Katibu Mkuu wa Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akitoa
taarifa mbele ya Wadau wa Sekta ya Afya wakati wa Kikao cha kusaini makubaliano
ya Mfumo wa Ukusanyaji wa takwimu takwimu wa kielektroniki kilichofanyika
mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.
Wadau wa Sekta ya Afya
wakifuatilia kwa makini taarifa ya mgeni
rasmi (Hayupo kwenye picha) ambae ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, jinsia, Wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa Kikao cha
kusaini makubaliano ya Mfumo wa Ukusanyaji wa takwimu takwimu wa kielektroniki.
Mwinyekiti wa DPG HEALTH Mhe.
Norzin Grigoleit-Dagyab akitutubia mbele ya Wadau wa Sekta ya Afya na Watumishi
wa Serikali wa Idara kuu ya Afya wakati wa Kikao cha kusaini makubaliano ya
Mfumo wa Ukusanyaji wa takwimu takwimu wa kielektroniki jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya na wa mwisho kulia ni Mwakilishi kutoka WHO Dkt.
Matthieu Kamwa.
Picha ya Pamoja ikiongozwa na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt.
Mpoki Ulisubisya akiwa na Wadau mbali mbali wa Sekta ya Afya katika Kikao cha
kusaini makubaliano ya Mfumo wa Ukusanyaji wa takwimu wa kielektroniki kilichofanyika
mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja ya Viongozi
wa Sekta ya Afya wakiwa wameshika mikataba iliyosainiwa ya makubaliano ya Mfumo
wa Ukusanyaji wa takwimu wa kielektroniki ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya.
Na WAMJW-DAR ES SALAAM.
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya
jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imeazimia kukusanya na kutumia takwimu kwa
njia ya kielektroniki nchi nzima ili kuweza kumudu na kutoa huduma za afya kwa
ubora zaidi nchini.
Hayo yamezungumzwa na Katibu Mkuu Wizara ya afya Dkt.
Mpoki Ulisubisya wakati wa kutia Sahihi ya makubaliano ya kuanzisha mfumo wa
ukusanyaji takwimu za afya utakaotekelezwa na Wizara ya afya,Wadau wa
Maendeleo,Asasi za Kiraia na Shirika la Afya Duniani (WHO) uliofanyika leo
jijini Dar es salaam.
“Takwimu ni muhimu sana amabazo zitazomuwezesha mtoa
huduma kujua mgonjwa historia yake ya ugonjwa
na matibabu aliyopewa awali,kuwapa Uwezo utumishi kujua tunahitaji
rasilimali watu kwa kiasi gani katika
kituo cha Afya” alisema Dkt. Ulisubsya.
Aidha, Dkt. Ulisubisya amesema kuwa kwa kuanzia zoezi hilo
litaanza kwenye mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na Manyara hatimaye kufikia nchi
nzima mpaka kufika 2020 ili kuweza kuwa
na takwimu za afya.
Dkt. Ulisubisya amesema kuwa mfumo wa kujaza takwimu
kwenye makaratasi umepitwa na wakati kwani kadri makaratasi ya takwimu
yanapokuwa mengi na makosa ya utoaji huduma unaweza kutokea kwani mpaka uanze kutafuta takwimu zilizopita
inachukua muda mrefu tofauti na kuhifadhi takwimu kielektroniki.
Mbali na hayo Dkt. Ulisubisya amesema kuwa mpaka hivi sasa
hali ya utoaji wa chanjo imefikia asilimia 97 na lengo letu ni kufikia asilimia
100 kupitia mfumo huu wa kukusanya takwimu kwa njia ya kielektroniki.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani
(WHO) Dkt. Matthieu Kamwa amesema kuwa wapo
tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya
katika kutekeleza hilo ili kuweza kuboresha mifumo ya afya nchini.
“Unajua Takwimu ni utajiri hasa katika kutekeleza shughuli
za kutoa huduma za afya kwa wananchi hivypo hatuna budi kuunga mkono juhudu za
Serikali ya Tanzania katika kufanikisha hili jambo kwani litaturahisishia hata
sisi katika kutoa miongozo ya afya” alisema Dkt. Kamwa.
0 on: "SERIKALI YAAZIMIA KUKUSANYA TAKWIMU ZA AFYA KIELEKTRONIKI NCHI NZIMA."