Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 31 Januari 2018

TANGAZO LA KUITWA KAZINI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya.JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,
WAZEE NA WATOTO
 
 
 
 
TANGAZO LA KUITWA KAZINI
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto -Idara Kuu Afya anawajulisha wafuatao kuripoti kazini Makao Makuu ya Wizara Mjini Dodoma ndani ya siku 14 wakiwa na vyeti halisi vya  elimu ya Sekondari, Taaluma,usajili wa Baraza/Bodi ya kitaaluma,cheti cha kuzaliwa pamoja na nakala mbili za picha ndogo (passport)
Imetolewa na :

Katibu Mkuu-Afya
31/1/2018
ORODHA YA MAJINA YA WOAMBAJI WANAOTAKIWA KURIPOTI WIZARA YA AFYA MEANDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO KUKAMILISHA TARATIBU ZA AJIRA  


NA JINA CHEO KITUO CHA KAZI1 LILIAN DIDAS LYAKURWA KATIBU WA AFYA II KATIBU MKUU AFYA2 NKWIMBA NYALALI AFISA MUUGUZI MSAIDIZI II KATIBU MKUU AFYA3 MARY MATHIAS OTTARU AFISA AFYA MAZINGIRA II KATIBU MKUU AFYA4 JACOB R. TARIMO MUUGUZI  KATIBU MKUU AFYA5 SOPHIA ISSA LUCAS MHUDUMU WA AFYA KATIBU MKUU AFYA6 HAPPY ALEX YOHANES MHUDUMU WA AFYA KATIBU MKUU AFYA7 MARTHA ADRIANO MHUDUMU WA AFYA KATIBU MKUU AFYA8 JENIPHER JOSEPH GHULIKU MTEKNOLOJIA MSAIDIZI MAABARA KATIBU MKUU AFYA9 SURAIYA A. DULE MHUDUMU WA AFYA KATIBU MKUU AFYA10 NEEMA MWASENGA MHUDUMU WA AFYA KATIBU MKUU AFYA11 SCHOLASTICA OFAMAN MHUDUMU WA AFYA KATIBU MKUU AFYA12 BLANDINA VICTOR SHUMA AFISA MUUGUZI MSAIDIZI II KATIBU MKUU AFYA

WATOA HUDUMA ZA USINGIZI WANAHITAJIKA ZAIDI NCHINI.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya, akihutubia mapema leo wakati wa ufunguzi wa Mtaala wa Kufundishia watu watakaotoa Huduma ya Usingizi, tukio lililofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi MUHAS jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasilimali watu Dkt. Otilia Gowelle, akinyoosha mkono kama ishara ya kujitambulisha, wakati wa ufunguzi wa Mtaala wa Kufundishia watu watakaotoa Huduma ya Usingizi.
 
Mkurugenzi wa Mafunzo ya Shahada za mwanzo MUHAS ambae pia alimwakilisha Mkuu wa Chuo Prof. Mainem Moshi akiwasilisha taarifa fupi ya Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi MUHAS wakati wa ufunguzi wa Mtaala wa Kufundishia watu watakaotoa Huduma ya Usingizi.

Mlezi wa Wanafunzi kutoka Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi MUHAS Dtk. Edith Tarimo akiwasilisha Taarifa mbele ya mgeni rasmi ambae ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya.

Tukio la ufunguzi wa Mtaala wa Kufundishia watu watakaotoa Huduma ya Usingizi, katika ukumbi wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi MUHAS jijini Dar es salaam.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya, wakati wa ufunguzi wa Mtaala wa Kufundishia watu watakaotoa Huduma ya Usingizi, tukio lililofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi MUHAS jijini Dar es salaam.


Na WAMJWW-DSM.
Watumishi wa wa afya wa kutoa huduma za usingizi wanahitajika zaidi nchini ili kuweza kutoa huduma hiyo kwa wingi na ukaribu zaidi mara zinapohitajika kwa wagonjwa wanaohitaji upasuaji kwa usalama katika hospitali zetu .
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto Idara kuu ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa ufunguzi wa Mtaala wa kufundishia watu watakaotoka na Shahada ya Huduma ya Usingizi itakayotolewa na Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi MUHAS leo jijini Dar es salaam.
“Nawaagiza wenzetu wa MUHAS wahakikishe  kasi ya kuandaa mtaala wa kufundishia iongezwe na  uletwe haraka ili kuweza kupata wataalamu wa kutoa huduma za usingizi ili wakafanye kjazi kwenye Hospitali za Rufaa za Mkoa” alisema Dkt. Ulisubisya.
Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa kabla ya mtaala huu kupitishwa hapo nyuma wagonjwa awalikuwa wanapata huduma za usingizi pindi wanapohitaji kufanyiwa upasuaji kutoka kwa wataalamu waliopata mafunzo kwa mwaka mmoja au waliojifunza kwenye sehemu zao za kazi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo wa Shahada za Mwanzo MUHAS Prof. Mainem Moshi amesema kuwa tayari wameshapeleka mtaala wa wahandishi wa vifaa tiba kwani wanahitajika takribani wahandisi  elfu 8 nchini.
Aidha Prof. Mainem amesema kuwa kusimamishwa kwa mtaala wa kufundishia shahada ya udhamiri kwa kozi za ukunga kumepeleka vifo 556 katika kina mama laki moja kwa wamama wanaojifungua hivyo Serikali ipo haja ya kurudisha huu mtaala.

