Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto akiangalia kazi inavyoendelea katika hospitali hiyo.
Waziri ummy Mwalimu akiangalia ramani ya kituo hicho cha afya ambacho
kimejengwa kwa ushirikiano wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na
Shirika la SEDA Foundation, kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Dkt.Subi na kushoto ni mmoja wa Viongozi wa Shirika hilo.
Waziri Ummy Mwalimu akiangalia duka la dawa lililopo kwenye hospitali ya
Mkoa ya Sekoture ambapo upatikanani wa dawa kwa Mkoa wa Mwanza ni
asilimia 80.
Jengo la Maabara lililojengwa kwenye kituo hicho cha afya katika mpango
wa Serikali wa kuboresha huduma za dharura za uzazi kwenye vituo vya
afya nchini.(Picha zote na Wizara ya Afya)
Waziri Ummy Mwalimu akiangalia Ramani ya Ujenzi wa jengo la ghorofa nne
la Uzazi linalojengwa hospitali ya Mkoa ya Sekoture jijini Mwanza.
Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akikagua huduma za afya kwenye kituo cha afya cha kamanga kilichopo
Wilaya ya Sengerema.Waziri ummy yupo Mkoani Mwanza katika ziara ya
kikazi ya kujionea hali ya utoaji huduma za afya mkoani hapo.
Waziri Ummy Mwalimu na Naibu Waziri Dkt.Angela Mabula wakikagua ujenzi
wa jengo la dharura la uzazi kwenye kituo cha afya cha Karume kilichopo
kata ya Igombe Wialayani Ilemela,akiyevaa koti la bluu ni Mganga Mkuu wa
Wilaya hiyo Dkt.Florian Tinuga.
Mawaziri hao wakijadili jambo wakati wa ukaguzi wa jengo la upasuaji wa
kumtoa mtoto tumboni linalojengwa kwenye kituo cha afya cha Karume
,Wilayani Ilemela.
Na.WAMJW,Mwanza
Wakurugenzi wa
Halmashauri nchini wametakiwa kusimamia Fedha za kuboresha huduma za
dharura zinazotolewa na Serikali zitumike ipasavyo na si kwa matumizi
mengine.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo
ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu jijini hapa wakati akiwa
kwenye ziara ya kukagua shughuli za utoaji huduma za afya pamoja na
ujenzi wa huduma za dharura za Uzazi kwenye kituo cha afya cha Karume
kilichopo kata ya Igombe Wilayani Ilemela.
Waziri
Ummy alimpongeza Mkurugenzi wa Ilemela kwa matumizi mazuri ya fedha hizo
ambapo alijionea kazi nzuri inayoendelea katika kituo hicho ambapo
wametumia wajenzi wa kawaida na ujenzi huo unaenda vizuri na kwa kiwango
kinachoridhisha.
Aidha,alisema Fedha za kuboresha
miundombinu ya huduma za uzazi wa dharura zitumike kama haya angalau
kujengwe chumba cha upasuaji,maabara ya damu na tunamataka wodi ya
wazazi na nyumba moja ya mtumishi kuliko kujenga masuala mengine
“kama
fedha zitabaki unaweza kufikiri kujenga vitu vingine,kuliko kqenda
kutumika kwa masuala mengine kama baadhi ya sehemu nyingine
wanavyofanya, kama fedha zimebaki nipo tayari kukuruhusu kujenga kitu
kingine Mkurugenzi,hongera sana Mkurugenzi na viongozi wengine”.
Hata
hivyo alisema Tanzania ni moja ya nchi yenye vifo vingi vya akina mama
wajawazito na watoto”leo hii toka saa sita usiku tuanze siku hadi saa
sita usiku wanawake 30 wa kitanzania wanafariki kwa sababu tu ya
kutimiza wajibu wao wa kuleta kiumbe duniani”
“Kwahiyo
Mhe.Rais alichokifanya kwa kushirikiana na wadau tunaboresha huduma za
uzazi zikiwepo za upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni,hivyo tumefurahi
kuona hapa zile shilingi milioni mia tano zimetumika ipasavyo,binafsi
nimedhirika na kazi iliyofanywa hapa karume hivyo naahidi kuleta fedha
kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya kituo cha afya Buzurugwa”alisema Mh. Ummy.
Wakati huo huo nae naibu Waziri wa
Ardhi,Nyumba na Makazi na Mbunge wa Jimbo la Ilemele Dkt.Angela Mabula
alisema wao kama viongozi watahakikisha fedha zote zitakazoenda kwa
ajili ya afya itatumika ipasavyo na wataisimamia ili kuweza kuboresha
miundombinu ya sekta ya afya
Naye Mkuu wa Mkoa
wa Mwanza John Mongela amewataka wananchi wa Igombe kuendeleza
mshikamano wanaouonyesha ili kuendelea kufanya makubwa zaaidi kwa
kujiletea maendeleo”mchakato wa maendeleo chini ya Jemedari wetu rais
Magufunli ndo kwanza umeanza”.
0 on: "WAKURUGENZI WA HALMASHAURI WATAKIWA KUSIMAMIA FEDHA ZA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA AFYA"