Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumanne, 12 Februari 2019

DKT. NDUGULILE AKASIRISHWA NA KASI YA UJENZI WA MAABARA YA AFYA YA JAMII

Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifanya ukaguzi wa chumba kwa chumba ili kujidhisha na maendeleo ya ujenzi wa jengo la Maabara ngazi ya tatu yenye uwezo wa kuchukua vipimo vya magonjwa hatari Duniani kama Virusi vya Ebola, Mabag n.k, unaojengwa  katika eneo la Mabibo jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongoza katika ziara ya kukagua ujenzi wa jengo la Maabara ngazi ya tatu yenye uwezo wa kuchukua vipimo vya magonjwa hatari Duniani kama Virusi vya Ebola, Mabag n.k, leo katika eneo la Mabibo jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (Wakwanza Kulia) akipata maelezo ya mradi ulipofika kutoka kwa Meneja Mradi (Wapili kutoka kushoto) wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa jengo la Maabara ngazi ya tatu yenye uwezo wa kuchukua vipimo vya magonjwa hatari Duniani kama Virusi vya Ebola, Mabag n.k, leo katika eneo la Mabibo jijini Dar es salaam.

Muonekano wa jengo la Maabara ngazi ya tatu lenye  uwezo wa kuchukua vipimo vya magonjwa hatari Duniani kama Virusi vya Ebola, Mabag n.k, jengo hilo lililokamilika kwa 90%, linajengwa katika eneo la Mabibo jijini Dar es salaam.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile baada ya ukaguzi wa ujenzi wa jengo la Maabara ngazi ya tatu yenye uwezo wa kuchukua vipimo vya magonjwa hatari Duniani kama Virusi vya Ebola, Mabag n.k, unaojengwa  katika eneo la Mabibo jijini Dar es salaam.


DKT. NDUGULILE AKASIRISHWA NA KASI YA UJENZI WA MAABARA YA AFYA YA JAMII.

Na WAMJW - DSM
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amekasirishwa na kasi ndogo ya ujenzi wa Maabara  ya Afya ya Jamii ngazi ya tatu, inayoshughurikia magonjwa hatari ya mlipuko kama vile Ebola, Mabag, Kipindupindu hali inayopelekea  kuchelewesha utoaji wa huduma hizo kwa Wananchi.

Hayo yamejiri leo wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa jengo hilo lililo eneo la Mabibo jijini Dar es salaam  ili kujidhihirishia thamani ya pesa zilizotumika na kiasi cha ujenzi wa jengo hilo ulipofika.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa haoni sababu ya msingi iliyopelekea kuchelewa kukamilika kwa ujenzi wa Maabara hiyo kwani fedha zote zipo, hivyo kukasirishwa kwa kasi ndogo ya ujenzi wa Maabara hiyo ulioanza tangu mwaka 2016.

" Nitoe asikitiko yangu kwamba, kazi hii imechukua muda mrefu sana, tangia 2016, wenzetu waliozipata fedha hizi wengi wamekwisha kamilisha kazi zao, sisi Tanzania bado tunasua sua, kibong'oto, Temeke, Mawenzi na hapa, najambo linalonisikitisha sana fedha tunazo" alisema Dkt. Ndugulile

pia, Dkt. Ndugulile amesema kuwa ujenzi wa Maabara hiyo utaisaidia Serikali kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho inakipeleka nje ya nchi kwaajili yakupima sampuli za magonjwa hayo, hivyo kukamilika kwa Maabara hiyo kutaifanya Tanzania kuwa moja kati ya nchi chache barani Afrika inayotoa huduma hizo.

Aidha, Dkt Ndugulile ameonekana kutoridhishwa na usimamizi wa ujenzi wa Maabara hiyo, hivyo kutoa onyo katika matumizi ya fedha za ujenzi wa Maabara hiyo, hii ni kutokana na kufanya marekebisho ya mara kwa mara wakati ramani ya jengo hilo ipo.

"Fedha tunazo nyingi kupita maelezo, na ndiomaana mnaishia kuzitumia vibaya, matumizi ya hovyo yanapitishwa kwa haraka sana, lakini matumizi ya msingi yanasuasua, sasa niombe kwa niamba ya Kazi zote, hizi fedha tuliziomba kwa matumizi mahsusi kujenga hizi Maabara na isolation centers, naomba nitakaporudi haya tuliokubaliana mtimize" alisema Dkt Ndugulile

Kwa upande mwingie Dkt. Ndugulile amewata viongozi wa Wizara ya Afya kutokuwa kikwazo katika taratibu za ujenzi wa Maabara hiyo, ili kuepusha lawama kutoka kwa Wakandarasi, jambo litalosaidia katika kasi ya ujenzi wa Maabara hiyo.

"Taratibu za ndani, sisi kama Wizara naomba zisiwe kikwazo kwakweli, kwasababu gharama za mradi mnazijua, uendeshaji tunaujua, na tulikuwa tunazifahamu, fedha tunazo zakutosha, mzipitishe katika taratibu zake zote ili hawa Wakandarasi wasije kutulalamikia" Alisema Dkt. Ndugulile

Mwisho.

0 on: "DKT. NDUGULILE AKASIRISHWA NA KASI YA UJENZI WA MAABARA YA AFYA YA JAMII"