) na kufikia asilimia zaidi 80 ya mahitaji ya majokofu na vishikwambi katika vituo vyote hapa nchini.
Ndugu Wanahabari,
Majokofu haya ya kutunzia chanjo yatasambazwa na kufungwa katika vituo vipya na vituo vyenye majokofu yenye teknolojia iliyopitwa na wakati. Ifahamike kuwa, majokofu haya yanayotumia teknolojia ya kisasa ambapo, nishati ya jua inatumika kutoa ubaridi na hayahitaji kutumia betri, hivyo kuziondolea gharama halmasahuri za ununuzi wa gesi kila mwezi au manunuzi ya betri, kama yalivyo majokofu mengine yanayotumia nishati ya jua.
Ndugu Wanahabari,
Halmashauri zote za Tanzania Bara pamoja na Wilaya za Zanzibar zitapokea majokofu haya kwa awamu kuu mbili. Awamu ya kwanza itahusisha mikoa 15 ambayo ni Dodoma, Geita, Kagera, Kigoma, Lindi, Tanga, Mara, Mbeya, Mtwara, Mwanza, Shinyanga, Songwe, Unguja, Pwani na Singida. Na awamu ya pili itahusisha mikoa iliyobaki.
Ndugu Wanahabari,
Kama nilivyoeleza awali, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tamisemi, kupitia Mpango wa Taifa wa Chanjo imeanza kukusanya taarifa za chanjo kwa kutumia mifumo ya kielektroniki, ambapo katika ngazi ya kituo kishikwambi kitatumika kukusanya taarifa za chanjo kupitia mfumo wa kielektroniki wa leja ya Watoto (Tanzania electronic immunization Registry - TimR).
Ndugu Wanahabari,
Taarifa zilizokusanywa zitatumwa wilayani katika mfumo ujulikanao kama “Vaccine Information Management System (VIMS)” na kutumwa katika Mfumo Mkuu wa Kielektroniki wa Wizara (District Health Information System DHIS-2.
Ndugu Wanahabari,
Mfumo wa VIMS tayari umeanza kutumika katika mikoa na wilaya zote nchini na mfumo wa TimR kwa sasa unatumika mikoa ya Arusha, Tanga, Kilimanjaro na Dodoma. Wizara inakusudia kusambaza mfumo wa TimR katika mikoa ya Mwanza, Morogoro, Mtwara, Geita, Njombe na Dar es Salaam kabla ya kufika mwezi Aprili mwaka huu.
Ndugu Wanahabari,
Vile vile, ili kuhakikisha ufanisi na ufuatiliaji wa utendaji kazi wa majokofu ya kuhifadhia chanjo, Wizara ya Afya kwa kushikiana na wadau wa shirika la JSI na Nexleaf kwa ufadhili wa Gavi, inatarajia kufunga vifaa vya kupima na kufuatilia halijoto katika vituo takribani 5,000 kati ya vituo zaidi ya 7,000 kote nchini.
Ndugu Wanahabari,
Vifaa hivi vinamuwezesha Afisa Chanjo kujua utendaji kazi wa jokofu ikiwa ni pamoja na kujua halijoto ya jokofu katika vituo vya huduma za afya bila ya kulazimika kufika katika kituo husika. Vifaa hivi vinatuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) pindi halijoto inapopanda au kushuka.
Ndugu Wanahabari,
Tanzania itakuwa ni miongoni mwa nchi chache duniani zenye mfumo huu wa kisasa wa kufuatilia utendaji kazi wa majokofu ya chanjo na kuhakikisha watoto wanapatiwa chanjo zenye ubora wa hali ya juu wakati wote.
Ndugu Wanahabari,
Kwa namna ya pekee, napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza watoa huduma za chanjo hapa nchini, Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, pamoja na Waratibu wa Chanjo wa Mikoa na wilaya zote kwa kuwezesha nchi yetu ya Tanzania kufikisha viwango vya juu vya utoaji wa huduma za chanjo.
Ndugu Wanahabari,
Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa mwaka 2017 nchi yetu ilifikisha kiwango cha uchanjaji cha asilimia 98 na kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya tatu duniani kwa viwango vya juu vya utoaji wa huduma za chanjo. Mafanikio ya huduma za chanjo hapa nchini, pamoja na afua zingine, imeiwezesha nchi kufikia malengo ya milenia (MDG 4) kwa kupunguza vifo vya Watoto chini ya miaka mitano kwa theluthi 2/3.
Ndugu Wanahabari,
Napenda kuchukua fursa hii kuwasisitiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri pamoja na Waratibu wa Chanjo katika ngazi za mikoa na halmashauri, kuhakikisha kuwa watoa huduma wote wa chanjo wanafundishwa jinsi ya kufanya matengenezo madogomadogo ya majokofu (planned preventive maintenance) ili kuhakikisha kuwa vifaa hivi vinadumu kwa muda mrefu kama ilivyokusudiwa. Ni matarajio ya Wizara na Serikali kuwa, vifaa hivi vitaongeza upatikanaji wa huduma za chanjo karibu na wananchi na hivyo kupunguza idadi ya Watoto ambao hawajafikiwa na huduma za chanjo.
Ndugu Wanahabari,
Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wadau wote wa chanjo kwa kuendelea kutoa ufadhili na kuhakikisha kuwa kila mtoto anafikiwa kwa huduma za chanjo.
Ndugu Wanahabari,
Mwisho kabisa, napenda kuwahimiza wazazi na walezi wote hapa nchini kuwapeleka watoto wao katika vituo vya kutolea huduma za afya ili wakapate chanjo mbalimbali zinazotolewa kukinga magonjwa anuai. Halikadhalika, ninawahimiza mabinti wote waliotimiza umri wa miaka 14 wajitokeze ili kupata chanjo ya kuwakinga dhidi ya maambukizi ya saratani ya mlango wa kizazi kwani chanjo hii inatolewa bila malipo yoyote katika vituo vya serikali na binafsi. Dozi ya kwanza ya chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi inatolewa wakati wowote binti anapofikisha umri wa miaka 14 na dozi ya pili inatolewa miezi sita (6) baada ya dozi ya kwanza.

