Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akisisitiza jambo wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga Balozi Dkt
Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya
kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi
wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akisisitiza jambo wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga
Balozi Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara
ya Afya kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha
Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab
Chaula.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu (kushoto) akiwa na Naibu wake Dkt. Faustine Ndugulile (kulia)
wakifuatilia alichakuwa akiongea Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad
Bakari Kambi (hayupo pichani) wakati wa hafla ndogo ya kuwaaga Dkt Mpoki
Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya kabla
yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya
wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula
wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy
Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya kabla yakuteuliwa katika nafasi
nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu
Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Idara ya Afya Dkt Dorothy Gwajima.
Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya
akiteta jambo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi
wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy
Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya kabla yakuteuliwa katika nafasi
nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu
Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula, hafla ilofanyika katika ofisi za
Wizara ya Afya jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto wakifuatilia maelekezo kutoka kwa Waziri Ummy wakati
wa Hafla ndogo ya kuwaaga Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima
waliohudumu Wizara ya Afya kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na
kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Dkt Zainab Chaula. Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za Wizara ya Afya
jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akisaini Biblia Takatifu aliyopewa kama zawadi Balozi Dkt. Mpoki
Ulisubisya wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga Baozi Dkt Mpoki Ulisubisya
Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya kabla yakuteuliwa
katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula, hafla ilofanyika katika
ofisi za Wizara ya Afya jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mhe.Ummy
Mwalimu akimkabidhi Zawadi Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa Hafla
ndogo ya kumuaga yeye na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya
Afya kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha
Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab
Chaula.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mhe.Ummy
Mwalimu akimkabidhi Zawadi Naibu Katibu Mkuu Idara ya Afya TAMISEMI Dkt. Dorothy Gwajima wakati wa Hafla
ndogo ya kumuaga yeye na Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya waliohudumu Wizara ya
Afya kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha
Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab
Chaula.
Wakwanza kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akifuatilia alichakuwa akiongea Mganga Mkuu wa
Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga
Balozi Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara
ya Afya kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha
Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab
Chaula (Wakatikati) na (Wakwanza kishoto) ni Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI
Idara ya Afya Dkt Dorothy Gwajima.
Mkurugenzi wa MSD ambae pia ni mwakilishi wa Wakurugenzi wa Taasisi zote
za Wizara ya Afya Laurean Bwanakunu akitoa salamu za taasisi zote za
Afya wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt.
Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya kabla yakuteuliwa katika
nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula, hafla hiyo imefanyika katika
ofisi za Wizara ya Afya jijini Dodoma.
Na WAMJW - DOM
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo amewaongoza watumishi katika halfa fupi ya
kumuaga rasmi aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Mpoki Ulisubisya
ambae ameteuliwa kuwa Balozi, na aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Tiba
Wizara ya Afya, ambaye amekuwa Naibu Katibu Mkuu Idara ya Afya TAMISEMI
Dkt. Dorothy Gwajima na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na
aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Idara ya Afya TAMISEMI Dkt. Zainab Chaula
ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Afya na aliyekuwa Mganga Mkuu wa
Dar es salaam ambaye kwa sasa ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara Tiba Wizara
ya Afya Dkt. Grace Maghembe
Katika
hafla hiyo Waziri Ummy amewashukuru watumishi wote wakiongozwa na Dkt
Mpoki Ulisubisya kwa ushirikiano waliouonesha katika kipindi chote
walichofanya kazi Wizara ya Afya na kuwasihi kuendeleza uchapaji kazi
ili kusukuma gurudumu la Maendeleo hususani maendeleo ya Sekta ya Afya.
Aidha,
Waziri Ummy amewakaribisha Watumishi wote walioamia katika Wizara ya
Afya, Waziri Ummy amesema kwamba licha ya mafanikio makubwa ambayo Sekta
ya Afya imepiga, bado kuna changamoto nyingi ambazo zinapaswa
kutatuliwa ikiwemo suala la uhaba wa watumishi, na upatikanaji wa Dawa
na vifaa tiba.
Naye Naibu
Waziri wa Afya, Dkt. Fustine Ndugulile amewakumbusha Watumishi wa Sekta
ya Afya juu ya uwajibikaji na kuwatoa hofu kuwa, kama Serikali milango
yao ipo wazi muda wote, hivyo kwa yoyote mwenye wazo zuri la kujenga na
kuipeleka mbele Sekta ya Afya asisite kuwaona.
Kwa
upande wake, aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Mhe. Balozi Dkt.
Mpoki Ulisubisya amewashukuru Watumishi wote wa Sekta ya Afya
wakiongozwa na Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu kwa ushirikiano
waliomuonesha katika kipindi chote alichohudumu katika Wizara ya Afya,
kisha kuahidi kuwa Balozi Mzuri huko atakoenda ili kuikuza Sekta ya
Afya.
Naye, Katibu Mkuu
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab
Chaula amewakumbusha Watumishi wa Sekta ya Afya juu ya umoja na
ushirikiano baina yao, huku akisisitiza kila mmoja ni lazima ahakikishe
anatimiza wajibu wake ili kusukuma mbele Maendeleo ya Sekta ya Afya.
Kwa
upande wake, aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Wizara ya Afya ambae
sasa ni Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Idara ya Afya Dkt Dorothy Gwajima
ameahidi kuwa daraja zuri na imara baina ya Wizara ya Afya na TAMISEMI
kutokana na kuzijua Wizara zote mbili kiundani na kuahidi kuendeleza
mazuri yote yalioachwa na Dkt. Zainab Chaula.
Mwisho.
0 on: "TUENDELEE KUSHIRIKIANA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA"