Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akizungumza na baadhi ya watoto waishio katika
Mazingira magumu waliopo katika Makazi ya Watoto yaliyopo Kurasini
jijini Dar es salaam wakati alipofanya ziara leo katika makazi hayo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile(kulia) akikagua mazingira ya Makazi ya Watoto
wanaoishi katika Mazingira magumu yaliyopo Kurasini jijini Dar es salaam
wakati alipofanya ziara leo katika makazi hayo kushoto ni Afisa
Mfawidhi wa Makazi hayo Bi. Beatrice Mgumiro
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akifungua bomba la maji wakati akikagua mazingira ya
Makazi ya Watoto wanaoishi katika Mazingira magumu yaliyopo Kurasini
jijini Dar es salaam wakati alipofanya ziara leo katika Makazi hayo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile(kulia) akijadiliana jambo na Afisa Mfawidhi wa Makazi
ya watoto waishio katika mazingira magumu Kurasini Bi. Beatrice
Mgumiro (kushoto) wakati alipokuwa akikagua mazingira wanamolala watoto
wakati alipofanya ziara yake leo katika Makazi hayo jijini Dar es
Salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile(kushoto) akihakikisha kuwa watoto wanapatiwa chakula
bora kwa kukuroga chakula wakati alipofanya ziara yake leo katika
Makazi ya Watoto yaliyopo Kurasini jijini Dar es salaam kulia ni Afisa
Mfawidhi wa Makazi hayo Bi. Beatrice Mgumiro.
Makazi ya Watoto waliokuwa wanaishi katika mazingira yaliyopo Kurasini jijini Dar es salaam
Na WAMJW – DSM
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile amelaani mauaji na matendo ya kikatili yote
yanayofanywa dhidi ya Watoto, huku akivishukuru vyombo vya Dola kwa
hatua za haraka wanazoendelea kuchukua katika kudhibiti matukio hayo.
Ameyasema
hayo leo wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya Makazi ya Watoto
wanaoishi katika Mazingira magumu yaliyopo Kurasini jijini Dar es
salaam.
Dkt. Ndugulile
amesema kuwa Serikali haiwezi kuvumikia mambo yakikatili yanayofanywa
dhidi ya Watoto na haki zao, hivyo itawachukulia hatua yeyote atakae
bainika amekwenda kinyume na kuvunja sheria zinazomlinda mtoto.
"Tunalaani
sana, mauaji haya ya Watoto, na tunavishukuru vyombo vya Dola vimeweza
kuchukua hatua za haraka kuhakikisha kwamba vinadhibiti matukio haya"
alisema Dkt. Ndugulile
Mbali
na hayo Dkt. Ndugulile ametoa rai kwa Waganga wote wa Tiba Asili na
Tiba Mbadala kuacha kutumia viungo wala miili ya Watoto kama njia
yakutatua matatizo kwa wateja wao, hivyo hatua kali zitachukuliwa kwa
watakao kaidi agizo hilo.
Dkt.
Ndugulile ameongeza kuwa Waganga wa Tiba Asili na Tiba mbadala wote ni
lazima wahakikishe wanajisajili katika Mamlaka na Baraza husika ili
kuepuka usumbufu na hatua kali dhidi yao pindi watakapobainika
hawajafanya hivyo.
Ameongea
kuwa Waganga wa Jadi watakaobainika na kujihusisha na shughuli
zisizosajiliwa katika shughuli za Tiba Asili na Tiba Mbadala
watachukuliwa hatua kali sana za kisheria dhidi yao na hata wale ambao
watajihusisha pamoja na waganga hao.
Dkt.
Ndugulile pia ameutaka Uongozi wa Makazi ya watoto waishio katika
mazingira magumu kuwajibika katika baadhi ya mambo ikiwemo masuala ya
usafi wa mazingira , Mabweni na mavazi kwa watoto uzingatiwe na kuaagiza
kuweka magodoro mapya, mashuka na chandarua katika mabweni hayo.
Naye
Afisa Mfawidhi wa Makazi hayo Bi. Beatrice Mgumiro amesema kuwa makazi
hayo yanajumla ya watoto 70 ambapo watoto 54 wapo katika makazi hayo na
watoto 16 wapo wanasoma katika shule za bweni.
Bi.
Beatrice amemuhakikishia Naibu Waziri kuwa atatekeleza maagizo yote
aliyompa na ameishukuru Serikali kwa uangalizi wa karibu wa watoto
waishio katika mazingira magumu kwa kutoa huduma muhimu kwa watoto hao
ikiwemo malazi chakula na elimu.
MWISHO.
0 on: "SERIKALI YALAANI MAUAJI YA WATOTO"