Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa ameshika bango kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya Kimataifa ya Uuguzi Sasa Kampeni inayolenga kuinua hadhi na muonekano wa kada ya uuguzi nchini.
Wadau wa Kampeni ya Uuguzi Sasa wakiwa wameinua mabango kuashiria kampeni hiyo kuzinduliwa rasmi.
Wauguzi wakisikiliza kwa umakini yanayoendela kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Uuguzi Sasa
Picha ya wadau wa kampeni ya uuguzi sasa waliojitokeza kwenue uzinduzi wa kampeni hiyo inayokenga kuinua hadhi na muonekano wa kada ya uuguzi nchini.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) akimpongeza Mwalimu Mstaafu wa Kada ya Uuguzi Mwl. justina Venant (kulia) kwa kumpatia cheti cha utumishi ulitukuka wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uuguzi Sasa.
Picha ya pamoja ya Viongozi na Watendaji wa Serikali pamoja na wadau wa Sekta ya Afya wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Uuguzi Sasa.
Na WAMJW - Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewataka wauguzi kutimiza wajibu wao
na kutoa huduma bora wakati wa kazi kulingana na miongozo na maadili ya kazi ya
uuguzi na ukunga.
Waziri Ummy ametoa agizo hilo leo
Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kimataifa ya Uuguzi Sasa
inayolenga kuinua hadhi na muonekano wa kada ya Uuguzi.
“Nataka kuona wauguzi wanafanya
kazi kwa kuzingatia miongozo na maadili ya taaluma ya kada ya uuguzi na kuwa na
heshima na utu kwa wagonjwa” alisema Waziri Ummy na kuendela “Nimefurahi kuona
kwenye kampeni hii mmejipanga kuondoa changamoto zilizopo”
Aidha Waziri Ummy amewataka viongozi
kuwatambua wauguzi ambao wamekuwa hawana kauli nzuri na kuwachukulia hatua ili
kuondokana na vitendo vya wauguzi kutoa kauli za kebehi kwa wateja na kuwaasa
wauguzi kuacha lugha za kebehi na zisizowafurahisha wateja kwani kufanya hivyo
kuwachafua taswira ya wauguzi nchini.
Licha ya changamoto zilizopo Waziri
Ummy hakusita kutoa pongezi kwa wauguzi ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika
utoaji wa huduma za afya nchini. “Napenda kuwapongeza wauguzi wote kwa kazi
mnayofanya, Kazi ya wauguzi wanne inafanywa na muuguzi mmoja, Kazi ya wakunga
watano, inafanywa na mkunga mmoja” alisema Waziri Ummy.
Naye Rais wa Chama cha Wauguzi
nchini Tanzania (TANNA) Bw. Paul Magesa amekiri kuwepo kwa baadhi ya wauguzi
wasio na maadili katika kazi amabo wamekuwa wakitoa kauli mbaya kwa wagonjwa
huku akiahidi kuwa kupitia chama anachoongoza changamoto hizo zitatatuliwa
ndani ya muda mfupi.
Aidha Bw. Magesa alitumia nafasi
hiyo kuipongeza Serikali kwa kuongeza bajeti ya dawa nchini ambapo sasa dhana
ya wauguzi kuwa ndio wezi wa dawa inaanza kufutika katika jamii.
“Hapo awali tulionekana sisi
wauguzi ndio wezi wa dawa, tunaotumia vibaya dawa lakini ukweli ni kwamba dawa
hazikuwepo, kitendo cha Serikali kuongeza bajeti ya dawa kimetusafisha sisi
wauguzi” alisema Bw. Paul Magesa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara
ya Uuguzi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Bw.
Gustav Moyo amesema kuwa Kampeni ya Uuguzi Sasa imekuja wakati mwafaka kuja
kutatua changamoto zilizopo muda mrefu ambazo zimekuwa zikikwamisha utendaji
kazi wa wauguzi nchini.
Bw. Gustav amesema
kuwa Uuguzi sasa ni kampeni ya kimataifa inayokusudia kuongeza hadhi na muonekano
wa kada ya uuguzi nchini ambayo inalenga kuwawezesha wauguzi na wakunga kufikia
na kumudu malengo ya afya ya karne ya 21 pamoja na changamoto zake.
0 on: "WAUGUZI WATAKIWA KUZINGATIA MAADILI KATIKA SEHEMU ZAO ZA KAZI"