Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumamosi, 23 Februari 2019

TAARIFA WAKATI WA UPOKEAJI WA MAJOKOFU YA KUTUNZIA CHANJO NA VISHIKWAMBI KWA AJILI YA KUKUSANYA TAARIFA ZA CHANJO KATIKA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA HAPA NCHINI

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akitoa mfano kupitia kadi ya Kliniki, namna gani Mfumo utafanyakazi kwa kutumia kishikwambi, wakati akipokea majokofu ya kutunzia chanjo na vishikwambi (tablets) kwaajili ya kukusanyia taarifa katika vituo vya Afya hapa nchini, tukio limefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akipokea majokofu ya kutunzia chanjo, kutoka kwa Mkuu wa Masuala ya Afya UNICEF Kyaw Aung (Watatu kushoto)  tukio limefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam. Kulia kwa Waziri Ummy ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof Muhammad Bakari Kambi, Mkurugenzi wa Kinga Dkt. Leonard Subi na Meneja wa Mpango wa chanjo Taifa Dafrosa Lyimo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu   akipokea vishikwambi (tablets) kwaajili ya kukusanyia taarifa katika vituo vya Afya hapa nchini, kutoka kwa Mkuu wa Masuala ya Afya UNICEF Kyaw Aung, (Wakwanza kushoto)  tukio limefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam. Pembeni kwa Waziri Ummy ni Meneja wa Mpango wa chanjo Taifa Dafrosa Lyimo.



TAMKO LA WAZIRI WA AFYA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), WAKATI  WA UPOKEAJI WA MAJOKOFU YA KUTUNZIA CHANJO NA VISHIKWAMBI KWA AJILI YA KUKUSANYA TAARIFA ZA CHANJO KATIKA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA HAPA NCHINI TAREHE 22.02.2019, D’ SALAAM.

