Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi katika
ufunguzi wa jengo la mama na mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana, mapema
leo jijini Dar es salaam, katikati ni Naibu waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimjulia hali moja ya mama aliyekuwa
akiuguliwa na mtoto wake, akifanya hivyo baada ya kuzindua jengo la mama na
mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana, kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Mhe. Poul Makonda.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakisalimiana na Mbunge wa Ilala Mhe.
Azan Zungu wakati wa Uzinduzi wa jengo la mama na mtoto lililopo katika
Hospitali ya Amana, wa pili ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Poul Makonda
na wa mwisho ni Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa mama aliyekuwa akiuguliwa na mtoto
wake, akifanya hivyo baada ya kuzindua jengo la mama na mtoto lililopo katika
Hospitali ya Amana, kulia kwake ni Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile.
Picha ya pamoja ikiongozwa na
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, kulia
kwake ni Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Poul
Makonda.
Na WAMJW. DSM
SERIKALI yaendelea kuongeza
vituo vya Afya nchini ikiwa ni moja ya jitihada za Serikali za kuboresha Huduma
za afya nchini jambo litakalo saidia kupunguza msongamano wa wagonjwa katika
Hospitali za Wilaya na Mkoa kwa kuwa huduma zote zitakuwa zimeishia kwenye
ngazi ya Kata.
Hayo yamebainishwa na Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa ufunguzi
wa jengo la mama na mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana, mapema leo jijini
Dar es salaam.
“Kumekuwa na ongezeko kubwa
la vituo vya Afya nchini kutoka vituo vya Afya 6321 kwa mwaka 2010 hadi vituo
vya Afya 7680 kwa mwaka 2016, na kazi ya nyongeza inaendelea, kwaiyo
tunaamini vituo hivi vitaweza kupunguza
msongamano katika hospitali za Wilaya, pamoja na Hospitali za Mkoa”, alisema
Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Mhe. Waziri Mkuu alisema
kwamba Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
ametenga kiasi cha Zaidi ya Bilioni 100 ikiwa ni fedha za kuboresha Vituo vya
Afya nchini ili kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi katika maeneo yote
nchini.
“Tumeanza kuboresha Vituo vya
Afya kwa kujenga Wodi yakinamama wanaojifungua, thieta, wodi za magonjwa yakawaida,
maabara, tunaongeza na nyumba za watumishi, ili kila kituo cha Afya kiwe na
miundombinu hiyo ili utoaji huduma uwe rahisi” alisema Mh. Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa.
Mhe. Waziri Mkuu aliendele
kusema kwamba Serikali imetumia Zaidi ya Bilioni 161 katika kuendelea kuboresha
Huduma za Mama na Mtoto kwa lengo la kuokoa Maisha ya mama na mtoto jambo
ambalo ni moja kati ya changamoto kubwa nchini.
Aidha Mhe. Waziri Mkuu alisema
kwamba Serikali imeendelea kuboresha Huduma za Afya kwa kutenga kiasi cha shilingi
Bilioni 129 kwaajili ya vifaa vya kuwezesha kundesha shughuli za upasuaji
katika kila kituo cha Afya ambacho kinaboreshwa.
Wakati akitoa taarifa ya Afya
ya Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Poul Makonda alisema
kwamba wakina mama 126,164 walipata nafasi ya kujifungua katika vituo vya Afya,
huku wakinamama 202 ambao ni sawa na Asilimia 0.5 walilazimika kujifungua kwa
wakunga, na Asilimia 1.5 zaidi ya akinamama 1976 walijifungua njiani wakielekea
kupata huduma, idadi inayoonekana kuwa kubwa sana katika Mkoa wa Dar Es salaam.
Idadi ya 2016 inaonesha Zaidi
ya akina mama 85 walikuwa wanapoteza Maisha kati ya kina mama 100,000 waliokuwa
wanajifungua lakini kwa sasa tangu maboresho yafanyike ni akina mama 57 kati ya
akina mama 100,000 wanaojifungua ndio hupoteza Maisha, huku mikakati thabiti
yakupunguza vifo hivyo ikiendelea kuwekwa.
Mhe. Makonda aliendelea
kusema kwamba zaidi ya watoto ambao wanafanikiwa kuwa hai na kuwa salamakatika
kujifungua ni Zaidi ya watoto 126,712, na watoto 131 huzaliwa wakiwa tayari
wameshakufa, idadi hii ikilinganishwa .
Pia Mhe. Makonda alimshukuru
AMSONS GROUP ambayo imetoa mchango mkubwa katika ujenzi wa Jengo hilo la Mama
na Mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana huku akiwataka Wadau wengine kuiga
mfano huo katika dhana ya kusukuma gurudumu la maendeleo katika jamii zetu.
Nae Naibu
waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano tangu iingie madarakani imeongeza
Bajeti ya Dawa kutoka Bilioni 30 mpaka sasa ni Bilioni 270 likiwa ni ongezeko
la Zaidi ya mara 9, huku Wastani wa upatikanaji wa dawa ukiwa Zaidi ya asilimia
80.
“Serikali wakati inaingia
madarakani Bajeti ya dawa ilikuwa ni Bilioni 30, mwaka unaofuata ikafikia
Bilioni 200, na hivi tunavyoongea Bajeti ya Dawa ni Bilioni 270, likiwa ni
ongezeko la mara 9, kama msaidizi wako nasimama kifua mbele na kusema ya kwamba
hatuna uhaba wa Dawa muhimu”, alisema Dkt. Ndugulile.
0 on: "SERIKALI YAENDELEA KUSOGEZA HUDUMA ZA AFYA KWA WANANCHI KWA KUONGEZA VITUO VYA AFYA NCHINI."