Jumanne, 30 Januari 2018

SERIKALI YA TANZANIA YATIA SAINI MKATABA NA MFUKO WA FEDHA WA PAMOJA WA SHILINGI TILIONI 1.1 KWAAJILI YA KUPAMBANA NA UKIMWI, MALARIA NA KIFUA KIKUU.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kupokea msaada kutoka mfuko wa fedha wa pamoja (Global Fund) kilichofanyika jana katika Ofisi za Waziri Mkuu jijini Dar es salaam.

Meza kuu, Ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (wapili) wakati wa kikao cha kupokea msaada kutoka mfuko wa fedha wa pamoja (Global Fund), kushoto kwake ni Mwakilishi kutoka Global Fund Tatjana Peterson, kulia kwake ni Pro. Faustine Kamuzora, wa mwisho ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya. 

Picha ya pamoja ikionesha zoezi la kutia saini baina ya Serikali ya Tanzania na Mfuko wa Fedha wa pamoja (Global funds).

Picha ya Pamoja ya Makabidhiano ya Mkataba yaliyo sainiwa na Serikali ya Tanzania na Mfuko wa Fedha wa pamoja (Global funds).
Kikao cha Makubaliano ya kusaini Shilingi Tilioni 1.1 kati ya Serikali na Mfuko wa fedha wa pamoja kilichofanyika jana katika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam.

 
Na WAMJWW. DSM
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jnsia, Wazee na Watoto imetia saini Shilingi Tilioni 1.1 na mfuko wa fedha wa pamoja (Global Fund) kwa ajili ya kupambana na magonjwa ya UKIMWI, MALARIA na KIFUA KIKUU.
Hayo yamebainishwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) wakati wa kikao cha Makubaliano ya kusaini fedha hizo kilichofanyika jana katika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam.
“Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, napenda kuwashukuru sana Global funds, kwa kuendelea kushirikiana nasi katika kutatua changamoto za rasilimali fedha katika kupambana na UKIMWI, MALARIA na KIFUA KIKUU” alisema Mh. Ummy Mwalimu.
Mh. Ummy aliendelea kusema kwamba utekelezwaji wa makubaliano ya shughuri hii utasimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu huku miradi ikitekelezwa na Wizara ya Afya, Ofisi ya Raisi TAMISEMI pia Mashirikayasiyo yakiserikali na Sekta Binafsi.
Pia Waziri Ummy amewataka Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Katibu Mkuu wa TAMISEMI kuhakikisha fedha hizo zilizotolewa na Mfuko wa Fedha wa pamoja kutumika kikamilifu ili kuweza kupata matokeo yaliyotarajiwa ya Asilimia 90 ya wananchi kupima UKIMWI ili kujua hali zao, Asilimia 90 ya Watanzania walio na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI waweze kutumia dawa ya kufubaza Virusi hivyo (ARV) na Asilimia 90 ya wanaotumia dawa za ARV, Virusi viwe vimefubazwa (90,90,90).
Mbali na Hayo Mh. Ummy Mwalimu amesema kuwa Asilimia 40 ya Watanzania wameweza kufika katika vituo na kupata tiba, huku lengo ni kuhakikisha kwamba itakapofika mwaka 2020, asilimia 70 ya wenye maambukizi ya Kifua kikuu wawe wanajulikana na kuanza kupata huduma za matibabu mara moja.
Kwa upande wa Malaria fedha hizo zitatumika katika kupunguza maambukizi ya Malaria ili kufikia Asilimia 1 ifikapo mwaka 2020.
Akiwawakilisha Makatibu Wakuu wenzake Prof Faustine Kamuzora ameahidi kusimia matumizi sahihi ya fedha zote walizopokea kutoka kwa Mfuko huo katika kuhakikisha utekelezaji unafanyika kwa ufanisi mkubwa na kwa maadili ili kufikia malengo waliyojipangia.
“Tutahakikisha kwamba fedha zote zilizopatikana zinatumika vizuri na kuhakikisha kwamba matokeo makubwa yanapatikana, Afya za Watanzania zinahimarika kwa kufanya usimamizi mzuri.” Alisema Prof Kamuzora.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Global Fund Tatjana Peterson ameahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika kupambana na magonjwa ya UKIMWI, Malaria na Kifua Kikuu.
Nae msindika Makohozi Bw. Paskali Mbagala ameishukuru Serikali kwa kuendelea kusogeza huduma ya kupima na kutibu magonjwa ya Kifua Kikuu kwa wananchi hususani wa vijijini, jambo lililosaidia kupunguza vifo vya watu wengi.
Akiwasilisha Taarifa ya Baraza la watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi, Mwenyekiti wake Bw. Justine Bunyoka ameiomba Serikali kuendeleza ushirikiano wa karibu na Mfuko huo ili kurahisisha kufikisha Huduma kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi.

