SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imedhamiria kupambana na Saratani ya mlango wa kizazi nchini kwa kuwapa kinga wasichana kuanzia umri wa miaka 9 mpaka 14 ili kuondoa tatizo hilo nchini.
Hayo
yamebainishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) mapema leo wakati akifungua mkutano wa
wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es
salaam.
“Katika
kukabiliana na ugonjwa wa Saratani, kuimarisha afya ya wanawake
Tanzania pamoja na kupunguza vifo vitokanavyo na Saratani , Wizara ya
Afya itaanza kutoa chanjo ya kuwakinga wasichana dhidi ya Saratani ya
mlango wa kizazi mwaka huu”. Alisema Mhe. Ummy Mwalimu.
0 on: "TANZANIA KUONDOA TATIZO LA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI KWA WANAWAKE"