Ndugu Wanahabari,
Naomba nichukue fursa hii kumshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kutuwezesha kukutana hii leo katika hafla muhimu.
Ndugu Wanahabari,
Kama mnavyofahamu, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  ilikusudia kuwa kila kijiji kiwe na zahanati na kila kata iwe na kituo cha afya kwa nia ya kuzileta na kusogeza huduma za afya karibu zaidi na wananchi. Kati ya huduma hizo muhimu ni pamoja na upatikanaji wa chanjo mbalimbali kwa ajili ya kuzuia magonjwa mbalimbali yakiwamo ugonjwa kupooza unaosababishwa na virusi ya Polio, ugonjwa wa kifaduro na donda koo, surUu rubella, kansa ya mlango wa kizazi, n.k. Chanjo hizi hutunzwa, kusafirishwa na kutolewa kwa walengwa zikipitia mfumo wa mnyororo baridi toka zinakotengenezwa hadi kituo cha kutolea huduma. Aidha, Wizara hutunza na kufuatilia takwimu mbalimbali za chanjo zinazoonyesha maendeleo ya utoaji huduma kwa kutumia mtandao wa komputa kote nchini.
Ndugu Wanahabari,
Napenda kuutarifu umma wa Tanzania kuwa, Serikali kwa kushirikiana na shirika la Gavi, imefanikiwa kununua jumla ya majokofu 1,385 yenye thamani ya shilingi bilioni 13,991,270,300 (serikali imechangia 20% na Gavi 80%) kwa ajili ya kuimarisha mnyororo baridi wa utunzaji wa chanjo katika vituo vya kutolea huduma za afya hapa nchini. Majokofu 1,190 yanatumia nishati ya jua na kila jokofu lina thamani ya shilingi milioni 10,879,000 (USD 4,730) na majokofu 195 yanatumia umeme, na kila jokofu lina thamani ya shilingi milioni 5,361,000 (USD 2,331). Vilevile Serikali na shirika la Gavi imenunua jumla ya vishikwambi (tablets) 1,249 vyenye gharama ya shilingi  bilioni 1,598,720,000 kwa ajili ya kukusanya na kuhifadhi taarifa za chanjo kwa njia ya mtandao, na kila kishikwambi kina thamani ya shilingi milioni 1,280,000.
Ndugu Wanahabari,
Majokofu na vishikwambi tunavyopokea leo ni awamu ya kwanza, ambapo mapema mwezi Mei tutapokea jumla ya vishikwambi 2100 venye thamani ya shilingi bilioni 2,688,000,000 na mwishoni mwa mwaka huu, tutapokea awamu nyingine ya majokofu (kati ya 800-1000) yenye thamani ya shilingi bilioni 11,533,357,820 (USD 5,014,503) na kufikia asilimia zaidi 80 ya mahitaji ya majokofu na vishikwambi katika vituo vyote hapa nchini.
Ndugu Wanahabari,
Majokofu haya ya kutunzia chanjo yatasambazwa na kufungwa katika vituo vipya na vituo vyenye majokofu yenye teknolojia iliyopitwa na wakati. Ifahamike kuwa, majokofu haya yanayotumia teknolojia ya kisasa ambapo, nishati ya jua inatumika kutoa ubaridi na hayahitaji kutumia betri, hivyo kuziondolea gharama halmasahuri za ununuzi wa gesi kila mwezi au manunuzi ya betri, kama yalivyo majokofu mengine yanayotumia nishati ya jua.
Ndugu Wanahabari,
Halmashauri zote za Tanzania Bara pamoja na Wilaya za Zanzibar zitapokea majokofu haya kwa awamu kuu mbili. Awamu ya kwanza itahusisha mikoa 15 ambayo ni Dodoma, Geita, Kagera, Kigoma, Lindi, Tanga, Mara, Mbeya, Mtwara, Mwanza, Shinyanga, Songwe, Unguja, Pwani na Singida. Na awamu ya pili itahusisha mikoa iliyobaki.
Ndugu Wanahabari,
Kama nilivyoeleza awali, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tamisemi, kupitia Mpango wa Taifa wa Chanjo imeanza kukusanya taarifa za chanjo kwa kutumia mifumo ya kielektroniki, ambapo katika ngazi ya kituo kishikwambi kitatumika kukusanya taarifa za chanjo kupitia mfumo wa kielektroniki wa leja ya Watoto (Tanzania electronic immunization Registry - TimR).
Ndugu Wanahabari,
Taarifa zilizokusanywa zitatumwa wilayani katika mfumo ujulikanao kama “Vaccine Information Management System (VIMS)” na kutumwa katika Mfumo Mkuu wa Kielektroniki wa Wizara (District Health Information System DHIS-2.
Ndugu Wanahabari,
Mfumo wa VIMS tayari umeanza kutumika katika mikoa na wilaya zote nchini na mfumo wa TimR kwa sasa unatumika mikoa ya Arusha, Tanga, Kilimanjaro na Dodoma. Wizara inakusudia kusambaza mfumo wa TimR katika mikoa ya Mwanza, Morogoro, Mtwara, Geita, Njombe na Dar es Salaam kabla ya kufika mwezi Aprili mwaka huu.
Ndugu Wanahabari,
Vile vile, ili kuhakikisha ufanisi na ufuatiliaji wa utendaji kazi wa majokofu ya kuhifadhia chanjo, Wizara ya Afya kwa kushikiana na wadau wa shirika la JSI na Nexleaf kwa ufadhili wa Gavi, inatarajia kufunga vifaa vya kupima na kufuatilia halijoto katika vituo takribani 5,000 kati ya vituo zaidi ya 7,000 kote nchini.
Ndugu Wanahabari,
Vifaa hivi vinamuwezesha Afisa Chanjo kujua utendaji kazi wa jokofu ikiwa ni pamoja na kujua halijoto ya jokofu katika vituo vya huduma za afya bila ya kulazimika kufika katika kituo husika. Vifaa hivi vinatuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) pindi halijoto inapopanda au kushuka.
Ndugu Wanahabari,
Tanzania itakuwa ni miongoni mwa nchi chache duniani zenye mfumo huu wa kisasa wa kufuatilia utendaji kazi wa majokofu ya chanjo na kuhakikisha watoto wanapatiwa chanjo zenye ubora wa hali ya juu wakati wote.
Ndugu Wanahabari,
Kwa namna ya pekee, napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza watoa huduma za chanjo hapa nchini, Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, pamoja na Waratibu wa Chanjo wa Mikoa na wilaya zote kwa kuwezesha nchi yetu ya Tanzania kufikisha viwango vya juu vya utoaji wa huduma za chanjo.
Ndugu Wanahabari,
Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa mwaka 2017 nchi yetu ilifikisha kiwango cha uchanjaji cha asilimia 98 na kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya tatu duniani kwa viwango vya juu vya utoaji wa huduma za chanjo. Mafanikio ya huduma za chanjo hapa nchini, pamoja na afua zingine, imeiwezesha nchi kufikia malengo ya milenia (MDG 4) kwa kupunguza vifo vya Watoto chini ya miaka mitano kwa theluthi 2/3.
Ndugu Wanahabari,
Napenda kuchukua fursa hii kuwasisitiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri pamoja na Waratibu wa Chanjo katika ngazi za mikoa na halmashauri, kuhakikisha kuwa watoa huduma wote wa chanjo wanafundishwa jinsi ya kufanya matengenezo madogomadogo ya majokofu (planned preventive maintenance) ili kuhakikisha kuwa vifaa hivi vinadumu kwa muda mrefu kama ilivyokusudiwa. Ni matarajio ya Wizara na Serikali kuwa, vifaa hivi vitaongeza upatikanaji wa huduma za chanjo karibu na wananchi na hivyo kupunguza idadi ya Watoto ambao hawajafikiwa na huduma za chanjo.
Ndugu Wanahabari,
Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wadau wote wa chanjo kwa kuendelea kutoa ufadhili na kuhakikisha kuwa kila mtoto anafikiwa kwa huduma za chanjo.
Ndugu Wanahabari,
Mwisho kabisa, napenda kuwahimiza wazazi na walezi wote hapa nchini kuwapeleka watoto wao katika vituo vya kutolea huduma za afya ili wakapate chanjo mbalimbali zinazotolewa kukinga magonjwa anuai. Halikadhalika, ninawahimiza mabinti wote waliotimiza umri wa miaka 14 wajitokeze ili kupata chanjo ya kuwakinga dhidi ya maambukizi ya saratani ya mlango wa kizazi kwani chanjo hii inatolewa bila malipo yoyote katika vituo vya serikali na binafsi. Dozi ya kwanza ya chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi inatolewa wakati wowote binti anapofikisha umri wa miaka 14 na dozi ya pili inatolewa miezi sita (6) baada ya dozi ya kwanza.

