Kaimu Mkurugenzi
msaidizi wa tiba asili na tiba mbadala kutoka Wizara ya Afya, maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Poul Mhame akiongea na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya leo jijini Dar es salaam.
Na WAMJW. Dar es salaam.
SERIKALI kupitia Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepanga kusitisha shughuli
za utoaji wa huduma zinazofanywa na waganga wa tiba asili na tiba mbadala pindi
muda wa kujisajili utakapokuwa umwekwisha.
Amebainisha hayo Kaimu Mkurugenzi
msaidizi wa tiba asili na tiba mbadala kutoka Wizara ya Afya, maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Poul Mhame mapema leo pindi alipoongea na
waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.
“Waganga wa Tiba asili na Tiba
mbadala na vituo vyao watalazimika kusitisha utoaji huduma wanazotoa pindi muda
wa usajili cha itafika mwisho” Alisema Dkt. Mhame
Dkt. Mhame aliendelea kusema
kuwa Serikali ilianza usajili wa Waganga wa Tiba asili takribani miaka saba
ilopita na mpaka sasa ni waganga 16,300 tu ndio waliofanikiwa kujisajili huku
mchakato huo ukiendelea mpaka sasa.
Dkt. Mhame alielezea
kusikitishwa sana na idadi ndogo ya Waganga wa tiba asilia kujisajili inayoendelea
kwa maeneo ya mjini hususania katika Manispaa, Miji, na Halmashauri, ikilinganishwa
na maeneo ya vijijini ambao wanaonekana kwenda kwa kasi sana,
“Ni Dhahiri kuwa taarifa hizi,
hazijawafikia wengi hususani waliopo vijijini kutokana na vyombo vya habari
vilivyopo kule, lakini wengi waliopo mijini hawana sababu zakusema hawajui”
Alisema Dkt. Mhame.
Aidha, Dkt, Mhame amewashauri
Wanganga wa Tiba asili kutumia fursa hii kwa muda uliobaki kwa kwenda ofisi za Waganga
wa Halmashauri zao kujaza fomu na kuziwasilisha ili waweze kujisajili na
kuondokana na usumbufu huo.
“Itakuwa si busara kwa mganga
alipo Dar es salaam akakutwa hajajisajili kwa kipindi chote cha miaka saba,
asilalamike kwamba hana taarifa” Alisema Dkt Mhame.
Kwa upande mwingine Dkt.
Mhame aliwataka wanaojihusisha na uzalishaji wa Dawa kusajili dawa hizo huku
akiwahasa wataalamu mbali mbali kama vile Madaktari, Wafamasia, Wakemia, Maafisa
lishe kushirikiana kwa ukaribu katika kuboresha huduma za tiba Asili kwa
kutumia taalama zao kwa kushirikiana na Waganga wa Tiba Asilia ili kuweza kupata
soko linalostahili na lenye usalama na ufanisi wakutosha.
0 on: "SERIKALI YAPANGA KUSITISHA UTOAJI HUDUMA YA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA KWA WAGANGA WASIOJISAJILI"