Waziri wa afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikatiakitembelea maeneo ya
Hospitali ya Taaluma na Tiba Mloganzila alipotyembelera hospitali hiyo ili
kuangalia hali ya utoaji huduma leo jijini Dar es salaam.. wa kwanza kushoto ni
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo na Huduma za Hospitali hiyo Prof. Aboud Said.
PICHA NA ALLY DAUD.
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu leo Januari 10 ,2018 ametembelea Hospitali ya Taaluma na Tiba
ya Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Cha Muhimbili (MUHAS) kampasi ya
Mloganzila iliyofunguliwa rasmi na Mhe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Novemba 25
,2017 .
Lengo la kutembelea hospitali hiyo ni kuangalia utoaji wa
huduma za afya zinazotolewa katika hospitali hiyo.
Baada ya kutembelea hospitali hiyo Waziri Ummy ameagiza Idara
yote ya magonjwa ya ndani (Internal Medicine) iliyopo hospitali ya Taifa ya
Muhimbili kuhamia mara moja katika hospitali hiyo wakiwemo Madaktari,Madaktari
Bingwa,Wauguzi pamoja na wataalmu wengine wa idara hiyo.
Wakati huo huo Waziri Ummy ameagiza kuhamisha wagonjwa
waliopo wodi namba 3,4,5,6,7 na 8 zilizopo kwenye jengo la Mwaisela Muhimbili
na kupelekwa hospital ya Mloganzila isipokuwa wagonjwa walio mahututi na wenye
sababu maalumu na baada ya kuondoka wagonjwa hao wodi hizo zifanyiwe ukarabati mara
moja. .”Nawaagiza waganga wafawidhi wa hospitali za Rufaa za
Temeke,Mwananyamala na Amana kuanzia sasa rufaa zote za wagonjwa wa magonjwa ya
ndani zije Mlongazila”, Alisema Mhe.Ummy.
Aidha, Waziri Ummy alisema Wizara imeshapokea Hospitali za
Rufaa za Mikoa kutoka TAMISEMI hivyo amemuagiza Katibu mkuu wa Wizara hiyo kukamilisha
kuwapangia baadhi ya Madaktari Bingwa waliopo hospitali hiyo ya Taifa na
kuwapeleka hospitali za Rufaa za Mkoa na Kanda mapema Februari mwaka huu.
“Tumeomba kibali Utumishi wa Umma ili kuwahamisha Madaktari
Bingwa zaidi ya ishirini (20) waliopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
pamoja na mishahara yao,”Madaktari wetu ni Wazalendo wapo tayari kwenda kutoa
huduma za matibabu ya kibingwa kwenye hospitali zetu za Mikoa na Kanda”.
Alisema Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kwa dhati
kuwahudumia wananchi wote ikiwemo kupata huduma za matibabu ya kibingwa bila
kubagua hivyo Wizara yake imejipanga kununua vifaa na vifaa tiba na kuvisambaza
kwenye hospitali hizo za rufaa za Mikoa. Alitaja Madaktari bingwa
watakaohamishiwa kwenye hospitali za rufaa za mikoa na kanda miongoni mwao ni
wa Magonjwa ya akina Mama na Uzazi, Watoto,Upasuaji
wa jumla,Radiolojia,Usingizi Macho pamoja na Magonjwa ya ndani.
Mloganzila ni Hospitali ya Taaluma na Tiba ambayo imewekwa vifaa
tiba vya kisasa na teknolojia ya hali ya juu na ina vitanda 571 vya kulaza
wagonjwa na vyumaba 13 vya upasuaji na inatoa
huduma masaa ishirini na nne.
Imetolewa na
Catherine Sungura
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- Afya
10/1/2018
|
0 on: "WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEA HOSPITALI YA TAALUMA NA TIBA MLOGANZILA"