ASANTENI KWA KUNISIKILIZA





MGAWANYO WA MAJOKOFU
S/N
MKOA
WILAYA
IDADI YA MAJOKOFU
1
DODOMA
BAHI
9
KONDOA DC
21
KONGWA DC
20
MPWAPWA DC
28
JUMLA
78
2
GEITA
BUKOMBE DC
6
CHATO DC
14
GEITA DC
17
GEITA TC
7
MBOGWE DC
12
NYANG’WALE DC
8
JUMLA
64
3
KAGERA
BIHARAMURO
6
BUKOBA DC
25
KARAGWE DC
23
KYERWA DC
22
MISENYI DC
21
MULEBA DC
24
NGARA DC
20
BUKOBA MC
7
JUMLA
148
4
KIGOMA
BUHIGWE DC
6
KAKONKO DC
4
KASULU TC
5
KIBONDO DC
3
KIGOMA DC
14
KIGOMA MC
1
UVINZA DC
10
JUMLA
43
5
LINDI
KILWA DC
23
LINDI DC
25
LINDI MC
5
NACHINGWEA DC
20
LIWALE DC
21
RUANGWA DC
11
JUMLA
105
6
MARA
BUNDA DC
10
BUTIAMA DC
18
MUSOMA DC
25
MUSOMA MC
11
SERENGETI DC
28
TARIME DC
25
RORYA
28
JUMLA
145
7
MBEYA
BUSOKELO DC
10
CHUNYA DC
21
KYELA DC
18
MBARALI DC
18
MBEYA CITY
3
MBEYA DC
20
RUNGWE DC
21
JUMLA
111
8
MTWARA
MASASI DC
29
MASASI TC
7
MTWARA MC
6
MTWARA DC
10
NANYAMBA
11
NANYUMBU DC
15
NEWALA DC
14
NEWALA TC
9
TANDAHIMBA DC
6
JUMLA
107
9
MWANZA
BUCHOSA DC
17
ILEMELA DC
15
KWIMBA DC
27
MAGU DC
11
MISUNGWI DC
26
SENGEREMA DC
16
UKEREWE DC
18
NYAMAGANA DC
16
JUMLA
146
10
PEMBA
CHAKE CHAKE
8
MICHEWENI
10
MKOANI
11
WETE
8
JUMLA
37
11
SHINYANGA
KISHAPU DC
25
MSALALA DC
16
SHINYANGA DC
17
SHINYANGA MC
10
USHETU DC
17
KAHAMA TC
7
JUMLA
92
12
SONGWE
ILEJE DC
26
MBOZI DC
28
MOMBA DC
23
SONGWE DC
15
TUNDUMA TC
4
JUMLA
96




13
UNGUJA
KASKAZINI A
5
KASKAZINI B
8
KATI
14
KUSINI
5
MAGHARIBI
14
MJINI
12
JUMLA
58
14
PWANI
BAGAMOYO DC
8
CHALINZE DC
22
JUMLA
30
15
SINGIDA
ITIGI DC
5




16
TANGA
BUMBULI
9
HANDENI DC
19
KILINDI DC
14
KOROGWE DC
16
KOROGWE TC
2
LUSHOTO DC
8
MKINGA DC
14
MUHEZA DC
24
PANGANI DC
14
JUMLA
120






JUMLA KUU
1385





                                                                                                                                             
MGAWANYO WA VISHIKWAMBI
S/No
MKOA
IDADI YA VISHIKWAMBI
1
DAR ES SALAAM
300
2
MWANZA
350
3
MTWARA
100
4
NJOMBE
236
5
GEITA
143
6
MOROGORO
120

JUMLA
1249


0 on: "TAARIFA WAKATI WA UPOKEAJI WA MAJOKOFU YA KUTUNZIA CHANJO NA VISHIKWAMBI KWA AJILI YA KUKUSANYA TAARIFA ZA CHANJO KATIKA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA HAPA NCHINI"