Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akielezea jambo katika kikao na ugeni kutoka Ireland (haupo katika picha), uliofika kujadili namna gani Serikali hizo mbili zinaweza kushirikiana katika kuleta maendeleo nchini hususani katika Sekta ya Afya.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika kikao na ugeni kutoka Ireland ulioongozwa na Balozi wa Ireland nchini Tanzania Mhe. Paul Sherlock (Wakwanza Kushoto), uliofika kujadili namna gani
Serikali hizo mbili zinaweza kushirikiana katika kuleta maendeleo nchini
hususani katika Sekta ya Afya.
Na WAMJW - DSM
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amekutana na
Balozi wa Ireland nchini Tanzania Mhe. Paul Sherlock ambaye pia
aliongozana na wajumbe wengine kutoka Ireland.
Katika
Mkutano huo masuala mbalimbali yameongelewa ikiwemo masuala ya
ushirikiano baina ya nchi ya Tanzania na Ireland katika shughuli za
Maendeleo hususan katika Sekta ya Afya katika masuala ya Lishe, Hifadhi
ya Jamii na masuala ya uongozi bora.
Dkt.
Ndugulile ameishukuru Serikali ya Ireland kwa kuisaidia Serikali ya
Tanzania katika shughuli za Maendeleo hususan katika Sekta ya Afya
kupitia Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO's).
Dkt.
Ndugulile aliendelea kusema kuwa Serikali ya Ireland na Serikali ya
Tanzania zimeingia makubaliano ya kuleta Wataalamu wa Afya ili
kuwajengea uwezo Wataalamu wa Tanzania
"Tangu
2007 Ireland ina mahusiano ya muda mrefu na Tanzania kupitia Hospitali
ya CCBRT, huku Wataalamu wake wakitoa huduma za upasuaji wa Fistula na
upasuaji wa mifupa" alisema Dkt. Ndugulile
Mbali
na hayo Dkt. Ndugulile aliweka wazi vipaumbele vya Serikali ili
kuimarisha Sekta ya Afya, ikiwemo masuala ya Afya ya uzazi,Mama na
Mtoto, Afya ya vijana balehe, kuboresha miundombinu, matumizi ya mifumo
ya takwimu na huduma za dharura.
Mwisho
ameishukuru Serikali ya Ireland kwa msaada wanaoipatia Tanzania na
ameahidi kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na Serikali
ya Ireland katika kuimarisha Maendeleo hususan katika Sekta ya Afya.
#TunaboreshaAfya
0 on: "DKT. NDUGULILE APOKEA UGENI KUTOKA IRELAND"