Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akisisitiza jambo leo wakati akiongea na Waandishi wa Habari
katika siku ya Saratani Duniani, iliyofanyika katika Ukumbi wa Idara ya
Habari Bunge jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akiteta jambo na Mkurugenzi wa Ubora kutoka Wizara ya Afya Dkt.
Mohammed Mohammed ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya.
Mkurugenzi wa Ubora ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt.
Mohammed Mohammed akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya
Afya Dkt. Grace Maghembe leo katika tamko la siku ya Saratani Duniani
lililofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Bunge jijini Dodoma.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu wakati akitoa tamko
la siku ya Saratani Duniani, leo jijini Dodoma
Waandishi wa Habari wakifuatilia tamko la Saratani lililosomwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo katika Ukumbi wa Idara ya habari Bungeni jijini Dodoma.
CHANJO YA MLANGO WA KIZAZI HAIHUSIANI NA UZAZI WA MPANGO.
Na WAMJW - DOM
WAZIRI
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu
amewatoa hofu Wananchi kwa kusisitiza kuwa chanjo ya kuwakinga wasichana
na Saratani ya Mlango wa kizazi haihusiani na uzazi wa mpango wala
kumzuia msichana kuja kupata uja uzito baadae.
Ameyasema
hayo leo wakati akiongea na Waandishi wa Habari katika siku ya Saratani
Duniani, iliyofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari Bunge jijini
Dodoma, huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni "NITAFANYA JITIHADA ZOTE
KUPUNGUZA JANGA LA SARATANI DUNIANI".
Waziri
Ummy amesema kuwa Chanjo ya Mlango wa kizazi ni salama na
imethibitishwa na Shirima la Afya Duniani kwaajili yakuwakinga Wasichana
dhidi ya maambulizi ya Saratani ya Mlango wa kizazi.
"
Chanjo ya kuwakinga wasichana na saratani ya mlango wa kizazi
haihusiani na uzazi wa mpango, ni chanjo ambayo imethibitishwa na
Shirika la Afya Duniani kwaajili yakuwakinga wasichana dhidi ya
maambukizi ya Saratani ya mlango wa Kizazi" Alisema Waziri Ummy
Waziri
Ummy amesema kuwa katika kila wagonjwa wa Saratani 100, takribani
wagonjwa 31 ni wanawake wa Saratani ya Mlango wa kizazi, hivyo amewahasa
wazazi na walezi nchini kuhakikisha wasichana wanaostahili kupata
chanjo hii, wanaipata bila vikwazo vyovyote ili kutokomeza kabisa
Saratani hii nchini.
"Katika
kila wagonjwa wa Saratani 100, Wagonjwa takribani 31 ni wanawake wa
Saratani hii ya Mlango wa kizazi, kwahiyo hatuna haja ya kuiogopa chanjo
hii kwasababu ndio itayowakinga watoto wetu na maambukizi ya Saratani
ya mlango wa kizazi" alisema Waziri Ummy.
Aidha,
Waziri Ummy amesema kuwa kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Tafiti za Saratani (IARC), zinaonyesha kwamba kwa Tanzania kunatokea
mgonjwa 1 wa Saratani kwa kila watu 1000, hivyo Tanzania inakua na
wagonjwa wapya wa Saratani 55,000 kwa mwaka na takribani wagonjwa 28,610
hufariki kwa mwaka, ambapo ni vifo asilimia 52 ya wagonjwa wapya.
Aliendelea
kusema kuwa Taarifa kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road zinaonesha
kwamba kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wa Saratani mwaka hadi mwaka,
huku akisema kuwa Mwaka 2015 wagonjwa wapya 5,764, huku mwaka 2016
wagonjwa wapya 6,338, na mwaka 2017 wagonjwa wapya 7,091, pia mwaka
2018 wagonjwa wapya 7,649.
Kwa
upande mwingine Waziri Ummy amedai kuwa Serikali imeanzisha huduma
kwenye vituo 624 vilivyopo katika Halmashauri mbalimbali nchini ambapo
jumla ya wanawake 375,522 walifanyiwa uchunguzi wa saratani ya mlango wa
kizazi na saratani ya matiti mnamo mwaka 2017, ukilinganisha na
wanawake 416,841 waliofanyiwa uchunguzi huo mwaka 2018. Kati ya hao,
wanawake 16,147 waligundulika kuwa na mabadiliko ya awali mwaka 2017, na
wanawake 18,341 mwaka 2018.
0 on: "CHANJO YA MLANGO WA KIZAZI HAIHUSIANI NA UZAZI WA MPANGO"