Mganga Mkuu wa Serikali Prof.
Muhammed Bakari Kambi akipokea cheti cha kutambua mchango mkubwa uliofanywa na
Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Malaria kutoka mwakilishi wa WHO Dkt. Ritha
Njau tukio lililofanyika mapema leo Serena jijini Dar es salaam.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof.
Muhammed Bakari Kambi akiongea na wadau wa Afya na waandishi wa habari katika
kikao cha kupokea cheti cha kutambua mchango mkubwa uliofanywa na Serikali
katika kupambana na ugonjwa wa Malaria.
Meneja wa Mpango wa Kupambana
na Kudhibiti Malaria nchini Dkt. Ally Mohamed akiwasilisha taarifa mbele ya
wadau na waandishi wa Habari katika kikao cha kupokea cheti cha kutambua
mchango mkubwa uliofanywa na Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Malaria
kutoka mwakilishi wa WHO Dkt. Ritha Njau tukio lililofanyika mapema leo Serena
jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa WHO Dkt. Ritha
Njau akijiandaa kumkabidhi cheti Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammed Bakari
Kambi
Wadau wa Afya wakifuatilia
kwa umakini taarifa ilokuwa ikiwasilishwa na Meneja wa Mpango wa Kupambana na
Kudhibiti Malaria nchini Dkt. Ally
Mohamed (hayupo kwenye picha)wakati wa kikao cha kupokea cheti cha kutambua
mchango mkubwa uliofanywa na Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Malaria.
Na
WAMJW-Dar es salaam.
SERIKALI
ya Jamhuri wa Muungano Tanzania imepata tuzo kutoka Shirika la Afya Duniani
(WHO) kwa kutambua mchango mkubwa uliofanywa katika jitihada ya kudhibiti
Ugonjwa wa Malaria nchini.
Akikabidhiwa
Tuzo hiyo wakati wa mkutano wa siku mbili ulioanza leo wa kujadili mafanikio na
changamoto katika kudhibiti Malaria,Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Muhammad Bakari Kambi alisema tuzo
hiyo imetolewa kwa Serikali na Watanzania kwa ujumla na Shirika hilo kanda ya Tanzania
Prof.Kambi
alisema tuzo hiyo imetolewa kwa kuanisha mchango mkubwa uliofanywa na Serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
katika kuweka Mikakati,Rasilimali fedha na kufanya kazi kwa ukaribu na wahisani
mbalimbali katika kupambana na Malaria
Prof.
Kambi aliendelea kusema kuwa ushiriki wa Tanzania katika tafiti mbalimbali
ambazo zimechangia katika udhibiti wa Malaria ikiwemo utafiti wa kutumia
vyandarua vyene viuatirifu vya kuzuia mbu pamoja na tafiti za awali za chanjo za kudhibiti
Malaria.
“Mafanikio
mengine ni upungufu wa Ugonjwa wa
Malaria kutoka wagonjwa milioni 18 kwa mwaka 2008 hadi wagonjwa milioni 5.5 kwa
mwaka 2017.Pia Malaria imekua chanzo kikubwa cha vifo vya watoto wenye umri
chini ya miaka mitano hivyo kumekua na upungufu kutoka vifo 112 kati ya watoto
1,000 mwaka 2005 hadi vifo 79 kati ya
watoto 1,000 mwaka 2016”.Alisema
Aidha,
kipengele kingine katika vita dhidi ya udhibiti wa ugonjwa wa Malaria ni kwamba,
Tanzania ndio nchi pekee Barani Afrika kuwa na kiwanda kinachotengeneza
vyandarua vyenye dawa ya kudhibiti mbu aenezaye Malaria.
Naye,Kaimu Mwakilishi Mkazi wa WHO, Dkt. Ritha
Njau amesema tuzo hiyo imetolewa kwa Tanzania baada ya kufanikiwa kupunguza maambukizi
ya Malaria kwa kipindi cha miaka 10, hivyo WHO imeona ni vema kutoa tuzo hiyo
ikiwa ni katika kutambua mafanikio hayo.
Wakati
huo huo,Meneja Mpango wa Kudhibiti Malaria Nchini Dkt. Ally Mohammed alisema
hali ya maambukizi ya Malaria nchini hivi sasa imepungua na kufika asilimia 7.3
ambapo lengo ni kutokomeza malaria nchini.
Dkt. Ally
Mohammed Alitaja mikoa ya Kigoma, Geita na Kagera hali ya malaria bado ipo juu,
hivyo mkutano huo utaweza kujibu maswali kwanini mikoa hiyo maambukizi ya
malaria bado juu na kitu gani kifanyike ili kuweza kutokomeza ugonjwa huo.
0 on: "TANZANIA YAPOKEA TUZO YA KUPAMBANA NA UGONJWA WA MALARIA KUTOKA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO)"