TAARIFA KWA UMMA.

- Hakuna maoni

SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WATUMISHI WA AFYA NCHINI KATIKA KUBORESHA SEKTA HIYO.

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.

Watumishi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga pamoja na Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (Hayupo kwenye Picha) wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga.

Afisa Uuguzi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Jane Mazigo akitoa maelezo mbele ya Mgeni rasmi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga.

Mwenyekiti wa Baraza la Uuguzi na Ukunga aliyemaliza muda wake Stuart Mbelwa akipokea Cheti kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa Baraza la Uuguzi na Wakunga, Kulia ni Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Lena Mfalila
Mwenyekiti aliyeingia kuliongoza Baraza la Uuguzi na Ukunga Abner Mathube akiahidi kuchapa kazi mbele ya mgeni rasmi ambae ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga.

Picha ya Pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati akizindua Baraza la Uuguzi na Ukunga katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.


Na WAMJWW.DSM.

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeahidi kuendelea kutatua changamoto za zinazowakabili watumishi wa Kada ya Afya nchini ikiwemo kuboresha miundombinu inayowazunguka.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) mapema leo wakati akizindua Baraza la Wauguzi na Wakunga katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.
“Asilimia 80% ya Kazi zote za kutoa huduma za Afya, zinafanywa na Wauguzi na Wakunga, kwaiyo wakati tunazungumzia kuboresha huduma za, Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuzifanyika kazi changamoto hizo ikiwemo suala la watumishi” alisema Mh. Ummy Mwalimu.
Mh. Ummy aliendelea kusema kwamba, sambamba na changamoto Wauguzi na Wakunga wanazoendelea kukumbana nazo Serikali itaendelea kutimiza wajibu wake wa kutatua changamoto hizo katika kuboresha Huduma za Afya.
Kwa upande mwingine Mh. Ummy alimwagiza Mwenyekiti mpya wa Baraza hilo Bw. Abner Mathube Kusimamia mabadiliko ya kanuni za maadili ya Baraza hilo ambazo zimeonekana kupitwa na wakati, hivyo kutofanya kazi kwa ufanisi unaostahili na kushindwa kuendana na wakati huu.
“Nimeelekeza zile kanuni za maadili za mwaka 2007 ni lazima zifanyiwe marekebisho, kwani  zimepitwa na wakati, ili tuweze kusimamia taaluma hii vizuri ya Uuguzi na Ukunga.” Alisema Mh. Ummy Mwalimu.
Pia Mh. Ummy Mwalimu amelitaka Baraza hilo kujizatiti katika kutoa taarifa za Baraza mbele ya umma katika kueleza shughuli za kila mara za Baraza hilo, jambo litakalosaidia kuwafahamisha wananchi juu ya majukumu ya baraza hilo.
“Jamii haipati taarifa kuhusu utendaji kazi wa Baraza, tunatakiwa kuliona Baraza linakuja mbele, angalau kila robo mwaka katika kila kipindi, kukaa kimya kunafanya wananchi waone Baraza halina meno wala maamuzi” Alisema Mh. Ummy Mwalimu.
Kwa upande mwingine Mh. Ummy amelitaka Baraza hilo kuwachukulia hatua Waauguzi na Wakunga wanaenda kinyume na maadili ya kazi yao, huku akikemea matumizi ya lugha chafu yanayofanywa na baadhi ya wauguzi wachache ambao kwa kiasi kikubwa wanaitia doa kada hiyo.
Aidha, Mh. Ummy amemshukuru mwenyekiti aliyemaliza muda wake Stuart Mbelwa kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kuliongoza Baraza hilo ikiwemo kusimamia wauguzi na wakunga nchini, kusimamia vyuo na vituo vya kutolea huduma za Afya na kuweza kukamilisha jengo la kuwaendeleza Wauguzi na Wakunga, huku akiwataka waamishe kazi zote za Baraza hilo katika jengo hilo lililopo Kibaha.
Mwisho Waziri Ummy aliahidi kuvifungia au kuvishusha hadhi Vituo vya Afya ambavyo havitakidhi vigezo vya kutoa huduma kwa jamii, huku akiwataka Wakurugenzi kujenga tabia ya kuvitembelea vituo hivyo ili kujionea mahitaji ya Vituo hivyo.
“Tutafungia au kuvishusha hadhi Vituo vya Afya ambavyo havikidhi vigezo, kwa hili hatutooneana aibu, wala kujali hiki ni kituo cha Afya cha serikali au chabinafsi, wakishindwa kutoa Huduma Bora hatutasita kuvifungia” alimaliza Mh. Ummy Mwalimu.