ASANTENI KWA KUNISIKILIZA

MGAWANYO WA MAJOKOFU
S/N
MKOA
WILAYA
IDADI YA MAJOKOFU
1
DODOMA
BAHI
9
KONDOA DC
21
KONGWA DC
20
MPWAPWA DC
28
JUMLA
78
2
GEITA
BUKOMBE DC
6
CHATO DC
14
GEITA DC
17
GEITA TC
7
MBOGWE DC
12
NYANG’WALE DC
8
JUMLA
64
3
KAGERA
BIHARAMURO
6
BUKOBA DC
25
KARAGWE DC
23
KYERWA DC
22
MISENYI DC
21
MULEBA DC
24
NGARA DC
20
BUKOBA MC
7
JUMLA
148
4
KIGOMA
BUHIGWE DC
6
KAKONKO DC
4
KASULU TC
5
KIBONDO DC
3
KIGOMA DC
14
KIGOMA MC
1
UVINZA DC
10
JUMLA
43
5
LINDI
KILWA DC
23
LINDI DC
25
LINDI MC
5
NACHINGWEA DC
20
LIWALE DC
21
RUANGWA DC
11
JUMLA
105
6
MARA
BUNDA DC
10
BUTIAMA DC
18
MUSOMA DC
25
MUSOMA MC
11
SERENGETI DC
28
TARIME DC
25
RORYA
28
JUMLA
145
7
MBEYA
BUSOKELO DC
10
CHUNYA DC
21
KYELA DC
18
MBARALI DC
18
MBEYA CITY
3
MBEYA DC
20
RUNGWE DC
21
JUMLA
111
8
MTWARA
MASASI DC
29
MASASI TC
7
MTWARA MC
6
MTWARA DC
10
NANYAMBA
11
NANYUMBU DC
15
NEWALA DC
14
NEWALA TC
9
TANDAHIMBA DC
6
JUMLA
107
9
MWANZA
BUCHOSA DC
17
ILEMELA DC
15
KWIMBA DC
27
MAGU DC
11
MISUNGWI DC
26
SENGEREMA DC
16
UKEREWE DC
18
NYAMAGANA DC
16
JUMLA
146
10
PEMBA
CHAKE CHAKE
8
MICHEWENI
10
MKOANI
11
WETE
8
JUMLA
37
11
SHINYANGA
KISHAPU DC
25
MSALALA DC
16
SHINYANGA DC
17
SHINYANGA MC
10
USHETU DC
17
KAHAMA TC
7
JUMLA
92
12
SONGWE
ILEJE DC
26
MBOZI DC
28
MOMBA DC
23
SONGWE DC
15
TUNDUMA TC
4
JUMLA
96
13
UNGUJA
KASKAZINI A
5
KASKAZINI B
8
KATI
14
KUSINI
5
MAGHARIBI
14
MJINI
12
JUMLA
58
14
PWANI
BAGAMOYO DC
8
CHALINZE DC
22
JUMLA
30
15
SINGIDA
ITIGI DC
5
16
TANGA
BUMBULI
9
HANDENI DC
19
KILINDI DC
14
KOROGWE DC
16
KOROGWE TC
2
LUSHOTO DC
8
MKINGA DC
14
MUHEZA DC
24
PANGANI DC
14
JUMLA
120


JUMLA KUU
1385

                                                                                                                                             
MGAWANYO WA VISHIKWAMBI
S/No
MKOA
IDADI YA VISHIKWAMBI
1
DAR ES SALAAM
300
2
MWANZA
350
3
MTWARA
100
4
NJOMBE
236
5
GEITA
143
6
MOROGORO
120

JUMLA
1249